Tuesday 31 August 2010

PITIA: www.sokainbongo.com

Van Persie nje!
Nyota wa Arsenal Robin van Persie atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa baada ya kuumia enka katika Mechi ya Ligi Kuu Jumamosi kati ya Blackburn na Arsenal ambayo Ze Gunners walishinda 2-1.
Van Persie atazikosa Mechi za Makundi za Nchi yake Uholanzi za EURO 2012 za Wiki hii na ijayo dhidi ya San Marino na Finland na tayari Holland imemteua Straika Mkongwe Ruud van Nistelrooy anaechezea Hamburg kuchukua nafasi yake.
Van Persie, Miaka 27, Msimu uliokwisha alikaa nje kwa Miezi mitano baada ya kuumia enka.
Queiroz afungiwa Miezi 6
Sakata la Kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Carlos Queiroz, limeingia papya baada ya Shirika la Kuzuia Madawa Marufuku kwa Wanamichezo huko Ureno, ADop, kumfungia Msaidizi huyo wa zamani wa Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, kwa Miezi 6 kwa kuwazuia Maafisa wao kutenda kazi yao.
Awali Chama cha Soka cha Ureno, FPF, kilimfungia Queiroz kwa Siku 30 kwa kumwona ana hatia ya kuwatukuna Maafisa wa ADop lakini ilimsafisha kwa kosa kubwa la kuwazuia kutenda kazi yao Maafisa hao.
Makosa ya Queiroz yanadaiwa kutendeka Mwezi Mei wakati Timu ya Ureno ilipokuwa kambini huko Ureno kujitayarisha kwenda Afrika Kusini kwa Fainali za Kombe la Dunia.
Katika kesi yake na FPF Agosti 19, Sir Alex Ferguson aliruka hadi Ureno kwenda kutoa utetezi wa Msaidizi wake huyo wa zamani.
Kufuatia kifungo hiki cha Miezi 6, Magazeti huko Ureno yamedai huenda Queiroz akatimuliwa kama Kocha wa Ureno.
Queiroz amekuwa akidai sakata hilo limekuzwa kwa sababu ya njama za Makamu wa Rais wa FPF, Amandio de Carvalho, kutaka afukuzwe kazi ya Ukocha wa Ureno.
Kwa madai hayo, FPF imefungua uchunguzi mwingine dhidi ya Queiroz.

No comments:

Powered By Blogger