Friday, 3 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Houllier kutua Villa?
Kocha wa zamani wa Liverpool, Mfaransa Gerrard Houllier, Miaka 63, amefanyiwa usaili na Mmiliki wa Aston Villa, Randy Lerner, na kuna kila dalili mwenye mali huyo kutoka Marekani ameridhishwa na Houllier na huenda akamuajiri kuchukua nafasi ya Umeneja iliyoachwa wazi na Martin O’Neill aliyetimka ghafla Wiki mbili zilizopita.
Houllier aliondoka Liverpool Miaka 6 iliyopita na amekuwa Mwajiriwa wa FFF, Chama cha Soka Ufaransa, kama Mkurugenzi wa Ufundi tangu aondoke kuiongoza Klabu ya Lyon.
Alipokuwa na Liverpool, Houllier aliiwezesha Klabu hiyo itwae Vikombe vitatu kwa mpigo-UEFA Cup, FA Cup na LEAGUE Cup-Mwaka 2001.
Wengine waliofanyiwa usaili na Mmiliki wa Villa ni Bosi wa zamani wa West Ham Alan Curbishley na Kaimu Meneja wa sasa wa Aston Villa Kevin MacDonald lakini Houllier ndie anaetajwa kuwa ana nafasi kubwa kupewa Umeneja.
‘Vijeba’ kuipaisha Chelsea!
Frank Lampard anaamini kuwa Chelsea, iliyoanza Ligi Kuu Msimu huu kwa kishindo cha kushinda Mechi zake 3 kwa jumla ya mabao 14-0, itawika tena mbali ya kuwa na Wachezaji ‘vijeba’.
Lampard amewaponda Watu wanaodai Wachezaji wengi Chelsea ni ‘vijeba’ na yeye amedai wao watawaonyesha uwezo wao kwa kutetea vyema Ubingwa wao.
Chelsea wameanza Msimu huu wa Ligi Kuu kwa kuzishindilia West Bromwich Albion na Wigan Athletic bao 6-0 kila moja na kuipiga Stoke City 2-0.
‘Vijeba’ wanaotajwa kwenye Timu hiyo ni Lampard, Miaka 32, John Terry, Miaka 29, na Didier Drogba, atakaetimiza Miaka 33 Mwezi Machi mwakani.
Lampard amesema: “Ni upuuzi kusikia ati tumekwisha, ni wazee tumebakisha mwaka tu....kauli hizo zimeendela Mwaka na kitu sasa! Tizama Watu wamekuwa wakimsifia Paul Scholes na hizo sifa ni za kweli kwani leo ukimwondoa, Man United lazima watataka kumpata Mtu kama yeye lakini hawataweza kumpata mwenye uwezo kama yeye!”

No comments:

Powered By Blogger