Saturday 29 August 2009

Man U 2 Arsenal 1
Diaby aipa ushindi Man U!!!
Old Trafford leo iliwaka moto, ingawa Timu zote zilionekana kuwa kidogo chini ya kiwango, baada ya Manchester United na Arsenal kupambana kwenye mechi ya Ligi Kuu na Man U kutoka na ushindi wa 2-1.
Arsenal, walioonekana kuwa juu kidogo kipindi cha kwanza, walipata bao kupitia Arshavin dakika ya 41 alipopiga shuti kali ambalo Kipa Foster alishindwa kuzuia.
Mpaka mapumziko Man U 0 Arsenal 1.
Kipindi cha pili, Man U waliweza kucheza vizuri zaidi na dakika ya 58 Wayne Rooney akaangushwa na Kipa Almunia na Refa Mike Dean akaamua ni penalti.
Rooney alipiga penalti hiyo na kufunga.
Dakika 5 baadae Man U walipata frikiki upande wa kulia na Giggs akaidondosha katikati ya goli na ndipo Diaby, akiwa hayuko kwenye presha yeyote, akapiga kichwa na kujifunga mwenyewe.
Dakika 90 zilipomalizika zikaongezwa dakika 5 za nyongeza na Arsenal walimudu kufunga bao muda huo kupitia van Persie lakini Mshika Kibendera alikuwa tayari ameashiria ofsaidi kwa Gallas ambae alitoa pasi kwa van Persie.
Uamuzi huo, ulioonekana ni sahihi kwenye marudio ya video, ulimkasirisha Arsene Wenger na akaipiga teke chupa ya maji na ndipo Mwamuzi wa Akiba alipomwita Refa Mike Dean alieamuru Wenger atoke nje Uwanjani.
Kichekesho kilikuwa Wenger [pichani] akaenda moja kwa moja kusimama mbele ya Washabiki wa Man U waliokuwa wakimshangilia.
Vikosi:
Manchester United: Foster, O’Shea, Brown, Vidic, Evra, Fletcher, Carrick, Giggs, Nani, Rooney, Valencia.
Akiba: Kuszczak, Berbatov, Anderson, Owen, Neville, Park, Scholes
Arsenal: Almunia, Sagna, Gallas, Vermaelen, Clichy, Eboue, Denilson, Song Billong, Diaby, Arshavin, van Persie.
Akiba: Mannone, Eduardo, Ramsey, Silvestre, Wilshere, Gibbs, Bendtner.
Refa: Mike Dean (Wirral)
Liverpool waifunga Mtu Kumi Bolton 3-2
Liverpool wakicheza nyumbani kwa Bolton, huku mechi ikiwa suluhu 2-2, walipata msaada mkubwa kwa Refa Alan Wiley aliemtoa Sean Davis baada ya kumpa Kadi mbili za njano ya pili ikionekana haistahili na ndipo Nahodha na mhimili wao Steven Gerrard alipowafungia bao la 3 na la ushindi.
MATOKEO LIGI KUU ENGLAND
JUMAMOSI AGOSTI 29
Chelsea 3 v Burnley 0
Blackburn v West Ham
Bolton 2 v Liverpool 3
Stoke 1 v Sunderland 0
Tottenham 2 v Birmingham 1
Wolves 1 v Hull City 1
Evra aishutumu Arsenal, adai Refa alimtaka ajichunge asiumizwe!!!
Beki wa Manchester United Patrice Evra ameishutumu Timu ya Arsenal kwa jinsi walivyokuwa wakimchezea rafu na kuwa na nia ya kumuumiza katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu mwezi Mei iliyochezwa Old Trafford iliyoisha 0-0 na kuwapa Ubingwa Manchester United.
Evra amesema anaamini vitendo hivyo vilivyofanywa na Wachezaji wa Arsenal ni kisasi baada ya Man U kuwafunga mechi zote 2 za Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na yeye kutoa kauli kuwa matokeo hayo yametofautisha nani mtoto na nani mwanaume.
Evra amesema hata Refa wa mechi hiyo, Mike Dean [pichani kulia], ambae pia ndie Refa wa mechi ya leo kati ya Timu hizo, alimuonya kuwa inabidi awe mwangalifu au ataumizwa.
Evra amesema: “Vitendo vya Arsenal ni aibu. Niliulizwa kama walikuwa wananiwinda na nikajibu ndio! Nilishangaa kwani Arsenal siku zote wanacheza mpira mzuri na si watu wa fujo! Namshukuru Refa. Kuna wakati Refa alikuja kwangu na kuniambia ‘angalia, sijui nini kinaendelea lakini mara baada ya mapumziko Wachezaji wote wa Arsenal wanataka kukuumiza. Usilipize kisasi!"
Chelsea 3 Burnley 0
Wakiwa nyumbani Stamford Bridge Chelsea leo wamepata ushindi wao wa 4 katika mechi zao 4 za Ligi Kuu msimu huu walipowafunga Wababe wa Manchester United na Everton, Burnley, Timu iliyopanda Daraja msimu huu, kwa mabao 3-0.
Bao la kwanza la Chelsea lilipatikana kabla tu ya mapumziko baada ya Drogba kupiga krosi ya chinichimi golini na mpira kuguswa na Carlisle wa Burnley na kisha kumparaza Anelka na kutinga wavuni.
Bao la pili lilifungwa na Ballack kwa kichwa baada ya krosi ya Lampard.
Ashley Cole akafunga bao la 3 kufuatia gonga kati yake na Lampard.
Vikosi:
Chelsea: Cech, Bosingwa, Carvalho, Terry, Ashley Cole, Essien, Ballack, Deco, Lampard, Anelka, Drogba.
Akiba: Hilario, Ivanovic, Mikel, Malouda, Kalou, Sturridge, Belletti.
Burnley: Jensen, Mears, Carlisle, Bikey, Jordan, Alexander, Blake, Elliott, McCann, Paterson, Steven Fletcher.
Akiba: Penny, Kalvenes, McDonald, Gudjonsson, Thompson, Guerrero, Eagles.
Refa: Mark Clattenburg (Tyne & Wear).
CARLING CUP: DRO YA Raundi ya 3 yatatolewa!!
Mabingwa Watetezi wa Kombe la Carling, Manchester United, wamepangiwa kucheza na Wolverhamton kwenye mechi ya Raundi ya Tatu kugombea Kombe hilo na mechi hiyo itafanyika nyumbani kwa Manchester United Old Trafford.
Mshindi wa pili wa Kombe hili Tottenham Hotspur watasafiri kwenda kupambana na Preston.
Mechi za Raundi ya Tatu zinatakiwa kuchezwa wiki ya kuanzia Septemba 21.
RATIBA KAMILI YA RAUNDI YA 3:
Arsenal v West Brom
Chelsea v QPR
Bolton v West Ham
Barnsley v Burnley
Hull City v Everton
Leeds v Liverpool
Manchester United v Wolves
Manchester City v Fulham
Sunderland v Birmingham
Peterborough v Newcastle
Carlisle United v Portsmouth
Nottingham Forest v Blackburn
Stoke v Blackpool
Scunthorpe United v Port Vale
Preston v Tottenham Hotspurs
Aston Villa v Cardiff City
MECHI YA LEO: Ferguson v Wenger, Wanasemaje?
Leo ni Bigi Mechi kati ya Manchester United na Arsenal Timu zinazotambulika huko England kuwa ni miongoni mwa Timu Vigogo Wanne wa Ligi Kuu wengine wakiwa ni Liverpool na Chelsea.
Ni kawaida kabla ya mechi zinazowakutanisha Vigogo hao, Waandishi kuwabana Mameneja wa Timu hizo na kutaka maoni na mitazamo yao.
Mechi kati ya Manchester United na Arsenal inawakutanisha Mameneja Sir Alex Ferguson wa Manchester United na Arsene Wenger wa Arsenal ambao ndio Mameneja waliodumu muda mrefu wakiwa uongozini kwenye Ligi Kuu England kupita wengine wote.
Mbali ya hilo, ushindani wa Klabu hizi, siku za nyuma, ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kujenga uhasama ndani na nje ya Uwanja.
Lakini, Sir Alex Ferguson, licha ya kukiri kuwa msimu huu Arsenal watakuwa moja ya Timu zinazostahili kutwaa Ubingwa, amesema haamini ushindani huo utaibua tena uhasama uliokuwepo siku za nyuma.
Wengi wanaamini kushindwa kwa Arsenal kwa misimu kadhaa ya hivi karibuni kutwaa Ubingwa, kitu ambacho Wenger anakiunga mkono, ndiko kumesababisha uhasama upungue lakini Ferguson anapinga hilo. Ferguson anasema: “Sikubaliani na hilo! Nadhani kitu kikubwa ni kwamba Wachezaji wamebadilika! Sasa hatuna Roy Keane na wao hawana Patrick Viera! Hao wawili walikuwa ni cheche na Manahodha waliotawala Timu zao! Uhasama kati yao ulisukumwa hadi kwa Mameneja!”
“Vilevile……” Ferguson anaongeza. “……mimi na Wenger tuko hapa muda mrefu na ni kitu cha kawaida watu kutofautiana. Kwa sasa Mameneja wanakuja, siku mbili baadae hawapo! Nadhani sisi wawili tutaondoka pamoja jua likichuwama!”
Kuhusu Arsenal ya msimu huu, Ferguson anasema ni Timu nzuri na itakuwemo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa.
Nae Wenger amekiri kuwa Ulimwengu wote wa soka unaichukulia mechi ya leo kama kipimo kwa Arsenal hasa baada ya kuanza msimu kwa kishindo kwa kushinda mechi zao zote mbili za Ligi Kuu walipoiua Everton 6-1 nyumbani kwa Everton Goodison Park na kuifumua Portsmouth 4-1 Emirates Stadium na pia kuitoa Timu ngumu Celtic kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa kuifunga mechi zote mbili kwa mabao 2-0 na 3-1.
Lakini katika mechi ya leo Arsenal itaukosa mhimili wao Nahodha Cesc Fabregas ambae ni majeruhi na Wenger ameelezea hilo.
Anasema: “Cesc anatupa utulivu. Yeye ni bingwa wa kuusoma mchezo na pia Mfungaji. Lakini nguvu za pamoja za Diaby, Denilson na Song itafidia pengo lake.”
Wenger ameongeza kwa kuisifia ngome yake ambayo kwa sasa inaongozwa na Masentahafu Gallas na Vermaelen.
Vilevile Wenger alisema kwa sasa Manchester United iko kipindi cha mpito baada ya Ronaldo kuondoka na kufananisha na kuondoka Arsenal kwa Thierry Henry kwenda Barcelona mwaka 2007.
Wenger anasema: “Mchezaji akiwa na nguvu kwenye Timu, mara nyingi mchezo huchezwa kupitia kwake. Kwetu, hakuna mtu aliebisha au kusita kumpasia Henry. Mchezaji wa aina hiyo akiondoka, wengine wanaibuka lakini inachukua muda. Kwetu walitokea Adebayor na Hleb. Naamini Man U wana dosari kumkosa Ronaldo lakini wataibuka wengine. Na wapo Rooney na Berbatov wenye uwezo kufunga goli 20 kila mmoja.”
Wenger pia akamsifia Michael Owen na kumwelezea kuwa ni mjanja, Mfungaji mzuri sana na mwenye akili kwenye boksi.
Barcelona wanyakua Super Cup!!
Barca 1 Shakhtar 0
Barcelona wameanza msimu mpya wa UEFA kwa kunyakua UEFA Super Cup hapo jana huko Monaco Uwanja wa Louis II baada ya kupata bao dakika ya 115 mfungaji akiwa Mchezaji Pedro alietokea benchi na hivyo kuwabwaga Mabingwa wa UEFA CUP Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Mechi ilikuwa 0-0 hadi dakika 90 za kawaida kumalizika na ndipo dakika 30 za nyongeza zikaingia.

