Saturday, 11 October 2008
Bulgaria v Italy, [Kundi la 8, saa 3:15]
England v Kazakhstan, [Kundi la 6, saa 1:15]
Sweden v Portugal, [Kundi la 1, saa 3:00]
Phil Brown, Meneja wa Hull City, timu iliyopanda daraja msimu huu kuingia LIGI KUU, ameshinda tuzo ya kuwa MENEJA BORA LIGI KUU UINGEREZA kwa mwezi wa Septemba.
Timu ya Phil Brown, Hull City ilianza mwezi Septemba kwa kuwafunga Newcastle 2-1, wakatoka suluhu ya 2-2 na Everton, kisha wakaonyesha maajabu makubwa pale walipowafunga vigogo Arsenal kwa bao 2-1 tena Arsenal wakiwa nyumbani kwao Emirates Stadium.
Jumapili iliyopita, Hull City waliendeleza wimbi la ushindi pale waliposhinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Tottenham.
Tuzo hii ya Meneja Bora wa Mwezi hutolewa na Wadhamini wa LIGI KUU BARCLAYS.
NAE ASHLEY YOUNG APATA TUZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI SEPTEMBA
Winga huyu mwenye miaka 23 alifunga mabao mawili na kuwatengenezea wenzake kufunga mabao mawili kwa mwezi Septemba na kuifanya Timu yake Aston Villa kushinda mechi 3 mfululizo kwa mwezi Septemba.
Ashley Young sasa ameingia orodha ya Wachezaji wachache waliomudu kushinda tuzo hii zaidi ya mara moja. Wengine walioko kwenye orodha hiyo ni Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney na Steven Gerrard.
Friday, 10 October 2008
Klabu ya Chelsea imeishitaki Klabu ya FC Lyn Oslo ya Norway pamoja na aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Klabu hiyo Morgen Andersen kuhusu uhamisho wa Mchezaji Jon Mikel Obi wakidai warudishiwe Pauni Milioni 16 walizolipia uhamisho wake kwa sababu walidanganywa kuwa Mikel Obi alikuwa na mkataba na Klabu hiyo.
Mashtaka haya yanafuatia kupatikana na hatia kwa Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa Klabu hiyo ya Norway,Morgen Andersen, kwenye Mahakama ya Norway kwamba aligushi mikataba kuhusu Mchezaji huyo Jon Mikel Obi.
Mwezi Juni, 2006, Chelsea waliilipa Klabu ya FC Lyn Oslo Pauni Milioni 4 na Manchester United Pauni Milioni 12 kwa ajili ya uhamisho wa Mikel Obi. Wakati huo Jon Mikel Obi alikuwa tayari ameshasaini mkataba kujiunga na Manchester United ingawa baadae Obi aligoma kwenda Man U akidai mapenzi yake yako Chelsea na ndipo Man U wakalifikisha suala hilo FIFA na baadae Chelsea wakakubali kuilipa Man U.
Chelsea imetoa tamko rasmi kuhusu sakata hili kwa kusema: 'Wakati wa uhamisho wa Obi, Chelsea, Lyn na Man U tulikubaliana kulipia malipo ya Pauni Milioni 16 na kwamba huo ndio utakuwa mwisho wa sakata la Mchezaji Obi. Lakini, kwa sababu sasa Mahakama imedhihirisha kwamba kiongozi wa Klabu ya Lyn alidanganya basi sisi tunawadai wao pesa zetu!'
Chelsea ilimalizia tamko hili kwa kusema waziwazi mashtaka yao yanawahusu Klabu ya Lyn na Mkurugenzi Mkuu wao Morgan Andersen pekee na sio Manchester United.
John Terry hakufanya mazoezi ya Timu ya England hapo jana na nafasi yake kwenye mechi hiyo huenda ikachukuliwa na mmoja kati ya Matthew Upson, Wes Brown au Joleon Lescott.
Endapo hatocheza basi Unahodha wakati wa mechi utachukuliwa na Rio Ferdinand ambae ni Naibu Nahodha wa England.
FLETCHER ATEULIWA NAHODHA SCOTLAND
Darren Fletcher amechukua nafasi ya Nahodha wa siku zote Barry Ferguson ambae ameumia enka na Naibu wake Stephen McManus amefungiwa mechi kwa kuwa na adhabu ya kadi.
Darren Fletcher, mwenye umri wa miaka 24, ni mara ya nne kuteuliwa kuwa Nahodha wa Nchi yake Scotland.
