Wednesday, 26 August 2009

Vurugu Carling Cup Uwanjani Upton Park: West Ham 3 Millwall 1
Mashabiki wavamia Uwanja!!!!

FA kuchunguza!!!
FA, Chama cha Soka cha England, kimesema kitafanya uchunguzi juu ya vurugu zilizotokea ndani na nje ya Uwanja wa Uptown Park jana usiku ambako mtu mmoja alichomwa kisu katika mechi ya Timu mbili zote za mjini London zenye upinzani wa jadi West Ham na Millwall zilipokuwa zikicheza mechi ya mtoano ya Kombe la Carling.
Timu hizi hazijawahi kukutana tangu Aprili 2005 kwa vile West Ham iko Ligi Kuu na Millwall inacheza Madaraja mawili chini yake yaani Ligi 2.
Vurugu hizo zilianza nje ya uwanja kabla ya mechi pale mamia ya Mashabiki wasio na Tiketi ambao Polisi imesema walipanga kuleta fujo kuanza kurusha chupa, matofali na kuchoma moto.
Ndani ya uwanja, West Ham wakiwa nyuma kwa bao 1 lililofungwa na Harris wa Millwall dakika ya 26, waliweza kusawazisha dakika ya 87 kupitia Junior Stanislas na kusababisha Mashabiki kuvamia uwanja wakishangilia.
Katika dakika 30 za muda wa nyongeza, alikuwa Junior Stanislas tena alieifungia West Ham bao la pili kwa penalti na Mashabiki kwa mara ya pili wakavamia uwanja kushangilia.
Hapo ndipo Refa akasimamisha mechi na kuwatoa nje Wachezaji huku Polisi na Wasimamizi wakijitahidi kuwaondoa Mashabiki uwanjani.
Mmoja wa watu waliojitahidi kuwatuliza Washabiki ni Mchezaji wa West Ham Jack Collison ambae Baba yake Mzazi alifariki Jumapili kwa ajali ya pikipiki na ambae alisema licha ya msiba huo yuko tayari kucheza mechi hiyo.
FA imesema Shabiki yeyote atakaegundulika kushiriki fujo hizo atafungiwa maisha kuingia kwenye Viwanja.

No comments:

Powered By Blogger