Shakhtar Donetsk ya Ukraine ilikosa bao la wazi pale Mnigeria Julius Aghahowa alipopiga shuti lakini Kipa wa Barca Victor Valdes aliokoa.
Barca, wakimchezesha Mchezaji mpya kutoka Inter Milan Zlatan Ibrahimovic, walishindwa kung’ara pengine kwa kumkosa mpishi Andres Iniesta kwenye Kiungo ambae hakucheza kwani ni majeruhi.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Puyol, Pique, Abidal, Xavi, Toure Yaya (Busquets 100), Keita, Messi, Ibrahimovic (Pedro 81), Henry (Bojan 96).
Akiba hawakucheza: Pinto, Gudjohnsen, Maxwell, Muniesa.
Kadi: Messi, Pedro.
Goli: Pedro 115.
Shakhtar Donetsk: Pyatov, Srna, Kucher, Chigrinsky, Rat, Ilsinho, Gai (Kobin 78), Hubschman, Willian (Aghahowa 91), Fernandinho (Jadson 78), Luiz Adriano.
Akiba hawakucheza: Khudzamov, Gladkyy, Polyanskyi, Chyzhov.
Kadi: Ilsinho, Srna, Kucher, Kobin.
Watazamaji: 17,000.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium).
Benitez atoa visingizio, asema Gerrard yuko chini ya kiwango, alaumu Wachezaji!!
Bosi wa Liverpool Rafael Benitez, baada ya Timu yake kupigwa mechi 2 kati ya 3 za Ligi Kuu walizocheza, ameanza kutoa visingizio kibao pamoja na kudai Nahodha wake ambae ndie mhimili mkubwa, Steven Gerrard, yuko chini ya kiwango.
Msimu huu, ndani ya wiki mbili tu, Liverpool tayari wamepoteza jumla ya mechi sawa na zile walizopoteza msimu mzima uliopita.
Benitez amesema: “Gerrard anajua amecheza mechi chini ya kiwango. Ni rahisi kujua hilo kwani kiwango chake ni juu sana. Tuna Wachezaji watatu wataanza kucheza hivi karibuni baada ya kupona nao ni Fabio Aurelio, Danny Agger na Alberto Aquilan. Wao wataleta tofauti!”
Liverpool siku ya ufunguzi wa Ligi Kuu walifungwa 2-1 na Tottenham wakiwa ugenini na Jumatatu iliyopita nyumbani kwao Anfield walipigwa na Aston Villa 3-1.
Mbali ya Gerrard, Benitez pia alilaumu Timu yake: “Tuna tatizo, tunafungwa mechi! Tatizo si mfumo, tatizo ni Wachezaji!”
UHAMISO LIGI KUU……..kwa ufupi tu:
-Sunderland wamekamilisha taratibu za kumsajili Beki kutoka Ghana John Mensah kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu kutoka Klabu ya Lyon ya Ufaransa.
Mensah, miaka 26, atajumuika na Wachezaji wengine wapya wa Sunderland kina Paulo da Silva, Lee Cattermole, Lorik Cana, Fraizer Campbell na Darren Bent.
-Meneja wa Chelsea Carlo Anxelotti ametangaza kuwa Andriy Shevchenko ataondoka Klabuni hapo kwa makubaliano ya hiari baada ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kukosa namba.
Shevchenko, Raia wa Ukraine, alijiunga na Chelsea mwaka 2006 kwa ada ya Pauni Milioni 30 na msimu uliokwisha alipelekwa Klabu yake ya zamani AC Milan kwa mkopo.
Haijajulikana Shevchenko ataenda timu ipi.

