Monday 30 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fergie kumtosa Hargreaves?
Klabu zote za Ligi Kuu England zinatakiwa ziwasilishe Listi zao za Wachezaji 25 Jumatano Septemba 1 na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, yuko kwenye mtihani mkubwa wa kuamua kama katika Listi hiyo amweke Owen Hargreaves ambae alikuwa na matatizo ya magoti yote mawili yaliyofanyiwa upasuaji lakini hajatengemaa na imebidi arudishwe tena kwa Dakta Richard Steadman aliemfanyia operesheni huko Colorado, Marekani.
Hargreaves yuko huko Colorado kwa Wiki 7 sasa na haijulikani atapona lini tatizo la magoti yake ambalo limedumu Miaka miwili.
Timu zikiwasilisha Listi zao za Wachezaji 25 haziruhusiwi kuzibadilisha hadi Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa tena Januari Mwakani.
Ferguson amesema: “Hatuna tatizo kuhusu Wachezaji walio chini ya Miaka 21 kwani Klabu ruksa kusaini idadi yeyote ya hao. Tatizo lipo kwa Hargreaves kama atakuwa fiti. Tukimwingiza na asipone hatuwezi kumbadili hadi Januari.”
Ronaldo kukosa Mechi za EURO 2012
Cristiano Ronaldo atakuwa nje ya uwanja kwa Wiki 3 baada ya kuumia enka hapo jana katika sare ya 0-0 kati ya Real Mallorca na Real Madrid.
Hivyo atazikosa Mechi za Nchi yake Ureno za Makundi za EURO 2012 dhidi ya Cyprus na nyingine na Norway zitakazochezwa Wiki hii na Jumanne Wiki ijayo.
Pia, Mchezaji huyo wa bei mbaya katika historia, atazikosa Mechi za Klabu yake Real Madrid za La Liga dhidi ya Osasuna na ile ya kwanza ya UEFA CHAMPIONS LIGI Real watakapocheza na Ajax.

No comments:

Powered By Blogger