Thursday 27 August 2009

Klabu leo kujua Wapinzani wao Makundi ya UEFA Champions League
Dro ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kuamua Timu zipi zinakuwa Kundi lipi itafanyika leo huko Monaco saa 1 usiku saa za Kibongo.
Zipo jumla ya Timu 32 zitakazogawanywa Makundi manane ya Timu 4 kila moja zitakazocheza mtindo wa ligi wa nyumbani na ugenini.
Timu za Uingereza ambazo ziko kwenye hizo 32 ni Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal za England na Rangers ya Scotland.
Mechi za kwanza za Makundi hayo zitachezwa Septemba 15 na 16.
Timu hizo 4 za England zote zipo kwenye Kapu la Kwanza hivyo haziwezi kuwa Kundi moja ila Rangers wa Scotland wapo Kapu la Pili hivyo wanaweza kuwa Kundi moja na yeyote kati ya hizo Timu 4 za England.
Vile vile, kwa vile Real Madrid wako Kapu la Pili upo uwezekano wa Ronaldo kuwa Kundi moja na Timu yake ya zamani Manchester United.
Timu za Manchester United, Chelsea, Liverpool na Rangers zimeingizwa moja kwa moja hatua ya Makundi ila Arsenal ndio ilibidi waanze hatua ya mtoano kwa vile walimaliza Ligi nafasi ya 4.
Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE msimu huu itafanyika Uwanja wa Real Madrid Bernabeu Stadium hapo tarehe 22 Mei 2010.
Kapu la Kwanza
Barcelona
CHELSEA
LIVERPOOL
MANCHESTER UNITED
AC Milan
ARSENAL
Sevilla
Bayern Munich
Kapu la Pili
Lyon,
Inter Milan
Real Madrid
CSKA Moscow
Porto
AZ Alkmaar
Juventus
RANGERS
Kapu la Tatu
Olympiakos
Marseille
Dinamo Kiev
Stuttgart
Fiorentina
Atletico Madrid
Bordeaux
Besiktas
Kapu la Nne
Wolfsburg
Standard Liege
Maccabi Haifa
FC Zurich
Rubin Kazan
Unirea Urziceni
APOEL Nicosia
Debrecen
Chama cha Soka Scotland na Celtic walilia Eduardo afungiwe!!
UEFA yasema itachunguza!!!
Baada ya kujidondosha na kusababisha Arsenal wapewe penalti na kisha kuifunga yeye mwenyewe, Eduardo wa Arsenal, ameshikiwa bango na SFA, Chama cha Soka cha Scotland na Wachezaji wa Celtic kwamba anastahili kufungiwa na UEFA.
Penalti hiyo ya utata ilisababisha Arsenal kupata bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 walioupata jana dhidi ya Celtic kwenye mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Kiungo wa Celtic Massimo Donati ambae aliipatia Celtic bao lao moja amesema ni wajibu wa UEFA kumfungia Eduardo kwa udanganyifu huku Bosi wa SFA, Gordon Smith, akiunga mkono hatua za kumfungia Eduardo.
Ingawa Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger, hapo nyuma amekuwa akiwalaumu sana Wachezaji wanaojidondosha na kutaka wachukuliwe hatua kali, safari hii, ingawa alikiri Kipa wa Celtic Artur Boruc hakumgusa Eduardo na hivyo haikustahili kuwa penalti, hakuunga mkono msimamo wake wa nyuma na badala yake akatoa utetezi wa ajabu kuwa Eduardo alikuwa akimkwepa Kipa na ndio maana akaanguka.
Wakati huo huo, UEFA imesema itachunguza kitendo cha Eduardo na akipatikana na hatia atafungiwa mechi mbili.

No comments:

Powered By Blogger