Friday 28 August 2009

Vigogo Ligi Kuu kupambana: Ni Man U v Arsenal,Old Trafford kesho!!!!!
Kesho saa moja na robo usiku, saa za bongo, Uwanja wa Old Trafford unategemewa kufurika kwa Watazamaji kushuhudia pambano la kwanza la msimu huu la Vigogo wa Ligi Kuu England wakati Mabingwa Watetezi Manchester United watakapo wakaribisha Arsenal.
Tangu msimu uanze, Manchester United wamecheza mechi 3, kushinda mbili na kufungwa moja wakati Arsenal wamecheza mechi 2 na kushinda zote.
Msimu uliopita, kwenye Ligi, Arsenal alishinda mechi ya kwanza kwake Emirates na mechi ya marudiano Old Trafford ilikuwa suluhu 0-0 lakini ndio iliyowapa Ubingwa Manchester United.
Timu hizi pia zilikutana kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Manchester United walishinda mechi zote mbili.
Katika mechi 8 za mwisho kwa Arsenal kucheza Old Trafford, Arsenal wamefungwa mechi 6, suluhu moja[ile droo ya 0-0 msimu uliopita] na mara ya mwisho kushinda ilikuwa mwaka 2006 Emmanuel Adebayor alipofunga bao moja la ushindi.
Hii itakuwa mechi ya 41 kwa Timu zinazoongozwa na Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger kukutana uso kwa uso na Ferguson ameshinda mara 15 Wenger mara 14 na suluhu ni mara 11.
Manchester United
Majeruhi: Ferdinand, Hargreaves, Obertan, Rafael, Van der Sar.
Arsenal
Majeruhi: Djourou, Fabianski, Fabregas, Nasri, Walcott.
Refa: Mike Dean
Wasaidizi: Simon Beck, Richard West
Refa wa Akiba: Lee Probert
RATIBA KAMILI LIGI KUU ENGLAND
JUMAMOSI AGOSTI 29
[saa 8 dak 45 mchana]
Chelsea v Burnley
[saa 11 jioni]
Blackburn v West Ham
Bolton v Liverpool
Stoke v Sunderland
Tottenham v Birmingham
Wolves v Hull City
[saa 1 na robo usiku]
Manchester United v arsenal
JUMAPILI, AGOSTI 30
[saa 9 na nusu mchana]
Portsmouth v Man City
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Fulham
Klabu za Uingereza zapangwa Makundi ngangari!!!
Klabu za Uingereza Fulham, Everton na Celtic zimepangwa Kwenye Makundi magumu katika EUROPA LIGI kufuatia Dro iliyofanyika mchana huu huko Monaco.
Fulham iko Kundi moja na Vigogo wa Italia Roma, Basle na CSKA Sofia KUNDI E wakati Everton wako KUNDI I pamoja na timu ya Ureno Benfica, AEK Athens na BATE Borislov.
Celtic, ambao waling’olewa na Arsenal kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE, wametupwa KUNDI C pamoja na Hamburg, Hapoel Tel Aviv na Rapid Vienna.
Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Alhamisi, Septemba 17 na Timu mbili za juu toka kila Kundi zitajumuika pamoja na Timu 8 zitakazomaliza nafasi ya 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kufanya jumla ya Timu 32 zitakazocheza hatua ya mtoano.
Mgawo wa Makundi ni:
KUNDI A
Ajax
Anderlecht
Dinamo Zagreb
Politehnica Timisoara
KUNDI B
Valencia
Lille
Slavia Prague
Genoa
KUNDI C
Hamburg
Celtic
Hapoel Tel-Aviv
Rapid Vienna
KUNDI D
Sporting
Heerenveen
Hertha Berlin
FK Ventspils
KUNDI E
Roma
Basle
Fulham
CSKA Sofia
KUNDI F
Panathinaikos
Galatasaray
Dinamo Bucuresti
SK Sturm Graz
KUNDI G
Villarreal
Lazio
Levski Sofia
SV Red Bull Salzbug
KUNDI H
Steaua Bucuresti
Fenerbahce
FC Twente
FC Sheriff
KUNDI I
Benfica
Everton
AEK Athens
BATE
KUNDI J
Shakhtar Donetsk
Club Brugge
Partizan Belgrade
Toulouse
KUNDI K
PSV
FC Copenhagen
Sparta Prague
CFR Cluj-Napoca
KUNDI L
Werder Bremen
FK Austria Vienna
Athletic Bilbao
Nacional
UEFA yamshitaki Eduardo kwa udanganyifu!!!
UEFA imemfungulia mashtaka Mchezaji wa Arsenal Eduardo kwa “kumdanganya” Refa wakati alipojidondosha ndani ya boksi na kupata penalti aliyoifunga yeye mwenyewe katika mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na kuipatia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Celtic.
Ikiwa Eduardo atapatikana na hatia UEFA inaweza kumfungia kucheza mechi mbili. Kesi yake itasikilizwa na Bodi ya Nidhamu Septemba 1 na akifungiwa atazikosa mechi za Arsenal za UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya ugenini dhidi ya Standard de Liege ya Ubelgiji tarehe 16 Septemba na ya pili ni ile ya tarehe 29 Septemba na Olympiacos itakayochezwa Emirates Stadium.
Hatua hiyo ya UEFA imemkera Bosi wa Arsenal Arsene Wenger ambayo ameiita ni ya “aibu kubwa”.
Wenger amelalamika: “Hatua hii inamwonyesha Mchezaji ni laghai na hilo halikubaliki. Hatukubali UEFA wanavyolichukulia hili suala. Unaweza ukalumbana ni penalti au lakini huwezi ukasema Mchezaji alikuwa na nia ya kumdanganya Refa!”
Hata hivyo video zimedhihirisha Eduardo hakuguswa na Kipa wa Celtic Artur Boruc lakini Refa kutoka Spain Manuel Gonzalez alitoa penalti katikati ya kipindi cha kwanza huku timu zikiwa 0-0.
RATIBA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
JUMANNE SEPTEMBA 15
[saa 3 dak 45 usiku bongo]
KUNDI A
Juventus v FC Girondins Bordeaux
Maccabi Haifa FC v FC Bayern Munchen
KUNDI B
VfL Wolfsburg v PFC CSKA Moskva
Besiktas JK v Manchester United FC
KUNDI C
FC Zurich v Real Madrid CF
Olympique Marseille v AC Milan
KUNDI D
Chelsea FC v FC Porto
Club Atletico de Madrid v APOEL FC
JUMATANO Septemba 16

