Saturday 14 June 2008

RATIBA YA LIGI KUU MSIMU 2008/09 KUTOLEWA JUMATATU
Msimu wa LIGI KUU UINGEREZA wa 2008/09 utaanza rasmi wikiendi ya tarehe 16 AGOSTI 2008 na ratiba kamili ya msimu huo itatangazwa JUMATATU tarehe 16 JUNI 2008.
RATIBA ITAONEKANA HAPA SIKU HIYOHIYO.

Mbali ya kuanza rasmi msimu wa ligi tarehe 16 AGOSTI 2008, kawaida msimu huzinduliwa rasmi wiki moja kabla kwa MABINGWA WATETEZI WA LIGI KUU kupambana na BINGWA WA KOMBE LA FA katika UWANJA WA WEMBLEY kuwania NGAO YA HISANI.

Hivyo tarehe 10 AGOSTI 2008, MAN U, ambae ndie BINGWA WA LIGI KUU, watacheza na PORTSMOUTH, alienyakua KOMBE LA FA msimu uliopita.

KUNDI C: ni kweli KUNDI LA KIFO!

Netherlands 4-1 France

Italy 1-1 Romania

Uholanzi imeshajikita Robo Fainali huku Romania yenye pointi 2 iko mlangoni kuingia robo fainali wakati 'vizito' Italia na Ufaransa wakiwa na pointi moja kila mmoja wako hatarini kutolewa.

Endapo Romania ataifunga Uholanzi, timu ambayo itakuwa ikikamilisha ratiba tu, kwenye mechi ya mwisho basi mechi ya Italia na Ufaransa haina maana yeyote.
Pichani kipa wa Italia Buffon akiokoa penalti iliyopigwa na Adrian Mutu wa Italia na kuiwezesha Italia kutoka 1-1 na Romania.
MECHI ZA LEO:
KUNDI D
saa 1 usiku: SWEDEN vs SPAIN
saa 3.45 usiku: UGIRIKI vs URUSI

Friday 13 June 2008

Leo kufa au kupona kwa 'vizito' Italy na France
Mabingwa wa Dunia Italy wako kwenye hatari ya kutolewa kwenye Euro 2008 endapo watafungwa mechi ya leo watakapokumbana na Romania wakati kipigo kwa France kwenye mechi yao na Uholanzi kutawaweka France njia panda.
Uholanzi wanaongoza kundi hili la C lililobatizwa 'KUNDI LA KIFO' kwa kuwa na pointi 3 wakifuatiwa na France na Romania wenye pointi 1 huku Italy hawana kitu.
Wakati Italy wakipigana kufa kupona, kikosi cha Uholanzi chini ya Marco van Basten wanapewa nafasi kubwa kubeba EURO 2008 hasa baada ya kuwabamiza Italia siku ya Jumatatu kwa mabao 3-0.
Nao Wafaransa, waliotoka 0-0 na Romania, watakuwa wakiomba nyota wao waliokuwa majeruhi hasa Nahodha Patrick Vieira na mshambuliaji Thierry Henry wawe na uwezo wa kucheza leo.
EVRA AONGEZA MKATABA
Mlinzi alieng'ara sana msimu uliopita, Mfaransa Patrice Evra, ameongezewa mkataba na klabu yake ya Manchester United na hivyo atabaki OLD TRAFFORD hadi mwaka 2012.
Evra, ambae kwa sasa yuko kwenye kikosi cha Ufaransa EURO 2008, ameshashinda LIGI KUU UINGEREZA mara 2 na KLABU BINGWA ULAYA mara moja tangu ajiunge MAN U.
Akiwa mwenye furaha, Evra alisema: 'Misimu miwili ilopita ilikuwa kama ndoto nzuri kwangu! Ni furaha na sifa kubwa kuwa mmoja wa timu hii bora na kufundishwa na Sir Alex Ferguson na wasaidizi wake.'

UVUMI….wachezaji kuhama na…………..!!!



  • Meneja mpya wa Chelsea Scolari ana kitita cha Mamilioni ya Pauni za Kiingereza alizopewa na mmiliki Abramovitch kuwabeba Fernando Torres, Frank Ribery na Kaka.

  • Nyota wa Arsenal Emmanuel Adebayor ana shauku kuhama Emirates Stadium kwenda AC Milan.

  • Nia ya Arsenal kumsaini kiungo wa Marseille Samir Nasri inaelekea itapigwa chini na Atletico Madrid ambao nao wanamtaka mchezaji huyo.

