Saturday, 3 October 2009

MAN U 2 SUNDERLAND 2
Mabingwa Watetezi Manchester United, wakicheza chini ya kiwango, itabidi wamshukuru Anton Ferdinand, mdogo wake Rio Ferdinand aliekuwa benchi la Man U, kwa kujifunga mwenyewe na kuisawazishia Man U dakika za majeruhi.
Mpaka mapumziko Sunderland walikuwa mbele kwa bao 1-0 Mfungaji akiwa Darren Bent dakika ya 8 kwa goli ambalo wengi wanaamini Kipa Ben Foster angeweza kulicheza.
Dimitar Berbatov alisawazisha kipindi cha pili kwa goli zuri sana.
Lakini ni Kipa Ben Foster tena badala ya kupanchi mpira akataka kudaka na kumpa mwanya Straika Kenwyne Jones kuushindilia wavuni.
Kama kawaida, Sir Alex Ferguson alibadilisha Kikosi chake tofauti na kile kilichocheza Jumatano kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE na hilo liliathiri sana uchezaji.
LIGI KUU ENGLAND: Baada ya kukosa Mishahara Portsmouth wapata pointi zao za kwanza!!
Wolves 0 Portsmouth 1
Portsmouth ambao wamefungwa mechi zao zote tangu Ligi Kuu ianze msimu huu na juzi kutangazwa Wachezaji hawajalipwa Mishahara na pia Mmiliki wao toka Dubai Sulaiman al Fahim kulazwa hospitalini ili afanyiwe operesheni kutoa vijiwe kwenye figo, leo imepata pointi zake za kwanza tena ikiwa ugenini baada ya kuifunga Wolverhampton bao 1-0.
Goli la ushindi kwa Portsmouth lilifungwa na Hassan Yebda, Mchezaji Mfaransa, ambae yuko Portsmouth kwa mkopo kutoka Benfica.
MATOKEO MECHI ZA LEO Jumamosi, Oktoba 3
Bolton 2 v Tottenham 2
Burnley 2 v Birmingham 1
Hull City 2 v Wigan 1
Wolverhampton 0 v Portsmouth 1
Fergie na Torres ni Bora Septemba
Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na Straika wa Liverpool, Fernando Torres, wameshinda Tuzo ya Ligi Kuu England ya Meneja Bora na Mchezaji Bora kwa mwezi Septemba.
Sir Alex Ferguson ameshinda Tuzo ya Meneja Bora ikiwa ni mara yake ya 24 kuitwaa kwa kuiongoza Manchester United kushika uongozi kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda mechi zao zote za mwezi Septemba ambapo walianza kwa kuifunga Tottenham huko White Hart Lane 3-1, kisha kuwafunga Watani wao Man City 4-3 Old Trafford na kushinda Britannia Stadium 2-0 dhidi ya Stoke City.
Man U vilevile walicheza mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwezi Septemba na kuifunga Besiktas 1-0 ugenini huko Ugiriki na pia kuilaza Wolfsburg Old Trafford 2-1.
Fernando Torres ametunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora ikiwa ni mara yake ya pili kuipata kwa kufunga mabao matano mwezi Septemba. Torres, mpaka sasa, ndie anaeongoza kwa Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu akiwa na bao 8.
Berbatov aliwahi kutekwa nyara!!!
Mshabuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, ametoboa kuwa miaka 10 iliyopita alitekwa nyara na Gangsta mkubwa huko kwao Bulgaria aitwae Georgi Iliev aliewatuma vibaraka wake watatu kumkamata ili kumlazimisha asaini Klabu ya Levski Kjustendil iliyomilikiwa na jambazi hilo.
Wakati huo, Berbatov alikuwa Mchezaji wa CSKA Sofia huko Bulgaria.
“Ni kweli!” Berbatov alithibitisha. “Ilitisha lakini nilifanikiwa kumpigia simu Baba yangu alieniokoa!”
Akizungumzia presha anayoipata kwa kuchezea Klabu kubwa kama Manchester United, Berbatov alisema: “Ni presha kubwa! Sibishi kuwa mtu akilipa pesa nyingi kwa ajili yako anategemea vitu vikubwa toka kwako!”
Kesho ni “Ze Bi Mechi” huko Scotland: Rangers v Celtic!!!
Ingawa Timu hizo vigogo za Scotland hazifanyi vizuri kwenye mashindano ya UEFA huko Ulaya huku Rangers wakiwa mkiani kwenye Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Celtic wakiwa mkiani pia Kundini mwao kwenye EUROPA LIGI, kesho Uwanja wa Ibrox, nyumbani kwa Rangers, moto utawaka kwenye “dabi” inayozikutanisha Timu za Glasgow huko Scotland.
Mpaka sasa Celtic yuko mbele ya Rangers kwa pointi 4 baada ya mechi 6 na ndie anaeongoza Ligi Kuu Scotland akiwa na pointi 16.
Rangers ndie Bingwa Mtetezi wa Scotland.
TATHMINI MECHI ZA LIGI KUU WIKIENDI HII: “Ze Bigi Mechi” ni Jumapili Chelsea v Liverpool!!!
Chelsea watakuwa wenyeji wa Liverpool Uwanjani Stamford Bridge katika “Ze Bigi Mechi” siku ya Jumapili.
Chelsea walianza Ligi vizuri mno lakini wikiendi iliyopita walipata kipigo kitakatifu mikononi mwa Wigan walipokung’utwa 3-1 mechi ambayo ilimfanya Nahodha wa Chelsea John Terry kuwalaumu Wachezaji wenzake na pia kumfanya Meneja wao Carlo Ancelotti ajisahau kwa hasira na kuzungumza na Wachezaji wake Kitaliano.
Vinara wa Ligi Kuu na Mabingwa Watetezi Manchester United watawakaribisha Sunderland Old Trafford, Blacburn Rovers watasafiri hadi Emirates Stadium kucheza na Arsenal, West Ham na Fulham watacheza katika “dabi” ya London.
Ingawa Chelsea walipigwa kwenye Ligi Kuu wikiendi iliyopita walirudia tena ushindi pale walipocheza katikati ya wiki ugenini huko Cyprus na kuifunga Apoel Nicosia bao 1-0 kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Wapinzani wa Chelsea Jumapili hii, Liverpool, walionja joto ya jiwe walipotandikwa 2-0 na Fiorentina huko Italia kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE siku ya Jumanne.
Mechi hiyo ilimfanya BosI wao Rafa Benitez kuiponda timu yake na kuwaambia walicheza mchezo mbovu ingawa aliahidi Jumapili watabadilika.
Chelsea watacheza mechi ya Jumapili kwa kujiamini hasa kwa vile hawajapoteza mchezo wa Ligi hapo kwao Stamford Bridge tangu Novemba, 2008 ingawa safari hii watapambana na Straika anaeng’ara sana Fernando Torres.
Lakini jambo la kutia wasiwasi kwa Liverpool ni udhaifu wa ngome yao hasa Jamie Carragher anaeonyesha kupwaya mno msimu huu.
Jumamosi, Tottenham wanasafiri hadi Kaskazini Magharibi mwa England kwenda Uwanja wa Reebok kucheza na Bolton Wanderers iliyo chini ya Meneja Gary Megson ambae ameifanya timu yake katika mechi tatu za hivi karibuni kuvuna pointi 7. Tottenham ambao kawaida hawafanyi vizuri uwanjani Reebok watajipa moyo kidogo hasa kwa kuanza kampeni yao ya Ligi msimu huu kwa mguu mzuri mno.
Wolverhampton Wanderers watapambana na Portsmouth walio mkiani na ambao wamefungwa mechi zao zote za Ligi msimu huu.
Burnley na Birmingham City, timu zilizopanda Daraja msimu huu, zitakutana uso kwa uso na Burnley watajifariji mno kwa takwimu ya kuwa na pointi 9 ambazo zote wamezipatia Uwanja wa nyumbani Turf Moor ikiwa pamoja na kuzifunga Manchester United na Everton.
Hull City, timu inayozama kwa spidi kali msimu huu, itawakaribisha KC Stadium Wigan ambao ndio wababe wa Chelsea waliyoifunga mechi yao ya mwisho ya Ligi goli 3-1. Msimu uliokwisha katika mechi kama hii, Wigan walibandika Hull mabao 5-0.
Mabingwa Manchester United wataialika Sunderland Old Trafford huku Veterani wao Ryan Giggs akiwa ndie Staa wao kwa hivi karibuni. Sunderland iko chini ya Mchezaji wa zamani wa Mabingwa hao Steve Bruce.
Jumapili Arsenal wanacheza na Blackburn Emirates Stadium ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Arsene Wenger tangu kuingia kwa mwaka wake wa 14 akiwa na Arsenal ambayo ni rekodi katika historia ya Klabu hiyo kwa kuwa ni Meneja aliedumu muda mrefu zaidi.
Mechi ya ushindani ni ile ‘dabi’ ya Timu za London West Ham v Fulham Klabu ambazo msimu huu zinasuasua na ziko chini kwenye msimamo wa Ligi zote zikiwa zimefungwa mechi 4 katika 5 walizocheza mwisho.
Huko Goodison Park, Wenyeji Everton wakiwa na Mshambuliaji wao Luis Saha ambae yuko kwenye fomu watapambana na Stoke City. 
FIFA U20 WORLD CUP EGYPT 2009:
Ghana, Germany, Korea na Uruguay zaingia Raundi ya Pili!!
Kipigo cha Cameroun chaibeba Nigeria kusonga mbele kama Mshindi wa 3!!!
Cameroun ilichapwa mabao 3-0 na Germany na hivyo kuipa mwanya Nigeria iliyomaliza Kundi lake nafasi ya 3 kuingia kama mmoja wa Washindi wa 3 bora na kuibwaga Cameroun.
Katika Kundi la Cameroun, Germany ndie Mshindi wa 1 na South Korea wa pili.
Ghana amemaliza Kundi D akiwa Mshindi wa kwanza na Uruguay wa pili.
Washindi wa Kwanza na wa Pili kila Kundi wanasonga mbele pamoja na Washidi wa nafasi ya tatu bora 6 kati ya Timu 8 zitakazomaliza nafasi hiyo.
Mpaka sasa Timu zilizoingia Raundi ya Pili ni:
KUNDI A: Egypt, Paraguay
KUNDI B: Spain, Venezuela, Nigeria
KUNDI C: Germany, South Korea
KUNDI D: Ghana, Uruguay
KUNDI E: Brazil, Czech Republic
KUNDI F: UAE na nyingine kujulikana leo.
MATOKEO MECHI ZA JANA Ijumaa, Oktoba 2:
Germany 3 v Cameroun 0
Uzbekistan 1 v England 1
South Korea 3 v USA 0
Uruguay 2 v Ghana 2
MECHI ZA LEO Jumamosi, Oktoba 3:
-South Africa v Honduras
-Hungary v UAE
-Australia v Brazil
-Costa Rica v Czech Republic
RATIBA LIGI ZA ULAYA:
BUNDESLIGA:
MATOKEO: Ijumaa, Oktoba 2:
Schalke 04 2 v Eintracht Frankfurt 0
RATIBA:
Jumamosi, Oktoba 3
Bayer 04 Leverkusen v FC Nurnberg
Bayern Munich v FC Koln
Hannover v SC Freiburg
VFL Bochum v VfL Wolfsburg
FSV Mainz v TSG Hoffeinheim
Borussia Munchen Gldbach v VB Borussia Dortmund
Jumapili, Oktoba 4
VfB Stuttgart v SV Werder Bremen
Hertha Berlin v Hamburger SV
ITALIA SERIE A:
Jumamosi, Oktoba 3
As Bari v Catania
Inter Milan v Udinese
Jumapili, Oktoba 4
Atalanta v AC Milan
Bologna v Genoa
AS Roma v Napoli
Sampdoria v Parma
Siena v Livorno
Cagliara v Chievo Verona
Fiorentina v SS Lazio
Palermo v Juventus
SPAIN LA LIGA:
Jumamosi, Oktoba 3:
Cd Tenerife v Deportivo La Coruna
FC Bacerlona v UD Almeria
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Jumapili, Oktoba 4
Real Valladolid v Athletic de Bilbao
Villareal v Espanyol
Sporting Gijon v Real Mallorca
Getafe v Osasuna
Xerez CD v Malaga CF
Racing de Santander v Valencia
Sevilla v Real Madrid