[saa 3 dak 45 usiku bongo]
KUNDI E
Liverpool FC v Debreceni VSC
Olympique Lyonnais v ACF Fiorentina
KUNDI F
FC Internazionale Milano v FC Barcelona
FC Dynamo Kyiv v FC Rubin Kazan
KUNDI G
VfB Stuttgart v Rangers FC
Sevilla FC v AFC Unirea Urziceri
KUNDI H
Olympiacos FC v AZ Alkmaar
R Standard de Liege v Arsenal FC


Villa nje, Fulham, Everton wapeta EUROPA LIGI!!!
Licha ya kufungwa ugenini bao 1-0 na Amkar Perm ya Urusi, Fulham imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI kwa jumla ya mabao 3-2 huku wenzao Everton wakijumuika nao baada ya pia kuwa ugenini na kutoka suluhu ya 1-1 na Sigma Olomouc ya Czech Republic na kutinga kwenye Makundi kwa jumla ya mabao 5-1.
Kwa Aston Villa, licha ya kushinda uwanjani kwao 2-1 dhidi ya Rapid Vienna ya Austria, Villa imebwagwa nje ya EUROPA LIGI kwa bao la ugenini kwani ilifungwa mechi ya kwanza bao 1-0 na hivyo jumla ya mabao kuwa 2-2 katika mechi mbili.
Droo ya kuamua Timu zipi zitakuwa Kundi lipi itafanywa leo huko Monaco kabla ya mechi ya leo kugombea SUPER CUP kati ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE, Barcelona, na Bingwa wa UEFA CUP, Shakhtar Donetsk.
Klabu za Uingereza zakwepa Vigogo Ulaya UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Klabu 5 za Uingereza zimewekwa kwenye Makundi ambayo Wadau wengi wamedai ni “laini kidogo” baada ya kuepuka kupangwa na Timu Vigogo wa Ulaya. Manchester United ambao walifika Fainali msimu uliopita wapo pamoja na CSKA Moscow, Besiktas na Wolfsburg KUNDI B.
Liverpool watamenyana na Lyon, Fiorentina na Debrecen wakati Chelsea wapo na Porto, Atletico Madrid na APOEL Nicosia.
Arsenal wamepangiwa na AZ Alkmaar, Olympiakos na Standard Liege wakati Rangers ya Scotland itacheza na Stuttgart, Sevilla na Unirea Urziceni.
Klabu za England zimekwepa kuwekwa na Real Madrid na Inter Milan huku Real akiwa Kundi moja na AC Milan, Marseille na FC Zurich.
Inter Milan yuko pamoja na Barcelona, Dynamo Kiev na Rubin Kazan.
Msimu uliokwisha Chelsea walitolewa nje na Brcelona kwenye Nusu Fainali kwa bao la Andres Iniesta la dakika za majeruhi na Mkurugenzi Mtendaji wao Peter Kenyon alizungumza baada ya upangaji Makundi na kusema: “Tunaanza upya na siku zote tunataka twende mbele zaidi. Hamna mechi rahisi au Kundi laini lakini tumewakwepa Vigogo!!”
Manchester United, kwa kuwa Kundi moja na CSKA Moscow, watarudi tena Uwanja wa Luzhniki walipowatoa Chelsea Fainali ya 2008 na kuwa Bingwa wa Ulaya na Mkuurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo David Gill ametamka: “Kwa ujumla, tunafurahia Kundi letu. Tuna shauku kubwa kurudi tena Moscow baada ya furaha ya 2008!”
Lakini, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Man U, alisema: “CSKA sasa wamejijenga sana na mechi za kuchezea Uturuki ni ngumu siku zote. Pia tunajua ubora wa Wolfsburg na mafanikio yao Bundesliga msimu uliopita.”
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Liverpool, Christian Purslow, amesema: “Tumefurahia!”
Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alionyesha tahadhari kuhusu KUNDI H ambalo wao wapo na kutamka: “Wengine wataangalia na kusema Arsenal atapita lakini tupo makini. Itakuwa ngumu ila tutatimiza kazi yetu.”
Yapo Makundi Manane yenye Timu 4 kila moja na mechi zitachezwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini huku mechi za kwanza zikichezwa Septemba 15 na 16.
Washindi wanane wa kila Kundi pamoja na Washindi wa pili wataingia hatua ya mtoano huku washindi wa tatu wakiingizwa EUROPA LIGI.
Fainali itachezwa Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium tarehe 22 May 2010 ambayo ni Jumamosi tofauti na hapo nyuma Fainali kuchezwa Jumatano.
UHAMISHO LIGI KUU ENGLAND!!!!!
Zikiwa zimebaki siku chache kabla dirisha la uhamisho halijafungwa hapo Agosti 31, spidi ya uhamisho imepamba moto huku Klabu nyingi bado zikichacharika kusaka Wachezaji.
Baadhi ya biashara zilizokamilika hivi karibuni ni pamoja na uhamisho wa Mlinzi na Nahodha wa Manchester City Richard Dunne, miaka 29, kuhamia Aston Villa.
Aston Villa pia imemchukua Stephen Warnock, miaka 27,kutoka Blackburn Rovers kwa mkataba wa miaka minne.
Warnock, anaeweza kucheza kama Kiungo au Beki wa kushoto, alijiunga na Blackburn mwaka 2007 akitokea Liverpool.
Mlinzi wa Portsmouth Sylvain Distin, miaka 31, amejiunga na Everton kwa mkataba wa miaka mitatu na ada ambayo haikutajwa.
Nao Wachezaji wa Middlesbrough iliyoshushwa Daraja msimu uliokwisha, Robert Huth, mlinzi kutoka Ujerumani na Tuncay Sanli wa Uturuki, wamejiunga na Stoke City.
Blackburn Rovers wamemsaini Pascal Chimbonda kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Tottenham Hotspur.
Bayern Munich wamchota Robben!
Real Madrid wamekubali kumuuza Winga wa zamani wa Chelsea, Mdachi Arjen Robben, kwa Bayern Munich kwa ada ya Pauni Milioni 22.
Robben, miaka 25, alitegemewa kuhama Real tangu Klabu hiyo iwanunue Cristiano Ronaldo na Kaka.
Nae Bosi mkubwa wa Bayern Munich, Hoeness, ametamka: “Robben ataimarisha Timu. Yeye akicheza Winga kulia na Ribery kushoto Timu itakuwa bomba!”

