Saturday 14 November 2009

NGOMA NGUMU!!! Misri 2 Algeria 0, mechi kuchezwa tena Jumatano huko Sudan kupata Mshindi kwenda Kombe la Dunia!!!
Mpaka dakika 90 kugonga, Misri walikuwa mbele bao 1-0 na hivyo wangekuwa nje Kombe la Dunia lakini, makosa ya Algeria ya kujidondosha makusudi ili kupoteza mwelekeo wa mchezo na pia muda, yaliwatokea puani!
Ziliongezwa dakika 6 na ndipo Misri wakapata bao la pili kwenye dakika ya 5 ya hiyo nyongeza na kushinda 2-0.
Lakini ushindi huo umewafanya walingane kila kitu na Algeria na hivyo mechi hiyo itachezwa Uwanja nyutro huko Sudan ili kupata Mshindi atakaetinga Fainali Kombe la Dunia kuungana na Nchi nyingine za Afrika, yaani Afrika Kusini, Ghana, Ivory Coast, Cameroun na Nigeria.
Cameroun nao wajikita Fainali Kombe la Dunia
Morocco 0 Cameroun 2
Togo 1 Gabon 0
Cameroun leo wameshinda ugenini huko Morocco na kupata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini huku wapinzani wao kutoka KUNDI A waliokuwa wakiwania nafasi hiyo pia, Gabon, kufungwa 1-0 ugenini na Togo.
Mabao ya Cameroun yalifungwa na Pierre Webo dakika ya 18 na Samuel Eto’o dakika ya 52.
Mechi ya Misri na Algeria, inayoanza muda mfupi tu kuanzia sasa, ndiyo itatoa Mwakilishi wa mwisho kutoka Afrika baada ya Timu za Afrika Kusini [Mwenyeji], Ghana [Mshindi KUNDI D], Nigeria [KUNDI B] na Ivory Coast [KUNDI E] kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia mapema.
Beckham aisaidia LA Galaxy kuingia Fainali ya Ubingwa MLS!!
Kiungo wa England, David Beckham, ametoa mchango mkubwa kwa Klabu yake Los Angeles Galaxy na kuisogeza mbele kuukaribia Ubingwa wa Ligi ya Marekani iitwayo MLS baada ya Timu hiyo kuifunga Houston Dynano 2-0 kwenye Nusu Fainali.
Mabao hayo mawili yalifungwa dakika za nyongeza, dakika ya 104 na 108.
Ni frikiki ya Beckham ndiyo ilimkuta Mfungaji Greg Berhalter na Landon akafunga la pili kwa penalti.
Wiki ijayo, LA Galaxy itacheza Fainali na Chicago Fire au Real Salt Lake mjini Seattle.
Nigeria waipiku Tunisia na kutinga Fainali Kombe la Dunia!!
Mozambique 1 Tunisia 0
Kenya 2 Nigeria 3
Nigeria imefanikiwa kuipiku Tunisia pale ilipoifunga Kenya mabao 3-2 mjini Nairobi Uwanja wa Nyayo na Tunisia kutunguliwa 1-0 na Msumbiji mjini Maputo, Uwanja wa Machava.
Kenya ndio walitangulia kupata bao Mfungaji akiwa Dennis Oliech dakika ya 16.
Nigeria walisawazisha dakika ya 65 kupitia Obafemi Martins na Yakubu Ayegbeni akaweka la pili dakika 2 baadae.
Kenya wakasawazisha dakika ya 79 kupitia Wetende na matokeo yangebaki 2-2 hata kama Tunisia angefungwa huko Msumbiji basi Tunisia angefuzu.
Lakini alikuwa Obafemi Martins ndie alieipeleka Nigeria Fainali baada ya kupachika bao la 3 na la ushindi dakika ya 83.
Huko Maputo, uwanja wa Machava, Mchezaji wa Msumbiji Dario Monteiro, dakika ya 81, ndie aliewakata maini Tunisia kwa kufunga bao la ushindi.
KIMBEMBE CHA KUTINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010!!!
Afrika kujua leo Nchi 3 zitakazoungana na Wenyeji Afrika Kusini, Ghana na Ivory Coast Fainali!!!
Wakati Bara la Afrika leo linategemewa kuzipata Nchi 3 zitazojumuika na Afrika Kusini, Ghana na Ivory Coast Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini kuanzia Juni 11 mwakani, Mabara ya Ulaya na Marekani leo wanacheza mechi zao za kwanza na kurudiana Jumatano Novemba 18 ili kupata washindi wakatakaoenda Fainali.
Kwa Afrika, Timu zinazogombea Nafasi hizo 3 ni ama Cameroun au Gabon toka KUNDI A, Tunisia au Nigeria toka KUNDI B, Misri au Algeria toka KUNDI C. 
RATIBA:
Afrika
Novemba 14
Mozambique v Tunisia
Togo v Gabon
Morocco v Cameroun
Rwanda v Zambia
Kenya v Nigeria
Burkina Faso v Malawi
Ivory Coast v Guinea
Egypt v Algeria
Sudan v Benin
Novemba 15
Ghana v Mali
Marekani
Novemba 14
Costa Rica v Uruguay
Ulaya
Novemba 14
Urusi v Slovenia
Republic of Ireland v Ufaransa
Greece v Ukraine
Ureno v Bosnia-Herzegovina
New Zealand yaingia Fainali Kombe la Dunia!!
New Zealand 1 Bahrain 0
Leo, ikicheza kwao huko Wellington, New Zealand Uwanja wa Westpac, New Zealand ilifunga bao kupitia Rory Fallon anaecheza Plymouth Argyle huko England dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza na kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni, 2010.
Hata hivyo Bahrain watajuta wenyewe kwani kipindi cha pili walipata penalti na wakakosa kufunga bao ambalo lingewawezesha kuipuku Ne Zealand kwa bao la ugenini.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa huko Bahrain, Timu hizi zilitoka sare 0-0.
Hii ni mara ya kwanza kwa New Zealand kuingia Fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 1982 walipowahi kuzicheza.