  • Sir Alex Ferguson tayari ameingia vitani na Luiz Felipe Scolari kwa kumtaka Meneja huyo mpya wa Chelsea ambaye kwa sasa anaiongoza Ureno kwenye EURO 2008 aache kumshawishi Cristiano Ronaldo kuhamia Real Madrid.

  • Na baada ya kuondoka Scolari kwenda Chelsea, Ureno itamchukua Meneja msaidizi wa Man U Carlos Queiroz ili awe Meneja wa Ureno.

MATOKEO KUNDI B:


Croatia 2-1 Germany


Croatio wametua Robo Fainali ya EURO 2008 baada ya mabao ya Darijo Srna na Ivica Olic kuwaua Ujerumani. Lukas Podolski alifunga bao moja kwa Ujerumani.


Austria 1-1 Poland
Refa wa Kiingereza Howard Webb jana aliwaokoa wenyeji wenza AUSTRIA kutolewa EURO 2008 kama wenzao USWISI baada ya kuwapa penalti dakika za majeruhi ambayo Ivica Vastic alifunga na kuwawezesha kutoka sare 1-1 na Poland na hivyo kubaki wanasuasua EURO 2008.
Nalo goli la kipindi cha kwanza la Poland lililofungwa na Roger Guerreiro, Mpoland aliezaliwa Brazil, lilikuwa la utata kwani mfungaji alionekana dhahiri ameotea.


LEO KUNDI C ['kundi la kifo']:


Saa 1 usiku: ITALIA vs RUMANIA
Saa 3.45 usiku: UHOLANZI vs UFARANSA



Thursday 12 June 2008

Rooney afunga ndoa Italy


Mchezaji wa MAN U Wayne Rooney amemuoa kipenzi chake cha tangu utotoni Coleen McLoughlin huko mjini Portofino, Italy hapo jana katika sherehe fupi, ndogo na iliyohusisha familia tu.

Mume na mke, wote wenye umri wa miaka 22, walikutana kwa mara ya kwanza wakiwa na miaka 12 na uhusiano wao kimahaba ulianza wakiwa na miaka 16 huko Liverpool ambako wote ndio walikulia.






MECHI ZA LEO:
KUNDI B

SAA 1 USIKU: CROATIA vs UJERUMANI

SAA 3.45 USIKU: AUSTRIA vs POLAND

KUNDI A:
URENO IKO ROBO FAINALI

CZECH 1 URENO 3

Christiano Ronaldo alipachika bao moja na kutengeneza jingine na kuiwezesha timu yake kuwa ya kwanza kutinga robo fainali baada ya ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Czech.

USWISI 1 UTURUKI 2

Wenyeji Uswisi, licha ya kuongoza kwa bao moja, wajikuta wakipigwa 2-1 na Uturuki na hivyo kuwa timu ya kwanza kutolewa nje ya mashindano.


CHELSEA WAMTAJA SCOLARI MENEJA MPYA

Luis Felipe Scolari, ambae aliingoza Brazil kuwa Bingwa wa Dunia mwaka 2002 pia kuifikisha Ureno fainali ya EURO 2004 na ambae ameshashinda vikombe tisa na klabu mbalimbali huko kwao Brazil, ametajwa ndie Meneja mpya wa Brazil.
Mbrazil huyo mwenye miaka 59 anakuwa Meneja wa nne tangu mmiliki Roman Abramovich ainunue klabu. Waliotangulia na kutimuliwa ni Claudio Ranieri, Jose Mourinho na Avram Grant.

Ataanza kazi rasmi tarehe 1 Julai 2008.

Wednesday 11 June 2008

Switzerland v Turkey

SAA 3.45 USIKU KIWANJA: St Jakob-Park, Basel

Nahodha wa Switzerland, Alex Frei, hatocheza kwa kuwa ni majeruhi baada ya kuumizwa goti katika mechi ya kwanza ya ufunguzi waliyofungwa na Czech bao 1-0 na ni pigo kubwa kwa Uswisi.

Lakini pia Uturuki watamkosa Nahodha wao Emre, mchezaji wa NEWCASTLE, Uingereza, alieumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Ureno.

Mechi hii kati ya USWISI na UTURUKI ina kivutio kikubwa na cha pekee sana kwani Uswisi inategemewa kuwachezesha wachezaji watatu ambao wana uraia wa nchi mbili-USWISI na UTURUKI- ambao ni viungo Gokhan Inler, Yakin na mshambuliaji Eren Derdiyok.