Thursday 27 August 2009

WACHEZAJI BORA ULAYA MSIMU WA 2008/9 WATAJWA!!!
MESSI NI MCHEZAJI BORA ULAYA!!!!!
Lionel Messi wa FC Barcelona amenyakua Tuzo ya Mshambuliaji Bora na Mchezaji Bora wa Ulaya kwa msimu wa 2008/9.
Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Dro maalum ya kupanga Timu kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Tuzo ya Kipa Bora imechukuliwa na Edwin van der Sar wa Manchester United.
John Terry wa Chelsea ametwaa Tuzo ya Beki Bora.
Tuzo ya Kiungo Bora imekwenda kwa Xavi wa Barcelona.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE: MAKUNDI YAJULIKANA!!!
Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa msimu wa 2009/10 yamejulikana baada ya kufanyika Dro maalum iliyoisha hivi punde huko Monaco.
Timu kwenye kila Kundi zitacheza mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini.
Mechi za kwanza za Makundi zitachezwa Septemba 15 na 16.
KUNDI A
-BAYERN MUNICH
-JUVENTUS
-BORDEAUX
-MACCABI HAIFA
KUNDI B
-MANCHESTER UNITED
-CSKA MOSCOW
-BESIKTAS
-VFL WOLFSBURG
KUNDI C
-AC MILAN
--REAL MADRID
-MARSEILLE
-FC ZURICH
KUNDI D
-CHELSEA
-PORTO
-ATLETICO MADRID
-APOEL
KUNDI E
-LIVERPOOL
-LYON
-FIORENTINA
-DEBRECENI
KUNDI F
-BARCELONA
-INTER MILAN
-DYNAMO KIEV
-FC RUBIN KAZAN
KUNDI G
-SEVILLA
-RANGERS
-STUTTGAT
-UNIREA URZICENI
KUNDI H
ARSENAL
-AZ ALKMAAR
-OLYMPIAKOS
-STANDARD DE LIEGE
Klabu leo kujua Wapinzani wao Makundi ya UEFA Champions League
Dro ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kuamua Timu zipi zinakuwa Kundi lipi itafanyika leo huko Monaco saa 1 usiku saa za Kibongo.
Zipo jumla ya Timu 32 zitakazogawanywa Makundi manane ya Timu 4 kila moja zitakazocheza mtindo wa ligi wa nyumbani na ugenini.
Timu za Uingereza ambazo ziko kwenye hizo 32 ni Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal za England na Rangers ya Scotland.
Mechi za kwanza za Makundi hayo zitachezwa Septemba 15 na 16.
Timu hizo 4 za England zote zipo kwenye Kapu la Kwanza hivyo haziwezi kuwa Kundi moja ila Rangers wa Scotland wapo Kapu la Pili hivyo wanaweza kuwa Kundi moja na yeyote kati ya hizo Timu 4 za England.
Vile vile, kwa vile Real Madrid wako Kapu la Pili upo uwezekano wa Ronaldo kuwa Kundi moja na Timu yake ya zamani Manchester United.
Timu za Manchester United, Chelsea, Liverpool na Rangers zimeingizwa moja kwa moja hatua ya Makundi ila Arsenal ndio ilibidi waanze hatua ya mtoano kwa vile walimaliza Ligi nafasi ya 4.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu huu itafanyika Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium hapo tarehe 22 Mei 2010.
Kapu la Kwanza
Barcelona
CHELSEA
LIVERPOOL
MANCHESTER UNITED
AC Milan
ARSENAL
Sevilla
Bayern Munich
Kapu la Pili
Lyon,
Inter Milan
Real Madrid
CSKA Moscow
Porto
AZ Alkmaar
Juventus
RANGERS
Kapu la Tatu
Olympiakos
Marseille
Dinamo Kiev
Stuttgart
Fiorentina
Atletico Madrid
Bordeaux
Besiktas
Kapu la Nne
Wolfsburg
Standard Liege
Maccabi Haifa
FC Zurich
Rubin Kazan
Unirea Urziceni
APOEL Nicosia
Debrecen
Chama cha Soka Scotland na Celtic walilia Eduardo afungiwe!!
UEFA yasema itachunguza!!!
Baada ya kujidondosha na kusababisha Arsenal wapewe penalti na kisha kuifunga yeye mwenyewe, Eduardo wa Arsenal, ameshikiwa bango na SFA, Chama cha Soka cha Scotland na Wachezaji wa Celtic kwamba anastahili kufungiwa na UEFA.
Penalti hiyo ya utata ilisababisha Arsenal kupata bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 walioupata jana dhidi ya Celtic kwenye mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Kiungo wa Celtic Massimo Donati ambae aliipatia Celtic bao lao moja amesema ni wajibu wa UEFA kumfungia Eduardo kwa udanganyifu huku Bosi wa SFA, Gordon Smith, akiunga mkono hatua za kumfungia Eduardo.
Ingawa Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger, hapo nyuma amekuwa akiwalaumu sana Wachezaji wanaojidondosha na kutaka wachukuliwe hatua kali, safari hii, ingawa alikiri Kipa wa Celtic Artur Boruc hakumgusa Eduardo na hivyo haikustahili kuwa penalti, hakuunga mkono msimamo wake wa nyuma na badala yake akatoa utetezi wa ajabu kuwa Eduardo alikuwa akimkwepa Kipa na ndio maana akaanguka.
Wakati huo huo, UEFA imesema itachunguza kitendo cha Eduardo na akipatikana na hatia atafungiwa mechi mbili.
Arsenal 3 Celtic 1
Arsenal wakiwa kwao Uwanjani Emirates jana waliifunga Celtic mabao 3-1 na hivyo kusonga mbele kwenye hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kushinda mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0.
Ushindi wa jana wa Arsenal ulisaidiwa sana na kupata bao la kwanza dakika ya 28 kwa penalti baada ya Eduardo kujiangusha kwa makusudi ndani ya boksi na kupata penalti hiyo aliyoifunga mwenyewe.
Bao la pili la Arsenal lilifungwa na Emmanuel Eboue dakika ya 53 kufuatia gonga murua na Arshavin akapachika la 3 dakika ya 74.
Celtic walipata bao lao dakika ya 90.
Wakati Arsenal wanaingia Dro ya Timu 32 leo jioni ya kuamua Makundi Manane ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE yatakayocheza kwa Ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini Celtic wataingizwa kwenye EUROPA LEAGUEyenye Timu 48 zitakazokuwa na Dro yao kuamua Makundi hapo kesho.
Vikosi vilikuwa:
Arsenal (4-3-3) Almunia; Sagna, Vermaelen, Gallas, Clichy; Eboue, Song, Denilson; Bendtner, Eduardo, Diaby.
Akiba: Mannone, van Persie, Ramsey, Silvestre, Wilshere, Arshavin, Traore.
Celtic (4-4-2) Boruc; Hinkel, Caldwell, Loovens, Fox; McGeady, Brown, Donati, Maloney; McDonald, Fortune.
Akiba: Zaluska, Naylor, Samaras, Flood, McCourt, Killen, O'Dea.
Refa: Manuel Enrique Mejuto Gonzalez (Spain)