Friday 13 November 2009

Chama cha Marefa chadokeza kinaweza kumshitaki Fergie!!
Alan Heighton, Katibu wa Chama cha Kutetea Haki za Marefa, amedokeza kuwa wanaweza kumshitaki Sir Alex Ferguson Mahakamani kwa kumkashifu Refa Alan Wiley kwa matamshi yake kuwa Refa huyo hayuko fiti kuchezesha mechi.
Jana Kamati ya Sheria ya FA ilimtia hatiani Ferguson na kumfungia mechi 4 na kumpiga faini Pauni 20,000 lakini atatumukia kifungo cha mechi 2 tu na 2 zimwekwa kiporo hadi mwisho wa msimu wa 2010/11 ili kuchunga mwenendo wake.
Ferguson hatoruhusiwa kukaa kwenye benchi la akiba kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Novemba 21 dhidi ya Everton itakayochezwa Old Trafford na ile ya wiki inayofuatia ya Portsmouth ambayo Man U watakuwa ugenini.
Alan Heighton amesema ataongea na Refa Alan Wiley ili watoe uamuzi kama watafungua mashitaka au la.
Mwenyewe Ferguson hajazungumza lolote kuhusu adhabu hiyo ya FA na inaaminika hatakata rufaa kuipinga adhabu hiyo.
Ferguson anatakiwa awasilishe rufaa leo na mwisho ni saa 2 usiku saa za bongo.
MAMENEJA WALIODUNGWA FAINI ZA JUU:
• £200,000, ILIPUNGUZWA HADI £75,000 Jose Mourinho, Chelsea (2005) : Kwa kumrubuni Mchezaji wa Arsenal Ashley Cole.
• £20,000 Graeme Souness, Newcastle (2005): Kwa kumponda Refa wa mechi dhidi na Everton.
• £15,000 Graeme Souness, Blackburn (2005) : Alitolewa nje ya Uwanja kwenye mechi dhidi ya Liverpool.
• £15,000 Arsène Wenger, Arsenal (2004) : Kwa kauli yake kuhusu Ruud van Nistelrooy, Mchezaji wa Man U.
FAINI ALIZOWAHI KUPIGWA Ferguson:
• £10,000 NA KUFUNGIWA MECHI 2 (2008): Kumponda Refa Mike Dean aliechezesha mechi Man U v Hull.
• £10,000 (2003): Kumtukana Refa kwenye mechi ya Man U v Newcastle.
• £5,000 (2003, na Uefa): Aliposema UEFA imefiksi mechi ya Robo Fainali Man U wakutane na Real Madrid.
• £2,000 (1999,na Uefa):Kwa kuponda Marefa kwenye mechi ya Man U v Inter Milan.
England v Brazil
Doha, Qatar
Jumamosi, Novemba 14, Brazil na England, Mataifa yenye historia kubwa ya Soka yatacheza Doha, Qatar Uwanja wa Khalifa [pichani] wenye uwezo wa kuingiza Watazamaji 50,000.
Hii ni mechi ya kirafiki tu kwani Nchi zote hizi mbili zimeshatinga Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini lakini hapa Doha hii ni BIGI MECHI na matayarisho yake ni sherehe kubwa, furaha kubwa na ni pia kampeni kubwa kwani nao Qatar mwaka 2022 wanalitaka Kombe la Dunia hapa.
Hapa, nje ya Uwanja wa Khalifa, kuna ‘Kijiji cha Soka’ambacho kitawakaribisha Mashabiki wanaokuja kuona pambano hilo.
Kijiji hicho cha Soka kimegawanywa mara mbili.
Kuna Kijiji cha Brazil ambacho kina mfano wa Bichi maarufu huko Brazil iitwayo Copcabana na kina Kiwanja kidogo cha kuchezea Soka ya Bichi. Pia ipo Bendi iitwayo Batucada inayopiga muziki wa Brazil.
Kijiji cha England kina ile saa kubwa na maarufu Mjini London, Big Ben. Kuna ukuta mkubwa wa kuchezea ile gemu ya video, Playstation na pia yapo mashindano ya kupiga mpira danadana.
Wale Askari ambao ni kivutio kikubwa huko England kwenye Jumba la Malkia, Buckingham Palace, pia wapo. Muziki unaangushwa na Bendi toka England iitwayo Bootleg Beatles.
Timu zote mbili zimetua Doha Jumatano usiku na pichani ni Kaka wa Brazil akikaribishwa Uwanja wa Ndege wa Doha.
Washabiki watakaokwenda kushudia mechi hiyo Uwanja wa Khalifa wameombwa wafike masaa matatu kabla mechi kuanza hiyo Jumamosi Novemba 14 saa 2 usiku saa za bongo [Hapa Doha pia ni saa 2 usiku].
Imeripotiwa kuwa Hoteli zote za hapa zimejaa na wageni wametoka kila kona ya huku Arabuni toka Nchi kama Saudi Arabia, Bahrain, Kuwait, Oman na UAE.
Pia wapo washabiki kutoka England.
Brazil na England zimewahi kukutana mara 22 na Brazil kushinda mara 10 na England mara 3.

Thursday 12 November 2009

FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Wenyeji Nigeria wametinga Fainali na watakumbana na Uswisi.
Kwenye mechi ya kwanza ya Nusu Fainali, Uswisi waliwang'oa Colombia 4-0 na wakafuata Wenyeji Nigeria waliowapiga Spain 3-1 kwenye Nusu Fainali ya pili.
Fainali itachezwa Jumapili, Novemba 15.
Algeria watua Cairo, mvua ya mawe yawakaribisha!!
Timu ya Taifa ya Algeria leo imetua Cairo, Misri kwa ajili ya pambano lao la Jumamosi kumpata mmoja atakaenda Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini na walipoingia tu Hotelini kwao na Basi llilowachukua toka Uwanja wa Ndege walikaribishwa na mvua kubwa ya mawe yaliyovurumishwa na Genge la Vijana karibu 200 waliokuwa wanasubiri nje ya Hoteli hiyo.
Inasemekena Wachezaji watatu wa Algeria wamejeruhiwa ingawa hali zao si mbaya.