Thursday, 9 October 2008
Wednesday, 8 October 2008
Aston Villa watacheza na Ajax na Hamburg wakati Tottenham watakabiliwa na Spartak Moscow na Udinese.
Lakini Manchester City, ambao watacheza na Schalke O4, Paris St Germain, Racing Santander na Timu ya Bosi wa zamani wa England Steve McClaren, FC Twente, ndio wenye mtihani mgumu zaidi.
Kila timu iko kwenye Kundi la Timu 5 na watacheza mechi 2 nyumbani na 2 ugenini na wapinzani tofauti.
Fainali ya UEFA CUP itafanyika mjini Istanbull, Uturuki tarehe 20 Mei 2009.
KUNDI A: Schalke 04 Paris St Germain MANCHESTER CITY Racing Santander FC Twente
KUNDI D: TOTTENHAM Spartak Moscow Udinese Dinamo Zagreb NEC Nijmegen
KUNDI G: Valencia Club Brugge Rosenborg FC Copenhagen Saint-Etienne
Monday, 6 October 2008
Kabinti kachanga kilichozaliwa ndani ya Familia ya Mashabiki wenda wazimu wa Klabu ya Everton iliopo jijini Liverpool huko Uingereza kilijikuta kikibatizwa majina matatu yaliyounganishwa yaani EVA-TONI-ANN na ukiyatamka basi unakuwa unataja EVERTONIAN na hiyo inamaanisha wewe ni Shabiki wa kutupwa wa Klabu ya Everton!
Baba mtoto huyo EVA-TONI-ANN aitwae Danny Pierce amesema hiyo ilikuwa ndoto yake tangu yuko mtoto shuleni alipoapa akipata binti basi atampa majina hayo kuonyesha mapenzi thabiti kwa Timu yake Everton.
Lakini ndoto hiyo haikutimia pale alipozaa watoto wawili wa kike wa kwanza na mkewe Bibi Claire Cooper aligomea jina hilo la Eva-Toni-Ann.
Lakini baada ya kukerwa sana na mumewe, Claire alikiri jina hilo lilianza kumwingia akilini ingawa alikuwa bado halipendi.
Pale alipozaliwa binti huyo mpya ikapigwa kura.
Wakaandika majina tofauti kwenye karatasi na kuvitia vikaratasi hivyo ndani ya kofia likiwemo lile la Eva-Toni-Ann.
Baba mtu Danny akatoa karatasi ndani ya kofia na liliposomwa jina lilikuwa ni Eva-Toni-Ann! Ilipokuja zamu ya Binti yao wa kwanza kuokota karatasi ndani ya kofia hiyo likatoka jina Eva-Toni-Ann!
Mamu mtu nae ilipofika zamu yake jina likawa hilo hilo Eva-Toni-Ann!
Baba wa mtoto huyo Eva-Toni-Ann anakiri kama angezaliwa dume basi angemwita Duncan- akimaanisha Duncan Ferguson aliyekuwa Mchezaji veterani na mahiri wa Everton.
Timu za Taifa za Nchi za Marekani Kusini zinaingia tena dimbani kuanzia Jumamosi hii katika mapambano ya Kundi lao ambalo lina Nchi 10. Mpaka sasa kila Nchi ishacheza mechi 8 na ikifika Jumatano ya tarehe 15 Oktoba 2008 watakuwa wameshavuka nusu ya mechi wanazotakiwa kucheza na hivyo kuleta picha kidogo nani anaweza akaingia FAINALI huko AFRIKA KUSINI mwaka 2010.
Baada ya mechi 8 kwa kila timu, Paraguay yuko kileleni akiwa na pointi 17 akifuatiwa na Brazil mwenye pointi 13 sawa na Argentina na Chile lakini Brazil yuko mbele kwa kufunga magoli mengi. Uruguay ana pointi 12, Colombia 10, Ecuador 9, Venezuela na Peru wana 7 kila mmoja na mkiani yuko Bolivia mwenye 5.
Timu nne za juu za Kundi hili zitaingia moja kwa moja FAINALI huko AFRiKA KUSINI mwaka 2010.
RATIBA:
Jumamosi 11 Oktoba 2008
Bolivia v Peru
Argentina v Uruguay
Colombia v Paraguay
Jumapili 12 Oktoba 2008
Venezuela v Brazil
Ecuador v Chile
Jumanne 14 Oktoba 2008
Bolivia v Uruguay
Jumatano 15 Oktoba 2008
Paraguay v Peru
Chile v Argentina
Venezuela v Ecuador
Brazil v Colombia
Klabu 40 za Ulaya zimegawanywa katika Vikapu vitano na dro itafanyika ili kupata Makundi manane ya timu 5 kila moja. Katika kila Kundi timu moja itacheza mechi 2 nyumbani na 2 ugenini na wapinzani tofauti.
