Friday 16 May 2008


MENEJA WA CHELSEA AVRAM GRANT MATATANI!!!!!!!


AVRAM GRANT leo ametakiwa na CHAMA CHA SOKA UINGEREZA kujieleza kufuatia kauli yake ya jana kwamba: 'Uingereza kuna Marefa wazuri ila kuna wachache ambao unaweza ukawarubuni, kama mlivyoona. Nadhani katkia mechi yetu OLD TRAFFORD Refa MIKE DEAN alihakikisha ushindi.Tunajua hilo. Ile KADI NYEKUNDU kwa MIKEL OBI haikustahili. [MECHI HIYO MAN 2 CHELSEA 0].

Nadhani PAUL SCHOLES angepewa KADI NYEKUNDU katika mechi ya WIGAN na WIGAN walistahili kupewa penalti. Lakini yote yamekwisha na nawapongeza MAN U'.


Nae, SIR ALEX FERGUSON, alijibu mapigo kwa kupuuza kauli hizo. Alisema: 'Hata sisi msimu huu hatukupata maamuzi mengi tuliyostahili. Kauli za AVRAM GRANT zinalenga mechi ya Jumatano na ndio maana anabwabwaja hivyo!!'


Ferguson akaendelea: 'Naweza kusema zaidi kuhusu uamuzi lakini yote yanaweza kuzua mjadala. Sisi tunaamini hatukupata maamuzi mengi kwetu. Na pengine kama tungepata tungeenda Chelsea tayari tuko MABINGWA lakini yote yamepita na msimu umekwisha'.


No comments:

Powered By Blogger