Sunday, 29 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Stoke wamshitaki Wenger
Stoke City imewasilisha malalamiko rasmi kwa FA na Ligi Kuu kuhusu matamshi ya Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, aliyoyatoa kumlaumu Mchezaji wao Ryan Shawcross.
Wenger, akiongea kabla ya mechi yao ya jana ya Ligi dhidi ya Blackburn, alizungumzia mchezo wa nguvu na rafu wa Blackburn na kuufananisha na Raga na katika kusema hayo alimtaja Mchezaji wa Stoke, Ryan Shawcross, alivyokuwa kwenye mechi ya Wiki iliyopita ya Ligi kati ya Stoke na Tottenham na kumfananisha Mchezaji huyo kama Mcheza Raga.
Kauli hizo za Wenger zimemkera Meneja wa Stoke, Tony Pulis, ambae amesema wameandika barua rasmi kwa FA na Ligi Kuu.
Pulis amelalamika: “Tumesikitishwa na kauli ya Wenger. Haikustahili hata kidogo.”
Alipoulizwa kama anaonaje pengine kumtaja Shawcross katika mechi na Tottenham huku Refa akiwa Chris Foy ambae ndie alichezesha pambano la jana kati ya Blackburn na Arsenal ilikuwa mbinu ya Wenger ili wapate imani ya Refa huyo katika mechi yao na Blackburn, Pulis alijibu: “Ni wewe umesema kuwa alitaka kumrubuni Refa awasaidie na mimi nakubaliana na wewe!”
Pulis akaongeza: “Yeye ana uhuru wa kusema atakalo. Sisi tumepigana Vita Kuu mbili za Dunia kulinda uhuru huo! Lakini kile alichosema kuhusu Shawcross ni kitu kibaya na sisi tutamshitaki.”
Lampard & Terry nje England!
Wachezaji wa Chelsea, Frank Lampard na John Terry, watazikosa Mechi za England za Makundi kugombea kuingia Fainali za EURO 2012 za Septemba 3 na Bulgaria na Septemba 7 na Uswisi baada ya Klabu yao kusema ni majeruhi.
Terry na Lampard walicheza Mechi ya Ligi Kuu hapo jana dhidi ya Stoke City ambayo walishinda 2-0 na Lampard kukosa penalti na kupumzishwa mara baada ya hapo lakini Terry aliendelea hadi mwishoni.
Chelsea imetamka Terry ana matatizo ya musuli za paja na Lampard inabidi afanyiwe operesheni kutibu ngiri.
Kwa sababu ya Mechi za Kimataifa za EURO 2012 Ligi Kuu itakuwa mapumzikoni hadi Jumamosi Septemba 11.
Ibrahimovic yuko AC Milan kwa mkopo
AC Milan na FC Barcelona zimekubaliana Straika Zlatan Ibrahimovic aende AC Milan kwa mkopo wa Msimu mmoja na AC Milan wamepewa nafasi ya kumchukua moja kwa moja baada ya mkopo huo kwisha kwa dau la Pauni Milioni 20.
Ibrahimovic alihamia Barcelona kutoka Inter Milan katika dili iliyomhusu pia Samuel Eto’o kubadilisha Klabu kutoka Barcelona kwenda Inter Milan.
Mwenyewe Ibrahimovic ametoboa kuwa hakuwa na uhusiano mzuri na Kocha wa Barca Pep Guardiola na hawajaongea kwa Miezi 6.

No comments:

Powered By Blogger