Friday, 2 October 2009

LIGI KUU ENGLAND :
RATIBA
[saa za bongo]
Jumamosi, Oktoba 3
[mechi zote saa 11 jioni isipokuwa ikitajwa]
Bolton v Tottenham
Burnley v Birmingham
Hull City v Wigan
Manchester United v Sunderland [saa 1 na nusu usiku]
Wolverhampton v Portsmouth
Jumapili, Oktoba 4
Arsenal v Blackburn [saa 9 na nusu mchana]
Chelsea v Liverpool [saa 12 jioni]
Everton v Stoke City [saa 11 jioni]
West Ham v Fulham [saa 11 jioni]
Jumatatu, Oktoba 5
Aston Villa v Man City
Keegan ashinda Kesi, kulipwa Pauni Milioni 2 fidia kwa kutimuliwa Newcastle!!
Meneja wa zamani wa Newcastle ameshinda kesi kwenye Tume ya Ajira aliyodai hakutendewa haki pale alipoandoka Newcastle na sasa Newcastle itabidi imlipe fidia ya Pauni Milioni 2 pamoja na riba.
Tume hiyo ilikubaliana na Keegan kuwa Klabu ilikiuka mkataba na Keegan pale ilipoamua kumnunua Kiungo kutoka Uruguay Ignacio Gonzalez bila ridhaa ya Keegan na hapo ndipo Keegan aliamua kung’atuka Newcastle Septemba 2008.
Keegan alijiunga na Newcastle Januari 2008 kuchukua nafasi ya Sam Allardyce alietimuliwa.
Owen kurudi uwanjani mapema!!
Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen anategemewa kurudi uwanjani mapema kuliko ilivyotegemewa awali baada ya Wataalam kuthibitisha maumivu yake ya paja si mabaya kama ilivyoogopwa.
Owen alicheza dakika 20 tu za kwanza kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE siku ya Jumatano Man U walipoifunga Wolfsburg 2-1.
Sir Alex Ferguson amethibitisha Owen anaweza kucheza mechi ya Ligi Kuu na Bolton tarehe 17 Oktoba na pia alisema Kipa Edwin van der Sar, alievunjika kidole cha mkono, na Beki Chipukizi Rafael da Silva, aliefanyiwa upasuaji begani, wote wamepona na wako mazoezini ingawa hawategemewi kucheza mechi ya kesho ya Ligi Kuu na Sunderland itakayochezwa Old Trafford.
Rooney kutocheza mkewe akijifungua!!
Straika nyota wa Manchester United, Wayne Rooney, amesema kwake familia yake ni muhimu kupita soka na hivyo hatocheza mechi siku mkewe akijifungua mtoto wao wa kwanza.
Mkewe Rooney, Coleen, ni mja mzito na anatarajiwa kujifungua mtoto wao wa kwanza tarehe 24 Oktoba, siku ambayo ndiyo bethidei ya Rooney, na tarehe hiyo ni siku 3 tu baada ya Manchester United kucheza Moscow, Urusi na CSKA Moscow kwenye UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Rooney amesema: “Ikitokea kitu kabla ya kusafiri kwenda Moscow basi sitoenda kucheza lakini kama mambo ni kama tunavyotegemea ntacheza tu!”
FIFA WORLD CUP U20 EGYPT 2009
Wenyeji Egypt, Spain, Paraguay na Venezuela zaingia Raundi ya Pili!!
Wenyeji Egypt wamesonga mbele kuingia Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 20 kwa kuwafunga Italy 4-2 na hivyo kuongoza Kundi A.
Paraguay, baada ya kutoka suluhu 0-0 na Trinidad 7 Tobago, imeshika nafasi ya pili na pia kusonga mbele.
Italia ipo nafasi ya 3 na itasubiri kukamilika kwa mechi za Makundi mengine ili kujua kama watafuzu kuingia Raundi ya Pili kwa Tiketi ya Timu zilizoshika nafasi ya 3 bora.
Nigeria waliomaliza nafasi ya 3 Kundi B wapo kwenye hali kama Italia.
Kundi B timu zilizofuzu ni Spain alieshika nafasi ya kwanza na Venezuela wa pili.
MATOKEO:Alhamisi, Oktoba 1:
-Tahiti 0 v Nigeria 5
-Venezuela 0 v Spain 3
-Italy 2 v Egypt 4
-Trinidad & Tobago 0 v Paraguay 0
MECHI ZA LEO Ijumaa, Oktoba 2:
Germany v Cameroun
South Korea v USA
Uruguay v Ghana
Uzbekistan v England