MATOKEO MECHI ZA JANA JUMATANO AGOSTI 26
[Timu iliyosonga mbele na jumla ya magoli kwenye mabano]
Apoel Nicosia 3 v FC Copenhagen 1 [Apoel 3-2]
Arsenal 3 v Celtic 1 [Arsenal 5-1]
Fiorentina 1 v Sporting 1[Fiorentina 3-3 kwa magoli ya ugenini]
Olympiacos 1 v FC Sheriff Tiraspol 0 [Olympiacos 3-0]
VfB Stuttgart 0 v Politehnica Timisoara 0 [Stuttgart 2-0]

Wednesday 26 August 2009

UEFA SUPER CUP IJUMAA!!!!
NI FC BARCELONA v FC SHAKHTAR DONETSK huko Monaco!!!

Dro ya Makundi UEFA CHAMPIONS LEAGUE kesho!!!
Vizito wa UEFA na Klabu kubwa za Ulaya kuanzia siku ya Alhamisi watamiminika katika “Ka-nchi” cha Monaco ili kushuhudia Dro ya Timu 32 zinazowania UEFA CHAMPIONS LEAGUE zitakapogawanywa katika Makundi manne ya Timu 4 kila moja na kucheza kwa mtindo wa Ligi wa nyumbani na ugenini.
Mara baada ya Dro hiyo, siku hiyo hiyo Alhamisi, kutafanyika tamasha maalum la kutoa Tuzo za Wachezaji Bora wa Ulaya kwa msimu wa 2008/9 Tuzo zikipewa kwa Mchezaji Bora wa Ulaya pamoja na Kipa Bora, Mlinzi Bora, Kiungo Bora na Mshambuliaji Bora.
Siku ya Ijumaa kutakuwa na Dro ya Timu 48 zinazoshindania EUROPA LEAGUE kugawanywa kwenye Makundi ili wacheze mtindo wa Ligi.
Kisha jioni siki hiyo hiyo, katika Uwanja uitwao Stade Loius II kutafanyika pambano la kuwania UEFA Super Cup katika ya Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE Barcelona ya Spain na Bingwa wa UEFA CUP Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Wenger: “Leo na Celtic ni Mechi Kubwa kupita Jumamosi na Man U!!!”
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametamka mechi ya leo ya marudiano ya mtoano wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Timu yake Arsenal na Celtic itakayochezwa nyumbani kwa Arsenal Emirates Stadium ni mechi kubwa kupita mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England watakayocheza Old Trafford na Mabingwa Manchester United.
Arsenal waliishinda Celtic mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0 na suluhu ya aina yeyote ile au hata wakifungwa 1-0 itawafanya watinge hatua ya Makundi ya michuano hiyo.
Wenger alisema: “Hii ni mechi muhimu kupita Jumamosi na Man U!! Ukifungwa leo hamna marudiano!! Tukifungwa Jumamosi na Man U bado tuna nafasi kwani tutabakiwa na mechi 35 za Ligi!!”
Mbali ya ushindi wa uwanjani katika mechi ya leo, Timu ambazo zitacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE huwa na uhakika wa kupata donge lisilopungua Pauni Milioni 25.
Mechi ya leo itaanza saa 3 dakika 45 saa za bongo.
Vurugu Carling Cup Uwanjani Upton Park: West Ham 3 Millwall 1
Mashabiki wavamia Uwanja!!!!

FA kuchunguza!!!
FA, Chama cha Soka cha England, kimesema kitafanya uchunguzi juu ya vurugu zilizotokea ndani na nje ya Uwanja wa Uptown Park jana usiku ambako mtu mmoja alichomwa kisu katika mechi ya Timu mbili zote za mjini London zenye upinzani wa jadi West Ham na Millwall zilipokuwa zikicheza mechi ya mtoano ya Kombe la Carling.
Timu hizi hazijawahi kukutana tangu Aprili 2005 kwa vile West Ham iko Ligi Kuu na Millwall inacheza Madaraja mawili chini yake yaani Ligi 2.
Vurugu hizo zilianza nje ya uwanja kabla ya mechi pale mamia ya Mashabiki wasio na Tiketi ambao Polisi imesema walipanga kuleta fujo kuanza kurusha chupa, matofali na kuchoma moto.
Ndani ya uwanja, West Ham wakiwa nyuma kwa bao 1 lililofungwa na Harris wa Millwall dakika ya 26, waliweza kusawazisha dakika ya 87 kupitia Junior Stanislas na kusababisha Mashabiki kuvamia uwanja wakishangilia.
Katika dakika 30 za muda wa nyongeza, alikuwa Junior Stanislas tena alieifungia West Ham bao la pili kwa penalti na Mashabiki kwa mara ya pili wakavamia uwanja kushangilia.
Hapo ndipo Refa akasimamisha mechi na kuwatoa nje Wachezaji huku Polisi na Wasimamizi wakijitahidi kuwaondoa Mashabiki uwanjani.
Mmoja wa watu waliojitahidi kuwatuliza Washabiki ni Mchezaji wa West Ham Jack Collison ambae Baba yake Mzazi alifariki Jumapili kwa ajali ya pikipiki na ambae alisema licha ya msiba huo yuko tayari kucheza mechi hiyo.
FA imesema Shabiki yeyote atakaegundulika kushiriki fujo hizo atafungiwa maisha kuingia kwenye Viwanja.

MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
[Kwenye mabano Timu inayosonga mbele na jumla ya magoli]
Anderlect 1 v Lyon 3 [Lyon imeshinda jumla magoli 8-2]
Atletico Madrid 2 v Panathinaikos 0 [Atletico 5-2]
Debrecin 2 v Levski Sofia o [Debrecin 4-1]
FC Zurich 2 v FK Ventspills 1 [FC Zurich 5-1]
Maccabi Haifa 3 v SV Red Bull Salzburg 0 [Haifa 5-1]
MECHI ZA LEO JUMATANO AGOSTI 26
[Matokeo mechi ya kwanza kwenye mabano]
[saa 3 dak 45 usiku]
Apoel Nicosia v FC Copenhagen [0-1]
Arsenal v Celtic [2-0]
Fiorentina v Sporting [2-2]
Olympiacos v FC Sheriff Tiraspol [2-0]
VfB Stuttgart v Politehnica Timisoara [2-0]

Tuesday 25 August 2009

Nahodha Fabregas majeruhi, kuikosa Celtic kesho!!!
Arsenal watamkosa Nahodha wao Cesc Fabregas kwa mechi ya kesho ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE watakayocheza na Celtic uwanjani kwao Emirates ambayo ni marudiano kwa kuwa Mchezaji huyo bado ana maumivu aliyoyapata kwenye mechi iliyokwisha ya Ligi Kuu dhidi ya Portsmouth na ikabidi atolewe uwanjani.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 22 pia atakuwa ni hatihati kucheza mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu uwanjani Old Trafford ambako Arsenal watakuwa wageni wa Mabingwa Manchester United.
Arsenal katika mechi ya kesho pia itawakosa kina Tomas Rosicky, Theo Walcott, Kipa Lukasz Fabianski, Samir Nasri na Johan Djourou.

