Wednesday 1 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Ferdinand arudi uwanjani, kucheza leo!
Beki mahari wa Manchester United ambae pia ni Nahodha wa England, Rio Ferdinand, leo anategemewa kucheza mechi yake ya kwanza tangu aumizwe goti huko Afrika Kusini wakati England ilipokuwa kambini kujitayarisha kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Rio aliumizwa goti mazoezini na Mchezaji mwenzake wa England Emile Heskey.
Leo usiku, Rio anategemewa kuchezea Timu ya Rizevu ya Manchester United itakayocheza na Oldham.
Wachezaji wengine mahiri wa Man United watakaocheza mechi ya leo ili kupimwa baada ya kutoka kwenye majeruhi ni Wes Brown, Anderson na Federico Macheda.
Ligi Kuu yamruhusu Van Der Vaart Spurs
Baada ya jana kutopitisha uhamisho wake, Wasimamizi wa Ligi Kuu leo wametoa baraka zao kwa Mholanzi Rafael Van der Vaart aliehamia jana Tottenham kutoka Real Madrid sekunde za mwisho kabla uhamiso kufungwa kuichezea Tottenham baada ya kukubali maombi ya Tottenham kuwa sababu za kiufundi ziliwachelewesha kukamilisha usajili wake katika muda uliopangwa.
Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp, alikiri waliaamua kumnunua Van Der Vaart masaa mawili kabla uhamisho kufungwa baada ya dau lake kushuka.

No comments:

Powered By Blogger