Man U warudi kileleni, Kijana wa miaka 17 awapa ushindi!!!!Wakichezesha kikosi hafifu bila Wachezaji wao vigogo kama vile Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Paul Scholes, Wayne Rooney na Dimitar Berbatov waliokosekana kwa ama kuwa na Kadi au kuwa majeruhi, Mabingwa Man U walijikuta wakichungulia kipigo kutoka kwa Aston Villa uwanjani kwao Old Trafford huku zikiwa zimesalia dakika 10 tu wakati walipokuwa nyuma kwa mabao 2-1.
Lakini Mchezaji Bora Duniani, Ronaldo, akawasawazishia na katika dakika za majeruhi, dakika ya 92, Mchezaji wa Timu ya Akiba ambae hajawahi kucheza Kikosi cha kwanza hata mara moja, kijana chipukizi wa miaka 17 Federico Macheda, aliibuka ndie shujaa mpya wa Manchester United pale alipofunga bao tamu sana baada ya kupata pasi murua toka kwa Giggs na kumhadaa beki kisha akapiga shuti lililopinda na kumuacha Kipa wa zamani wa Liverpool Brad Friedel akidaka hewa na kugalagala chini.
Kijana Federico Macheda alishangilia bao hili kwa kukimbia walipokaa familia yake na kumkumbatia Baba yake Mzazi aliekuwa akitokwa machozi kwa furaha.
Refa Mike Riley alimpa Macheda Kadi ya Njano kwa kwenda kwa mashabiki kushangilia.
Kwa ushindi wa leo, Man U wamerudi kileleni wakiwa na pointi 68 kwa mechi 30, Liverpool wa pili pointi 67 mechi 31, wa tatu ni Chelsea mechi 31 na pointi 64 na Arsenal waliocheza mechi 31 pia ni wa nne wakiwa na pointi 58.
Vikosi vilikuwa:
Man Utd: Van der Sar, Neville, O'Shea, Evans, Evra, Nani (Macheda 61), Carrick, Fletcher, Ronaldo, Giggs, Tevez (Welbeck 87).
Akiba hawakucheza: Foster, Park, Gibson, Martin, Eckersley.
Kadi: Macheda.
Goli: Ronaldo 14, 80, Macheda 90.
Aston Villa: Friedel, Luke Young, Cuellar, Davies, Shorey, Milner (Reo-Coker 76), Petrov, Barry, Ashley Young, Carew, Agbonlahor.
Akiba hawakucheza: Guzan, Delfouneso, Knight, Salifou, Gardner, Albrighton.
Kadi: Milner, Ashley Young.
Goli: Carew 30, Agbonlahor 58.
Watazamaji:75,409
Refa: Mike Riley (Yorkshire).
Everton 4 Wigan 0
Everton leo wameikung'uta Wigan mabao 4-0 Uwanjani kwao Goodison Park.
Mabao ya Everton yalifungwa na Jo [ba0 2], Fellaini na Osman.