Thursday, 1 October 2009


EUROPA LIGI: FC BATE Borisov 1 Everton 2
Everton waliokuwa ugenini huko Minsk, Belarus bila ya Wachezaji wao 7 wa Kikosi cha kwanza waliokosekana kwa kuwa majeruhi au wagonjwa walijikuta wako nyuma kwa bao moja hadi mapumziko lakini mabao ya kipindi cha pili ya Marouane Fellaini na Tim Cahill yaliwapa ushindi wa bao 2-1 kwenye mechi ya Kundi lao kwenye EUROPA LIGI.
Mechi nyingine za Timu za Uingereza zinazochezwa leo na zilizoanza muda si mrefu uliopita ni kati ya Celtic v Rapid Vienna na Fulham v Basle.
Rooney: Wanatuponda bureeee!!!!!
Wayne Rooney amesistiza Manchester United sasa inaanza kuwaonyesha waliokuwa wanaiponda kwa kudai kuwa kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kumewaathiri kwamba wao bado imara kwa vile wanaongoza Ligi Kuu England na pia wako juu kwenye Kundi lao kwenye mashindano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE baada ya kushinda mechi mbili ya kwanza ikiwa ugenini huko Uturuki walipoifunga Besiktas 1-0 na ya pili ile ya jana walipowabwaga Mabingwa wa Ujerumani Wolfsburg Old Trafford mabao 2-1.
Rooney amesema: “Binafsi nadhani tumelaumiwa bure! Ndio tulifungwa na Burnley lakini tumeshinda mechi zote nyingine!”
Rooney amekiri kuondoka kwa Ronaldo ni pengo lakini amesema Man U sasa wanacheza soka ya staili tofauti kwa vile msimu uliopita mipira ilichezwa kupitia Ronaldo lakini sasa Timu inacheza kitimu na Wafungaji ni wengi.
Mpaka sasa Rooney ndie anaeongoza kwa ufungaji ndani ya Man U kwa kupachika bao 6.
Wakati huohuo, Meneja wa Man U Sir Alex Ferguson ameahidi kumchezesha golini Kipa Ben Foster siku ya Jumamosi mechi ya Ligi Kuu huko Old Trafford watakapokutana na Sunderland. Jana, katika mechi na Wolfsburg, langoni alikuwa Kipa Tomasz Kuszczak.
FAINI NA KIFUNGO CHA NJE KWA ADEBAYOR!!!
Mshambuliaji wa Manchester City Emmanuel Adebayor leo ameamriwa kulipa Faini ya Pauni Elfu 25 pamoja na kufungiwa mechi 2 baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kwa kosa la kwenda kushangilia goli alilofunga mbele ya Mashabiki wa Arsenal siku Timu yake Man City ilipoipiga Arsenal 4-2 Uwanja wa City of Manchester kwenye mechi ya Ligi Kuu hivi karibuni.
Kitendo hicho kiliwakera Washabiki wa Arsenal na wakataka kuvamia uwanja lakini Polisi na Walinzi wakawadhibiti na purukashani hizo zilisababisha Mlinzi mmoja kupoteza fahamu.
Polisi wa Manchester walithibitisha kitendo cha Adebayor ndiyo chanzo cha zogo hilo la Washabiki.
Adebayor ambae alikuwa Mchezaji wa Arsenal kabla ya kuhamia Man City kwa sasa anatumikia kifungo cha mechi 3 kwa kosa la kumtimba kwa makusudi Mchezaji wa Arsenal Robin van Persie katika mechi hiyo hiyo.
Hata hivyo adhabu ya kufungiwa mechi 2 kwa utovu wa nidhamu inasimamishwa ili kuchunguza mwenendo wake na hivyo ataruhsiwa kucheza mechi akimaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 kwa kosa la van Persie adhabu ambayo sasa inakwisha na anategemewa kucheza mechi na Aston Villa Jumatatu ijayo. 

Wenger aweka rekodi Arsenal
Sasa Arsene Wenger ndie Meneja aliedumu muda mrefu katika historia ya Arsenal baada ya kuifikia na kuipita rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na George Alison ambae alikuwa Meneja wa Arsenal kwa miaka 13 hadi mwaka 1947.
Wenger, ambae ni Mfaransa, alianza kazi ya Umeneja Arsenal mwaka 1996 akitokea Japan.
Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Arsenal, Mike Dean, ndie aliemleta Wenger hapo Arsenal na wakati huo watu wengi walishangazwa na hatua hiyo hasa kwa vile Wenger alikuwa hatambuliki huko Uingereza.
Lakini katika msimu wake wa kwanza tu na Arsenal, Wenger alimudu  kuifanya Arsenal itwae Ubingwa na kunyakua Kombe la FA.
Dean anaeleza: "Tulimchukua huku Klabu kubwa kama Bayern Munich zilikuwa zikimtaka. Alifanya mabadiliko makubwa alipoingia Arsenal. Alibadili hali za Wachezaji kuanzia ulaji, mazoezi na maisha yao! Yeye ni msomi! Amesomea Udaktari, Uchumi na ana ufahamu wa mambo mengi!!"

