Tuesday 25 August 2009

Nahodha Fabregas majeruhi, kuikosa Celtic kesho!!!
Arsenal watamkosa Nahodha wao Cesc Fabregas kwa mechi ya kesho ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE watakayocheza na Celtic uwanjani kwao Emirates ambayo ni marudiano kwa kuwa Mchezaji huyo bado ana maumivu aliyoyapata kwenye mechi iliyokwisha ya Ligi Kuu dhidi ya Portsmouth na ikabidi atolewe uwanjani.
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 22 pia atakuwa ni hatihati kucheza mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu uwanjani Old Trafford ambako Arsenal watakuwa wageni wa Mabingwa Manchester United.
Arsenal katika mechi ya kesho pia itawakosa kina Tomas Rosicky, Theo Walcott, Kipa Lukasz Fabianski, Samir Nasri na Johan Djourou.

Katika mechi ya kwanza Arsenal waliishinda Celtic 2-0.
Everton wamsaini Kiungo Mrusi
Everton imemsajili Kiungo wa Kirusi Diniyar Bilyaletdinov kutoka Lokomotiv Moscow kwa ada ambayo haikutajwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambae amechezea mara 28 Timu ya Taifa ya Urusi amesaini mkataba wa miaka mitano.
Veterani Campbell ajiunga Notts County.
Notts County, muda wowote kuanzia sasa, watatangaza kumsaini Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya England, Sol Campbell, ambae pia alichezea Klabu za Tottenham na Arsenal hapo zamani.
Campbell, miaka 34, amekubali kuichezea Notts County Timu iliyo Ligi 2 [yaani baada ya Ligi Kuu kuna Daraja liitwalo Coca Cola Championship kisha Ligi 1].
Campbell, aliechezea England mara 73, kwa sasa ni Mchezaji huru baada ya mkataba wake na Portsmouth kumalizika bila kupata nyongeza.
Vidic aziponda tetesi za kuhama Man U!!!
Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic, ameziponda vikali sana tetesi kuwa yuko mbioni kuihama Man U.
Mchezaji huyo kutoka Serbia amezipinga habari hizo na kutamka: “Sijawahi kusema chochote kuhusu Barcelona au Real Madrid au AC Milan au klabu nyingine! Huwa sizungumzii mambo yangu ya baadae sasa sijui kwa nini mtu mwingine azungumze! Niliwaonyesha kwenye mechi na Wigan furaha niliyonayo kuichezea Man U!”
Kumbe Mchezaji wa West Ham “kachomwa kisu na shemejie!!!!”
Mtu mmoja, Worrell Whitehurst, miaka 25, ameburuzwa mahakamani akituhumiwa kuwachoma visu Mchezaji wa West Ham Calum Davenport na Mama yake Mzazi Ijumaa usiku na inasemekana mtu huyo ni bwana wa Dada yake Mchezaji huyo aitwae Cara ambae inadaiwa ana mimba ya mtuhumiwa huyo.
Hali ya Calum Davenport bado ni tete baada ya kuumizwa vibaya mguu wa kushoto na hasa kukatwa kwa mshipa mkuu wa damu
mguuni hapo.

No comments:

Powered By Blogger