RIO AIPONDA FIFA KWA KUPUUZIA UBAGUZI WA RANGI VIWANJANI
Staa wa Manchester United na Naibu Nahodha wa Timu ya England, Rio Ferdinand, ameishutumu vikali FIFA kwa kutokuwa na msimamo thabiti wa kutokomeza ubaguzi wa rangi hasa kwenye mechi za soka.
Rio alisema FIFA imekuwa ikizipiga faini hafifu Nchi na Klabu zenye Mashabiki Wabaguzi lakini haiendi mbali zaidi kwa kuchukua hatua kali za kuwafungia au kupiga marufuku Wabaguzi kuingia michezoni.
Hivi karibuni Mchezaji wa England Emily Heskey aliletewa vituko vya kibaguzi huko Zagreb, Croatia wakati England ilipoifunga Croatia 4-1 kwenye mechi ya mtoano wa Kombe la Dunia na FIFA ikaipiga faini Croatia na kuipa onyo kali.
Vilevile huko Uingereza, kwenye Uwanja wa Fratton Park nyumbani kwa Portsmouth, Mchezaji Sol Campbell wa Portsmouth aliletewa vituko vya kibaguzi na Washabiki wa Tottenham kwenye mechi ya LIGI KUU ambayo Tottenham ilifungwa 2-0.
Sol Campbell aliwahi kuichezea Tottenham huko nyuma. Suala hili lipo kwenye uchunguzi wa Polisi.
No comments:
Post a Comment