Saturday 29 August 2009

Evra aishutumu Arsenal, adai Refa alimtaka ajichunge asiumizwe!!!
Beki wa Manchester United Patrice Evra ameishutumu Timu ya Arsenal kwa jinsi walivyokuwa wakimchezea rafu na kuwa na nia ya kumuumiza katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu mwezi Mei iliyochezwa Old Trafford iliyoisha 0-0 na kuwapa Ubingwa Manchester United.
Evra amesema anaamini vitendo hivyo vilivyofanywa na Wachezaji wa Arsenal ni kisasi baada ya Man U kuwafunga mechi zote 2 za Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na yeye kutoa kauli kuwa matokeo hayo yametofautisha nani mtoto na nani mwanaume.
Evra amesema hata Refa wa mechi hiyo, Mike Dean [pichani kulia], ambae pia ndie Refa wa mechi ya leo kati ya Timu hizo, alimuonya kuwa inabidi awe mwangalifu au ataumizwa.
Evra amesema: “Vitendo vya Arsenal ni aibu. Niliulizwa kama walikuwa wananiwinda na nikajibu ndio! Nilishangaa kwani Arsenal siku zote wanacheza mpira mzuri na si watu wa fujo! Namshukuru Refa. Kuna wakati Refa alikuja kwangu na kuniambia ‘angalia, sijui nini kinaendelea lakini mara baada ya mapumziko Wachezaji wote wa Arsenal wanataka kukuumiza. Usilipize kisasi!"

No comments:

Powered By Blogger