Friday, 16 May 2008


MENEJA WA CHELSEA AVRAM GRANT MATATANI!!!!!!!


AVRAM GRANT leo ametakiwa na CHAMA CHA SOKA UINGEREZA kujieleza kufuatia kauli yake ya jana kwamba: 'Uingereza kuna Marefa wazuri ila kuna wachache ambao unaweza ukawarubuni, kama mlivyoona. Nadhani katkia mechi yetu OLD TRAFFORD Refa MIKE DEAN alihakikisha ushindi.Tunajua hilo. Ile KADI NYEKUNDU kwa MIKEL OBI haikustahili. [MECHI HIYO MAN 2 CHELSEA 0].

Nadhani PAUL SCHOLES angepewa KADI NYEKUNDU katika mechi ya WIGAN na WIGAN walistahili kupewa penalti. Lakini yote yamekwisha na nawapongeza MAN U'.


Nae, SIR ALEX FERGUSON, alijibu mapigo kwa kupuuza kauli hizo. Alisema: 'Hata sisi msimu huu hatukupata maamuzi mengi tuliyostahili. Kauli za AVRAM GRANT zinalenga mechi ya Jumatano na ndio maana anabwabwaja hivyo!!'


Ferguson akaendelea: 'Naweza kusema zaidi kuhusu uamuzi lakini yote yanaweza kuzua mjadala. Sisi tunaamini hatukupata maamuzi mengi kwetu. Na pengine kama tungepata tungeenda Chelsea tayari tuko MABINGWA lakini yote yamepita na msimu umekwisha'.


SAMMY LEE ARUDI LIVERPOOL!!!
Mchezaji nyota wa zamani wa LIVERPOOL, SAMMY LEE, amerudi tena LIVERPOOL na kuteuliwa kuwa MENEJA MSAIDIZI chini ya uongozi wa MENEJA wa sasa RAFAEL BENITEZ.
SAMMY LEE alikuwa kiungo nyota na mahiri wa timu ya LIVERPOOL iliyong'ara na kuwika katika miaka ya 1980.
Baada ya kustaafu uchezaji hapo LIVERPOOL, SAMMY LEE aliteuliwa kwenye timu hiyohiyo kuwa MENEJA wa TIMU YA AKIBA na baadae akafanya kazi chini ya MAMENEJA waliofuatia wa LIVERPOOL, GRAEME SOUNESS na GERARD HOULLIER.
Mwaka 2004, alifanya kazi kama mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya UINGEREZA na kisha 2005 alienda BOLTON kuwa msaidizi wa SAM ALLARDICE.
=====================================================================

FAINALI YA KOMBE LA F.A

JUMAMOSI, 17 MEI 2008=

PORTSMOUTH vs CARDIFF CITY
saa 11 jioni [bongo time]

Kesho ndio fainali ya 'vibonde' itakayochezwa WEMBLEY STADIUM ikizikutanisha timu ambazo si vigogo!
Wengi wanawajua wachezaji wa Portsmouth kwani wanawaona mara kwa mara katika mechi za LIGI KUU.
Wachezaji hao kama Kanu, Sule Muntari, Sol Campbell, David James n.k wanategemewa kushuka uwanjani kwa timu ya Portsmouth.
Jermaine Defoe ambae alitokea Tottenham Hotspurs mwanzoni mwa mwaka haruhusiwi kuichezea Potsmouth katika fainali hii kwani alishacheza mechi za F.A msimu huu akiwa na SPURS.
Wachezaji wa CARDIFF CITY ambao ni maarufu kwetu bila shaka watakuwa ni maveterani ROBBIE FOWLER na JIMMY FLOYD HASSELBAINK.
REFA KATIKA PAMBANI HILO ATAKUWA MIKE DEAN.
MIKE DEAN amechezesha mechi 28 za LIGI KUU msimu huu na ametoa KADI NYEKUNDU 9 na za NJANO 106.
================================================================================

Thursday, 15 May 2008




Portsmouth v Cardiff
FA CUP FINAL


UWANJA: Wembley Stadium


SIKU: JUMAMOSI, 17 May SAA: 11 JIONI [saa za bongo]


Fainali ya FA CUP ni Jumamosi hii ambapo inazikutanisha timu ambazo si vigogo. Portsmouth hivi juzi ilimaliza LIGI KUU UINGEREZA ikiwa nafasi ya 8 wakati CARDIFF walimaliza nafasi ya 12 katika ligi ya chini ya LIGI KUU iitwayo COCA COLA CHAMPIONSHIP.


XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX




RIO FERDINAND ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED.





Mchezaji ambae ni nguzo ya safu ya ulinzi ya MABINGWA WA UINGEREZA, MAN U, Rio Ferdinand [miaka 29], ametia sahihi mkataba mpya wa miaka 5.


Sambamba na Rio, Wes Brown, mlinzi alieng'ara na aliemudu vyema nafasi ya nahodha Garry Neville ambae alikuwa majeruhi karibu msimu wote, nae ametia saini mkataba.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx




RANGERS [SCOTLAND] 0 ZENIT ST PETERSBURG 2!


Timu ya ZENIT YA URUSI imenyakua Kombe la UEFA hapo jana baada ya kuifunga RANGERS YA SCOTLAND mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa UWANJA WA MANCHESTER CITY uitwao CITY OF MANCHESTER STADIUM.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RONALDO NA MENEJA WAKE, SIR ALEX FERGUSON WAPATA TUZO ZA JUU!!!

Ronaldo ameshinda tuzo ya MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU UINGEREZA na pia amenyakua KIATU CHA DHAHABU baada ya kuwa MFUNGAJI BORA katika ligi hiyo baada ya kupachika jumla ya mabao 31.
Hii ni mara ya kwanza tangu miaka 12 iliyopita kwa mcheza ji kufunga zaidi ya mabao 30 wakati ALAN SHEARER, akichezea BLACKBURN wakati huo nae alipofunga magoli 31.
NAE ALEX FERGUSON AMENYAKUA TUZO YA MENEJA BORA WA MSIMU HII IKIWA NI MARA YA 8 KWAKE.
FERGUSON ameshatwaa UBINGWA WA LIGI KUU MARA 10 na KOMBE LA FA MARA 5,.
************************************************************************************************
TIMU YA TATU KUPANDA LIGI KUU UINGEREZA
HULL CITY 4 WATFORD 1

Timu ya HULL CITY itapambana na BRISTOL CITY katika fainali itakayoamua timu ipi itaungana na WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY kupanda daraja na kwenda LIGI KUU UINGEREZA.
HULL CITY, hapo jana, iliifunga WATFORD mabao 4-1. Katika mechi ya kwanza HULL CITY ilishinda mabao 2-0.


Wednesday, 14 May 2008




BAADA YA MAN UNITED KUTWAA UBINGWA UINGEREZA, SIR ALEX FERGUSON ASHINDA TUZO YA MENEJA BORA WA MSIMU!






=====================================================================================
TIMU IPI ITAKUWA YA TATU KUPANDA DARAJA KUINGIA LIGI KUU?
Wakati WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY zimeshapanda daraja na kuingia LIGI KUU UINGEREZA kuchukua nafasi ya READING, BIRMINGHAM na DERBY zilizoshuka daraja, timu ya tatu itakayopanda daraja itajulikana baada ya kumalizika mtoano maalum kupata timu hiyo ambao kwa sasa unaendelea.
Katika mechi za kwanza za mtoano huo, HULL CITY 2 WATFORD 0 [Mechi ya marudiano leo usiku].
Timu ya BRISTOL CITY meshaingia fainali baada ya kuitoa CRYSTAL PALACE jumla ya bao 4-2.
MSHINDI KATI YA HULL CITY na WATFORD atapambana FAINALI NA BRISTOL CITY ili kupata timu ya tatu itakayopanda daraja.
*******************************************************************************************









Powered By Blogger