Saturday, 29 August 2009

Barcelona wanyakua Super Cup!!
Barca 1 Shakhtar 0
Barcelona wameanza msimu mpya wa UEFA kwa kunyakua UEFA Super Cup hapo jana huko Monaco Uwanja wa Louis II baada ya kupata bao dakika ya 115 mfungaji akiwa Mchezaji Pedro alietokea benchi na hivyo kuwabwaga Mabingwa wa UEFA CUP Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Mechi ilikuwa 0-0 hadi dakika 90 za kawaida kumalizika na ndipo dakika 30 za nyongeza zikaingia.

Shakhtar Donetsk ya Ukraine ilikosa bao la wazi pale Mnigeria Julius Aghahowa alipopiga shuti lakini Kipa wa Barca Victor Valdes aliokoa.
Barca, wakimchezesha Mchezaji mpya kutoka Inter Milan Zlatan Ibrahimovic, walishindwa kung’ara pengine kwa kumkosa mpishi Andres Iniesta kwenye Kiungo ambae hakucheza kwani ni majeruhi.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Puyol, Pique, Abidal, Xavi, Toure Yaya (Busquets 100), Keita, Messi, Ibrahimovic (Pedro 81), Henry (Bojan 96).
Akiba hawakucheza: Pinto, Gudjohnsen, Maxwell, Muniesa.
Kadi: Messi, Pedro.
Goli: Pedro 115.
Shakhtar Donetsk: Pyatov, Srna, Kucher, Chigrinsky, Rat, Ilsinho, Gai (Kobin 78), Hubschman, Willian (Aghahowa 91), Fernandinho (Jadson 78), Luiz Adriano.
Akiba hawakucheza: Khudzamov, Gladkyy, Polyanskyi, Chyzhov.
Kadi: Ilsinho, Srna, Kucher, Kobin.
Watazamaji: 17,000.
Refa: Frank De Bleeckere (Belgium).
Benitez atoa visingizio, asema Gerrard yuko chini ya kiwango, alaumu Wachezaji!!
Bosi wa Liverpool Rafael Benitez, baada ya Timu yake kupigwa mechi 2 kati ya 3 za Ligi Kuu walizocheza, ameanza kutoa visingizio kibao pamoja na kudai Nahodha wake ambae ndie mhimili mkubwa, Steven Gerrard, yuko chini ya kiwango.
Msimu huu, ndani ya wiki mbili tu, Liverpool tayari wamepoteza jumla ya mechi sawa na zile walizopoteza msimu mzima uliopita.
Benitez amesema: “Gerrard anajua amecheza mechi chini ya kiwango. Ni rahisi kujua hilo kwani kiwango chake ni juu sana. Tuna Wachezaji watatu wataanza kucheza hivi karibuni baada ya kupona nao ni Fabio Aurelio, Danny Agger na Alberto Aquilan. Wao wataleta tofauti!”
Liverpool siku ya ufunguzi wa Ligi Kuu walifungwa 2-1 na Tottenham wakiwa ugenini na Jumatatu iliyopita nyumbani kwao Anfield walipigwa na Aston Villa 3-1.
Mbali ya Gerrard, Benitez pia alilaumu Timu yake: “Tuna tatizo, tunafungwa mechi! Tatizo si mfumo, tatizo ni Wachezaji!”
UHAMISO LIGI KUU……..kwa ufupi tu:
-Sunderland wamekamilisha taratibu za kumsajili Beki kutoka Ghana John Mensah kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu kutoka Klabu ya Lyon ya Ufaransa.
Mensah, miaka 26, atajumuika na Wachezaji wengine wapya wa Sunderland kina Paulo da Silva, Lee Cattermole, Lorik Cana, Fraizer Campbell na Darren Bent.
-Meneja wa Chelsea Carlo Anxelotti ametangaza kuwa Andriy Shevchenko ataondoka Klabuni hapo kwa makubaliano ya hiari baada ya Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kukosa namba.
Shevchenko, Raia wa Ukraine, alijiunga na Chelsea mwaka 2006 kwa ada ya Pauni Milioni 30 na msimu uliokwisha alipelekwa Klabu yake ya zamani AC Milan kwa mkopo.
Haijajulikana Shevchenko ataenda timu ipi.

No comments:

Powered By Blogger