Katika mechi ya kwanza Arsenal waliishinda Celtic 2-0.
Everton wamsaini Kiungo Mrusi
Everton imemsajili Kiungo wa Kirusi Diniyar Bilyaletdinov kutoka Lokomotiv Moscow kwa ada ambayo haikutajwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambae amechezea mara 28 Timu ya Taifa ya Urusi amesaini mkataba wa miaka mitano.
Veterani Campbell ajiunga Notts County.
Notts County, muda wowote kuanzia sasa, watatangaza kumsaini Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya England, Sol Campbell, ambae pia alichezea Klabu za Tottenham na Arsenal hapo zamani.
Campbell, miaka 34, amekubali kuichezea Notts County Timu iliyo Ligi 2 [yaani baada ya Ligi Kuu kuna Daraja liitwalo Coca Cola Championship kisha Ligi 1].
Campbell, aliechezea England mara 73, kwa sasa ni Mchezaji huru baada ya mkataba wake na Portsmouth kumalizika bila kupata nyongeza.
Vidic aziponda tetesi za kuhama Man U!!!
Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic, ameziponda vikali sana tetesi kuwa yuko mbioni kuihama Man U.
Mchezaji huyo kutoka Serbia amezipinga habari hizo na kutamka: “Sijawahi kusema chochote kuhusu Barcelona au Real Madrid au AC Milan au klabu nyingine! Huwa sizungumzii mambo yangu ya baadae sasa sijui kwa nini mtu mwingine azungumze! Niliwaonyesha kwenye mechi na Wigan furaha niliyonayo kuichezea Man U!”
Kumbe Mchezaji wa West Ham “kachomwa kisu na shemejie!!!!”
Mtu mmoja, Worrell Whitehurst, miaka 25, ameburuzwa mahakamani akituhumiwa kuwachoma visu Mchezaji wa West Ham Calum Davenport na Mama yake Mzazi Ijumaa usiku na inasemekana mtu huyo ni bwana wa Dada yake Mchezaji huyo aitwae Cara ambae inadaiwa ana mimba ya mtuhumiwa huyo.
Hali ya Calum Davenport bado ni tete baada ya kuumizwa vibaya mguu wa kushoto na hasa kukatwa kwa mshipa mkuu wa damu
mguuni hapo.
Liverpool yakung’utwa 3-1 nyumbani!!!
Wakiwa ndani ya Anfield, Liverpool jana usiku walionja kipigo kikali cha pili katika mechi zao tatu za Ligi Kuu baada ya kufungwa na Timu ambayo haijawahi kushinda katika mechi zao 16 zilizopita kati yao na mara ya mwisho ilipigwa 5-0 lakini safari hii Aston Villa walisimama kidete na kuisambaratisha 3-1 Liverpool ndani ya ngome yao.
Msimu wote mzima uliopita Liverpool ilipoteza mechi 2 tu lakini msimu huu katika mechi 3 tu za kwanza Liverpool washafungwa mechi 2 na ni dhahiri Meneja Rafa Benitez ameanza kuona machungu.
Balaa kwa Liverpool lilianza pale Lucas alipojifunga mwenyewe dakika ya 34 na Davies wa Aston Villa akaongeza la pili dakika ya 45.
Lakini Mshambuliaji Fernando Torres akaipatia Liverpool bao lao moja dakika ya 72 na kidogo kufufua matumaini na lakini dakika 3 tu baadae ndipo Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alipomwangusha Nigel Reo-Cocker kwenye boksi na Ashley Young akampeleka Kipa Reina potea katika penalti na kupachika bao la tatu na kuwaua kabisa Liverpool.
Vikosi vilikuwa:
Liverpool: Reina, Johnson, Insua, Carragher, Skrtel, Gerrard, Benayoun [Babel 75], Mascherano, Lucas, [Voronin 66], Torres, Kuyt.
Aston Villa: Friedel, Davies, Shorey, Beye, Cuellar, Sidwell, Young [Heskey 80], Milner, Petrov, Reo-Cocker, Agbonlahor.
Refa: Martin Atkinson
Watazamaji: 43667

Monday 24 August 2009

Liverpool v Aston Villa
Leo, wakiwa nyumbani Anfield, Liverpool wanaikaribisha Aston Villa Klabu ambayo haijawahi kuifunga Liverpool katika mechi 16 za mwisho walizocheza kati yao.

Mechi ya mwisho kati ya Timu hizi ilikuwa ile ya Machi 22, 2009 wakati Liverpool ilipoilipua Villa mabao 5-0.
Msimu huu Aston Villa wamecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu na kubugizwa bao 2-0 nyumbani kwao na Timu ya Wigan. Mechi iliyofuata kwa Aston Villa ilikuwa ni ile ya mtoano wa EUROPA LEAGUE ambayo nayo walifungwa 1-0 na Rapid Vienna.
Liverpool wameshacheza mechi mbili za Ligi Kuu na ya kwanza walifungwa na Tottenham 2-1 huko London na ya pili wakicheza kwao Anfield walishinda 4-0 dhidi ya Stoke City.
Refa katika mechi ya leo itakayoanza saa 4 usiku saa za bongo ni Martin Atkinson.

Everton wakubali ada ya Lescott toka Man City
Manchester City na Everton hatimaye zimefikia makubaliano juu ya kuuzwa kwa Beki wa Everton Joleon Lescott, umri miaka 26, baada ya vuta ni kuvute.
Ada ya uhamisho haikutajwa ila inaaminika ni Pauni Milioni 24 na Lescott atathibitishwa kuwa Mchezaji wa Man City baada ya kufaulu upimaji wa afya yake na kufikia makubaliano na Klabu yake hiyo mpya juu ya marupurupu yake.
Tovuti ya Everton ilitoa tamko: “Uamuzi huu ni bora kwa Everton. Baada ya Manchester City kuonyesha nia ya kumnunua Joleon Lescott tabia, mwenendo na ari yake vilibadilika mno.”
Man City awali ilitaka kumchukua Nahodha wa Chelsea John Terry lakini iliposhindikana wakatoa ofa ya Pauni Milioni 15 kumnunua Lescott ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya England.
Ofa hiyo ikaongezwa hadi Pauni Milioni 18 lakini Meneja wa Everton David Moyes akang’ang’ania Lescott hauzwi.
Wiki mbili zilizopita Lescott akawasilisha ombi lake rasmi la kutaka kuhama.
Baada ya kuichezea Everton katika kipigo cha bao 6-1 na Arsenal, Moyes akambwaga Mchezaji huyo kwenye Kikosi cha Pili akidai ari yake imepungua.
Kwa sasa, Everton ambayo imeshafungwa mechi zake zote mbili za Ligi Kuu England, inabaki na Sentahafu mmoja tu na nae ni Mnigeria Joseph Yobo kwani Sentahafu wao mwingine wa kutegemewa Phil Jagielka ni majeruhi wa muda mrefu.
Wawili mbaroni kwa kumchoma visu Mchezaji wa West Ham
Polisi jijini London inawashikilia watu wawili kwa kumchoma visu Beki wa West Ham Calum Davenport, umri miaka 26, na Mama yake mzazi wakiwa nyumbani kwao Ijumaa usiku.
Hali ya Mchezaji huyo imeelezwa kuwa ni mbaya na ilibidi afanyiwe upasuaji.
Hali ya Mama yake pia ni mbaya ingawa Madaktari wameridhi
shwa nayo.

