Saturday 4 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Kocha Algeria ajiuzulu!
• Ni siku moja tu baada ya kwenda sare na Bongo!!!
Kocha wa Timu ya Taifa ya Algeria, Rabah Saadane, amejiuzulu wadhifa wake ikiwa ni siku moja tu baada ya kutoka sare 1-1 na Tanzania huko Algiers katika mechi ya Makundi kugombea kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Africa 2012.
Saadane alishika Ukocha Miaka mitatu iliyopita na aliiwezesha Algeria kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwezi Juni ikiwa ni mara yao ya kwanza baada ya Miaka 24.
Shirikisho la Soka la Algeria limetaja kujiuzulu kwa Saadane ni kutokana na matokeo ya jana na wao wamekubali matakwa yake.
CHEKI: www.sokainbongo.com

FRANCE: Jahazi latota!
• Kocha Blanc anung’unika hana Wapiga Mabao!!
Kocha wa Ufaransa, Laurent Blanc, ambae jana alisimamia Nchi hiyo kwa mara ya kwanza katika Mashindano rasmi na kuaibishwa kwa kuchapwa bao 1-0 nyumbani na Belarus kwenye Mechi ya Makundi kuwania kuingia Fainali za EURO 2012, amenung’unika na kusikitikia kutokuwa na Wachezaji wenye uwezo wa kufunga.
Kipigo hicho cha Belarus kimeendeleza maafa kwa Ufaransa ya toka huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambazo France ilitupwa nje Raundi ya Kwanza kwa kushika mkia Kundi lao na pia Timu kukumbwa na Skandali la ugomvi kambini, mgomo wa Wachezaji, kufukuzwa kwa Nicolas Anelka na hivi juzi sakata hilo likazaa kufungiwa baadhi ya Wachezaji.
Baada ya mechi ya jana, Blanc alisema: “Hatuwezi kusema tunao Wachezaji wanaojua kufunga. Tunao Wachezaji wanaojua kumiliki mpira lakini hatuna wale wenye kuleta mafanikio katika Mita 25 za mwisho.”
Hata hivyo, Banc amekiri Wachezaji wake wana morali ndogo kufuatia maafa ya Kombe la Dunia na Skandali lililofuata baada ya hapo.
Jumanne, Septemba 7, Ufaransa itasafiri kwenda kucheza na Bosnia kwenye mechi ya pili ya Makundi ya EURO 2012 huku Mastraika wake watatu wakiwa majeruhi.
Wachezaji hao ni Louis Saha, Loic Remy na Karim Benzema.
FIFA yageuka!
FIFA imefungua milango wazi kwa Wanachama wake, yaani Vyama vya Soka vya Nchi, kutumia ushahidi wa mikanda ya video ili kupata ushahidi na kuwahukumu Wachezaji wanaovunja sheria kwa kumhadaa Refa ili kupata penalti au kupata maamuzi yanayowafaa.
Miaka miwili iliyopita SFA, Chama cha Soka cha Scotland, kilitoa pendekezo la kutumia video lakini FIFA ikalipinga hilo kwa kutamka kuwa sheria zilizokuwepo halikubali hilo na kwamba uamuzi wa Refa ni wa mwisho.
Lakini, katika uamuzi uliofungua milango, FIFA imekiruhusu Chama cha Soka huko Australia kuwafungia Wachezaji wawili waliojiangusha kwa kusudi na kupata penalti na baadae ushahidi wa video ulionyesha walidanganya.
Huko Ulaya, UEFA tayari ilishatumia video kumhukumu Mchezaji aliemhadaa Refa na kupata penalti na baada ya mechi hiyo Mchezaji huyo, ambae alikuwa Eduardo wa Arsenal, akafungiwa mechi.
TEMBELEA: www.sokainbongo.com

Mechi za Yanga v Simba kutoonekana Dar!
Baada ya Serikali kuufunga Uwanja wa Uhuru kwa matengenezo na kugomea Uwanja wa Taifa kutumika na uamuzi wa Simba kuutumia Uwanja wa CCM Kirumba huko Mwanza, Mashabiki wa Magwiji hao wa Soka Tanzania wa Jijini Dar es Salaam watazikosa Mechi za Yanga v Simba Mwaka huu.
Oktoba 16, kwenye Ligi Kuu Vodacom, ni pambano la Simba v Yanga, na kwa vile Simba ndio wameteuliwa Wenyeji, pambano hilo litachezwa ‘nyumbani’ kwa Simba huko CCM Kirumba.
Hivyo Mashabiki wa Dar itabidi wangoje hadi Mwakani waone pambano la Yanga na Simba la marudiano.
Wakati Simba wameshatangaza Uwanja wa nyumbani na kubarikiwa na TFF, Yanga bado hawajasema ‘nyumbani’ ni wapi ingawa inasadikiwa itakuwa ni Uwanja wa Jamhuri huko Morogoro au Sheikh Amri Abeid huko Arusha.
Mfungaji ‘Hetriki’ Defoe amsifia Rooney
• Gwiji Wright ampongeza Defoe!
Mfungaji wa bao 3, Jermaine Defoe, aliepachika bao hizo hapo jana Uwanjani Wembley katika ushindi wa 4-0 wa England dhidi ya Bulgaria kwenye pambano la EURO 2012, amemsifia Wayne Rooney ambae ndie alikuwa mpishi mkuu wa bao zote 4 za England.
Defoe amekuwa Mchezaji wa kwanza wa England kufunga bao 3, ‘hetriki’, Uwanjani Wembley tangu ufunguliwe baada ya kujengwa upya na hivyo kufanya magoli yake kwa England kuwa 15 katika Mechi 44.
Mchezaji wa mwisho wa England kufunga bao 3 Uwanjani Wembley ni Alan Shearer Mwaka 1999 katika Mechi ya England na Luxemborg.
Defoe, ambae nusura aikose mechi kama asingeahirisha kufanyiwa operesheni ya nyonga, amefurahia mafanikio yake kwa kutamka: “Ni ngumu kuelezea furaha yangu…..huu ni usiku mtamu katika maisha yangu ya Soka! Ukicheza na Mchezaji Bora Rooney na ukiwa mjanja kuingia kwenye nafasi basi atakupata tu kwa pasi murua! Baada ya kufunga bao la pili, Rooney aliniambia ‘nenda kafunge la 3’! Kuambiwa hivyo na Mchezaji mahiri ni kitu poa sana!”
Defoe alitoboa pia kuwa kabla ya mechi aliambiwa na Gwiji la zamani la Arsenal na England, Ian Wright, kwamba wakati wake kufunga bao 3 umefika na baada ya mechi Wright alimtumia Defoe ujumbe wa simu uliosema: “Nakupenda JD, hongera kwa kazi njema!”
Wenger apona rungu la FA
Chama cha Soka England, FA, kimeamua kutomchukulia Arsene Wenger hatua yeyote kwa madai yake Stoke City ni Wacheza Raga kufuatia malalamiko rasmi ya Stoke City.
Meneja huyo wa Arsenal, akionyesha bado kukerwa na Mchezaji wa Stoke Ryan Shawcross kumvunja mguu Chipukizi wa Arsenal Aaron Ramsey mapema Mwaka huu, aliwafananisha Stoke na Wacheza Raga kwa uchezaji wao katika mechi na Tottenham ya Ligi Kuu Mwezi uliokwisha waliyofungwa 2-1.
Kauli hizo za Wenger zilimkera Meneja wa Stoke, Tony Pulis, alielalamika: “Tumesikitishwa na kauli ya Wenger. Haikustahili hata kidogo.”
Pulis, akihojiwa zaidi kuwa anaonaje pengine kumtaja Shawcross katika mechi na Tottenham huku Refa akiwa Chris Foy ambae ndie alichezesha pambano hilo na pia atachezesha la Blackburn na Arsenal ilikuwa mbinu ya Wenger ili wapate imani ya Refa huyo katika mechi yao na Blackburn, Pulis alijibu: “Ni wewe umesema kuwa alitaka kumrubuni Refa awasaidie na mimi nakubaliana na wewe!”
Pulis akaongeza: “Yeye ana uhuru wa kusema atakalo. Sisi tumepigana Vita Kuu mbili za Dunia kulinda uhuru huo! Lakini kile alichosema kuhusu Shawcross ni kitu kibaya na sisi tutamshitaki.”
Hata hivyo, FA imeamua kuwa kwa vile Wenger hakumtaja Refa Foy kwa jina na alikuwa akitoa maoni yake kwa ujumla hana kesi yeyote ya kujibu.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Algeria 1 Tanzania 1
Wakicheza ugenini, Uwanja wa Moustapha Tchaker huko Algiers, Taifa Stars ilienda sare ya 1-1 na Algeria, iliyosheheni Wachezaji toka Ligi za Ulaya, katika mechi ya kwanza ya Kundi lao ili kuwania kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za Mwaka 2012.
Taifa Stars walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 33 kupitia Abdi Kassim ambae frikiki yake kali ilitinga kimiani.
Lakini Algeria, wakiongozwa na Masupastaa wa Ulaya, Hasan Yebda, Ziaya na wengineo, walisawazisha dakika ya 45 Mfungaji akiwa Adlene Guedioura.
Mechi inayofuata kwa Taifa Stars ni ya ugenini pia huko Morocco Oktoba 7.
CHEKI: www.sokainbongo.com