"Mechi na Uturuki itakuwa spesho kwani familia yangu inatoka huko UTURUKI," Yakin alisema.

"Nna marafiki wengi Uturuki na wako moto na mechi hii ingawa lazima wataishabikia Uturuki. Hata Mama yangu ana wasiwasi wa kuwa na nchi zake zote mbili zikishindana lakini yeye daima yuko upande wa timu ya watoto wake."



Czech Republic v Portugal






SAA: 1 USIKU KIWANJA: Stade de Geneve, Geneva.

Kipa wa Czech Petr Cech ambae pia huichezea Chelsea ametamka kwamba Timu yao ya Czech haina haja ya kumuogopa Winga Cristiano Ronaldo katika mechi yao leo ya KUNDI A.
'Ndio ni mchezaji bora, mmoja wa wazuri sana duniani, lakini peke yake hawezi kushinda chochote.'
'Kitu ambacho kiko wazi........' Aliongeza Cech. ' ......mshindi wa leo atakuwa na pointi sita na ni wazi ukiwa na pointi 6 utasonga mbele. '

Tuesday 10 June 2008




Spain 4-1 Russia
Goli 3 zilizofungwa na David Villa dakika ya 20, 45 na 75 na lile la Fabregas zimeipatia ushindi Uhispania wa mabao 4-1 katika mechi yao ya kwanza waliyocheza na Urusi.
Timu zilikuwa:

Spain: Casillas, Sergio Ramos, Marchena, Puyol, Capdevila, Silva (Alonso 77), Senna, Xavi, Iniesta (Santi Cazorla 63), Villa, Torres (Fabregas 54). MAGOLI: Villa 20, 45, 75, Fabregas 90.
Russia:
Akinfeev, Aniukov, Shirokov, Kolodin, Zhirkov, Sychev (Bystrov 46), Zyryanov, Semak, Semshov (Torbinsky 57), Bilyaletdinov, Pavluchenko, Bystrov (Adamov 70).
GOLI: Pavluchenko 86.
WATAZAMAJI: 30,000
Refa: Konrad Plautz (Austria).

Greece 0-2 Sweden



Zlatan Ibrahimovic alifunga bao safi dakika ya 67 na Petter Hansson alimalizia patashika langoni mwa Ugiriki na kuwawezesha Sweden kuwabamiza MABINGWA WATETEZI WA ULAYA UGIRIKI 2-0.



MECHI ZA KESHO:
saa 1 usiku: URENO vs CZECH

saa 3 dak 45 usiku: USWISI vs UTURUKI
SAKATA LA RONALDO
MAN U wawashitaki REAL FIFA!
Mabingwa wa LIGI KUU UINGEREZA na ULAYA, MAN U wamewashitaka REAL MADRID kwenye bodi inayoongoza soka duniani FIFA kwa kumrubuni mchezaji wao Ronaldo kinyume na taratibu.
Taarifa iliyotolewa na MAN U iliripoti:
'Tarehe 27 MEI 2008, United ilitangaza rasmi nia yake kuishitaki Real endapo wataendelea kujihusisha na hatma ya baadae ya Ronaldo. Kwa bahati mbaya, Real wameendelea kumsakama mchezaji wetu. Klabu inaona haina njia ila kuwasilisha malalamiko yetu kwa FIFA.'
FIFA imethibitisha kupokoa kabrasha la malamiko hayo.




FRANCE 0
ROMANIA 0!

Katika mechi ilyopooza, Ufaransa na Romania zilitoka sare ya 0-0.

Kwenye mechi iliyofuata ya Kundi hilo C, kundi ambalo wengi wamelibatiza 'KUNDI LA KIFO', Uholanzi ilifanya mauaji makubwa baada ya kuibamiza Italia kwa mabao 3-0. Goli lenye utata la Ruud Van Nistelrooy kwenye dakika ya 26 na la pili la Wesley Sneijder dakika ya 31 liliwafanya Uholanzi kuwa mbele 2-0 hadi mapumziko.
Giovanni van Bronckhorst alipachika bao la tatu kwa kichwa dakika ya 80 na kuwaacha Uholanzi wakioongoza Kundi C.

LEO NI MECHI ZA KUNDI D wakati SPAIN na URUSI zitapocheza saa 1 usiku huko Innsbruck na watafuatiwa na UGIRIKI na SWEDEN mjini Salzburg saa 3 dakika 45.

