Friday, 28 August 2009

Vigogo Ligi Kuu kupambana: Ni Man U v Arsenal,Old Trafford kesho!!!!!
Kesho saa moja na robo usiku, saa za bongo, Uwanja wa Old Trafford unategemewa kufurika kwa Watazamaji kushuhudia pambano la kwanza la msimu huu la Vigogo wa Ligi Kuu England wakati Mabingwa Watetezi Manchester United watakapo wakaribisha Arsenal.
Tangu msimu uanze, Manchester United wamecheza mechi 3, kushinda mbili na kufungwa moja wakati Arsenal wamecheza mechi 2 na kushinda zote.
Msimu uliopita, kwenye Ligi, Arsenal alishinda mechi ya kwanza kwake Emirates na mechi ya marudiano Old Trafford ilikuwa suluhu 0-0 lakini ndio iliyowapa Ubingwa Manchester United.
Timu hizi pia zilikutana kwenye Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Manchester United walishinda mechi zote mbili.
Katika mechi 8 za mwisho kwa Arsenal kucheza Old Trafford, Arsenal wamefungwa mechi 6, suluhu moja[ile droo ya 0-0 msimu uliopita] na mara ya mwisho kushinda ilikuwa mwaka 2006 Emmanuel Adebayor alipofunga bao moja la ushindi.
Hii itakuwa mechi ya 41 kwa Timu zinazoongozwa na Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger kukutana uso kwa uso na Ferguson ameshinda mara 15 Wenger mara 14 na suluhu ni mara 11.
Manchester United
Majeruhi: Ferdinand, Hargreaves, Obertan, Rafael, Van der Sar.
Arsenal
Majeruhi: Djourou, Fabianski, Fabregas, Nasri, Walcott.
Refa: Mike Dean
Wasaidizi: Simon Beck, Richard West
Refa wa Akiba: Lee Probert
RATIBA KAMILI LIGI KUU ENGLAND
JUMAMOSI AGOSTI 29
[saa 8 dak 45 mchana]
Chelsea v Burnley
[saa 11 jioni]
Blackburn v West Ham
Bolton v Liverpool
Stoke v Sunderland
Tottenham v Birmingham
Wolves v Hull City
[saa 1 na robo usiku]
Manchester United v arsenal
JUMAPILI, AGOSTI 30
[saa 9 na nusu mchana]
Portsmouth v Man City
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Fulham

No comments:

Powered By Blogger