England yaichapa Bulgaria 4-0
• Rooney apika goli zote!
England imeanza kampeni yao ya kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa huko Poland na Ukraine kwa pamoja Mwaka 2012 kwa kuibamiza Bulgaria mabao 4-0 Uwanjani Wembley Jijini London katika Mechi ya Kundi G huku Jermaine akipachika bao 3 na Wayne Rooney kuzipika bao zote 4.
Jermaine Defoe alifunga mabao yake matatu dakika ya 3, 61 na 86.
Adam Johnson, alieingia kipindi cha pili badala ya Theo Walcott, alifunga bao lake dakika ya 83.
Katika Mechi nyingine ya Kundi G, Montenegro iliifunga Wales 1-0.
Mechi inayofuata kwa England ni Jumanne, Septemba 7 watakaposafiri kwenda kupambana na Timu ngumu Uswisi.
Vikosi vilivyoanza:
ENGLAND: Hart, G Johnson, Dawson, Jagielka, A Cole, Walcott, Milner, Barry, Gerrard, Defoe, Rooney.
BULGARIA: Mihailov, Ivanov, Milanov, Manolev, Iliyan Stoyanov, Yankov, Angelov, Stiliyan Petrov, Martin Petrov, Bojinov, Popov.
REFA: Viktor Kassai [Hungary]
VIGOGO WOTE ULAYA WASHINDA, FRANCE………!!!!
Wakati Vigogo wote wa Ulaya wakishinda mechi zao za kwanza za kuwania kuingia Fainali za EURO 2012, Ufaransa bado ni hali ile ile ya Kombe la Dunia walipofungwa nyumbani na Belarus kwa bao 1-0.
Bao la ushindi kwa Belarus lilifungwa dakika ya 86 na Kislyak.
EURO 2012 MATOKEO KAMILI:
Ijumaa, 3 Septemba 2010
Armenia 0 v Rep of Ireland 1
Kazakhstan 0 v Turkey 3
Andorra 0 v Russia 2
Moldova 2 v Finland 0
Faroe Islands 0 v Serbia 3
Montenegro 1 v Wales 0
Latvia 0 v Croatia 3
Romania 1 v Albania 1
Sweden 2 v Hungary 0
Lithuania 0 v Scotland 0
Luxembourg 0 v Bosnia-Hercegovina 3
Estonia 1 v Italy 2
Slovakia 1 v FYR Macedonia 0
Belgium 0 v Germany 1
Greece 1 v Georgia 1
Liechtenstein 0 v Spain 4
San Marino 0 v Netherlands 5
Slovenia 0 v Northern Ireland 1
England 4 v Bulgaria 0
France 0 v Belarus 1
Iceland 1 v Norway 2
Portugal 4 v Cyprus 4

Friday 3 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Houllier kutua Villa?
Kocha wa zamani wa Liverpool, Mfaransa Gerrard Houllier, Miaka 63, amefanyiwa usaili na Mmiliki wa Aston Villa, Randy Lerner, na kuna kila dalili mwenye mali huyo kutoka Marekani ameridhishwa na Houllier na huenda akamuajiri kuchukua nafasi ya Umeneja iliyoachwa wazi na Martin O’Neill aliyetimka ghafla Wiki mbili zilizopita.
Houllier aliondoka Liverpool Miaka 6 iliyopita na amekuwa Mwajiriwa wa FFF, Chama cha Soka Ufaransa, kama Mkurugenzi wa Ufundi tangu aondoke kuiongoza Klabu ya Lyon.
Alipokuwa na Liverpool, Houllier aliiwezesha Klabu hiyo itwae Vikombe vitatu kwa mpigo-UEFA Cup, FA Cup na LEAGUE Cup-Mwaka 2001.
Wengine waliofanyiwa usaili na Mmiliki wa Villa ni Bosi wa zamani wa West Ham Alan Curbishley na Kaimu Meneja wa sasa wa Aston Villa Kevin MacDonald lakini Houllier ndie anaetajwa kuwa ana nafasi kubwa kupewa Umeneja.
‘Vijeba’ kuipaisha Chelsea!
Frank Lampard anaamini kuwa Chelsea, iliyoanza Ligi Kuu Msimu huu kwa kishindo cha kushinda Mechi zake 3 kwa jumla ya mabao 14-0, itawika tena mbali ya kuwa na Wachezaji ‘vijeba’.
Lampard amewaponda Watu wanaodai Wachezaji wengi Chelsea ni ‘vijeba’ na yeye amedai wao watawaonyesha uwezo wao kwa kutetea vyema Ubingwa wao.
Chelsea wameanza Msimu huu wa Ligi Kuu kwa kuzishindilia West Bromwich Albion na Wigan Athletic bao 6-0 kila moja na kuipiga Stoke City 2-0.
‘Vijeba’ wanaotajwa kwenye Timu hiyo ni Lampard, Miaka 32, John Terry, Miaka 29, na Didier Drogba, atakaetimiza Miaka 33 Mwezi Machi mwakani.
Lampard amesema: “Ni upuuzi kusikia ati tumekwisha, ni wazee tumebakisha mwaka tu....kauli hizo zimeendela Mwaka na kitu sasa! Tizama Watu wamekuwa wakimsifia Paul Scholes na hizo sifa ni za kweli kwani leo ukimwondoa, Man United lazima watataka kumpata Mtu kama yeye lakini hawataweza kumpata mwenye uwezo kama yeye!”
CHEKI: www.sokainbongo.com