Monday 9 June 2008

Podolski awaadhibu Poland!
UJERUMANI 2 POLAND 0!
Magoli mawili yaliyofungwa na Podolski yameifanya UJERUMANI ibembee kwenye EURO 2008.
Podolski ambae alizaliwa Poland alifunga goli la kwanza dakika ya 20 na la pili dakika ya 72.

Sunday 8 June 2008




Austria 0-1 Croatia
Kama ilivyokuwa jana kwa USWISI na leo yamewakuta wenyeji wenza AUSTRIA walipofungwa 1-0 kwa bao la penalti dakika 3 tu tangu kuanza mchezo.
AUSTRIA kama wenyeji wenzao USWISI walitawala mechi yote ila walishindwa kutikisa nyavu.

Pichani ni MAREFA 12 watakaochezesha mechi za EURO 2008.
Kila Refa na wasaidizi wake wawili kwenye mechi watakuwa wanatoka nchi moja.
NCHI WATOKAZO MAREFA, MAJINA NA UMRI KATIKA MABANO:
AUSTRIA: Konrad Plautz [43], UGIRIKI: Kyros Vassaras [41], SLOVAKIA: Ľuboš Michĕl [39], UBELGIJI: Frank De Bleeckere, ITALIA: Roberto Rosetti [40], HISPANIA: Manuel Mejuto González [42], UINGEREZA: Howard Webb [36], UHOLANZI: Pieter Vink [40], SWEDEN: Peter Fröjdfeldt [44], UJERUMANI: Herbert Fandel [43], NORWAY: Tom Henning Øvrebø [41], USWISI: Massimo Busacca [38]

Ronaldo hajaamua 'hatma yake'
Jana baada ya kuiongoza nchi yake URENO kuishinda UTURUKI 2-0 kwenye mechi yao ya ufunguzi ya EURO 2008, Cristiano Ronaldo amesema hajaamua nini hatma yake na atatoa kauli baada ya Ureno kumaliza EURO 2008.
Real Madrid wanamuwinda staa huyo kwa udi na uvumba huku Manchester United waking’ang’ania hawataki katakata kusikia biashara hiyo wakidai Ronaldo bado ana mkataba wa miaka minne na wametishia kuishtaki Real FIFA kwa kumrubuni mchezaji huyo.
Hata hivyo, mchezaji mwenzake Ronaldo katika Timu ya Taifa ya Ureno Ricardo Carvalho, ambae ni beki wa Chelsea, anaamini Ronaldo atabaki Man United.
Hiyo jana, Carvalho aliongea:'Ana furaha Man U na atabaki huko'



USWISI 0 CZECH 1
Wenyeji Uswisi walicheza vizuri sana katika mechi ya ufunguzi ya EURO 2008 lakini wakajikuta wakipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Czech.
Bao la Czech lilifungwa na mchezaji alieingizwa kipindi cha pili Vaclav Sverkos katika dakika ya 70.
Uswisi walipata pigo pale Nahodha wao Alexander Frei alipoumia goti na hivyo atayakosa mashindano yote ya EURO 2008.
URENO 2 UTURUKI 0
Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Pepe dakika ya 61 na la pili lililofungwa na Raul Mereiles katika dakika za majeruhi zimeipa mwanzo mzuri Ureno waliposhinda 2-0 dhidi ya Uturuki hapo jana.

Mechi zote hizo ni za jana ni KUNDI A.
MECHI ZA LEO:
saa 1 usiku: AUSTRIA vs CROATIA
uwanja: ERNST HAPPEL STADION, mjini Vienna, Austria.
Wenyeji wenza wa EURO 2008 AUSTRIA wanatua uwanjani leo kuumana na CROATIA. Hii ni mara ya kwanza kwa AUSTRIA kucheza fainali za Mataifa ya Ulaya wakati CROATIA ni timu yenye sifa kwa kuwa timu nzuri na ngumu.
VIKOSI:
AUSTRIA
Meneja: Josef Hickersberger
Kepteni: Andreas Ivanschitz

