Saturday 26 July 2008

TEVEZ KUBAKI MAN U KWA MKATABA WA KUDUMU!!
DAU LA KUMBAKISHA MAN U LITAVUNJA REKODI UINGEREZA!
Muargentina Carlos Tevez ambae yuko MAN U kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili unaoisha mwakani atasainiwa MAN U kwa dau la Pauni milioni 32 ambalo litavunja rekodi ya kumnunua mchezaji Uingereza.

Rekodi ya sasa inashikiliwa na Chelsea pale walipomsaini Andrei Shevchenko kwa Pauni milioni 30 miaka miwili iliopita.
Carlos Tevez anamilikwa na Kampuni iitwayo MSI ingawa Man U walilazimika kuwalipa fidia Klabu ya West Ham aliyochezea Tevez kabla kuchukuliwa na Man U kwa mkopo Agosti, 2007.

Tevez ameshachezea Man U mechi 39 na kufunga mabao 19 yaliyoiwezesha Man U kutwaa Ubingwa wa LIGI KUU UINGEREZA na Ubingwa wa Klabu za ULAYA.
Kwa sasa anaonekana ni muhimu sana hasa kuhusu hatma ya hatihati ya 'kigeugeu' Ronaldo.


KIPA ROBINSON AJIUNGA BLACKBURN!

Aliekuwa Kipa nambari wani wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Paul Robinson, miaka 28, amesainiwa na Blackburn Rovers kutokea Tottenham Hotspurs kwa mkataba wa miaka mitano. Kipa huyo alikuwa na wakati mbaya katika msimu uliopita kwa kupoteza namba kwenye Timu ya Uingereza na vilevile Klabu yake ya Tottenham kumuona ameshuka kiwango kilichowalazimu kumnunua Kipa mwingine toka Klabu ya Uholanzi PSV Eindhoven Heurelho Gomes ambae ni raia wa Brazil.
Robinson inaelekea atachukua namba ya Kipa wa siku nyingi hapo Blackburn Mmarekani Brad Friedel anaekamilisha taratibu za kuhamia Aston Villa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Neville arefusha mkataba Everton
Nahodha wa Everton, Phillip Neville, miaka 31, ambae ni mdogo wake Nahodha wa Man U, Gary Neville, amesaini mkataba mpya Everton utakaomweka hapo hadi 2012.
Phillip Neville alijiunga Everton mwaka 2005 akitokea Man U timu aliyoichezea tangu akiwa chekechea pamoja na kaka yake Gary.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
OBAFEMI AFIWA NA MAMA MZAZI!
Kuukosa mwanzo wa msimu mpya LIGI KUU UINGEREZA!
Mshambuliaji wa Newcastle, Mnigeria Obafemi Martins, huenda akaukosa mwanzo wa msimu mpya wa LIGI KUU UINGEREZA baada ya kupata msiba mkubwa wa kufiwa na mama yake mzazi.
Mama wa mchezaji huyo, Alhaja Monsurati Martins, alifariki Alhamisi baada ya kupata mstuko alipokuwa akijisalimisha toka nyumbani kwake baada ya gari la mafuta kuwaka moto nje ya nyumba yao.
Obafemi ameruhusiwa kurudi kwao Lagos, Nigeria na atakosa maandalizi ya Klabu yake kwa ajili ya msimu mpya na hivyo kumweka hatihati kama atakuwa fiti kuanza kwa msimu huu.




Friday 25 July 2008


SULLEY MUNTARI KUTUA INTER MILAN?
Dau la Pauni milioni 12.7 liko njiani kumtoa Sulley Muntari wa Ghana mwenye miaka 23 kutoka Klabu ya Portsmouth kwenda Klabu ya Italia Inter Milan.
Taarifa zinasema baada ya Meneja wa Inter, Jose Mourinho, kumkosa Frank Lampard imebidi atafute kiungo wa haraka na karata imemwangukia Muntari ambae alisajiliwa na Portsmouth kutoka Klabu ya Italia Udinese mwezi Mei, 2007.

Thursday 24 July 2008

Sunderland wametangaza kumsaini kiungo wa Tottenham Teemu Tainio, umri miaka 28 ambae ni raia wa Finland, kwa mkataba wa miaka mitatu.
Wachezaji wengine wa Tottenham wanaohusishwa kujiunga na Sunderland ni Steed Malbranque, Younes Kaboul na Pascal Chimbonda.

Nao West Ham wamemsajili mchezaji wa Kimataifa wa Uswisi Valon Behrami kutoka Lazio ya Italia.
Behrami, miaka 23, hucheza kama beki wa kulia au kiungo, amesaini mkataba wa miaka mitano na aliichezea Uswisi mechi zake zote za EURO 2008.
Powered By Blogger