Wachezaji Portsmouth hawajalipwa Mishahara!!
Klabu ya Portsmouth imetangaza kuwa Wachezaji na Wafanyakazi
wa Klabu hiyo watalipwa Mishahara yao katika masaa 24 yajayo baada ya Mmiliki mpya wa Klabu hiyo kutoka Dubai Sulaiman al Fahim kutuma fedha kwa lengo hilo.
Klabu hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na matatizo ya kifedha hivi karibuni ilinunuliwa na Tajiri huyo kutoka Dubai ambae pia ndie aliesuka na kushughulikia ununuzi wa Manchester City kwa Familia moja ya Koo ya Kifalme kutoka Abu Dhabi.
Sulaiman al Fahim yeye binafsi ndie alieinunua Portsmouth.
FIFA U20 WORLD CUP EGYPT 2009:
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumatano, Septemba 30:
Australia 0 Costa Rica 3
Brazil 0 Czech Republic 0
Hungary 4 South Africa 0
UAE 1 Honduras 0
MECHI ZA LEO Alhamisi, Oktoba 1:
Trinidad & Tobago v Paraguay
Italy v Egypt
Venezuela v Spain
Tahiti v Nigeria
Man U 2 Wolfsburg 1
Owen acheza dakika 20 tu, aumia!!!
Manchester United wakiwa nyumbani Old Trafford walijikuta wako nyuma kwa bao 1-0 bao lilofungwa dakika ya 56 kwa kichwa na Edin Dzeko lakini wakajitutumua na kusawazisha dakika 3 baadae pale frikiki ya Ryan Giggs ilipobabatiza ukuta wa Wolfsburg na kumhadaa Kipa wao.
Mshambuliaji wa Man U Michael Owen alianza mechi ya jana lakini alidumu dakika 20 tu na ilibidi atolewe nje baada ya kujitonesha paja aliloumia wiki iliyokwisha na Dimitar Berbatov akaingia badala yake.
Kutolewa kwa Owen ni pigo kwa Mchezaji huyo anaelilia namba Kikosi cha Timu ya England hasa kwa kuwa Kocha wa England Fabio Capello alikuwa shuhuda wa mechi hiyo.
Zikiwa zimesalia dakika 12, Giggs, baada ya hekaheka za Rooney, alimtengeneza mpira murua Michael Carrick aliefumua shuti na kuipa ushindi Manchester United.
Kwa ushindi wa jana, Man U wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 6, Wolfsburg na CSKA Moscow ni wa pili wakiwa na pointi 3 kila mmoja. Besiktas yuko mkiani bila pointi.
Mechi zinazofuata Kundi hili ni Oktoba 21 kati ya CSKA Moscow v Man U NA Wolfsburg v Besiktas.
Apoel Nicosia 0 Chelsea 1
Katika mechi mbili za UEFA CHAMPIONS LEAGUE za Kundi ambazo Chelsea wameshazicheza, Mshambuliaji Nicolas Anelka ndie mkombozi kwa kuifungia bao moja na la ushindi katika mechi hizo.
Mechi ya kwanza Anelka aliifunga FC Porto na jana huko Cyprus Anelka alipachika bao moja na la ushindi.
Kwa ushindi wa jana, Chelsea wanaongoza Kundi lao kwa pointi 6, FC Porto wa pili akiwa na pointi 3 na wamwisho ni Apoel Nicosia na Atletico Madrid waliofungana wakiwa na pointi moja moja.
Mechi zinazofuata ni Chelsea v Atletico Madrid na FC Porto v Apoel Nicosia.
Wakati Fergie akimsifia Giggs, Ancelotti akasirishwa na Chelsea yake!!!
Sir Alex Ferguson amemminia sifa Veterani wake Ryan Giggs kwa kusababisha ushindi wa jana dhidi ya Wolfsburg alipofunga bao la kwanza na la kusawazisha na kutengeneza la pili na la ushindi.
Ferguson amesema: “Giggs ni tishio! Amepata sifa nyingi miaka yake yote ya uchezaji na sijui utaongeza nini! Kitu cha kushangaza ni kuwa bado anaonekana mbichi!!”
Giggs, anaetimiza miaka 36 mwezi ujao, jana alifunga goli lake la 150 na pia kuungana na Raul wa Real Madrid kwa kuwa Wachezaji pekee waliofunga mabao katika misimu 14 ya UEFA waliyocheza.
Na huko Chelsea, licha ya ushindi wa ugenini wa bao 1-0 walipoifunga Apoel Nicosia, Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amekasirishwa na uchezaji hafifu wa Timu yake na imedaiwa aliwabatukia Wachezaji wake baada ya mechi.
Chelsea wikiendi iliyokwisha walifungwa 3-1 kwenye Ligi Kuu na Wigan na jana ulikuwa ndio mchezo wao wa kwanza baada ya kipigo hicho na mechi inayofuata ni ile ‘Ze Bigi Mechi” Jumapili watakapovamiwa na Liverpool Stamford Bridge kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Ancelotti amesema: “Sikuridhika. Nataka Chelsea icheze vyema. Nataka wadhibiti, wacheze kwa moyo. Lazima tubadilike.Matokeo ni mazuri lakini uchezaji mbovu!”
Real 3 Marseille 0
Mabao ya kipindi cha pili ya Wachezaji wa bei mbaya, Ronaldo [mawili] na Kaka [moja], yaliwapa ushindi wa 3-0 juu ya Marseille ya Ufaransa ambayo ilicheza mtu 10 nusu saa ya mwisho baada ya Souleymane Diawara kuonekana kumchezea faulo Ronaldo na kutolewa nje.
Faulo hiyo iliipa Real penalti ambayo Kaka aliifunga.
MATOKEO MECHI ZA Jumatano, Septemba 30:
AC Milan 0 v FC Zurich 1
Apoel Nicosia 0 v Chelsea 1 
Bayern Munich 0 v Juventus 0
Bordeaux 1 v Maccabi Haifa 0
CSKA Moscow 2 v Besiktas 1
FC Porto 2 v Atletico Madrid 0
Manchester United 2 v Wolfsburg 1 
Real Madrid 3 v Marseille 0
MECHI ZIJAZO ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Jumanne, 20 Oktoba 2009
AZ Alkmaar v Arsenal
Barcelona v Rubin Kazan
Debrecen v Fiorentina
Inter Milan v Dynamo Kiev
Liverpool v Lyon
Olympiakos v Standard Liege
Rangers v Unirea Urziceni
VfB Stuttgart v Sevilla
________________________________________
Jumatano, 21 Oktoba 2009
Bordeaux v Bayern Munich
CSKA Moscow v Man United
Chelsea v Atletico Madrid
FC Porto v Apoel Nicosia
FC Zurich v Marseille
Juventus v Maccabi Haifa
Real Madrid v AC Milan
Wolfsburg v Besiktas
________________________________________
Jumanne, 3 Novemba 2009
AC Milan v Real Madrid
Apoel Nicosia v FC Porto
Atletico Madrid v Chelsea
Bayern Munich v Bordeaux
Besiktas v Wolfsburg
Maccabi Haifa v Juventus
Man United v CSKA Moscow
Marseille v FC Zurich________________________________________
Jumatano, 4 Novemba 2009
Arsenal v AZ Alkmaar
Dynamo Kiev v Inter Milan
Fiorentina v Debrecen
Lyon v Liverpool
Rubin Kazan v Barcelona
Sevilla v VfB Stuttgart
Standard Liege v Olympiakos
Unirea Urziceni v Rangers