England bila Mastaa maarufu kuivaa Bulgaria leo!
• Bulgaria kumchokoza Rooney apande munkari?
England leo inaingia Uwanja wa nyumbani Wembley Jijini London kuivaa Bulgaria katika mechi ya kwanza ya Kundi G ili kuwania nafasi ya kucheza Fainali za EURO 2012 huko Poland na Ukraine, Nchi mbili Wenyeji kwa pamoja, Mwaka 2012.
Lakini England inayoingia leo Wembley ni tofauti na ile England iliyokuwa huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kutolewa Raundi ya Pili na Ujerumani kwa kubamizwa 4-1.
Mbali ya majeruhi kadhaa ambao hawakuteuliwa kwenye mechi hii, Wachezaji wengine wamejitoa tayari wakiwa kambini kama vile Kipa Scott Carson wa West Bromwich aliejitoa baada ya kupata msiba kwenye Familia.
Hivyo, imebidi Kocha Fabio Capello amwite Kipa wa Timu ya Vijana wa Chini ya Miaka 21, Scott Loach, kuziba nafasi yake.
Pia Straika Peter Crouch ameondoka baada ya kushindwa kupona tatizo la mgongo.
Wengine ambao waliachwa tangu awali ni John Terry na Frank Lampard, ambao ni majeruhi, David James na Ledley King, ambao wameachwa tu kwa sababu ya viwango, na Jamie Carragher ambae amestaafu kwa mara ya pili sasa.
Wadau wengi wataikodolea macho nafasi ya Masentahafu kwani kwenye mechi hii, Jagelka wa Everton na Matthew Upson wa West Ham, ndio wanaotegemewa kucheza pamoja na hawa hawajahi kucheza pamoja hata mara moja.
Ingawa Capello analijua hilo lakini ameonyesha kutokuwa na wasiwasi pale aliposema Mafulbeki wake Glen Johnson na Ashley Cole watakuwepo kuwasaidia Masentahafu hao.
Pia Capello amedokeza Kikosi chake kwa kuwataja baadhi kama vile Kipa Joe Hart, Wayne Rooney, Steve Gerrard, Gareth Barry, Ashley Cole, Glen Johnson na Jagielka.
Wakati huohuo, Kocha wa Bulgaria, Stanimir Stoilov amesisitiza Bulgaria haitamwinda Wayne Rooney ili kumchokoza ili apandishe hasira ingawa amemtaka Refa wa mechi hiyo kutoka Hungary, Viktor Kassai, awe anazichunga hasira za Rooney.
Wadau, licha ya kushangazwa na kauli ya Stoilov, wamechukulia hilo kama vita ya kisaikolojia.
Carragher: ‘Ubingwa Liverpool hamna!’
• Kesho mechi yake ya kumuenzi Liverpool
Huku kesho akiwa ameandaliwa Mechi maalum kuuenzi utumishi wake Liverpool, Beki Mkongwe wa Liverpool, Jamie Carragher, ameungama kuwa Msimu huu Liverpool haina ubavu wa kuchukua Taji la Ligi Kuu England na badala yake ni bora wapiganie Vikombe tu kama vile Carling Cup na FA Cup.
Msimu uliokwisha Liverpool ilimaliza ikiwa nafasi ya 7 na hiyo ni nafasi ya chini kabisa kwao kumaliza Ligi Kuu tangu ianzishwe.
Carragher, ambae hajawahi kuichezea Klabu yeyote nyingine mbali ya Liverpool na pia hajawahi kuwa Bingwa wa Ligi Kuu, amekiri ni ngumu kwao kushindana na Vigogo kama Chelsea na Manchester United na hata Manchester City, ambao utajiri wao umewafanya walundike Mastaa kibao.
Jumamosi hii, huko Anfield, itafanyika mechi maalum ili kuenzi utumishi wa Jamie Carragher kwa Klabu ya Liverpool kwa kucheza na Kombaini ya Everton, Klabu nyingine kubwa Jijini Liverpool ambao ni Mahasimu wakubwa.
Inategemewa Mastaa wa zamani wa Liverpool, kina Michael Owen, Danny Murphy, Jerzy Dudek, Luis Garcia na Emile Heskey, watavaa tena Jezi za Liverpool pamoja na Carragher katika mechi hiyo.
Kuhusu Michael Owen kurudi tena Liverpool baada ya ‘kuisaliti’ na kwenda kwa Wapinzani wao wa Jadi, Manchester United, Carragher ametamka: “Sidhani kama hilo litawakera Washabiki. Owen ametoa mchango mkubwa kwa Liverpool na aliondoka hapa kwenda Real Madrid huku Mkataba wake ukikaribia kwisha. Alijiunga Man United wakati akiwa na shida ya kujifufua kiuchezaji hivyo yeye kuikataa nafasi kubwa ya kujiunga Klabu kubwa Man United ungekuwa ujinga.”
Carragher pia akafananisha ujio wa Owen kama ule wa Gwiji la Man United, Sir Bobby Charlton, ambae alivaa Jezi ya Liverpool katika mechi ya kumuenzi Mchezaji Mahiri wa Liverpool Tommy Smith na akasema hadhani kwa Owen kuvaa tena Jezi ya Liverpool ni mbaya zaidi ya Bobby Charlton, ambae ni Man United damu ile mbaya, alievaa Jezi hiyo katika tamasha hilo maalum.

Thursday 2 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello apuuza lawama
Kocha wa England Fabio Capello, huku akikabiliwa na mtihani mgumu hapo kesho wakati England itakapocheza na Bulgaria Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya Kundi G ili kufuzu Fainali za EURO 2012, amedai hana presha yeyote.
Baada ya kufanya kinyume cha matarajio ya wadau wengi huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Capello amekuwa akilaumiwa lakini Mtaliana huyo amekiri lawama hizo ni sehemu ya kazi yake na amesema: “Hiyo ni sehemu ya kazi ya Meneja. Ukishinda, wewe ni bora. Ukifungwa, wewe hufai!”
Hata hivyo, Capello ametoboa kuwa amejifunza toka yale yaliyotokea huko Afrika Kusini na hivyo amebadilika kidogo.
Kuhusu Bulgaria, Capello ametamka: “Bulgaria sio Timu rahisi kwani uwezo wao kiufundi ni mkubwa na wanajihami kwa kutumia Watu 9 na kushambulia kwa kustukiza na kasi kubwa. Lakini, ni lazima tushinde, inabidi tucheze vizuri na tunaomba Mashabiki watusapoti wakati wa mechi.”
CHEKI: www.sokainbongo.com

