Wednesday 11 November 2009

Utata wa Marefa: Bosi wao kuitisha kikao cha Marefa wote!!
Kufuatia maamuzi yenye utatanishi ya kuzibeba baadhi ya Timu, ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu England, Bosi wa Marefa, Keith Hackett, amesema ataitisha kikao cha Marefa wote wanaochezesha Ligi Kuu ili kuongea na kulijadili suala hilo.
Keith Hackett ambae ni Meneja Mkuu wa PGMOB [Professional Games Match Officials Board] ameamua kuitisha kikao hicho baada ya kukithiri kwa maamuzi mabovu yanayozibeba baadhi ya Timu na kuziua nyingine.
Moja ya Timu iliyonufaika na uamuzi tata wa Marefa hao ni Liverpool iliyokuwa imefungwa 2-1 na Birmingham Uwanjani kwake Anfield siku ya Jumatatu kwenye Ligi Kuu na Mchezaji wake David Ngog, dakika ya 71, akajidondosha kwenye boksi bila kuguswa na mtu na Refa Peter Walton akaamua ni penalti licha ya kupingwa na Wachezaji wa Birmingham na ndipo Nahodha Steven Gerrard akapiga adhabu hiyo na kuwapa Liverpool dro ya 2-2 bila kutarajia.
Timu nyingine iliyonufaika na Marefa hivi karibuni ni Chelsea ambayo ilipata kigoli cha kupewa na Refa Martin Atkinson na kuifunga Manchester United 1-0 Uwanjani Stamford Bridge. Goli hilo hilo lilitokana na frikiki isiyostahili na kufungwa huku wakicheza rafu na kuwa ofasaidi lakini yote hayo Refa huyo hakuyaona.
Hackett amesisitiza ni kuwaweka sawa Marefa ili wawe makini zaidi.
Terry: “Liverpool hawawezi kuchukua Ubingwa!!!”
Wakati Timu yake iko mbele pointi 5 na kuongoza Ligi Kuu na pia pointi 11 mbele ya Liverpool ambayo iko nafasi ya 7, Nahodha wa Chelsea John Terry amewaponda Liverpool na kudai hawana nafasi ya kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Terry amesema: “ Liverpool wako nyuma sana!! Ubingwa ni sisi, Arsenal au Man U!!”
Terry ameendelea kujigamba kuwa wao hawatalegeza kamba na wana nia ya kuziacha Timu nyingine kwa pointi nyingi.
Hata hivyo, Chelsea wanakabiliwa na ratiba ngumu kama ifuatavywo:
-Novemba 21 Chelsea v Wolves
-Novemba 29 Arsenal v Chelsea
-Desemba 5 Man City v Chelsea
-Desemba 12 Chelsea v Everton
Kipa wa Ujerumani ajiua!!
Robert Enke, Kipa wa Klabu ya Hannover na Timu ya Taifa ya Ujerumani, ambae alitegemewa kuwepo kwenye Kikosi cha Ujerumani kitakachocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni mwakani, amefariki baada ya kugongwa na Treni karibu na nyumbani kwake.
Polisi imethibitisha kifo cha Kipa huyo na uchunguzi wa awali umebaini amejirusha mbele ya Treni na pia aliacha barua ya kuaga kabla hajajiua.
Gari ya Kipa huyo ilikutwa imepaki huku ikiwa wazi na waleti yake iko kitini karibu na tukio hilo kwenye makutano ya Reli na Barabara.
Madereva wawili wa Treni hiyo walisema walimwona mtu Relini lakini licha ya kufunga breki Treni hiyo ilishindwa kusimama kwani ilikuwa spidi ya zaidi ya maili 100 kwa saa.
Wiki chache zilizopita Kipa huyo aligundulika ana ugonjwa wa tumbo uliotokana na bacteria na virusi na Watu wa karibu nae walisema alikuwa amechanganyikiwa.
Enke alikuwa hajachezea Klabu yake Hannover kwa miezi miwili kutokana na kuugua.
Mbali ya Hannover, Enke pia alichezea Klabu za Borussia Monchengladbach, Tenerife, Fenerbahce, Barcelona na Benfica.
Ronaldo kutocheza Ureno!!!
Shirikisho la Soka la Ureno limetamka kuwa Cristiano Ronaldo hawezi kucheza mechi za Kombe la Dunia za Ureno v Bosnia-Herzegovina za Jumamosi Novemba 14 na marudiano Novemba 18 kwa vile enka yake haijapona.
Shirikisho hilo lilikuwa lipo kwenye mvutano mkubwa na Klabu ya Ronaldo Real Madrid iliyokuwa haitaki achezee Ureno ili apate muda mzuri wa kupona hiyo enka na ikabidi Shirikisho hilo lilazimishe Ronaldo aende Ureno kupimwa na Madaktari wa Timu ya Taifa ambao ndio wamethibitisha hayuko fiti.
Mechi kati ya Ureno na Bosnia-Herzegovina ni muhimu sana kwani mshindi ndie atakaeenda Finali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini.

No comments:

Powered By Blogger