Sunday 8 November 2009

Capello aonya Wachezaji majeruhi!!
Bosi wa England, Fabio Capello, amesema Kikosi chake hakina nafasi kwa Mchezaji ambae hayuko fiti na wasitegemea watachukuliwa kwenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani ikiwa hawakuthibitisha uimara wao.
Capello anategemewa kutangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil Jumamosi tarehe 14 Novemba 2009 huko Doha, Qatar muda wowote leo.
Capello amemzungumzia Rio Ferdinand na kusema ikiwa atakuwa fiti kabla hajateua Kikosi chake cha mwisho basi ataenda nae Afrka Kusini lakini ameonya kuwa Ledley King, Beki wa Tottenham, na Kipa David James wana mashaka makubwa kutokana na kuwa majeruhi.
Kuhusu David James, Capello alisema: "James anacheza vizuri lakini tangu aumie akicheza mechi baadae hawezi kufanya mazoezi siku mbili!"

No comments:

Powered By Blogger