Petrov aikandya England!
• ‘Ni Wachezaji wazuri, ila si Timu!’
Petrov, anaechezea Klabu ya Bolton na pia Timu ya Taifa ya Bulgaria ambayo kesho inapambana na England Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya Kundi G kuwania kuingia Fainali za EURO 2018, amedai England ina Wachezaji wazuri lakini si Timu chini ya Mtaliana Fabio Capello.
England haikufanya vizuri kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na ilinyukwa 4-1 na Germany na kwabagwa nje Raundi ya Pili na matokeo hayo yaliwafanya baadhi ya Mashabiki kwazomea Wachezaji wa England walipocheza Mechi ya kirafiki Uwanjani Wembley dhidi ya Hungary Mwezi uliopita.
Petrov amenena: “Kila mtu anajua England ina majina na Wachezaji wazuri sana. Lakini sidhani wana Timu. Sijui kwanini. Hawafanyi lolote. Ni wakati mgumu kwa England.”
Bulgaria itaingia Uwanjani bila ya Nyota wao Dimitar Berbatov wa Manchester United ambae alitangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa Mwezi Mei.
Mourinho: ‘Mimi si Mchawi!’
Jose Mourinho, maarufu kama ‘Mtu spesheli’, amesema yeye si mchawi na hivyo Watu wasitegemee vimbwanga kila Mechi na ametoa kauli hiyo baada ya Timu yake Real Madrid kutoka sare 0-0 na Real Mallorca huku Wapinzani wao Barcelona wakimchapa Real Santander 3-0 katika Mechi za ufunguzi za La Liga wikiendi iliyokwisha.
Hata hivyo, Mourinho amejigamba kuwa yeye ndio anastahili kuwa Kocha wa Real kwani ataleta utulivu na mafanikio.
Mourinho alitamka: “Mie si Harry Porter [Akiitaja Filamu maarufu]. Yeye ni Mchawi. Ukweli hamna uchawi. Uchawi ni hadithi tu na mimi naishi kwenye Soka ambalo ni ukweli tu!”
Mourinho ametua Real Madrid baada ya mafanikio makubwa na Inter Milan Msimu uliopita alipoiwezesha kutwaa Mataji Matatu makubwa-Ubingwa wa Italia, Kombe la Italia na Ubingwa wa Ulaya- na sasa jukumu lake huko Spain ni kuipora Barcelona Ubingwa wa La Liga ambao wameuchukua mara mbili mfululizo na pia kufanya vizuri kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambako wameshindwa kuvuka hatua ya Robo Fainali tangu 2004.
Mourinho amejigamba kuwa yeye haogopi kufukuzwa Real kwani ana uhakika siku ya pili tu atapata Timu nyingine.
CHEKI: www.sokainbongo.com

VIKOSI WACHEZAJI 25: Majina 25 Kila Timu yatangazwa!!
• Hargreaves ndani Man United!!
Jana kila Timu ya Ligi Kuu England, ikiwa siku ya mwisho ya usajili wa Vikosi vya Wachezaji 25, iliwasilisha kwa Wasimamizi wa Ligi Kuu Listi zao na Klabu ya Tottenham imemwacha Difenda mahiri Jonathan Woodgate huku Manchester United ikimteua Owen Hargreaves kuwa mmoja wa Wachezaji wao.
Woodgate na Hargreaves ni majeruhi wa muda mrefu.
Woodgate alionekana uwanjani mara ya mwisho Novemba 2009 na Hargreaves amecheza mechi moja tu katika Miaka miwili iliyopita baada ya kupasuliwa magoti yake yote mawili huko Marekani.
Katika Listi ya Arsenal hakuna hata Mwingereza mmoja mbali ya Theo Walcott na Jack Wilshere ambao ingawa hawapo Kikosini ila ni ruksa kucheza kwa kuwa wapo chini ya Umri wa Miaka 21.
Sheria mpya za Ligi Kuu zimeitaka kila Klabu iwasilishwe Majina ya Wachezaji 25 kabla ya Saa 1 usiku, saa za bongo, Septemba 1 na ndani ya Wachezaji hao 25, wanane ni lazima wawe ‘wamelelewa’ nyumbani, ikimaanisha ni lazima wawe wamesajiliwa England au Wales na kukaa kwa Miaka mitatu kwenye Klabu zao kabla hawajatimiza Miaka 21.
Lakini Klabu zimepewa uhuru kuchezesha idadi ya zaidi ya Wachezaji 25 ikiwa tu Wachezaji hao wa ziada wako chini ya umri wa Miaka 21 [Mchezaji anahesabiwa hajatimiza Miaka 21 ikiwa Januari 1 ya Mwaka wa Msimu anaocheza hajafikisha umri huo].
Arsenal wameitumia Sheria hiyo kwa kusajili Kikosi cha Wachezaji 20 tu badala ya 25 huku 7 wakiwa ni wale ‘waliolelewa’ nyumbani na 13 ni wale ‘vijeba’ huku Chipukizi Theo Walcott na Jack Shilshere, licha ya kutosajiliwa rasmi katika Kikosi, wako huru kuichezea Arsenal kwa vile hawajatimiza Miaka 21.
Nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas, amesajiliwa kama mmoja wa Wachezaji 7 ‘waliolelewa’ nyumbani kwa vile alikuwepo hapo kwa zaidi ya Miaka mitatu kabla hajatimiza Miaka 21.
Vikosi kamili vya TIMU VIGOGO:
Arsenal [Wachezaji 20]
WALIOLELEWA NYUMBANI:
-Nicklas Bendtner
-Denilson
-Johan Djourou
-Cesc Fabregas
-Vito Mannone
-Gael Clichy
-Alex Song
WENGINEO:
-Manuel Almunia
-Andrey Arshavin
-Marouane Chamakh
-Abou Diaby
-Emmanuel Eboue
-Lukasz Fabianski
-Laurent Koscielny
-Samir Nasri
-Tomas Rosicky
-Bacary Sagna
-Robin Van Persie
-Thomas Vermaelen
-Sebastien Squillaci
Chelsea – [Wachezaji 19]
WALIOLELEWA NYUMBANI:
-Ashley Cole
-John Terry
-Frank Lampard
-Ross Turnbull
WENGINEO:
-Petr Cech
-Branislav Ivanovic
-Michael Essien
-Ramires
-Yossi Benayoun
-Didier Drogba
-John Mikel Obi
-Florent Malouda
-Jose Bosingwa
-Yuri Zhirkov
-Paulo Ferreira
-Salomon Kalou
-Alex
-Nicolas Anelka
-Henrique Hilário
Liverpool- [Wachezaji 21]
WALIOLELEWA NYUMBANI:
-Brad Jones
-Glen Johnson
-Steven Gerrard
-Joe Cole
-Jamie Carragher
-Jay Spearing
-Stephen Darby
-Paul Konchesky
WENGINEO:
-Daniel Agger
-Fabio Aurélio
-Fernando Torres
-Milan Jovanovic
-Sotirios Kyrgiakos
-Maxi Rodríguez
-Dirk Kuyt
-Lucas Leiva
-Jose Reina
-Martin Skrtel
-Christian Poulsen
-Ryan Babel
-Raul Meireles
Manchester United- [Wachezaji 24]
WALIOLELEWA NYUMBANI
-Gary Neville
-Jonny Evans
-Rio Ferdinand
-Wes Brown
-Wayne Rooney
-Ryan Giggs
Michael Carrick
-Paul Scholes
-John O’Shea
-Darren Fletcher
-Darron Gibson
-Ritchie De Laet
-Michael Owen
WENGINEO
-Edwin Van Der Sar
-Bebé
-Patrice Evra
-Anderson
-Dimitar Berbatov
-Ji-Sung Park
-Nemanja Vidic
-Luis Valencia
-Tomasz Kuszczak
-Javier Hernández
-Owen Hargreaves
Ferdinand yuko fiti
Rio Ferdinand jana alicheza Mechi yake ya kwanza tangu aumie goti mazoezini huko Afrika Kusini kabla kuanza Fainali za Kombe la Dunia na hivyo kulikosa Kombe hilo.
Rio, Miaka 31, alicheza dakika 45 za kwanza za mechi ya Rizevu wa Manchester United dhidi ya Oldham na Kocha wa Timu hiyo ya Rizevu, Ole Gunnar Solskjaer, amethibitisha kuwa Mchezaji huyo yuko fiti kurejea Kikosi cha Kwanza.
Mechi za Man United zifuatazo ni ile ya Ligi Kuu Septemba 11 na Everton huko Goodison Park, Septemba 14 na Rangers kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI huko Old Trafford na kisha Ligi Kuu na Liverpool pia Uwanjani Old Trafford Septemba 19.
Katika mechi hiyo ya Rizevu, Anderson, ambae aliumia goti Mwezi Februari, alicheza kwa dakika zote 90 na Macheda, ambae pia alikuwa majeruhi, alicheza na kufunga bao la pili na la ushindi katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Oldham.

