Friday 28 August 2009

UEFA yamshitaki Eduardo kwa udanganyifu!!!
UEFA imemfungulia mashtaka Mchezaji wa Arsenal Eduardo kwa “kumdanganya” Refa wakati alipojidondosha ndani ya boksi na kupata penalti aliyoifunga yeye mwenyewe katika mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na kuipatia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Celtic.
Ikiwa Eduardo atapatikana na hatia UEFA inaweza kumfungia kucheza mechi mbili. Kesi yake itasikilizwa na Bodi ya Nidhamu Septemba 1 na akifungiwa atazikosa mechi za Arsenal za UEFA CHAMPIONS LEAGUE ya ugenini dhidi ya Standard de Liege ya Ubelgiji tarehe 16 Septemba na ya pili ni ile ya tarehe 29 Septemba na Olympiacos itakayochezwa Emirates Stadium.
Hatua hiyo ya UEFA imemkera Bosi wa Arsenal Arsene Wenger ambayo ameiita ni ya “aibu kubwa”.
Wenger amelalamika: “Hatua hii inamwonyesha Mchezaji ni laghai na hilo halikubaliki. Hatukubali UEFA wanavyolichukulia hili suala. Unaweza ukalumbana ni penalti au lakini huwezi ukasema Mchezaji alikuwa na nia ya kumdanganya Refa!”
Hata hivyo video zimedhihirisha Eduardo hakuguswa na Kipa wa Celtic Artur Boruc lakini Refa kutoka Spain Manuel Gonzalez alitoa penalti katikati ya kipindi cha kwanza huku timu zikiwa 0-0.

No comments:

Powered By Blogger