Thursday 27 August 2009

Arsenal 3 Celtic 1
Arsenal wakiwa kwao Uwanjani Emirates jana waliifunga Celtic mabao 3-1 na hivyo kusonga mbele kwenye hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kushinda mechi ya kwanza ugenini kwa bao 2-0.
Ushindi wa jana wa Arsenal ulisaidiwa sana na kupata bao la kwanza dakika ya 28 kwa penalti baada ya Eduardo kujiangusha kwa makusudi ndani ya boksi na kupata penalti hiyo aliyoifunga mwenyewe.
Bao la pili la Arsenal lilifungwa na Emmanuel Eboue dakika ya 53 kufuatia gonga murua na Arshavin akapachika la 3 dakika ya 74.
Celtic walipata bao lao dakika ya 90.
Wakati Arsenal wanaingia Dro ya Timu 32 leo jioni ya kuamua Makundi Manane ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE yatakayocheza kwa Ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini Celtic wataingizwa kwenye EUROPA LEAGUEyenye Timu 48 zitakazokuwa na Dro yao kuamua Makundi hapo kesho.
Vikosi vilikuwa:
Arsenal (4-3-3) Almunia; Sagna, Vermaelen, Gallas, Clichy; Eboue, Song, Denilson; Bendtner, Eduardo, Diaby.
Akiba: Mannone, van Persie, Ramsey, Silvestre, Wilshere, Arshavin, Traore.
Celtic (4-4-2) Boruc; Hinkel, Caldwell, Loovens, Fox; McGeady, Brown, Donati, Maloney; McDonald, Fortune.
Akiba: Zaluska, Naylor, Samaras, Flood, McCourt, Killen, O'Dea.
Refa: Manuel Enrique Mejuto Gonzalez (Spain)

MATOKEO MECHI ZA JANA JUMATANO AGOSTI 26
[Timu iliyosonga mbele na jumla ya magoli kwenye mabano]
Apoel Nicosia 3 v FC Copenhagen 1 [Apoel 3-2]
Arsenal 3 v Celtic 1 [Arsenal 5-1]
Fiorentina 1 v Sporting 1[Fiorentina 3-3 kwa magoli ya ugenini]
Olympiacos 1 v FC Sheriff Tiraspol 0 [Olympiacos 3-0]
VfB Stuttgart 0 v Politehnica Timisoara 0 [Stuttgart 2-0]

No comments:

Powered By Blogger