Wednesday 1 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ferdinand arudi uwanjani, kucheza leo!
Beki mahari wa Manchester United ambae pia ni Nahodha wa England, Rio Ferdinand, leo anategemewa kucheza mechi yake ya kwanza tangu aumizwe goti huko Afrika Kusini wakati England ilipokuwa kambini kujitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Rio aliumizwa goti mazoezini na Mchezaji mwenzake wa England Emile Heskey.
Leo usiku, Rio anategemewa kuchezea Timu ya Rizevu ya Manchester United itakayocheza na Oldham.
Wachezaji wengine mahiri wa Man United watakaocheza mechi ya leo ili kupimwa baada ya kutoka kwenye majeruhi ni Wes Brown, Anderson na Federico Macheda.
Ligi Kuu yamruhusu Van Der Vaart Spurs
Baada ya jana kutopitisha uhamisho wake, Wasimamizi wa Ligi Kuu leo wametoa baraka zao kwa Mholanzi Rafael Van der Vaart aliehamia jana Tottenham kutoka Real Madrid sekunde za mwisho kabla uhamiso kufungwa kuichezea Tottenham baada ya kukubali maombi ya Tottenham kuwa sababu za kiufundi ziliwachelewesha kukamilisha usajili wake katika muda uliopangwa.
Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, alikiri waliaamua kumnunua Van Der Vaart masaa mawili kabla uhamisho kufungwa baada ya dau lake kushuka.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Mtu mwenye kasi sana Duniani ataka kuchezea Man United!
Bingwa wa Mbio za Mita 100, Usain Bolt, ameelezea nia yake ya kucheza Soka kwenye Klabu aipendayo ambayo ni Manchester United.
Katika Kitabu cha maisha yake, Usain Bolt, Miaka 24, ameandika: “Ikitokea ntacheza Soka, nitasaini kwa Timu niipendayo Manchester United. Watu wanasema hilo haliwezekani laki wao hawajaniona nnavyocheza hivyo huwezi jua nini kitatokea. Ikiwa Sir Alex Ferguson ataniona kwenye zile mechi za hisani anaweza kushawishika naweza kumbadili Ryan Giggs.”
Bolt ameshawahi kufanya mazoezi mara kadhaa na Man United kwenye Kituo chao huko Carrington na ameshahudhuria Mechi nyingi huko Old Trafford.
VUVUZELA HAZITAKIWI ULAYA!
UEFA imepiga marufuku Vuvuzela katika Mashindano yote ya Ulaya baada ya ala hiyo kupata umaarufu Dunia nzima kufuatia Fainali za Kombe la Dunia zilizochezwa huko Afrika Kusini Mwezi Juni na Julai.
Klabu kadhaa za Ulaya tayari zimeshazipiga marufuku Vuvuzela kutotumika katika Viwanja vyao na sasa UEFA imezikataa kwenye Mashindano ya UEFA CHAMPIONS LIGI, EUROPA LIGI na Mechi za EURO 2012.
PITIA: www.sokainbongo.com

Spurs yamchukua Van der Vaart lakini dili haijabarikiwa
Wasimamizi wa Ligi Kuu bado hawajabariki uhamisho wa sekunde za mwisho wa Staa wa Uholanzi Rafael Van der Vaart kutoka Real Madrid kwenda Tottenham kwa ada ya Pauni Milioni 8.
Awali anga za habari zilidai Van der Vaart, Miaka 27, amehamia Bayern Munich kwa dau la Pauni Milioni 18 lakini Meneja wa Spurs, Harry Redknapp, amedai dili hiyo ilibomoka na yeye kujulishwa masaa mawili kabla uhamisho kufungwa na ndipo alipoamua kumnyakua kwa vile ni Mchezaji wa kiwango cha juu.
Redknapp ametamka: “Ni Mchezaji mzuri na atatoa mchango mkubwa kwetu. Ilikuwa dili ya dakika za mwisho. Asubuhi sikuwa hata na nia ya kumchukua. Nadhani baada ya kushindikana kuhamia Ujerumani ndipo dau lake likaporomoka kadri Dirisha la kufungwa uhamisho lilipokaribia.”
Van der Vaart ni mmoja wa Wachezaji waliocheza na kuisaidia Uholanzi kufika Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini ambako walifungwa 1-0 na Spain.
Kiungo huyo wa Uholanzi alihamia Real Madrid kutoka Hamburg ya Ujerumani Mwaka 2008 lakini uchezaji wake huko Real ulikuwa wa nadra.
Ligi Kuu imesema itatoa tamko lake kuhusu uhamisho huo leo.
Stoke yachota Watatu
Huku dakika zikiyoyoma kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo jana, Stoke City ilifanikiwa kuwachukua Wachezaji watatu kwa mpigo ambo ni Eidur Gudjohnsen, Marc Wilson na Jermaine Pennant.
Gudjohnsen, aliewahi kuchezea Chelsea na Barcelona, amechukuliwa kwa mkopo kutoka Monaco na Wilson ametokea Portsmouth ambao pia wamepewa Wachezaji wawili, Liam Lawrence na David Kitson, katika dili hiyo.
Pennant, aliewahi kuzichezea Arsenal, Liverpool, Leeds United na Birmingham, ametua Stoke kwa mkopo kutoka Real Zaragoza ya Spain.
Yobo kuhamia Fenerbahce
Everton imethibitisha kuwa Beki wao kutoka Nigeria Joseph Yobo atahamia Klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkopo wa Msimu mmoja huku kukiwa na kipengele kuwa Fenerbahce wanaweza kumchukua moja kwa moja baada ya kwisha mkopo huo kwa dau la Pauni Milioni 5.
Yobo, ambae Mkataba wake na Everton unakwisha 2014, amekuwa akichezea hapo kwa Miaka 9 sasa na amecheza mechi zaidi ya 250.
Mnigeria huyo hivi karibuni amekuwa akikosa namba ya kudumu kwani Meneja wa Everton David Moyes amekuwa akiwapanga nafasi za Sentahafu Phil Jagielka na Sylvain Distin huku John Heitinga na Jack Rodwell pia wakiwa na uwezo wa kucheza pozisheni hizo.
Ingawa Dirisha la Uhamisho huko England tayari limefungwa jana huko Uturuki linafungwa rasmi Jumatano Septemba 1.