Wednesday, 30 September 2009

LEO UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Apoel Nicosia v Chelsea
Leo saa 3 dakika 45 usiku, saa za bongo, Chelsea wanashuka Uwanja wa GSP Nicosia uliopo mjini Nicosia, Visiwani Cyprus, kucheza na Wenyeji wao Apoel Nicosia katika mechi ya pili Kundini mwao katika kinyang’anyiro cha UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Chelsea watashuka dimbani bila Nyota wao Michael Ballack, John Mikel Obi na Ashley Cole ambao ni majeruhi pamoja na Didier Drogba na Jose Bosingwa ambao bado wako kifungoni.
Ingawa Apoel Nicosia hawapewi nafasi kubwa kwenye mechi hii, Kocha wao Ivan Jovanovic anaamini wanaweza kufanya vizuri hasa baada ya kucheza vizuri katika mechi ya kwanza walipokuwa ugenini huko Spain na kutoka suluhu na Atletico Madrid.
Chelsea waliifunga FC Porto ya Ureno bao 1-0 katika mechi ya awali ya Kundi hili.
Mechi nyingine kwenye Kundi hili ni FC Porto v Atletico Madrid.
Manchester United v VfB Wolfsburg
Ndani ya Old Trafforf jijini Manchester, Mashetani Wekundu Man U watakwaana na Mabingwa wa Ujerumani Wolfsburg katika mechi ya pili ya Kundi lao kuwania Kombe la UEFA Champions LEAGUE.
Mechi nyingine ya leo kwenye Kundi hili ni kati ya CSKA Moscow v Besiktas.
Man U ilishinda mechi yake ya kwanza Kundini kwa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Besiktas na Wolfsburg, ikiwa nyumbani, iliibamiza CSKA Moscow 3-1.
Man U leo huenda ikaikosa nguvu kazi ya Winga Park Ji-sung ambae ni mgonjwa na pia upo wasiwasi kuhusu Michael Owen ambae ana tatizo dogo pajani.
Kipa Veterani Edwin van der Sar ameshapona na ameanza mazoezi lakini inaaminika leo Ben Foster ataendelea kuwa golini kwani van der Sar hajapata mazoezi ya kutosha.
Wolfsburg huenda wakamkosa Nahodha wao Josue mwenye matatizo ya goti ambalo alifanyiwa operesheni hivi karibuni.
Hata hivyo, nguvu ya Wolfsburg ni Mshambuliaji hatari toka Brazil Grafite na mwingine kutoka Bosnia, Edin Dzeko, Wachezaji ambao hupewa sapoti kubwa na mwenzao kutoka Bosnia pia aitwae Zvjezdan Misimovic.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
“BWAWA LA MAINI” laingia ruba!!! Benitez aishambulia Timu yake!!
Jovetic aichoma mkuki moyoni Liverpool!!
Fiorentina 2 Liverpool 0
Arsenal, Barcelona, Lyon zapeta, Inter ngoma ngumu Urusi!!!
Rangers yatandikwa 4-1 kwao!!
Huko Florence, Italia, Fiorentina ilitandaza soka safi hasa kipindi cha kwanza na na kuibandika Liverpool bao 2-0 kwenye pambano la UEFA CHAMPIONS LEAGUE hapo jana.
Mabao yote ya Fiorentina yalifungwa na Kijana wa miaka 19 kutoka Montenegro, Stevan Jovetic, kwenye kipindi hicho cha kwanza huku akishirikiana vyema na Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu.
Kipigo hicho kimemfanya Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, aishambulie Timu yake kwa maneno: “Walituzidi kila kitu, tulikuwa wabovu kila sehemu kipindi cha kwanza! Lakini naamini Jumapili tutabadilika tukicheza na Chelsea!”
Mechi nyingine kwenye Kundi hili la Liverpool ilikuwa ni kati ya Debrecen na Lyon na Lyon kuibuka mshindi wa mabao 4-0.
Nao, Arsenal, wakicheza nyumbani Emirates Stadium, walitawala kabisa mechi yao na Olympiakos inayofundishwa na Mbrazil Zico lakini ilibidi wasubiri hadi dakika ya 78 ndipo walipopata bao la kwanza kupitia Robin van Persie na kisha dakika ya 86 Mrusi Andry Arshavin akaongeza la pili.
Nazo, Barcelona na Lyon, zilishinda mechi zao huku Barca ikiipiga Dynamov Kiev 2-0 kwa mabao ya Lionel Messi na Pedro Rodriguez na Lyon kushinda ugenini kwa mabao 4-0 dhidi ya Debrecen.
Timu ya Kocha Jose Mourinho, Inter Milan, ikicheza ugenini huko Urusi, waliambulia suluhu ya 1-1 walipocheza na Rubin Kazan na kumaliza mechi hiyo wakiwa mtu 10 baada ya Mchezaji wao Mario Baloteli kutolewa nje kwa Kadi mbili za Njano.
Rangers ya Scotland ilichabangwa nyumbani kwake mabao 4-1 na Sevilla ya Spain huku mabao yote yakitinga kipindi cha pili.
Mabao ya Sevilla yalifungwa na Konko, Adriano, Luis Fabiano na Fredi Kanoute.
Bao la Rangers liliwekwa na Nacho Novo.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA JANA Jumanne, Septemba 29:
Arsenal 2 Olympiakos 0
AZ Alkmaar 1 Standard Liege 1
Barcelona 2 Dynamo Kiev 0
Debrecen 0 Lyon 4
Fiorentina 2 Liverpool 0
Rangers 1 Sevilla 4
Rubin Kazan 1 Inter Milan 1
Unirea Urziceni 1 VfB Stuttgart 1
MECHI ZA LEO Jumatano, Septemba 30:
AC Milan v FC Zurich
Apoel Nicosia v Chelsea
Bayern Munich v Juventus
Bordeaux v Maccabi Haifa
CSKA Moscow v Besiktas
FC Porto v Atletico Madrid
Manchester United v Wolfsburg
Real Madrid v Marseille
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009:
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumanne, Septemba 29:
-South Korea 1 Germany 1
-Uruguay 3 Uzbekistan 0
-USA 4 Cameroun 1
-Ghana 4 England 0
MECHI ZA LEO: Jumatano, Septemba 30:
-Australia v Costa Rica
-Brazil v Czech Republic
-Hungary v South Africa
-UAE v Honduras

