Saturday 7 November 2009

RATIBA LIGI KUU England:
Jumamosi, Novemba 7
Aston Villa v Bolton
Blackburn v Portsmouth
Tottenham v Sunderland
Wolves v Arsenal
Jumapili, Novemba 8
Chelsea v Man U
Hull City v Stoke
West Ham v Everton
Wigan v Fulham
ZE BIGI MECHI: Chelsea v Man U
Stamford Bridge, Jumapili Novemba 8, Saa 1 usiku [Bongo Taimu]
Chesea, anaeongoza Ligi, atakuwa nyumbani Stamford Bridge, kupambana na Mabingwa Watetezi Manchester United ambao wako nafasi ya pili.
Msimu uliokwisha, mechi kama hii iltoka sare 1-1 huku Ji-Sung Park akiifungia goli Man U na Salomon Kalou kusawazisha dakika ya 80.
Nini wanasema:
Sir Alex Ferguson: "Chelsea ni mechi kubwana rekodi yetu uwanjani kwao si nzuri kwa miaka ya hivi karibuni. Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi hii na wataishughulikia kwa ubora zaidi kuliko ile mechi ya Anfield.”
Gary Neville: "Kwa sasa Chelsea wako juu. Ni mechi ngumu.”
Vikosi:
Chelsea (Pengine, 4-4-2): Cech; Ivanovic, Carvalho, Terry, A Cole; Essien, Ballack, Lampard, J Cole; Anelka, Drogba.
Manchester United (Pengine, 4-4-2): Van der Sar; O'Shea, Brown, Evans, Evra; Valencia, Scholes, Carrick, Nani; Berbatov, Rooney.
Refa: Martin Atkinson.
Msimu uliokwisha: Chelsea 1 Man United 1; Man United 3 Chelsea 0.
Ferdinand kuwa nje kwa muda mrefu!!
Beki mahiri wa Manchester United, Rio Ferdinand, anategemewa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kushindwa kupona musuli ya mguuni.
Meneja wake Sir Alex Ferguson amesema: “Hajapona. Na atakuwa nje muda mrefu!”
Hivyo, Ferdinand ataikosa mechi ya kesho ya Ligi Kuu na Chelsea na pia kuichezea England huko Doha, Qatar Novemba 14 ambapo England itacheza na Brazil.
Jumamosi hii, Ferdinand anatimiza miaka 31 na msimu huu amekuwa akikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kwani aliukosa mwezi mzima wa kwanza wa msimu huu baada ya kuchanika musuli pajani akiwa mazoezini.
Kifungo cha kusajili Wachezaji Chelsea chasimamishwa!!
CAS [Court of Arbitration for Sport] imesimamisha kifungo walichopewa Chelsea na FIFA cha kutosajili Wachezaji hadi 2011 baada ya kukiuka sheria na kumchukua Mchezaji Gael Kakuta kutoka Lens ya Ufaransa.
CAS imetamka kuwa kifungo hicho kitasimama hadi rufaa ya Chelsea itakaposikilizwa na uamuzi kutoka.
Rufaa hiyo inategemewa kusikilizwa mwakani.
Uamuzi huo unamaanisha Chelsea wanaweza kusajili Wachezaji mwezi Januari 2010 wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa lakini Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, amesema hana nia ya kusajili mtu.
Hata hivyo, mwezi huo wa Januari, Chelsea itawapoteza Wachezaji Michael Essien, Didier Drogba, Salomon Kalou na John Mikel Obi ambao wote watakuwa na Timu zao za Taifa kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika kwa Mataifa ya Afrika yatakayochezwa Januari huko Angola.
Viera akasirika kuachwa Ufaransa!
Patrick Viera amesema Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech amefanya makosa makubwa kutomchagua Kikosi cha Ufaransa ambacho kitacheza na Republic of Ireland kwenye mechi ya mtoano kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wiki ijayo.
Viera ameshaichezea Ufaransa mara 107 na msimu huu huko Klabuni kwake Inter ya Italia hana namba.
Viera, mwenye miaka 33, ametamka: "Mie najijua mwenyewe na Ufaransa hamna bora kama mie!”

No comments:

Powered By Blogger