Timu 3 za juu za kila Kundi zitaingia hatua inayofuata ya mtoano itakayojumuisha timu 8 zitakazochukua nafasi ya tatu katika Makundi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
VIKAPU VYA DRO VIMEGAWANYWA IFUATAVYO:
KAPU LA 2: VfB Stuttgart, Ajax, Olympiacos, Deportivo La Coruna, Club Brugge, Spartak Moscow, Paris SG, Heerenveen.
KAPU LA 3: Rosenborg, Udinese, Feyenoord, SC Braga, Slavia Prague, MANCHESTER CITY, Galatasaray, Sampdoria.
Meneja wa England Fabio Capello hakumchagua Michael Owen kwenye kikosi chake cha Wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ya England kitakachocheza mechi za mtoano za Kundi la 6 la Nchi za Ulaya ambalo lina timu za Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra.
Wengi walitegemea Owen ataitwa baada ya kupona lakini ameachwa na badala yake Peter Crouch amechukuliwa.
England Jumamosi inayokuja tarehe 11 Oktoba inacheza na Kazakhstan Uwanja wa nyumbani Wembley na Jumatano tarehe 15 Oktoba 2008 watakuwa ugenini kupambana na Belarus.
Kikosi kamili cha England [kwenye mabano Klabu wanazochezea]:
Timu za Mataifa ya Ulaya siku ya Jumamosi tarehe 11 Oktoba na Jumatano tarehe 15 Oktoba 2008 zitajimwaga viwanja mbalimbali katika mechi za Makundi ya Nchi za Ulaya kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Nchi hizi za Ulaya zimegawanywa Makundi 9 na bingwa wa kila Kundi anaingia moja kwa moja Fainali hizo. Washindi wa pili Wanane Bora kutoka kwenye Makundi hayo 9 watagawanywa mechi 4 za mtoano za nyumbani na ugenini ili kupata timu nyingine nne zitakazoenda Fainali.
Uingereza ambayo ipo Kundi la 6 pamoja na Croatia, Ukraine, Belarus, Kazakhstan na Andorra inaongoza Kundi hilo ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda mechi zake mbili za kwanza ilipozifunga Andorra 2-0 na Croatia 4-1.
Uingereza Jumamosi inacheza na Kazakhstan Uwanja wa nyumbani Wembley na Jumatano watakuwa ugenini kupambana na Belarus.
RATIBA: Jumamosi, 11 Oktoba 2008 [saa zilizotajwa ni zabongo]
Belgium v Armenia, [Kundi la 5, saa 3:45]
Bulgaria v Italy, Kundi la 8, saa 3:15]
Denmark v Malta, [Kundi la 1, saa 3:15]
England v Kazakhstan, Kundi la 6, saa 1:15]
Estonia v Spain, [Kundi la 5, saa 3:45]
Faroe Islands v Austria, [Kundi la 7, saa 12:00]
Finland v Azerbaijan, [Kundi la 4, saa 11:00]
Georgia v Cyprus, [Kundi la 8, saa 1:30]
Germany v Russia, [Kundi la 4, saa 3:45]
Greece v Moldova, [Kundi la 2, saa 3:30]
Holland v Iceland, [Kundi la 9, saa 3:45]
Hungary v Albania, [Kundi la 1, saa 2:45]
Luxembourg v Israel, [Kundi la 2, saa 3:15]
Poland v Czech Republic, [Kundi la 3, 1saa 3:30]
Romania v France, [Kundi la 7, saa 2:15]
San Marino v Slovakia, [Kundi la 3, saa 3:30]
Scotland v Norway, [Kundi la 9, saa 11:00]
Serbia v Lithuania, [Kundi la 7, saa 3:15]
Slovenia v Northern Ireland, [Kundi la 3, saa 3:45]
Sweden v Portugal, [Kundi la 1, saa 3:00]
Switzerland v Latvia, [Kundi la 2, saa 12:45]
Turkey v Bosnia-Herzegovina, [Kundi la 5, saa 3:00]
Ukraine v Croatia, [Kundi la 6, saa 4:00]
Wales v Liechtenstein, [Kundi la 4, saa 1:30]
LIGI KUU UINGEREZA KUSIMAMA KUPISHA KOMBE LA DUNIA WIKIENDI HII!!