Wednesday, 11 June 2008

Switzerland v Turkey

SAA 3.45 USIKU KIWANJA: St Jakob-Park, Basel

Nahodha wa Switzerland, Alex Frei, hatocheza kwa kuwa ni majeruhi baada ya kuumizwa goti katika mechi ya kwanza ya ufunguzi waliyofungwa na Czech bao 1-0 na ni pigo kubwa kwa Uswisi.

Lakini pia Uturuki watamkosa Nahodha wao Emre, mchezaji wa NEWCASTLE, Uingereza, alieumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Ureno.

Mechi hii kati ya USWISI na UTURUKI ina kivutio kikubwa na cha pekee sana kwani Uswisi inategemewa kuwachezesha wachezaji watatu ambao wana uraia wa nchi mbili-USWISI na UTURUKI- ambao ni viungo Gokhan Inler, Yakin na mshambuliaji Eren Derdiyok.

"Mechi na Uturuki itakuwa spesho kwani familia yangu inatoka huko UTURUKI," Yakin alisema.

"Nna marafiki wengi Uturuki na wako moto na mechi hii ingawa lazima wataishabikia Uturuki. Hata Mama yangu ana wasiwasi wa kuwa na nchi zake zote mbili zikishindana lakini yeye daima yuko upande wa timu ya watoto wake."



No comments:

Powered By Blogger