Thursday 2 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Petrov aikandya England!
• ‘Ni Wachezaji wazuri, ila si Timu!’
Petrov, anaechezea Klabu ya Bolton na pia Timu ya Taifa ya Bulgaria ambayo kesho inapambana na England Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya Kundi G kuwania kuingia Fainali za EURO 2018, amedai England ina Wachezaji wazuri lakini si Timu chini ya Mtaliana Fabio Capello.
England haikufanya vizuri kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na ilinyukwa 4-1 na Germany na kwabagwa nje Raundi ya Pili na matokeo hayo yaliwafanya baadhi ya Mashabiki kwazomea Wachezaji wa England walipocheza Mechi ya kirafiki Uwanjani Wembley dhidi ya Hungary Mwezi uliopita.
Petrov amenena: “Kila mtu anajua England ina majina na Wachezaji wazuri sana. Lakini sidhani wana Timu. Sijui kwanini. Hawafanyi lolote. Ni wakati mgumu kwa England.”
Bulgaria itaingia Uwanjani bila ya Nyota wao Dimitar Berbatov wa Manchester United ambae alitangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa Mwezi Mei.
Mourinho: ‘Mimi si Mchawi!’
Jose Mourinho, maarufu kama ‘Mtu spesheli’, amesema yeye si mchawi na hivyo Watu wasitegemee vimbwanga kila Mechi na ametoa kauli hiyo baada ya Timu yake Real Madrid kutoka sare 0-0 na Real Mallorca huku Wapinzani wao Barcelona wakimchapa Real Santander 3-0 katika Mechi za ufunguzi za La Liga wikiendi iliyokwisha.
Hata hivyo, Mourinho amejigamba kuwa yeye ndio anastahili kuwa Kocha wa Real kwani ataleta utulivu na mafanikio.
Mourinho alitamka: “Mie si Harry Porter [Akiitaja Filamu maarufu]. Yeye ni Mchawi. Ukweli hamna uchawi. Uchawi ni hadithi tu na mimi naishi kwenye Soka ambalo ni ukweli tu!”
Mourinho ametua Real Madrid baada ya mafanikio makubwa na Inter Milan Msimu uliopita alipoiwezesha kutwaa Mataji Matatu makubwa-Ubingwa wa Italia, Kombe la Italia na Ubingwa wa Ulaya- na sasa jukumu lake huko Spain ni kuipora Barcelona Ubingwa wa La Liga ambao wameuchukua mara mbili mfululizo na pia kufanya vizuri kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambako wameshindwa kuvuka hatua ya Robo Fainali tangu 2004.
Mourinho amejigamba kuwa yeye haogopi kufukuzwa Real kwani ana uhakika siku ya pili tu atapata Timu nyingine.

No comments:

Powered By Blogger