Tuesday 31 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fainali ya FA Cup yazua utata!
Chama cha Soka cha England, FA, na Wasimamizi wa Ligi Kuu wanahaha kutafuta ufumbuzi wa lini Fainali ya Kombe la FA ichezwe ili isigongane na Mechi za mwisho mwisho za Ligi.
Utata wa Fainali hiyo ya Kombe la FA umezuka kwa sababu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itachezwa Mei 28 Uwanjani Wembley Jijini London ambako pia Fainali ya FA Cup huchezwa.
Na ili ukubaliwe kuwa Mwenyeji wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ni lazima uhakikishe Kiwanja kitakachochezewa Fainali hiyo hakichezwi Mechi yeyote kwa Wiki mbili kabla ya Fainali hiyo ili kukiandaa vyema.
Sharti hilo linamaanisha Fainali ya FA Cup itabidi ichezwe Mei 14 wakati Mechi za Mwisho za Ligi Kuu zinachezwa Mei 22.
Kawaida Fainali ya Kombe la FA huchezwa Wiki moja baada ya Ligi Kuu kumalizika.
Ni mara moja tu Fainali hiyo ilichezwa Wiki moja kabla Ligi Kuu kumalizika na hiyo ilikuwa Msimu wa Mwaka 2000/1.
Utata huu pia umechangiwa na kuihamisha Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kutoka kuchezwa Siku ya Jumatano na kupelekwa Jumamosi utaratibu ambao ulianza Msimu uliokwisha.
FA imetamka itakaa chini na Wasimamizi wa Ligi Kuu ili kutoa ufumbuzi wa utata huo.
Werder Bremen yamchukua Silvestre
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Mikael Silvestre amejiunga na Klabu ya Ujerumani German Werder Bremen kwa Mkataba wa Miaka miwili.
Silvestre amejiunga Bremen kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Arsenal kumalizika Mwezi Juni.
Silvestre, Miaka 33, alieichezea Timu ya Taifa ya Ufaransa mara 40, alianza Soka la Kulipwa huko Ufaransa na Klabu ya Rennes na kuhamia Inter Milan kisha Manchester United Mwaka 1999 alikokaa hadi 2008 na kujiunga na Arsenal.
Kocha wa Bremen Thomas Schaaf amesema Silvestre ni hazina kwa Wachezaji Chipukizi na bado anao uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwa Klabu hiyo.
CHEKI: www.sokainbongo.com

PILIKA PILIKA KABLA DIRISHA LA UHAMISHO KUFUNGWA
UHAMISHO WA DAKIKA ZA MWISHO:
Robinho [Man City-AC Milan] ADA HAIJATAJWA
Marcus Bent [Birmingham - Wolves]: MKOPO
Salif Diao [Mchezaji Huru - Stoke]: Bure
Alexander Hleb [Barcelona - Birmingham]: MKOPO
Martin Jiranek [Spartak Moscow - Birmingham]: ADA HAIKUTAJWA Paul Konchesky [Fulham - Liverpool] HAIKUTAJWA
Zurab Khizanishvili [Blackburn - Reading] MKOPO
Rodrigo Moreno [Benfica - Bolton] MKOPO
Matt Phillips [Wycombe - Blackpool] £325,000
Stipe Pletikosa [Spartak Moscow - Tottenham] MKOPO
Gylfi Sigurdsson [Reading - Hoffenheim] £6m
Leo Dirisha la Uhamisho linafungwa rasmi saa 2 usiku , saa za bongo, na Klabu kadhaa ziliingia mbioni kukamilisha usajili wa dakika za mwisho na mojawapo ya Uhamisho kivutio ni ule wa Supastaa Robinho kutua AC Milan.
Robinho amekuwa hataki kukaa Manchester City alikotua baada ya kuhama Real Madrid na Msimu uliopita ilibidi apelekwe kwao acheze Santos kwa mkopo.
Nae Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Alexander Hleb, amerudi tena Ligi Kuu baada ya kuwa Barcelona na ataichezea Birmingham kwa mkopo.
Fulbeki Paul Konchesky amehamia Liverpool kumfuata Meneja wake wa zamani Roy Hodgson kutokea Fulham.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Hodgson aiangukia Spain kuhusu Torres
Roy Hodgson ameibembeleza Spain isimchezeshe Straika wake wa Liverpool Fernando Torres katika Mechi ya Makundi ya EURO 2012 Wiki hii na Liechtnstein na pia mechi inayofuata ya kirafiki dhidi ya Argentina ili kumpumzisha na kumpa muda wa kutosha kuendelea na tiba ya goti lake chini ya usimamizi wa Wataalam wa Viungo wa Liverpool.
Meneja huyo wa Liverpool amemwomba Meneja wa Spain Vicente Del Bosque amwondoe Torres kwenye Kikosi cha Spain ili abakie Liverpool kutibu goti lake lililomsumbua Msimu wote uliokwisha.
Hodgson amesema Torres anahitaji muda zaidi na Madaktari wa Klabu hiyo la sivyo akichezeshwa mechi mfululizo ataathirika baadae kadri Msimu unavyoendelea.
Mpaka sasa Spain haijatoa tamko lolote kuhusu Torres.
PITIA: www.sokainbongo.com

Van Persie nje!
Nyota wa Arsenal Robin van Persie atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa baada ya kuumia enka katika Mechi ya Ligi Kuu Jumamosi kati ya Blackburn na Arsenal ambayo Ze Gunners walishinda 2-1.
Van Persie atazikosa Mechi za Makundi za Nchi yake Uholanzi za EURO 2012 za Wiki hii na ijayo dhidi ya San Marino na Finland na tayari Holland imemteua Straika Mkongwe Ruud van Nistelrooy anaechezea Hamburg kuchukua nafasi yake.
Van Persie, Miaka 27, Msimu uliokwisha alikaa nje kwa Miezi mitano baada ya kuumia enka.
Queiroz afungiwa Miezi 6
Sakata la Kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Carlos Queiroz, limeingia papya baada ya Shirika la Kuzuia Madawa Marufuku kwa Wanamichezo huko Ureno, ADop, kumfungia Msaidizi huyo wa zamani wa Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, kwa Miezi 6 kwa kuwazuia Maafisa wao kutenda kazi yao.
Awali Chama cha Soka cha Ureno, FPF, kilimfungia Queiroz kwa Siku 30 kwa kumwona ana hatia ya kuwatukuna Maafisa wa ADop lakini ilimsafisha kwa kosa kubwa la kuwazuia kutenda kazi yao Maafisa hao.
Makosa ya Queiroz yanadaiwa kutendeka Mwezi Mei wakati Timu ya Ureno ilipokuwa kambini huko Ureno kujitayarisha kwenda Afrika Kusini kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Katika kesi yake na FPF Agosti 19, Sir Alex Ferguson aliruka hadi Ureno kwenda kutoa utetezi wa Msaidizi wake huyo wa zamani.
Kufuatia kifungo hiki cha Miezi 6, Magazeti huko Ureno yamedai huenda Queiroz akatimuliwa kama Kocha wa Ureno.
Queiroz amekuwa akidai sakata hilo limekuzwa kwa sababu ya njama za Makamu wa Rais wa FPF, Amandio de Carvalho, kutaka afukuzwe kazi ya Ukocha wa Ureno.
Kwa madai hayo, FPF imefungua uchunguzi mwingine dhidi ya Queiroz.

Monday 30 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fergie kumtosa Hargreaves?
Klabu zote za Ligi Kuu England zinatakiwa ziwasilishe Listi zao za Wachezaji 25 Jumatano Septemba 1 na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, yuko kwenye mtihani mkubwa wa kuamua kama katika Listi hiyo amweke Owen Hargreaves ambae alikuwa na matatizo ya magoti yote mawili yaliyofanyiwa upasuaji lakini hajatengemaa na imebidi arudishwe tena kwa Dakta Richard Steadman aliemfanyia operesheni huko Colorado, Marekani.
Hargreaves yuko huko Colorado kwa Wiki 7 sasa na haijulikani atapona lini tatizo la magoti yake ambalo limedumu Miaka miwili.
Timu zikiwasilisha Listi zao za Wachezaji 25 haziruhusiwi kuzibadilisha hadi Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa tena Januari Mwakani.
Ferguson amesema: “Hatuna tatizo kuhusu Wachezaji walio chini ya Miaka 21 kwani Klabu ruksa kusaini idadi yeyote ya hao. Tatizo lipo kwa Hargreaves kama atakuwa fiti. Tukimwingiza na asipone hatuwezi kumbadili hadi Januari.”
Ronaldo kukosa Mechi za EURO 2012
Cristiano Ronaldo atakuwa nje ya uwanja kwa Wiki 3 baada ya kuumia enka hapo jana katika sare ya 0-0 kati ya Real Mallorca na Real Madrid.
Hivyo atazikosa Mechi za Nchi yake Ureno za Makundi za EURO 2012 dhidi ya Cyprus na nyingine na Norway zitakazochezwa Wiki hii na Jumanne Wiki ijayo.
Pia, Mchezaji huyo wa bei mbaya katika historia, atazikosa Mechi za Klabu yake Real Madrid za La Liga dhidi ya Osasuna na ile ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI Real watakapocheza na Ajax.
CHEKI: www.sokainbongo.com