FIFA wamejulishwa kuhusu mkasa huo.
Chelsea yapata pigo, Bosingwa nje miezi mitatu!!
Fulbeki wa kulia wa Chelsea Jose Bosingwa atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu baada ya kupasuliwa goti la kushoto ambalo aliumia katikati ya mwezi Oktoba.
Bosingwa, miaka 27, alijiunga Chelsea Mei 2008 kutoka Klabu ya Nchini kwao Ureno FC Porto.
Chelsea vilevile wana pengo kwa Fulbeki wao wa kushoto Ashley Cole ambae alipata ufa kwenye mfupa wa ugoko mguuni lakini habari njema kwao ni kuwa hahitaji upasuaji ingawa atakuwa nje mwezi mzima.
Ingawa Chelsea imepata afueni baada ya CAS, Mahakama ya Usuluhishi kwenye Michezo, kuisimamisha adhabu waliyopewa na FIFA ya kutosajili Mchezaji hadi 2011 baada ya kuvunja sheria walipomteka Chipukizi Gael Kakuta kutoka Lens ya Ufaransa, Klabu hiyo imesema haisajili mtu dirisha la usajili litakapokuwa wazi Januari 2010 licha ya ukweli watakuwa na pengo kuu mwezi huo wa Januari wakati Wachezaji wao akina Didier Drogba, Salomon Kalou, Michael Essien na John Obi Mikel watakapokuwa Angola kuchezea Nchi zao Kombe la Mataifa ya Afrika.
Fergie awatakia heri Wachezaji wake waliomo kimbembe cha Kombe la Dunia wikiendi hii!!
Wachezaji wanne wa Manchester United wako kwenye vita kubwa Jumamosi hii na Jumatano ijayo ili kuzifanikisha Nchi zao kuingia Fainali za Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini kwa karata ya mechi za mchujo na wote wametakiwa kila la heri na Meneja wao Sir Alex Ferguson.
Wachezaji hao wanne ni Patrice Evra, Nani, John O'Shea na Darron Gibson.
Wachezaji O’Shea na Gibson watachezea Nchi yao Republic of Ireland na watapambana na Patrice Evra na Ufaransa yake.
Ferguson amenena: “Ireland inabidi washinde mechi ya kwanza kwao uwanjani Croke Park, Ireland ili wawe na nafasi kwani ni ngumu kwao kushinda ugenini Paris!”
Kuhusu Mchezaji wake mwingine Nani na Ureno ambayo Kocha wao ni Msaidizi wake wa zamani Carlos Queiroz wanaocheza na Bosnia-Herzegovina , Ferguson ametamka: “Ni mechi ngumu! Bosnia walimaliza Kundi lao nyuma ya Spain, sio watu rahisi! Mechi ambayo Ureno watajutia ni ile na Denmark wakiwa nyumbani wanaongoza 2-1 na bado dakika 5 tu lakini wakafungwa 3-2, hilo liliwafanya wakose kuongoza Kundi lao! Angekuwa Ronaldo fiti ningesema wana uhakika kuwafunga Bosnia lakini bila ya yeye ni ngumu! Ila naomba kwa ajili ya Carlos Queiroz washinde!”
Kipa Cudicini apata ajali ya Pikipiki, aumia vibaya!!!
Kipa wa Tottenham, Carlo Cudicini, miaka 36, amepata ajali baada ya Pikipiki yake kugongana na Gari Ford Fiesta leo asubuhi na inasemekana amevunjika mikono yote miwili na pia kuumia kiuno.
Habari za ajali hiyo zimethibitishwa na Klabu yake Tottenham ambayo imesema yuko hospitalini na itawapa Washabiki taarifa zaidi hapo baadae.
Cudicini alihamia Tottenham kutoka Chelsea alikokaa kwa miaka 10 na kabla aliwahi kuzichezea Klabu za Italia AC Milan na Lazio.
Baba yake Mzazi, Fabio, alikuwa Kipa wa wa AC Milan katika miaka ya 1960.
Kindumbwendumbwe cha Misri na Algeria kitarudiwa Sudan endapo Mshindi hapatikani Jumamosi hii!!
FIFA imetangaza kuwa endapo mechi kati ya Misri na Algeria ambayo itachezwa Cairo, Misri Jumamosi hii ili kupata Timu moja itakayoenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani itashindwa kutoa Mshindi, basi mechi hiyo itarudiwa Novemba 18 huko Sudan.
Algeria na Misri wako Kundi moja na Algeria anaongoza akiwa na pointi 13 na Misri ni wa pili akiwa na pointi 10.
Ili Misri kumpiku Algeria na kwenda Fainali ni lazima ashinde 3-0 lakini mechi ikiisha kwa ushindi wa 2-0 kwa Misri basi Timu hizo zitalingana kila kitu, yaani pointi na magoli, na hivyo itabidi ichezwe uwanja nyutro ambao FIFA umeamua ni Sudan.
Matokeo mengine yeyote yataipa ushindi Algeria.
FIFA iliipa kila Nchi chagua lake la uwanja wa nyutro na Ageria ikachagua Tunisia na Misri ikachagua Sudan na ndipo ikapigwa kura ambayo Misri walishinda.
Ferguson afungiwa mechi 2 na kupigwa Faini!!!
Leo, Kamati ya Sheria ya FA, Chama cha Soka England, kimemtia hatiani Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kwa kutamka kuwa Refa Alan Wiley hakuwa fiti kuchezesha mpira mara tu baada ya mechi ya Ligi Kuu kati ya Man U na Sunderland iliyomalizika 2-2 hapo Oktoba 3 na kumfungia kutokaa benchi la Timu yake kwa mechi 4 na kulipa Faini ya Pauni Elfu 20 lakini atatumikia kifungo cha mechi 2 tu na mbili nyingine zinasimamishwa ili kuchunga mwenendo wake hadi mwishoni mwa msimu wa 2010/11 na ikiwa hapatikani na kosa jingine adhabu hiyo ya mechi 2 zilizosimamishwa itafutwa.
Ingawa Ferguson aliomba radhi kwa matamshi yake hayo na pia kuomba kwa FA aende mwenyewe kujieleza inaelekea utetezi wake haukufanikiwa. 

Drogba kujenga Hospitali kwao Abidjan, Ivory Coast!!
Zimeibuka taarifa kuwa Mshambuliaji Nyota wa Chelsea ambae ni raia wa Ivory Coast, Didier Drogba, ameamrisha kitita atakacholipwa na Kampuni ya Pepsi kwa kumtumia ili kujitangaza ambacho ni Pauni Milioni 3 zitumike zote kujenga Hospitali yenye vitanda 200 huko kwao Abidjan, Ivory Coast.
Hospitali hiyo inayotarajiwa kumalizika mwakani 2010 pia itatumika kuwalea watoto yatima.
Mwenyewe Drogba ametamka: “Mwanzoni mwaka huu nilikwenda Hospitali huko Abidjan na nilistushwa kuona hali mbaya mno!! Hapo ndipo nikaamua kujenga Hospitali ili kusaidia watu!”
Yemen 2 Bongo 1
Katika mechi ya pili kwa Yemen na Tanzania huko Sanaa, Yemen, jana Taifa Stars ilifungwa bao 2-1 Uwanjani Ali Mohsin Muraisi.
Mechi ya kwanza Timu hizi zilitoka sare 1-1.
Yemen ndio ilipata bao la kwanza kwa penalti iliyofungwa na Tamer Hanash dakika ya 13 na Bongo wakasawazisha dakika ya 34 kupitia Abdel Halim Mohmad.
Yemen wakapata bao la pili dakika ya 37 Mfungaji akiwa Akram Al-Warafi.

