Saturday 26 July 2008



KIPA ROBINSON AJIUNGA BLACKBURN!

Aliekuwa Kipa nambari wani wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Paul Robinson, miaka 28, amesainiwa na Blackburn Rovers kutokea Tottenham Hotspurs kwa mkataba wa miaka mitano. Kipa huyo alikuwa na wakati mbaya katika msimu uliopita kwa kupoteza namba kwenye Timu ya Uingereza na vilevile Klabu yake ya Tottenham kumuona ameshuka kiwango kilichowalazimu kumnunua Kipa mwingine toka Klabu ya Uholanzi PSV Eindhoven Heurelho Gomes ambae ni raia wa Brazil.
Robinson inaelekea atachukua namba ya Kipa wa siku nyingi hapo Blackburn Mmarekani Brad Friedel anaekamilisha taratibu za kuhamia Aston Villa.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Neville arefusha mkataba Everton
Nahodha wa Everton, Phillip Neville, miaka 31, ambae ni mdogo wake Nahodha wa Man U, Gary Neville, amesaini mkataba mpya Everton utakaomweka hapo hadi 2012.
Phillip Neville alijiunga Everton mwaka 2005 akitokea Man U timu aliyoichezea tangu akiwa chekechea pamoja na kaka yake Gary.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
OBAFEMI AFIWA NA MAMA MZAZI!
Kuukosa mwanzo wa msimu mpya LIGI KUU UINGEREZA!
Mshambuliaji wa Newcastle, Mnigeria Obafemi Martins, huenda akaukosa mwanzo wa msimu mpya wa LIGI KUU UINGEREZA baada ya kupata msiba mkubwa wa kufiwa na mama yake mzazi.
Mama wa mchezaji huyo, Alhaja Monsurati Martins, alifariki Alhamisi baada ya kupata mstuko alipokuwa akijisalimisha toka nyumbani kwake baada ya gari la mafuta kuwaka moto nje ya nyumba yao.
Obafemi ameruhusiwa kurudi kwao Lagos, Nigeria na atakosa maandalizi ya Klabu yake kwa ajili ya msimu mpya na hivyo kumweka hatihati kama atakuwa fiti kuanza kwa msimu huu.




No comments:

Powered By Blogger