Tuesday, 29 September 2009

Daktari Mkuu FIFA ataka Marefa kutoa Kadi Nyekundu nyingi!!!
Daktari Mkuu wa FIFA, Michel D’Hooghe, amewataka Marefa wawe wakali zaidi na kutoa Kadi Nyekundu zaidi ili kudhibiti rafu mbaya ambazo huleta madhara makubwa kwa Wachezaji.
Daktari huyo katika utafiti wake amegundua kuwa kutokana na ongezeko la utajiri kwenye Soka vilevile rafu mbaya na kuumia vibaya kwa Wachezaji kumeongezeka kwani utajiri huo umeleta ushindani mkubwa na hivyo Timu na hasa Wachezaji wako tayari kujitoa muhanga ili kupata ushindi kwa njia yeyote ile.
Daktari D’Hooghe anasema: “Refa ndio ufunguo! Yeye akitoa Kadi Nyekundu anahakikisha Mchezaji anaadhibiwa palepale! Hilo litakuwa tishio kwa wengine!”
Utafiti wa Daktari D’Hooghe umeonyesha kuwa katika Fainali za Kombe la Dunia huko Korea na Japan mwaka 2002 Wachezaji 12 waliumia vibaya kwa kupigwa ngwala toka nyuma na vipepsi lakini katika Fainali za Kombe hilo huko Ujerumani mwaka 2006, baada ya Marefa kuagizwa kutoa Kadi Nyekundu bila woga kwa rafu hizo, ni Wachezaji wawili tu ndio waliumizwa.
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009:
Wenyeji Misri watunguliwa dakika za majeruhi!!
Misri 1 Paraguay 2
Misri, ambao ndio wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia la Vijana wa Chini ya Miaka 20, jana walifungwa na Paraguay mabao 2-1 na goli la ushindi la Paraguay iliyocheza na watu 10 baada ya Mchezaji wao Robert Huth kutolewa kipindi cha kwanza lilifungwa kwenye dakika ya 4 ya dakika za majeruhi.
Kwenye Kundi hili la Misri, Italy na Paraguay ndio wanaoongoza kwa kuwa na pointi 4 kila mmoja na Misri anafuatia akiwa na pointi 3 huku Trinidad & Tobago yuko mkiani bila pointi.
Mechi za mwisho Kundi hili ni Misri v Italy na Paraguay v Trinidad & Tobago.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Leo Arsenal v Olympiakos na Fiorentina v Liverpool
Arsenal watajimwaga nyumbani Emirates Stadium kuwakaribisha Olympiakos na Liverpool watakuwa Nchini Italia kupambana na Fiorentina zikiwa ni mechi za pili kwa kila Timu katika Makundi yao.
Arsenal alifungua dimba huko Ubelgiji na kuibwaga Standard Liege mabao 3-2 wakati Liverpool alianza kampeni zake nyumbani Anfield na kuwafunga Debrecen bao 1-0.
Leo Arsenal watacheza bila ya Kipa nambari wani Manuel Almunia ambae ni mgonjwa na nafasi yake itachukuliwa na Kipa mdogo toka Italia Vito Mannone ambae aling’ara kwenye mechi ya Ligi Kuu Arsenal aliyoifunga Fulham bao 1-0 hapo juzi.
Arsenal pia itawakosa Kiungo Denilson ambae ameumia na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili pamoja na Mshambuliaji Nicklas Bendtner aliepata ajali ya gari siku ya Jumapili.
Hata hivyo Arsenal wana habari njema kwamba huenda Chipukizi Nyota Theo Walcott ambae hajacheza tangu Juni kwa kuwa na maumivu huenda akawepo leo.
Olympiakos, ambao wana Kocha mpya Nyota wa zamani wa Brazil Zico alieanza kazi hiyo Septemba 17, walianza kampeni yao kwenye Kombe hili kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AZ Alkmaar.
Liverpool watapambana huko Italia na Fiorentina klabu ambayo ilipoteza mechi yake ya kwanza kwenye mashindano haya walipofungwa bao 1-0 na Lyon na pia Mshambuliaji wao nyota Alberto Gilardino kutolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kumpiga kipepsi Jeremy Toulalan wa Lyon katika mechi hiyo.
Kukosekana kwa Gilardino kutatoa nafasi kwa Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu na mwenziwe Stevan Jovetic kuanza mechi hii.
Liverpool watakuwa na pengo kwani itawakosa Viungo Javier Mascherano na Yossi Benayoun ambao ni majeruhi na pengo hilo huenda likazibwa na Albert Riera.
LIGI KUU England: Man City 3 West Ham 1
Ndani ya Uwanja wao City of Manchester, Manchester City jana usiku waliifunga West Ham mabao 3-1 katika mechi pekee ya Ligi Kuu.
Mabao mawili yaliyofungwa na Mchezaji wa zamani wa West Ham ambae baadae alihamia Manchester United, Carlos Tevez, na moja la Petrov ndio yaliyowaua West Ham.
Bao la West Ham lilifungwa na Mshambuliaji wao anaeinukia vizuri kwa sasa Carlton Cole.
Dakika 5 tu tangu mpira uanze krosi ya Petrov ilimkuta Tevez aliefunga huku goli likiwa jeupe na kuwaomba radhi Mashabiki wake wa zamani wa West Ham waliokuwa nyuma ya goli hilo.
Cole akaisawazishia West Ham dakika ya 24 lakini kwenye dakika ya 32 frikiki ya Petrov iliwapa Man City bao la pili.
Carlos Tevez akaihakikishia Timu yake Manchester City ushindi kwa bao la kipindi cha pili dakika ya 61.
Mpaka sasa Man City wako nafasi ya 6 wakiwa wamecheza mechi 5 na wana pointi 12.
FIFA U-20 WORLD CUP Egypt 2009:
MATOKEO MECHI ZA Jumatatu, Septemba 28:
-Nigeria 0 v Spain 2
-French Polynesia- Tahiti 0 v Venezuela 8
-Italy 2 v Trinidad and Tobago 1
-Egypt 1 v Paraguay 2

MECHI ZA LEO Jumanne Septemba 29:
-South Korea v Germany
-USA v Cameroun
-Uruguay v Uzbekistan
-Ghana v England