Wednesday 11 November 2009

Hargreaves njiani kurudi dimbani!!!
Mchezaji mahiri na kiraka wa Manchester United, Owen Hargreaves, yuko njiani kuonekana tena uwanjani baada ya kupona matatizo ya magoti na yupo kwenye mazoezi makali.
Hargreaves amekuwa nje ya Uwanja kwa miezi 14 sasa tangu aumie Septemba, 2008 kwenye mechi na Chelsea ya dro 1-1 huko Stamford Bridge na ikabidi afanyiwe upasuaji kwenye magoti yake yote mawili.
Hargreaves amesema: “Nikirudi Uwanjani Old Trafford nitajisikia furaha na naweza kuzimia kwa furaha! Nataka nirudi nilipe fadhila kwa Mashabiki waliokuwa na imani na mimi!”
Real yabwagwa nje Copa del Rey!!!
Timu ya Kijijini inayocheza Daraja la chini huko Spain, Alcorcon, imeitupa nje ya mashindano kugombea Kombe la Mfalme Timu kubwa na tajiri Real Madrid licha ya jana Real kushinda 1-0 kwani Alcorcon waliibamiza Real 4-0 mechi ya kwanza.
Real walichezesha vigogo wao wote akina Raul, Kaka, Van Nistelrooy na wengineo lakini walishindwa kukomboa goli 4 na walipata kigoli chao kimoja mwishoni kupitia Rafael van der Vaart.
Mahasimu wa Real, Barcelona, wamesonga mbele kwenye Kombe hilo baada ya jana kushinda 5-0 dhidi ya Cultural Leonesa. Katika mechi ya kwanza, Barca walishinda 2-0.
Utata wa Marefa: Bosi wao kuitisha kikao cha Marefa wote!!
Kufuatia maamuzi yenye utatanishi ya kuzibeba baadhi ya Timu, ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu England, Bosi wa Marefa, Keith Hackett, amesema ataitisha kikao cha Marefa wote wanaochezesha Ligi Kuu ili kuongea na kulijadili suala hilo.
Keith Hackett ambae ni Meneja Mkuu wa PGMOB [Professional Games Match Officials Board] ameamua kuitisha kikao hicho baada ya kukithiri kwa maamuzi mabovu yanayozibeba baadhi ya Timu na kuziua nyingine.
Moja ya Timu iliyonufaika na uamuzi tata wa Marefa hao ni Liverpool iliyokuwa imefungwa 2-1 na Birmingham Uwanjani kwake Anfield siku ya Jumatatu kwenye Ligi Kuu na Mchezaji wake David Ngog, dakika ya 71, akajidondosha kwenye boksi bila kuguswa na mtu na Refa Peter Walton akaamua ni penalti licha ya kupingwa na Wachezaji wa Birmingham na ndipo Nahodha Steven Gerrard akapiga adhabu hiyo na kuwapa Liverpool dro ya 2-2 bila kutarajia.
Timu nyingine iliyonufaika na Marefa hivi karibuni ni Chelsea ambayo ilipata kigoli cha kupewa na Refa Martin Atkinson na kuifunga Manchester United 1-0 Uwanjani Stamford Bridge. Goli hilo hilo lilitokana na frikiki isiyostahili na kufungwa huku wakicheza rafu na kuwa ofasaidi lakini yote hayo Refa huyo hakuyaona.
Hackett amesisitiza ni kuwaweka sawa Marefa ili wawe makini zaidi.
Terry: “Liverpool hawawezi kuchukua Ubingwa!!!”
Wakati Timu yake iko mbele pointi 5 na kuongoza Ligi Kuu na pia pointi 11 mbele ya Liverpool ambayo iko nafasi ya 7, Nahodha wa Chelsea John Terry amewaponda Liverpool na kudai hawana nafasi ya kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Terry amesema: “ Liverpool wako nyuma sana!! Ubingwa ni sisi, Arsenal au Man U!!”
Terry ameendelea kujigamba kuwa wao hawatalegeza kamba na wana nia ya kuziacha Timu nyingine kwa pointi nyingi.
Hata hivyo, Chelsea wanakabiliwa na ratiba ngumu kama ifuatavywo:
-Novemba 21 Chelsea v Wolves
-Novemba 29 Arsenal v Chelsea
-Desemba 5 Man City v Chelsea
-Desemba 12 Chelsea v Everton
Kipa wa Ujerumani ajiua!!
Robert Enke, Kipa wa Klabu ya Hannover na Timu ya Taifa ya Ujerumani, ambae alitegemewa kuwepo kwenye Kikosi cha Ujerumani kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni mwakani, amefariki baada ya kugongwa na Treni karibu na nyumbani kwake.
Polisi imethibitisha kifo cha Kipa huyo na uchunguzi wa awali umebaini amejirusha mbele ya Treni na pia aliacha barua ya kuaga kabla hajajiua.
Gari ya Kipa huyo ilikutwa imepaki huku ikiwa wazi na waleti yake iko kitini karibu na tukio hilo kwenye makutano ya Reli na Barabara.
Madereva wawili wa Treni hiyo walisema walimwona mtu Relini lakini licha ya kufunga breki Treni hiyo ilishindwa kusimama kwani ilikuwa spidi ya zaidi ya maili 100 kwa saa.
Wiki chache zilizopita Kipa huyo aligundulika ana ugonjwa wa tumbo uliotokana na bacteria na virusi na Watu wa karibu nae walisema alikuwa amechanganyikiwa.
Enke alikuwa hajachezea Klabu yake Hannover kwa miezi miwili kutokana na kuugua.
Mbali ya Hannover, Enke pia alichezea Klabu za Borussia Monchengladbach, Tenerife, Fenerbahce, Barcelona na Benfica.
Ronaldo kutocheza Ureno!!!
Shirikisho la Soka la Ureno limetamka kuwa Cristiano Ronaldo hawezi kucheza mechi za Kombe la Dunia za Ureno v Bosnia-Herzegovina za Jumamosi Novemba 14 na marudiano Novemba 18 kwa vile enka yake haijapona.
Shirikisho hilo lilikuwa lipo kwenye mvutano mkubwa na Klabu ya Ronaldo Real Madrid iliyokuwa haitaki achezee Ureno ili apate muda mzuri wa kupona hiyo enka na ikabidi Shirikisho hilo lilazimishe Ronaldo aende Ureno kupimwa na Madaktari wa Timu ya Taifa ambao ndio wamethibitisha hayuko fiti.
Mechi kati ya Ureno na Bosnia-Herzegovina ni muhimu sana kwani mshindi ndie atakaeenda Finali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.

