Thursday 2 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Capello apuuza lawama
Kocha wa England Fabio Capello, huku akikabiliwa na mtihani mgumu hapo kesho wakati England itakapocheza na Bulgaria Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya Kundi G ili kufuzu Fainali za EURO 2012, amedai hana presha yeyote.
Baada ya kufanya kinyume cha matarajio ya wadau wengi huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Capello amekuwa akilaumiwa lakini Mtaliana huyo amekiri lawama hizo ni sehemu ya kazi yake na amesema: “Hiyo ni sehemu ya kazi ya Meneja. Ukishinda, wewe ni bora. Ukifungwa, wewe hufai!”
Hata hivyo, Capello ametoboa kuwa amejifunza toka yale yaliyotokea huko Afrika Kusini na hivyo amebadilika kidogo.
Kuhusu Bulgaria, Capello ametamka: “Bulgaria sio Timu rahisi kwani uwezo wao kiufundi ni mkubwa na wanajihami kwa kutumia Watu 9 na kushambulia kwa kustukiza na kasi kubwa. Lakini, ni lazima tushinde, inabidi tucheze vizuri na tunaomba Mashabiki watusapoti wakati wa mechi.”

No comments:

Powered By Blogger