Alexander Manninger (AC Siena),Juergen Macho (AEK Athens), Ramazan Ozcan (TSG 1899 Hoffenheim), Gyorgy Garics (Napoli), Ronald Gercaliu (Austria Vienna), Martin Hiden (Kaernten), Markus Katzer (Rapid Vienna), Juergen Patocka (Rapid Vienna)Emmanuel Pogatetz (Middlesbrough), Sebastian Proedl (Sturm Graz), Martin Stranzl (Spartak Moscow), Rene Aufhauser (Salzburg), Christian Fuchs (Mattersburg) Andreas Ivanschitz (Panathinaikos), Umit Korkmaz (Rapid Vienna), Christoph Leitgeb (Salzburg), Juergen Saeumel (Sturm Graz), Joachim Standfest (Austria Vienna), Ivica Vastic (Linz), Erwin Hoffer (Rapid Vienna), Roman Kienast (Ham-Kam),Roland Linz (Braga), Martin Harnik (Werder Bremen)
CROATIA
Meneja: Slaven Bilic [Mlinzi wa zamani WEST HAM na EVERTON]
Kepteni: Niko Kovac
Stipe Pletikosa (Spartak Moscow), Vedran Runje (RC Lens), Mario Galinovic, (Panathinaikos), Vedran Corluka (Manchester City), Dario Simic (AC Milan)Robert Kovac (Borussia Dortmund), Josip Simunic (Hertha Berlin), Dario Knezevic (Livorno), Hrvoje Vejic (Tom Tomsk), Danijel Pranjic (Heerenveen), Darijo Srna (Shakhtar Donetsk), Niko Kovac (Salzburg), Luka Modric (Tottenham)Niko Kranjcar (Portsmouth), Jerko Leko (Monaco), Ivan Rakitic (Schalke 04)Ognjen Vukojevic (Dinamo Zagreb), Nikola Pokrivac (Monaco), Mladen Petric (Borussia Dortmund), Ivica Olic (Hamburg SV), Ivan Klasnic (Werder Bremen), Igor Budan (Parma)Nikola Kalinic (Hajduk Split

saa 3 dakika 45 usiku: UJERUMANI vs POLAND
uwanja: WORTHERSEE STADION, mjini KLAGENFURT, AUSTRIA
Wakati Ujerumani wanawania ubingwa wa nne wa Kombe la Ulaya, Poland hajawahi kuchukua hata mara moja.
Vilevile, Poland wameandamwa na majeruhi huku kipa wa MAN U Tomasz Kuszczak akijitoa kwenye kikosi baada ya kuumia uti wa mgongo siku ya Ijumaa.
VIKOSI:
GERMANY
Meneja: Joachim Low
Kepteni: Michael Ballack
Jens Lehmann (Arsenal), Robert Enke (Hanover 96), Rene Adler (Bayer Leverkusen)Christoph Metzelder (Real Madrid), Per Mertesacker (Werder Bremen), Philipp Lahm (Bayern Munich), Arne Friedrich (Hertha Berlin), Marcell Jansen (Bayern Munich), Clemens Fritz (Werder Bremen), Heiko Westermann (Schalke 04), Michael Ballack (Chelsea), Thomas Hitzlsperger (VfB Stuttgart), Simon Rolfes (Bayer Leverkusen), Torsten Frings (Werder Bremen), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Piotr Trochowski (Hamburg SV), Tim Borowski (Werder Bremen), David Odonkor (Real Betis), Miroslav Klose (Bayern Munich), Lukas Podolski (Bayern Munich), Mario Gomez (VfB Stuttgart), Kevin Kuranyi (Schalke 04), Oliver Neuville (Borussia Moenchengladbach)
POLAND
Meneja: Leo Beehakker
Kepteni: Maciej Zurawski
Artur Boruc (Celtic), Tomasz Kuszczak (Manchester United), Lukasz Fabianski (Arsenal), Marcin Wasilewski (Anderlecht), Pawel Golanski (Steaua Bukarest), Mariusz Jop (FC Moscow), Jacek Bak (Austria Vienna), Michal Zewlakow (Olympiakos), Adam Kokoszka (Wisla Krakow), Jakub Wawrzyniak (Legia Warsaw), Dariusz Dudka (Wisla Krakow), Michal Pazdan (Gornik Zabrze), Mariusz Lewandowski (Shakhtar Donetsk)Jakub Blaszczykowski (Borussia Dortmund), Rafal Murawski (Lech Poznan), Lukasz Gargula (GKS Belchatow), Jacek Krzynowek (VfL Wolfsburg), Roger Guerreiro (Legia Warsaw), Wojciech Lobodzinski (Wisla Krakow), Euzebiusz Smolarek (Racing Santander), Maciej Zurawski (Larissa), Marek Saganowski (Southampton), Tomasz Zahorski (Gornik Zabrze)
MECHI ZA KESHO
saa 1 usiku: ROMANIA vs UFARANSA
saa 3 dakika 45: UHOLANZI vs ITALIA
Powered By Blogger