Tuesday 10 November 2009

Real wang’ang’ana Ronaldo majeruhi, Madaktari wa Timu ya Taifa ya Ureno kumcheki!!!
Winga wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amelazimika kusafiri hadi kwao Ureno ili Madaktari wa Timu ya Taifa ya Ureno wampime baada ya Klabu yake kugoma na kudai hayuko fiti kucheza na inabidi apumzishwe wiki mbili zaidi.
Ronaldo amechaguliwa Timu ya Ureno ambayo inakabiliwa na mechi muhimu sana za Mtoano ili kuingia Fainali Kombe la Dunia hapo Jumamosi Novemba 14 na Jumatano Novemba 18 watakapocheza na Bosnia-Herzegovina na mshindi kwenye mechi hiyo ndio anaetinga Fainali Kombe la Dunia mwakani.
Ronaldo aliumia enka yake Septemba 30 kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE kati ya Real Madrid na Marseille na hajacheza mechi 7 kwa Klabu yake ingawa aliichezea Ureno Oktoba 10 walipocheza na Hungary kwenye mechi ya Makundi Kombe la Dunia na ndipo akajiumiza tena kwenye enka hiyo hiyo majeruhi.
Bosi wa Ureno, Carlos Queiroz, ambae aliwahi kuwa Meneja wa Real Madrid na pia Msaidizi wa Sir Alex Ferguson Manchester United, amesema: “Sheria za FIFA zinatulinda na hivyo tutampima. Tunaheshimu kila Klabu lakini hii ni haki yetu kuridhika kuhusu Mchezaji wetu.”
Bendtner kufanyiwa operesheni!!
Arsenal imethibitisha kuwa Mshambuliaji wao toka Denmark, Nicklas Bendtner, atafanyiwa upasuaji ili kumtibu nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 4.
Bendtner aliumia Oktoba 31 Arsenal ilipowafunga Tottenham 3-0 kwenye Ligi Kuu Uwanjani Emirates.
Mshambuliaji huyo, alieifungia Arsenal goli 3 msimu huu katika mechi 13, atafanya hiyo operesheni huko Ujerumani.
Goli la mwisho alilofunga Bendtner ni lile lililowaua na kuwatoa Liverpool nje ya Kombe la Carling alipopachika bao la pili na kuwapa Arsenal ushindi wa 2-1. 
Liverpool: Uwanjani matokeo si mazuri, Wachezaji wazidi kujeruhiwa!!!
Ingawa Rafa Benitez amewapa faraja kidogo Wadau wa Liverpool pale alipotangaza Mhimili wao mkuu, Fernando Torres, halazimiki kufanyiwa upasuaji ili kutibu maumivu yake na pia Gerrard kuonekana uwanjani jana, lakini wasiwasi unazidi kutanda kwa matokeo ‘mabovu’ uwanjani na listi ya majeruhi kuongezeka kwa Wachezaji wanaotumainiwa.
Wachezaji Albert Riera na Yossi Benayoun waliocheza mechi ya jana Liverpool waliyotoka suluhu 2-2 na Birmingham walilazimika kutoka nje ya uwanja huku wakichechemea na Benitez amethibitisha itabidi wawe nje kwa muda pamoja na Mlinzi Dan Agger mwenye matatizo ya mgongo.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Wenyeji Nigeria na Spain waingia Nusu Fainali!!!
Nigeria ambao ndio wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17 wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kuifunga South Korea 3-1.
Katika Robo Fainali nyingine iliyochezwa jana, Spain waliitoa Uruguay kwa penalti 4-2 baada ya mechi kwisha bao 3-3.
Nigeria watakutana na Spain kwenye Nusu Fainali.
RATIBA NUSU FAINALI:
Alhamisi, Novemba 12:
Colombia v Uswisi
Nigeria v Spain 
Mwana wa Fergie atimuliwa Umeneja Peterborough!!!