Mourinho na Real yake mwendo kusuasua, Barca mwendo mdundo!
‘Mtu Spesheli’, Jose Mourinho, jana ameanza himaya yake kwenye La Liga huko Spain akiwa na Real Madrid yake kwa sare ya ugenini ya 0-0 walipocheza na Mallorca ambao walionekana bora zaidi kupita Real.
Mabingwa Barcelona, nao wakicheza awali ugenini, waliifumua Racing Santander kwa bao 3-0 kwa mabao ya Lionel Messi, Andres Iniesta na David Villa.
Ingawa Real kwenye Difensi, iliyokuwa na Beki wa zamani Chelsea Carvalho, walionekana imara, Kiungo na Ushambuliaji wao ulikuwa hafifu.
Mourinho aliwashangaza wengi pale alipowaweka benchi Wachezaji wapya wa Ujerumani waliosainiwa kwa mbwembwe nyingi, Sami Khedira na Mesut Oezil, ingawa waliingizwa baadae lakini hawakubadilisha chochote uwanjani.
TETESI………………..Rodwell kwenda Man United!!!!!!
Baadhi ya Magazeti huko Uingereza yameibua kuwa Nyota Chipukizi wa Everton, Jack Rodwell, yuko njiani kwenda Manchester United kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo kesho.
Inadaiwa Man United watatoa ada ya Pauni Milioni 10 pamoja na Kiungo Michael Carrick ambae amekuwa akisuasua Man United.
Rodwell, Miaka 19, ni Mchezaji anaesifiwa kuwa na kipaji kikubwa na mwenye uwezo wa kucheza Kiungo au Sentahafu na Wadau wamemfananisha na Rio Ferdinand alipokuwa mdogo.
Man United wamekuwa wakimfuatilia kwa kipindi kirefu Mchezaji huyo ambae alianza kuichezea Everton tangu akiwa na Miaka 7 na alieweka Rekodi ya kuchezea michuano ya Ulaya ya UEFA akiwa mdogo na umri wa Miaka 16 tu.
Rodwell alianza kucheza mechi za Ligi Kuu Mwaka 2008 na Msimu uliopita alicheza katika mechi ambayo Everton iliifunga Man United 3-1 na yeye kufunga bao moja.
Gyan kwenda Sunderland?
Nyota wa Ghana alieng’ara na pia kuvunja mioyo ya Afrika kwenye Kombe la Dunia, Asamoah Gyan, atahamia Klabu ya Sunderland ikiwa mazungumzo kati ya Rennes ya Ufaransa, Klabu yake ya sasa, na Sunderland yatafanikiwa.
Klabu hizo zina muda hadi kesho ili kukamilisha Uhamisho huo kabla Dirisha la Uhamisho halijafungwa Agosti 31.
Gyan alikosa kufunga penalti dakika ya mwisho ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia Ghana ilipocheza na Uruguay na hatimaye Ghana kubwagwa nje.
Capello ataja England ya EURO 2012
Kocha Fabio Capello ametangaza Kikosi chake cha England kitachocheza Mechi za Makundi za EURO 2012 dhidi ya Bulgaria hapo Ijumaa Septemba 3 na Uswisi Jumanne Septemba 7.
Capello amemrudisha tena kundini Kipa Scott Carson ambae hajaidakia England kwa Miaka miwili na pia kuwaita tena baadhi ya Wachezaji ambao alikuwa hawachagui siku za nyuma za hivi karibuni.
Miongoni mwa hao ni Matthew Upson, Michael Carrick, Shaun Wright-Phillips, Peter Crouch na Jermain Defoe.
Hata hivyo, Mchezaji wa Liverpool, Joe Cole, hakuchaguliwa kinyume cha matarajio ya wengi.
Wengine ambao hawakuchukuliwa kwa sababu ya kuwa majeruhi ni Wachezaji wawili wa Chelsea, John Terry na Frank Lampard, Rio Ferdinand na Bobby Zamora.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Scott Carson (West Brom), Ben Foster (Birmingham), Joe Hart (Manchester City).
WALINZI: Gary Cahill (Bolton), Ashley Cole (Chelsea), Michael Dawson (Tottenham), Kieran Gibbs (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), Matthew Upson (West Ham)
VIUNGO: Gareth Barry (Manchester City), Michael Carrick (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Manchester City), James Milner (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal), Shaun Wright-Phillips (Manchester City), Ashley Young (Aston Villa)
MASTRAIKA: Darren Bent (Sunderland), Carlton Cole (West Ham), Peter Crouch (Tottenham), Jermain Defoe (Tottenham), Wayne Rooney (Manchester United).

Sunday 29 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

LIGI KUU kusitishwa hadi Septemba 11
Mechi za Ligi Kuu England zitakuwa mapumzikoni hadi Septemba 11 ili kuzipisha Mechi za Kimataifa za Nchi za Ulaya kugombea kufuzu Fainali za EURO 2012 ambazo zitachezwa Wikiendi hii na katikati ya Wiki ijayo.
England itaingia dimbani hapo Ijumaa Septemba 3 kucheza na Bulgaria Uwanjani Wembley Jijini London na Jumanne Septemba 7 itacheza na Uswisi.
LIGI KUU England: RATIBA inayofuata
Jumamosi, 11 Septemba 2010
[Saa 8 dak 45 mchana]
Everton v Man United
[Saa 11 jioni]
Arsenal v Bolton
Fulham v Wolverhampton
Man City v Blackburn
Newcastle v Blackpool
West Brom v Tottenham
West Ham v Chelsea
Wigan v Sunderland
Jumapili, 12 Septemba 2010
[Saa 12 jioni]
Birmingham v Liverpool
Jumatatu, 13 Septemba 2010
[Saa 4 usiku]
Stoke v Aston Villa
Villa 1 Everton 0
Leo Aston Villa, baada ya kuchapwa 6-0 na Newcastle wiki iliyopita, wamejirekebisha na kuutumia vizuri Uwanja wao Villa Park kwa kuwafunga Everton bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu.
Bao la Villa lilifungwa na Luke Young dakika ya 9.
Everton walizidisha presha baada ya bao hilo lakini nguvu zao zote ziliishia kwa ama Kipa Brad Friedel, kutoa nje na mara moja kugonga mwamba baada ya shuti kali la Pienaar.
Matokeo ya mechi hii yamewafanya Villa wawe na pointi 6 kwa mechi 3 na wako nafasi ya 4 nyuma ya Chelsea, Arsenal na Man United.
Everton wao wako nafasi ya 3 toka mkiani wakiwa na pointi moja tu baada ya mechi 3.
CHEKI: www.sokainbongo.com