Monday, 28 September 2009

Arsenal yapata pigo! Kiungo Denilson nje miezi miwili! Klabu ya Arsenal leo imethibitisha kwamba Kiungo wao Mbrazil, Denilson, hataonekana uwanjani kwa miezi miwili baada ya kuvunjika mfupa mgongoni na inasemekana alipata maumivu hayo katika mechi ya tarehe 12 Septemba 2009 Arsenal ilipofungwa 4-2 na Manchester City.
Vile vile imejulikana leo kuwa Mshambuiaji wao kutoka Denmark Nicklas Bendtner hatacheza mechi ya kesho ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Olympiakos baada ya kupata ajali ya gari ingawa hamna taarifa zaidi zilizopatikana kuhusu janga hilo.
Cech ahoji Kadi Nyekundu aliyotwangwa!!!
Kipa wa Chelsea, Petr Cech, ambae alipewa Kadi Nyekundu na Refa Phil Dowd kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi walipofungwa na Wigan 3-1 baada ya kumwangusha Mshambuliaji Hugo Rodallega, amehoji uhalali wa Kadi hiyo kwa kudai kuwa yeye hakuwa mtu wa mwisho kwani Beki wake Ashley Cole alishakuwa nyuma yake kudhibiti shambulizi hilo.
Kwa Kadi hiyo, Cech ataikosa “Ze Bigi Mechi” ya Jumamosi wakati Chelsea watakapowakaribisha Liverpool Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu.
Steve Bruce amfokea Straika wake Bent kwa kuikacha Penalti!!!
Meneja wa Sunderland Steve Bruce amekerwa na kitendo cha Mshambuliaji wake Darren Bent kutopiga penalti na kumwachia Mshambuliaji mwenzake Kenwyne Jones kuipiga na kufunga bao la pili la Sunderland katika mechi ambayo Sunderland waliifunga Wolverhampton mabao 5-2 kwenye Ligi Kuu.
Katika mechi hiyo Sunderland walifunga bao la kwanza kwa penalti Mfungaji akiwa Darren Bent ambae Steve Bruce amemtaja kuwa ndie pekee mwenye majukumu ya kupiga penalti za Sunderland.
Mara baada ya mapumziko, huku Sunderland wakiwa 1-0 mbele, Sunderland wakapewa penalty baada ya Darren Bent kuangushwa kwenye boksi na ndipo Kenwyne Jones akamwomba Bent kupiga mkwaju huo na Bent akamwachia Jones aliefunga bao la pili.
Steve Bruce amesema: “Darren Bent ni mpigaji penalti bora duniani na yeye pekee ndie anatakiwa kupiga penalti zetu! Penalti ile ya pili ni muhimu, sasa je tungeikosa wakati tuna bao moja tu? Afadhali ingekuwa tuko mbele 5-0! Ntahakikisha kitendo hiki hakirudiwi!”
RATIBA YA SOKA WIKI HII:
UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Jumanne, Septemba 29
Arsenal v Olympiakos
AZ Alkmaar v Standard Liege
Barcelona v Dynamo Kiev
Debrecen v Lyon
Fiorentina v Liverpool
Rangers v Sevilla
Rubin Kazan v Inter Milan
Unirea Urziceni v VfB Stuttgart
Jumatano, Septemba 30
AC Milan v FC Zurich
Apoel Nicosia v Chelsea
Byern Munich v Juventus
Bordeaux v Maccabi Haifa
CSKA Moscow v Besiktas
FC Porto v Atletico Madrid
Manchester United v Wolfsburg
Real Madrid v Marseille
EUROPA LIGI:
Alhamisi, Oktoba 1
[Kuna jumla ya mechi 24 ila zinazotajwa hapa ni zile za Timu za Uingereza tu]
BATE v Everton
Celtic v Rapid Vienna
Fulham v Basle
LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi, Oktoba 3
Bolton v Tottenham
Burnley v Birmingham
Hull City v Wigan
Manchester United v Sunderland
Wolverhampton v Portsmouth
Jumapili, Oktoba 4
Arsenal v Blackburn
Chelsea v Liverpool
Everton v Stoke City
West Ham v Fulham
Jumatatu, Oktoba 5
Aston Villa v Man City
LEO MAN CITY v WEST HAM!!!!
Gianfranco Zola: "Bellamy alinifanya niwe Meneja Bora!!"
Meneja wa West Ham ambae aliwahi kuwa Staa wa Chelsea, Gianfranco Zola, amepasua kuwa Mchezaji mkorofi sana Craig Bellamy ambae sasa yuko Manchester City alimpa wakati mgumu alipokuwa West Ham na kumfanya yeye aongezeke uzoefu wa kuwa Meneja Bora.
Bellamy, Raia wa Wales, aliihama West Ham Januari mwaka huu na kujiunga na Manchester City.
Bellamy alipokuwa Liverpool ilibidi aihame Timu hiyo baada ya kudaiwa kumpiga na gongo la kuchezea Gofu mchezaji mwenzake John Riise na ashawahi kufarakana na Alan Shearer alipokuwa Newcastle.
Wiki moja iliyopita Bellamy alitawala vichwa vya habari Magazetini baada ya kumzaba kibao shabiki alievamia Uwanja wa Old Trafford baada ya mechi kati ya Man U na Man City kumalizika kwa ushindi wa 4-3 kwa Man U.
FA, Chama cha Soka cha England, kimempa onyo kali Bellamy kwa kitendo hicho.
Na leo usiku, Timu ya Craig Bellamy, Manchester City, itapambana na Klabu yake ya zamani, West Ham na Meneja wa West Ham, Gianfranco Zola ametamka: "Nilipenda kufanya nae kazi! Ni kitu kigumu kwani ni mtu mwenye munkari! Lakini ukimchukulia kwa njia ipasayo ni Mchezaji anaekulipa kwa juhudi zake uwanjani!"
Zola ameendelea: "Amenipa uzoefu na manufaa katika kazi ya Umeneja!"
John Terry awakandya wenzake Chelsea!!
Nahodha wa Chelsea, John Terry, amewalaumu sana Wachezaji wenzake kufuatia kipigo chao cha Jumamosi cha mabao 3-1 walichoangushiwa na Timu 'dhaifu' Wigan ambayo katika mechi zake mbili za nyuma ilibugizwa 5-0 na Manchester United na 4-0 na Arsenal.
Kipigo hicho toka kwa Wigan na ushindi wa Man U wa bao 2-0 dhidi ya Stoke City kumewafanya Man U ambao ndio Mabingwa Watetezi, kushika hatamu LIGI KUU England.
Chelsea, ambao hawajachukua Ubingwa kwa miaka mitatu sasa tangu wautwae kwa mara mbili mfululizo chini ya Meneja Jose Mourinho, inaelekea wamekerwa sana na kipigo hicho na kufikia hatua ya kumfanya Terry kudiriki kuanika mzozo wao wa ndani ya Klabu hadharani.
Terry amekaririwa akilalama: "Ni kawaida kucheza vibaya lakini hata ukicheza vibaya unategemea Wachezaji wenzako kujituma na kupigana! Timu nzima haikufanya hivyo! Timu kubwa zote zimeshinda wikiendi hii na hili linavunja moyo! Tuna mechi Jumatano, itabidi tufanye vizuri! Na Jumapili ijayo tuna mechi ngumu na Liverpool na itabidi tujitutumue!" 
RATIBA SOKA LEO: Jumatatu Septemba 28 [saa za bongo]
LIGI KUU England:
Manchester City v West Ham [saa 4 usiku]
FIFA KOMBE LA DUNIA U-20 MISRI 2009:
KUNDI B:
Nigeria v Spain [saa 11 jioni]
Tahiti v Venezuela [saa 1 dak 45 usiku]
KUNDI A:
Italy v Trinidad & Tobago [saa 1 dak 45 usiku]
Egypt v Paraguay [saa 4 na nusu usiku]