Peterborough United, Klabu inayocheza Daraja chini tu ya Ligi Kuu liitwalo Coca Cola Championship, imemwondoa kazini Meneja wao Darren Ferguson [pichani] ambae ni mtoto wa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kufuatia matokeo mabaya kwa Klabu hiyo.
Darren Ferguson, umri miaka 37, ndie alieibeba Timu hiyo na kuipandisha Klabu hiyo mfululizo Madaraja mawili juu kutoka LIGI 2 mpaka ilipo sasa kuanzia mwaka 2007.
Lakini msimu huu, kwenye Ligi ya Coca Cola Championship, Timu hiyo imekuwa ikifanya vibaya na Jumamosi ilipigwa 3-1 na Newcastle.
Katika mechi 140 alizokuwa Meneja hapo Peterborough, Darren Ferguson, ameshinda mechi 73 na kufungwa 40 tu.
KOMBE LA DUNIA: Mechi za Lala Salama, Nani kwenda Bondeni?
Tayari Nchi 23 zishapata Tiketi kucheza Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010, Fainali zitakazoanza Juni 11 na kumalizika Julai 11, na bado kuna nafasi 9 zikidai ili kufanya jumla ya Nchi 32 kwenye Fainali hizo.
LISTI KAMILI YA TIMU 23 ZILIZOINGIA FAINALI NI:
WENYEJI: Afrika Kusini
AFRIKA: Ghana na Ivory Coast [BADO TIMU 3]
ASIA: Australia, Japan, Korea Kaskazini, Korea Kusini
ULAYA: Denmark, England, Germany, Uholanzi, Serbia, Spain, Italy, Slovakia, Uswisi [BADO TIMU 4]
MAREKANI KUSINI: Brazil, Paraguay, Chile, Argentina
MAREKANI KASKAZINI, KATI NA CARIBBEAN: USA, Mexico, Honduras
TIMU ZITAKAZOINGIA FAINALI KUPITIA MECHI ZA MCHUJO [Moja kati ya mbili zifuatazo]:
-New Zealand au Bahrain [Mechi ya kwanza Nchini Bahrain ilikuwa 0-0]
-Costa Rica au Uruguay
-Urusi au Slovenia
-Ufaransa au Republic of Ireland
-Ureno au Bosnia-Herzegovina
-Ukraine au Greece
-AFRIKA [INATEGEMEA MATOKEO KWENYE MAKUNDI YAO]: Wenye matumaini makubwa kupata Nafasi 3 zilizobaki ni:
-KUNDI A- Cameroun au Gabon
Cameroun pointi 10
Gabon pointi 9
Cameroun, ambao watacheza ugenini huko Morocco, wanatakiwa waifunge Morocco ili watinge Fainali.
Gabon ni lazima washinde mechi yao na Togo itakayochezwa huko Togo na pia kuomba Cameroun watoke suluhu au wafungwe.
-KUNDI B- Tunisia au Nigeria
Tunisia pointi 11
Nigeria pointi 9
Tunisia watasafiri hadi Msumbiji na Nigeria watakuwa Kenya kwa mechi zao za mwisho.
Ikiwa Tunisia wataifunga Msumbiji basi watafanikiwa kwenda Fainali.
Lakini hata Tunisia wakitoka sare huko Msumbiji huku Nigeria afungwe au atoke sare na Kenya, Tunisia watapita.
Nigeria ni lazima waifunge Kenya na kuomba Tunisia afungwe au atoke dro.
-KUNDI C- Misri au Algeria
Algeria pointi 13
Misri pointi 10
Ni Misri au Algeria ndio watafika Fainali na Timu hizi zinakutana Mjini Cairo, Misri Jumamosi.
Wakati Algeria inahitaji suluhu tu, au hata wafungwe 1-0 tu, watasonga mbele, Misri ni lazima ishinde kwa goli 3-0 ili wapite.
Mechi ikiisha kwa ushindi wa 2-0 kwa Misri mechi hii inabidi irudiwe Nchi nyutro [si Misri wala Algeria] kwani zitakuwa zimelingana kila kitu.
RATIBA:
Afrika
Novemba 14
Mozambique v Tunisia
Togo v Gabon
Morocco v Cameroun
Rwanda v Zambia
Kenya v Nigeria
Burkina Faso v Malawi
Ivory Coast v Guinea
Egypt v Algeria
Sudan v Benin
Novemba 15
Ghana v Mali
Asia na Oceania
Novemba 14
New Zealand v Bahrain [Mshindi mechi hii ataingia Fainali lakini sare yeyote ya magoli, Bahrain atakuwa Fainali kwa magoli ya ugenini kwani mechi ya kwanza huko Bahrain ilikuwa 0-0] 
Marekani
Novemba 14
Costa Rica v Uruguay
Novemba 18
Uruguay v Costa Rica
Ulaya
Novemba 14
Urusi v Slovenia
Republic of Ireland v Ufaransa
Greece v Ukraine
Ureno v Bosnia-Herzegovina
Novemba 18
Ukraine v Greece
Bosnia-Herzegovina v Ureno
Ufaransa v Republic of Ireland
Slovenia v Urusi
LIVEPOOL 2 BIRMINGHAM 2
Wakiwa nyumbani Anfield, Liverpool jana chupuchupu kufungwa na Birmingham kama si kupewa penalti tata na Refa Peter Walton kwenye dakika ya 71 na Nahodha Steven Gerrard, alieingia toka benchi la akiba, kufunga bao la pili kwa penalti hiyo na kusawazisha.
Penalti hiyo ilikuja baada ya Fowadi wa Liverpool David Ngog kujiangusha bila kuguswa na kumhadaa Refa.
Liverpool walianza kupata bao dakika ya 13 Mfungaji akiwa Ngog na Birmingham wakasawazisha kupitia Benitez dakika ya 26 na Jerome akapachika bao la pili dakika ya 45.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Johnson, Agger, Insua, Skrtel, Riera [Gerrard, dak 45], Benayoun [Babel dak ya 77], Mascherano, Lucas [Aquilani, dak 82], Kuyt, Ngog.
Birmingham: Hart, Carr, Ridgewell, Johnson, Dann, Bowyer, Larsson, Tainio [Carsley, dak ya 15], Jerome, Benitez [McSheffrey, dak ya 86], Mac Fadden [Vignal, dak ya 76]

Monday 9 November 2009

FA yampa onyo Rooney kwa kauli: "MTU 12!! MTU 12!!' aliyoitoa baada ya mechi ya Chelsea jana!!!
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amepewa onyo na FA, Chama cha Soka England, na ametakiwa achunge mwenendo wake wa baadae baada ya kunaswa akipiga kelele kwenye Kamera ya TV 'MTU 12!! MTU 12!!', akimaanisha Refa kawabeba Chelsea,  mara tu baada ya mechi ya Ligi Kuu jana kumalizika huko Stamford Bridge kwa Chelsea kuifunga Man U 1-0 kwa goli la utata.
Pia FA imesema Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, hana hatia baada ya kutamka maamuzi ya Refa Martin Atkinson yalikuwa ni upuuzi wa hali ya juu na pia kusema maamuzi kama hayo yanawafanya watu wakose imani kwa Marefa. 
Kwa sasa Ferguson yupo matatani na FA akikabiliwa na kesi inayosubiri uamuzi baada ya kushitakiwa mwezi Oktoba pale alipodai Refa Alan Wiley hayuko fiti kuchezesha mara tu baada ya mechi kati ya Man U na Sunderland kwisha dro 2-2.
Fletcher: “Wenger ananiponza kwa Marefa!”