Sunday 23 August 2009

RATIBA YA SOKA YA WIKI IJAYO: LIGI KUU ENGLAND & UEFA CHAMPIONS LEAGUE
[saa za bongo]
JUMATATU AGOSTI 24
LIGI KUU ENGLAND
[saa 4 usiku]
Liverpool v Aston Villa
JUMANNE AGOSTI 25
UEFA CHAMPIONS LEAGUE [mechi za mtoano za marudiano]
[saa 3 dak 45 usiku]
Anderlect v Lyon
Atletico Madrid v Panathinaikos
Debrecin v Levski Sofia
FC Zurich v FK Ventspills
Maccabi Haifa v SV Red Bull Salzburg
JUMATANO AGOSTI 26
UEFA CHAMPIONS LEAGUE [mechi za mtoano za marudiano]
[saa 3 dak 45 usiku]
Apoel Nicosia v FC Copenhagen
Arsenal v Celtic
Fiorentina v Sporting
Olympiacos v FC Sheriff Tiraspol
VfB Stuttgart v Politehnica Timisoara
LIGI KUU ENGLAND
JUMAMOSI AGOSTI 29
[saa 8 dak 45 mchana]
Chelsea v Burnley
[saa 11 jioni]
Blackburn v West Ham
Bolton v Liverpool
Stoke v Sunderland
Tottenham v Birmingham
Wolves v Hull City
[saa 1 na robo usiku]
Manchester United v arsenal
JUMAPILI, AGOSTI 30
[saa 9 na nusu mchana]
Portsmouth v Man City
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Fulham

Fulham 0 Chelsea 2
Chelsea wameendeleza wimbi la ushindi huu ukiwa ushindi wao wa tatu mfululizo katika mechi 3 za Ligi Kuu England walizocheza mpaka sasa kwa kuwafunga Fulham wakiwa nyumbani Uwanjani Craven Cottage.
Ni Washambuliaji wao wakuu Didier Drogba na Nicolas Anelka waliowapatia mabao yao hayo mawili.
Drogba alipachika bao dakika ya 39 kipindi cha kwanza na Anelka dakika ya 76 kipindi cha pili.
Kilichowakuta Man U chawafika Everton: Burnley 1 Everton 0!!!!
Hadithi ni ile ile kama yaliyowafika Manchester United juzi walipofungwa na Timu iliyopanda Daraja msimu huu Burnley bao 1-0 na pia kukosa penalti iliyopigwa na Michael Carrick na leo Everton wamefungwa bao 1-0 na pia kukosa penalti iliyopigwa na Mchezaji wa zamani wa Manchester United Luis Saha alieutoa nje mkwaju huo wa penalti.
Kama ilivyo kwenye mechi na Manchester United, Everton walitawala kabisa huku wakikosa nafasi nyingi tu na kuwaacha Burnley wakipachika bao lao la ushindi kupitia kwa Wade Elliott dakika ya 34.
Everton mpaka sasa wamecheza mechi 2 na kufungwa zote wakati Burnley wamecheza 3 na kufungwa 1 na kushinda 2.
Tottenham yashinda mechi ya 3 mfululizo: West Ham 1 Tottenham 2
Inasemekana ni zaidi ya miaka 50 tangu mara ya mwisho kwa Tottenham kuanza msimu wa Ligi na kushinda mechi zao zote 3 za kwanza na leo wameshinda mechi yao ya 3 wakiwa ugenini baada ya kuifunga West Ham mabao 2-1.
Walikuwa ni West Ham waliopata bao la kwanza kupitia Carlton Cole aliefumua shuti kali.
Lakini dakika 5 baadae Carlton Cole akageuka kuwa mbaya pale alipotoa pasi ya kijinga kwa 'adui' Defoe ambae hakungoja kutoa shukrani bali akaisawazishia Timu yake.
Katika dakika ya 79 Winga Aaaron Lennon akaipa Tottenham bao la pili na la ushindi.
Moyes asalimu amri kmzuia Lescott asihamie Man City!!!
Bosi wa Everton David Moyes amekubali kuwa sasa hawezi tena kumzuia Beki wake Joleon Lescott kuhamia Manchester City.
Lescott, ambae kwa sasa ameondolewa kwenye Kikosi cha Kwanza cha Everton mara baada ya mechi ya kwanza ya Ligi Kuu waliyofungwa 6-1 na Arsenal kwa kile Moyes alichokiita kukosa ari, alishaandika barua rasmi kuomba kuhamia Man City.
Moyes amekiri: "Nilitaka abaki. Ni Mchezaji mzuri anaecheza nafasi nyingi za ulinzi lakini mwenyewe hataki kubaki na kabla ya mechi na Arsenal alinambia hataki kucheza mechi hiyo lakini nililazimika kumpanga kutokana na upungufu wa Walinzi na matokeo yake mnayajua!"
Benitez akiri Ubingwa mgumu msimu huu!!!
Rafa Benitez wa Liverpool amekiri kuwa msimu huu ni mgumu sana kwa Timu yeyote kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kupita misimu mingine yote iliyopita.
Mpaka sasa Liverpool wamefungwa mechi moja ambayo ni ile ya siku ya ufunguzi walipopigwa 2-1 na Tottenham huku nao Mabingwa Watetezi Manchester United wakipoteza mechi moja katika 3 walizocheza.
Timu pekee katika Timu "Vigogo" zilizoanza vizuri ni Chelsea na Arsenal huku Tottenham wakishinda mechi zao zote mpaka sasa.
Kesho Jumatatu usiku Liverpool wanapambana na Aston Villa.
Ferguson asifia safu yake ya Ushambulizi!!!
Sir Alex Ferguson amewasifia Washambuliaji wake Wayne Rooney, Michael Owen, Dimitar Berbatov na Nani ambao wote jana walipachika mabao katika kipigo cha 5-0 Manchester United walichowashushia Wigan.
Rooney jana alifunga mabao mawili yakiwa ni bao lake la 100 na 101 tangu aanze kuvaa Jezi za Man U.
"Ni kijana mdogo na hayo ni mafanikio makubwa sana!!" Ferguson akimzungumzia Rooney. "Na Owen ni mmliaziaji hatari sana ambae amepata kutokea nchi hii!!"
Powered By Blogger