Sunday, 27 September 2009

LIGI KUU England: Mvua ya Magoli yazidi kuteremka!!!
Sunderland 5 Wolverhampton 2
Wakiwa nyumbani Stadium of Light, Sunderland leo walishusha kipigo cha mabao 5-2 dhidi ya Wolverhampton na mawili kati ya mabao hayo ya Sunderland yalikuwa ni penalti.
Sunderland walipata bao la kwanza kwa penalti iliyofungwa na Darren Bent na hadi mapumziko bao lilikuwa hilo moja.
Kipindi cha pili tu kuanza, Sunderland wakapata penalti ya pili Mfungaji safari hii akiwa Kenwyne Jones.
Wolves walipata matumaini baada ya mpira kumbabatiza Defenda mpya wa Sunderland kutoka Ghana John Mensah na kutinga wavuni. Dakika chache baadae Wolves wakasawazisha kupitia kwa Straika wao Kevin Doyle.
Lakini Kenwyne Jones akawapeleka mbele tena Sunderland kwa mkwaju mkali na mabao kupitia Michael Turner na Darren Bent yakawamaliza Wolves.
LIGI KUU England itaendelea tena kesho usiku saa 4 saa za bongo wakati Manchester City watakapowakaribisha West Ham Uwanjani City of Manchester.
FIFA U-20 WORLD CUP-EGYPT 2009
Vumbi latimka Jngwani Misri: Mashindano ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 20 huko Misri!!
Tangu Alhamisi iliyokwisha, Nchi 24 toka kila kona ya Dunia zipo Nchini Misri kushiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 20 na fungua dimba ilikuwa kati ya Wenyeji Misri na Trinidad and Tobago na wenyeji hao kuibuka kidedea kwa kushinda mabao 4-1.
Nchi hizo zimegawanywa Makundi 6 ya Timu 4 kila moja na Timu mbili kila Kundi zitasonga mbele pamoja na Timu 4 zitakazomaliza kama Washindi wa Tatu kwenye Kundi lakini wenye matokeo bora:
KUNDI A: Egypt, Trinidad & Tobago, Paraguay, Italy.
KUNDI B: Nigeria, Venezuela, Spain, Tahiti
KUNDI C: USA, Germany, Cameroun, South Korea
KUNDI D: Ghana, Uzbekistan, England, Uruguay
KUNDI E: Brazil, Costa Rica, Czech Republic, Australia
KUNDI F: UAE, South Africa, Honduras, Hungary
Ijumaa Septemba 25 kulikuwa na mechi tatu na matokeo ni:
-Paraguay 0 Italy 0
-Nigeria 0 Venezuela 1
-Spain 8 French Polynesia- Tahiti 0
Jana Jumamosi mechi 4:
-USA 0 Germany 3
-Ghana 2 Uzbekistan 1
-Cameroun 2 South Korea 0
-England 0 Uruguay 1
Leo, Jumapili Septemba 27, mechi ni:
-Brazil 5 v Costa Rica 0
-UAE 2 v South Africa 2
-Czech Republic 2 v Australia 1
-Honduras v Hungary
[Matokeo mechi nyingine za leo tutaleta baadae]
Jumatatu, Septemba 28:
-Nigeria v Spain
-French Polynesia- Tahiti v Venezuela
-Italy v Trinidad and Tobago
-Egypt v Paraguay
Jumanne, Septemba 29:
-South Korea v Germany
-USA v Cameroun
-Uruguay v Uzbekistan
-Ghana v England
Jumatano, Septemba 30:
-Australia v Costa Rica
-Brazil v Czech Republic
-Hungary v South Africa
-UAE v Honduras
Alhamisi, Oktoba 1:
-Tahiti v Nigeria
-Venezuela v Spain
-Italy v Egypt
-Trinidad & Tobago v Paraguay
Ijumaa, Oktoba 2:
-Germany v Cameroun
-South Korea v USA
-Uzbekistan v England
-Uruguay v Ghana
Jumamosi, Oktoba 3:
-South Africa v Honduras
-Hungary v UAE
-Australia v Brazil
-Costa Rica v Czech Republic
Kufuatia kipigo cha jana, Ancellotti ataka Chelsea ikaze buti!!!!
Bosi wa Chelsea Carlo Ancellotti amekitaka Kikosi chake cha Chelsea kuibuka upya kufuatia kipigo cha 3-1 mikononi mwa Wigan kwenye Ligi Kuu hapo jana na kushinda mechi ya Jumatano watakapocheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Apoel Nicosia ya Cyprus huko Cyprus.
Mbali ya kipigo hicho, Kipa wa Chelsea Petr Cech alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kumchezea rafu fowadi wa Wigan Hugo Rodagella na kusababisha penalti iliyopigwa na Rodagella aliefunga na kuipa Wigan bao la pili.
Sasa Cech ataikosa ‘Bigi Mechi’ Jumapili ijayo Chelsea watakapovaana na Liverpool.
Ancellotti alikiri kupandwa na ghadhabu na kuzungumza Kitaliano na Wachezaji lakini alikubali pia Wigan walistahili kushinda kwa kuutumia uwanja wote vizuri.
Kocha wa Stoke akiri wamefungwa na Timu Bora!!!
Meneja wa Stoke City, Tony Pulis, ambae timu yake ilipigwa 2-0 na Manchester United hapo jana kwenye Ligi Kuu uwanjani kwake Britannia, amekubali kuwa walizidiwa kila kitu na timu bora.
Pulis alisema: “Ili kushindana na timu kama Man U, unahitaji kila Mchezaji wako acheze kwa nguvu zote na kiwango cha juu kabisa! Hatukufanya hivyo! Pia, wana Wachezaji wazuri na wazoefu sana kama Giggs na Scholes! Huna cha kufanya bali kuwaheshimu na kuwahusudu tu!!”
Nae Sir Alex Ferguson alizungumza kwa kusema safari bado ni ndefu ingawa kwa sasa wako kileleni.
Benitez ammwagia sifa Torres!!
Fernando Torres, baada ya kupachika mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-1 wa Liverpool walipoikung’uta Hull City jana kwenye Ligi Kuu uwanjani Anfield, amemwagiwa sifa kemkem na Meneja wake, Mhispania mwenzake, Rafa Benitez.
Benitez amesema: “Tulimnunua kwa Pauni Milioni 20 na hilo ni dau kubwa kwetu lakini sasa anaonyesha thamani yake! Tuna imani atazidi kuboreka!”
Na, Bosi wa Hull City Phil Brown, ameeleza kukerwa kwake kwa jinsi timu yake ilipoipa Liverpool zawadi ya magoli. Brown amesema: “Watu watasema Torres ndie aliewapa ushindi lakini ukweli ni kwamba tumewapa zawadi ya magoli kwa udhaifu wetu kujihami!”
Ronaldo ni shabiki wa Man U!!! Huganda kwenye TV wakicheza, hushangilia wakishinda!!!
Cristiano Ronaldo, ingawa kwa sasa ni Mchezaji wa Real Madrid baada ya kuihama Manchester United, ameungama kuwa yeye ni Shabiki mkubwa wa Mashetani hao Wekundu!
Ronaldo amesema: “Natizama mechi zao zote! Ingawa nipo Real, nafurahi sana wakishinda!”
Vilevile ameelezea furaha yake kumwona rafiki yake na Mreno mwenzake, Nani, akipata namba mara kwa mara na amekiri kuongea na Nani kwa simu mara kwa mara.
Ronaldo ameeleza: “Nani ni mchezaji mzuri sana na sasa atapata nafasi ya kupanda chati!”
UEFA yachunguza Klabu za Ulaya Mashariki kucheza ‘fiksi!’
UEFA imetangaza kuwa ipo kwenye uchunguzi wa kesi 40 za upangaji matokeo kwenye mechi za UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Kombe la UEFA kwa kipindi cha miaka minne iliyopita inayohusisha Klabu za Nchi za Ulaya Mashariki na kati ya hizo mechi 15 ni za katika miaka miwili iliyopita.
Peter Limacher, Mkuu wa Kitengo cha Nidhamu cha UEFA, amesema: “Ni Klabu za Ulaya Mashariki. Wakijua wameshatoka kwenye mashindano, huamua sasa tupate faida na wanapanga matokeo! Uchunguzi utachukua muda lakini tunao ushirikiano wa Polisi.”
Mwezi uliokwisha UEFA ilitangaza inachunguza Klabu 3 za Macedonia baada ya kuwafungia Mabingwa wa Nchi hiyo Klabu ya FK Pobeda kutoshiriki michezo ya Ulaya kwa miaka minane.
Moja ya mechi zinazochunguzwa ni ile ya Klabu ya Macedonia FK Milano ilipokung’utwa jumla ya mabao 12-2 katika mechi 2 walipotolewa na Klabu ya Croatia Slaven Koprivnica katika Raundi ya Pili ya EUROPA LIGI mwezi Julai mwaka huu.
Van Persie aipa ushindi Arsenal lakini Kipa wao 'mpya' Mannone ndie shujaa!!!
Bao la kifundi dakika ya 52 la Robin van Persie liliipa ushindi Arsenal ugenini Craven Cottage walipoifunga timu ngumu Fulham katika mechi ya 'dabi' ya Timu za London ya LIGI KUU lakini ni Kipa wao 'mpya' Chipukizi Vito Mannone toka Italia, anaecheza tu kwa sababu Kipa nambari wani Manuel Almunia na msaidizi wake Lukasz Fabianski hawapo, ndie alieibeba Arsenal kwa kuzuia mabao ya wazi mengi sana.
LEO LIGI KUU [saa 12 jioni saa za bongo]:
Sunderland v Wolverhampton
Powered By Blogger