Darren Fletcher anaamini kabisa Marefa sasa wanamsakama mno kufuatia matamshi ya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger,  mwanzoni mwa msimu, alipokuwa akinung’unika baada ya Arsenal kupigwa 2-1 na Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu Uwanjani Old Trafford, na kudai Man U imecheza 'kinyume na soka' na Wachezaji wake kucheza rafu.
Ingawa baada ya mechi hiyo Wenger hakumtaja kwa jina Kiungo huyo wa Man U, lakini ilikuwa ‘siri ya wazi’ maneno yake hayo na hasa alipotamka kwamba kuna Mchezaji katika mechi hiyo alikuwa akicheza rafu mfululizo bila ya kuonywa na Refa yalimlenga Fletcher.
Fletcher amesema: “Kauli ya Bwana Wenger sasa inaanza kuwafanya Marefa waone mie ni Mchezaji mchafu! Ile frikiki iliyowapa goli Chelsea sio faulo! Sikucheza rafu, niliupiga mpira kwa kisigino na Cole akajirusha juu! Sasa tunaanza kuona madhara ya Wenger! Lakini itabidi tuipandishe soka yetu ili maamuzi haya mabovu yasituumize zaidi!”
Tangu msimu uliopita chati ya Darren Fletcher imepanda juu sana hapo Manchester United na sasa anaonekana ni Mchezaji muhimu sana.
Wadau wengi wanaamini kukosekana kwake kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, baada ya kupewa Kadi 'feki' kwenye Nusu Fainali ambazo Man U waliwapiga Arsenal nje ndani, ndiko kulisababisha Barcelona kushinda Fainali hiyo.
Baada ya mechi ya leo, Ligi Kuu kupisha kitimtim cha Kombe la Dunia hadi Novemba 21!!!
Baada ya mechi ya leo ya Ligi Kuu saa 5 usiku, saa za kibongo, Liverpool kuikaribisha Birmingham Uwanjani Anfield, Ligi Kuu England itakaa pembeni hadi Jumamosi, Novemba 21 ili kupisha mapambano ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010 ambayo yatachezwa Jumamosi Novemba 14 na marudiano ni Jumatano, Novemba 18.
Ratiba kuhusu mechi hizo tutawaletea kesho. 
Vilevile, kwa Timu za Taifa ambazo zimefuzu kuingia Fainali hizo za Kombe la Dunia, kipindi hiki ni Kalenda ya FIFA kwa Timu za Taifa kucheza mechi kadhaa za kirafiki na hivyo kuna mechi kadhaa za kirafiki za Timu hizo.
RATIBA YA LIGI KUU NI KAMA IFUATAVYWO:
Jumatatu, 9 Novemba 2009
Liverpool v Birmingham
Jumamosi, 21 Novemba 2009
Birmingham v Fulham
Burnley v Aston Villa
Chelsea v Wolves
Hull City v West Ham
Liverpool v Man City
Man U V Everton
Sunderland v Arsenal
Jumapili, 22 Novemba 2009
Bolton v Blackburn
Stoke v Portsmouth
Tottenham v Wigan
Jumatano, 25 Novemba 2009
Fulham v Blackburn
Hull City v Everton
Ancelotti afurahia kumfunga “Mpinzani Bora!!!”
Carlo Ancelotti wa Chelsea amekiri kuwa amefurahishwa sana na kumfunga “Mpinzani Bora” baada ya Timu yake kuifunga Manchester United hapo jana kwenye Ligi Kuu Uwanjani Stamford Bridge bao 1-0.
Ingawa Chelsea walishinda kwa goli la utata lililolalamikiwa na Manchester United, mechi hiyo ilitawaliwa na Man U.
Ancelotti amesema: “Ilikuwa mechi ngumu! Kulikuwa hamna nafasi kwenye Kiungo, ilikuwa taabu kutengeneza nafasi! Sasa tuko pointi 5 mbele lakini inabidi tusilewe ushindi kwa kuifunga Timu Bora na Mpinzani wetu mkubwa!”
Wes Brown asisitiza Drogba alimchezea rafu Chelsea walipofunga goli!!
Rooney asikika akipiga kelele kwenye Kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!!’
Mlinzi wa Manchester United Wes Brown amesisitiza kuwa Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba alimchezea rafu wakati Chelsea wanafunga goli lao na Refa Martin Atkinson alipaswa kulikataa.
Chelsea walifunga goli lao dakika ya 76 kwa John Terry kupiga kichwa mpira wa frikiki ya Frank Lampard na mpira kumparaza Anelka, aliekuwa ofsaidi na kutinga wavuni.
Manchester United waliilalamikia frikiki hiyo kwa madai Darren Fletcher alicheza mpira na hakumgusa Ashley Cole aliejirusha.
Vilevile wamedai wakati Terry anapiga kichwa kufunga Drogba alimkamata na kumwangusha chini Brown.
Brown ametamka kwa masikitiko: “Sidhani Refa alichezesha vizuri! Lile goli si halali na hata frikiki ni utata mtupu! Lakini tutafanyaje ikiwa Refa haoni yote hayo?”
Mara baada ya mechi kwisha, mshambuliaji Nyota wa Manchester United Wayne Rooney alisikika akipiga kelele kwenye kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!” bila shaka akimaanisha Refa alikuwa upande wa Chelsea.
Kikosi cha England kucheza na Brazil huko Doha, Qatar chatajwa!
Kocha wa England, Fabio Capello, amekitangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil huko Doha, Qatar tarehe 14 Novemba 2009.
Katika Kikosi hicho wapo Darren Bent wa Sunderland ambae mara ya mwisho kuichezea England ni miezi 12 iliyopita kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Beki wa Aston Villa, Stephen Warnock, ambae amechukuliwa badala ya Ashley Cole wa Chelsea anaesemekana kaumia.
Pia yupo Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone, ambae ni mara ya kwanza kuitwa England.
Ingawa Beckham ametajwa kwenye Kikosi hicho lakini taarifa za baadaye zimesema hatowezi kujiunga na Timu kwa vile Klabu yake LA Galaxy ilishinda Nusu Fainali yake ya Ligi ya MLS hapo jana na hivyo kutinga Fainali.
Kikosi kamili ni: Foster (Manchester United), Green (West Ham), Hart (Manchester City); Bridge, Lescott (Manchester City), Brown (Manchester United), Cahill (Bolton), Johnson (Liverpool), Terry (Chelsea), Upson (West Ham), Warnock (Aston Villa); Barry, Wright-Phillips (Manchester City), Beckham (Los Angeles Galaxy), Carrick (Manchester United), Huddlestone, Jenas (Tottenham), Lampard (Chelsea), Milner, Young (Aston Villa); Bent (Sunderland), Crouch, Defoe (Tottenham), Rooney (Manchester United).