‘Timu Tajiri’ Man City yanyongwa sekunde ya mwisho!
Timu inayosifika ndio tajiri kupita zote, Manchester City, leo huko Stadium of Light imechapwa bao 1-0 na Wenyeji Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu na bao hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na Darren Bent kwa njia ya penalti.
Penalti iliyoipa ushindi Sunderland ilitolewa na Refa Mike Dean baada ya Beki Micah Richards kumpandia Darren Bent.
Vikosi vilivyocheza:
Sunderland: Mignolet, Richardson, Turner (Bardsley, dakika ya 46), Bramble, Ferdinand, Cattermole, Malbranque, Henderson, Al-Muhammadi, Campbell (Welbeck, dak 46), Bent
Man City: Hart, Richards, Kompany, Lescott (Adebayor, dak 75), Kolo Toure, Milner, A Johnson, Barry, De Jong, Yaya Toure, Tevez (Jo, dak 90)
Refa: Mike Dean
Torres aipa ushindi Liverpool
Straika mahiri wa Liverpool, Fernando Torres, leo huko Anfield ameweza kufunga bao moja na la ushindi dhidi ya West Bromwich Albion waliosimama kidete.
Bao hilo la Torres lilifungwa dakika ya 65 na sasa Liverpool wana pointi 4 baada ya Mechi 3 za Ligi Kuu.
Baada ya Liverpool kupata bao lao, West Brom ilibidi wacheze Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Morrison kumchezea Torres rafu mbaya sana na Refa kumtwanga Kadi Nyekundu.
Vikosi vilivyocheza:
Liverpool: Reina, G Johnson, Agger, Carragher, Skrtel, Gerrard, Lucas, C Poulsen, Torres (Babel, dakika ya 89), Jovanovic (Maxi, dak ya 59), Kuyt
West Brom: Carson, Olsson, Shorey, Tamas, Jara, Morrison, Brunt, Dorrans (Tchoyi, dak ya 75), Mulumbu, Odemwingie, Fortune (Wood, dak ya 82)
Refa: Probert
CHEKI: www.sokainbongo.com

Bolton 2 Birmingham 2
Mtu 10 Bolton Wanderers walipigana kutoka bao 2-0 nyuma na kufanya gemu imalizike 2-2 Uwanjani kwao Reebok.
Birmingham walipata bao la kwanza dakika ya 3 tu kupitia Roger Johnson kufuatia krosi kutoka kushoto.
Kipa wa Bolton, Jussi Jaaskelainen, alitolewa kwa Kadi Nyekundu muda mfupi kabla ya haftaimu kwa kumnasa kibao Roger Johnson.
Kipindi cha pili, dakika ya 50, Craig Gardner akafunga bao la pili kwa Birmingham.
Bolton walifunga bao lao la kwanza dakika ya 71 kwa penalti Mfungaji akiwa Kevin Davies na Robbie Blake akasawazisha kwenye dakika ya 81 baada ya frikiki nzuri sana.
Liverpool wamchota Meireles wa Porto
Liverpool imemsaini Kiungo wa Kimataifa wa Ureno, Raul Meireles, kutoka FC Porto kwa dau la Pauni Milioni 11.5 na amesaini Mkataba wa Miaka minne.
Meireles, ambae alicheza Mechi zote za Ureno huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia, amechukuliwa kama mbadala wa Kiungo Javier Mascherano alieondoka Liverpool kwenda Barcelona.
Msimu huu Liverpool, pamoja na Meireles, Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa ni Milan Jovanovic, Joe Cole, Christian Poulsen, Jonjo Shelvey na Danny Wilson.
Ferguson amsifia Rooney
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemsifia Straika wake Wayne Rooney baada ya kuumaliza ukame wa magoli alipofunga bao la kwanza kwa penalti katika ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham katika Mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Old Trafford hapo jana.
Ferguson amesema: ‘Mastraika siku zote wana uchu wa kufunga lakini tuzungumzie uchezaji wa Rooney. Yeye anajituma mno uwanjani.”
Licha ya kufunga bao moja, Rooney pia ndie alielipika bao moja la Man United kati ya mengine mawili yaliyofungwa.
Kwa vile Ligi Kuu inasimama hadi Septemba 11 kupisha Mechi za Kimataifa za Nchi za Ulaya kuwania kufuzu Fainali za EURO 2012, Rooney anategemewa kujiunga na Timu ya England ambayo Ijumaa Septemba 3 itacheza na Bulgaria na kisha Jumanne Septemba 7 kucheza na Uswisi.
CHEKI: www.sokainbongo.com

Stoke wamshitaki Wenger
Stoke City imewasilisha malalamiko rasmi kwa FA na Ligi Kuu kuhusu matamshi ya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, aliyoyatoa kumlaumu Mchezaji wao Ryan Shawcross.
Wenger, akiongea kabla ya mechi yao ya jana ya Ligi dhidi ya Blackburn, alizungumzia mchezo wa nguvu na rafu wa Blackburn na kuufananisha na Raga na katika kusema hayo alimtaja Mchezaji wa Stoke, Ryan Shawcross, alivyokuwa kwenye mechi ya Wiki iliyopita ya Ligi kati ya Stoke na Tottenham na kumfananisha Mchezaji huyo kama Mcheza Raga.
Kauli hizo za Wenger zimemkera Meneja wa Stoke, Tony Pulis, ambae amesema wameandika barua rasmi kwa FA na Ligi Kuu.
Pulis amelalamika: “Tumesikitishwa na kauli ya Wenger. Haikustahili hata kidogo.”
Alipoulizwa kama anaonaje pengine kumtaja Shawcross katika mechi na Tottenham huku Refa akiwa Chris Foy ambae ndie alichezesha pambano la jana kati ya Blackburn na Arsenal ilikuwa mbinu ya Wenger ili wapate imani ya Refa huyo katika mechi yao na Blackburn, Pulis alijibu: “Ni wewe umesema kuwa alitaka kumrubuni Refa awasaidie na mimi nakubaliana na wewe!”
Pulis akaongeza: “Yeye ana uhuru wa kusema atakalo. Sisi tumepigana Vita Kuu mbili za Dunia kulinda uhuru huo! Lakini kile alichosema kuhusu Shawcross ni kitu kibaya na sisi tutamshitaki.”
Lampard & Terry nje England!
Wachezaji wa Chelsea, Frank Lampard na John Terry, watazikosa Mechi za England za Makundi kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 za Septemba 3 na Bulgaria na Septemba 7 na Uswisi baada ya Klabu yao kusema ni majeruhi.
Terry na Lampard walicheza Mechi ya Ligi Kuu hapo jana dhidi ya Stoke City ambayo walishinda 2-0 na Lampard kukosa penalti na kupumzishwa mara baada ya hapo lakini Terry aliendelea hadi mwishoni.
Chelsea imetamka Terry ana matatizo ya musuli za paja na Lampard inabidi afanyiwe operesheni kutibu ngiri.
Kwa sababu ya Mechi za Kimataifa za EURO 2012 Ligi Kuu itakuwa mapumzikoni hadi Jumamosi Septemba 11.
Ibrahimovic yuko AC Milan kwa mkopo
AC Milan na FC Barcelona zimekubaliana Straika Zlatan Ibrahimovic aende AC Milan kwa mkopo wa Msimu mmoja na AC Milan wamepewa nafasi ya kumchukua moja kwa moja baada ya mkopo huo kwisha kwa dau la Pauni Milioni 20.
Ibrahimovic alihamia Barcelona kutoka Inter Milan katika dili iliyomhusu pia Samuel Eto’o kubadilisha Klabu kutoka Barcelona kwenda Inter Milan.
Mwenyewe Ibrahimovic ametoboa kuwa hakuwa na uhusiano mzuri na Kocha wa Barca Pep Guardiola na hawajaongea kwa Miezi 6.
Powered By Blogger