Sunday 8 November 2009

Yemen 1 Bongo 1
Leo Timu ya Taifa ya Tanzania, baada ya kushushiwa kipigo cha 5-1 na Misri siku ya Jumatano, ilikuwa Nchini Yemen kucheza na Wenyeji wao na mechi kuisha sare 1-1.
Mpaka haftaimu ngoma ilikuwa 0-0.
Kipindi cha pili, Bongo walifunga dakika ya 68  kupitia Mchezaji alietajwa ni Poko na Yemen wakasawazisha dakika ya 79 Mfungaji akiwa Ali Mubarak.
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
Colombia kuikwaa Uswisi Nusu Fainali!!
Colombia na Uturuki zilitoka sare 1-1 hadi dakika 120 na mshindi akapatikana kwa matuta na Colombia amepita kwa penalti 5-3.
Katika mechi nyingine ya Robo Fainali, Uswisi imeitoa Italy 2-1 na hivyo kukutana na Colombia kwenye Nusu Fainali tarehe 12 Novemba 2009.
RATIBA Jumatatu Novemba 9:
ROBO FAINALI
Spain v Uruguay
Nigeria v South Korea
WASHINDI WA MECHI HIZI WATAKUTANA NUSU FAINALI.
Fergie: “Tumepoteza imani na Marefa!!”
Licha ya kuwalaumu Wachezaji wake kwa kushindwa kuugeuza umiliki wa mechi kuwa magoli, Sir Alex Ferguson amemlaumu pia Refa Martin Atkinson kwa kuwapa Chelsea frikiki iliyozua goli bila rafu kutendeka, kwa kukubali goli hilo huku Drogba akimuangusha Wes Brown na wakati huo huo mpira kuguswa na Anelka aliekuwa ofsaidi na kuingia wavuni ingawa Chelsea wanaficha kuwa Mfungaji si Anelka na kung’ang’ania Terry ndie aliefunga.
“Ni uamuzi mbovu!” Ferguson amelalamika. “Lakini utafanyaje? Unapoteza imani kwa Marefa! Wachezaji wote wanasema Refa hakututendea haki!”
Mbali ya goli hilo kukubalika, Man U wanadhani walionewa pale dakika ya 14 Valencia alipoangushwa na Terry kwenye boksi na Refa hakutoa penalti.
Na ikafuata Rooney kupewa pande tamu na akiwa akienda kumuona Kipa Cech, kwa mshangao, ikaamuliwa ni ofsaidi.
Lakini, juu ya yote, hakuna Mdau wa Man U anaeshangaa maamuzi ya Marefa kwa kipindi hiki ambacho Wadau hao wanadai Man U inaandamwa.
Chelsea 1 Man U 0
Chelsea mbele pointi 5!!!
Goli la dakika ya 76 alilofunga John Terry [au Anelka aliekuwa ofsaidi huku Drogba akimwangusha Brown!] kufuatia frikiki ambayo Washabiki wa Man U walilalamikia limewapa ushindi Chelsea wakiwa nyumbani Stamford Bridge wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa Manchester United na sasa kuongoza pointi 5 mbele kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Ingawa leo Manchester United walichezesha ukuta dhaifu bila ya Masentahafu wao Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ambao ni majeruhi, na ingawa Vidic alikuwa benchi, waliitawala mechi hii na pengine wangeweza kushinda.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Ivanovich, Carvalho, Terry, Cole, Essien, Lampard, Ballack, Deco, Drogba, Anelka.
Akiba: Hilario, Joe Cole, Mikel, Malouda, Paulo Ferreira, Kalou, Alex.
Manchester United: Van der Sar, O'Shea, Brown, Jonathan Evans, Evra, Fletcher, Carrick, Anderson, Valencia, Rooney, Giggs.
Akiba: Kuszczak, Owen, Vidic, Scholes, Fabio Da Silva, Obertan, Gibson.
Refa: Martin Atkinson
Matokeo Mechi za leo Ligi Kuu, Jumapili, Novemba 8:
Mechi zimeanza mapema [Chelsea na Man U inaendelea]
Hull 2 v Stoke 1
West Ham 1 v Everton 2
Wigan 1 v Fulham 1
Fergie atimiza Miaka 23 Man U na kutoboa Klabu nyingi za nje zilimtaka!!
Sir Alex Ferguson ametoboa kuwa katika miaka yake 23 aliyotimiza Ijuma iliyopita Klabu nyingi kubwa za nje ya England zimekuwa zikimpa ofa nono ya kwenda kufundisha lakini mwenyewe amekiri “huwezi ukaikimbia Manchester United!”
Katika miaka hiyo 23 akiwa Old Trafford na Manchester United, Sir Alex Ferguson amefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 11, Ubingwa wa Ulaya mara 2, Kombe la FA mara 5, Kombe la Ligi mara 3, Kombe la Washindi Ulaya mara 1, Kombe Klabu Bingwa Duniani mara 2 na UEFA Super Cup mara 1.
Ferguson amekiri: “Nimepata ofa nyingi tu lakini hakuna hata moja iliyonivutia!”
LIVERPOOL HAIUZI MTU!!!
Mmojawapo wa Wamiliki wawili Liverpool, Tom Hicks, amewahakikishia Mashabiki wao kuwa hata kama Liverpool itatolewa mapema kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE wao hawana nia ya kuuza Mchezaji yeyote.
Msimu huu Liverpool wameuanza kwa balaa kwani wapo nafasi ya 7 kwenye Ligi Kuu na pia wako hali mbaya kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE huku wakitakiwa washinde mechi zao zote 2 zilizobaki Kundini mwao na pia kuomba wengine wapate matokeo mabaya ili wao wasonge mbele.
Hali hii mbaya imefanya kuzagae habari kuwa Mastaa kama Fernando Torres na Steven Gerrard huenda wakang’oka na imebidi Mmiliki huyo Tom Hicks ajitokeze kutuliza watu.
Kipa wa Sunderland avunjika mkono!!
Sunderland imethibitisha kuwa Kipa Craig Gordon ambae pia huidakia Timu ya Taifa ya Scotland amevunjika mkono baada ya kuumizwa na Jermaine Defoe, Straika wa Tottenham, kwenye mechi ya Ligi Kuu jana ambayo Tottenham iliifunga Sunderland 2-0 uwanjani White Hart Lane.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 alitolewa na nafasi yake kushikwa na Marton Fulop.
Meneja wa Sunderland Steve Bruce amethibitisha kuumia kwa Gordon lakini hakusema atakuwa nje kwa muda gani.
Capello aonya Wachezaji majeruhi!!
Bosi wa England, Fabio Capello, amesema Kikosi chake hakina nafasi kwa Mchezaji ambae hayuko fiti na wasitegemea watachukuliwa kwenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani ikiwa hawakuthibitisha uimara wao.
Capello anategemewa kutangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil Jumamosi tarehe 14 Novemba 2009 huko Doha, Qatar muda wowote leo.
Capello amemzungumzia Rio Ferdinand na kusema ikiwa atakuwa fiti kabla hajateua Kikosi chake cha mwisho basi ataenda nae Afrka Kusini lakini ameonya kuwa Ledley King, Beki wa Tottenham, na Kipa David James wana mashaka makubwa kutokana na kuwa majeruhi.
Kuhusu David James, Capello alisema: "James anacheza vizuri lakini tangu aumie akicheza mechi baadae hawezi kufanya mazoezi siku mbili!"
FIFA U-17 WORLD CUP NIGERIA 2009
RATIBA ROBO FAINALI:
Jumapili Novemba 8:
Colombia v Turkey
Uswisi v Italy
Jumatatu Novemba 9:
Spain v Uruguay
Nigeria v South Korea
LIGI KUU England: Arsenal waibamiza Wolves 4-1 na kuchupa nafasi ya pili!!
Villa yaiua Bolton 5-1!!!
Matokeo Mechi za Jumamosi Novemba 7:
Wolves 1 Arsenal 4
Man City 3 Burnlay 3
Tottenham 2 Sunderland 0
Blackburn 3 Portsmouth 1
Aston Villa 5 Bolton 1
Jana Arsenal ikicheza ugenini iliibamiza Wolves mabao 4-1 na kushika nafasi ya pili wakiwa na pointi 25 sawa na Manchester United lakini Arsenal wana ubora wa magoli.
Chelsea yupo kileleni akiwa na pointi 27.
Mechi za leo Ligi Kuu, Jumapili, Novemba 8:
[saa 10 na nusu jioni]
Hull v Stoke
[saa 12 jioni]
West Ham v Everton
Wigan v Fulham
[saa 1 usiku]
Chelsea v Man U
Powered By Blogger