Thursday 1 October 2009

FAINI NA KIFUNGO CHA NJE KWA ADEBAYOR!!!
Mshambuliaji wa Manchester City Emmanuel Adebayor leo ameamriwa kulipa Faini ya Pauni Elfu 25 pamoja na kufungiwa mechi 2 baada ya kupatikana na hatia ya utovu wa nidhamu kwa kosa la kwenda kushangilia goli alilofunga mbele ya Mashabiki wa Arsenal siku Timu yake Man City ilipoipiga Arsenal 4-2 Uwanja wa City of Manchester kwenye mechi ya Ligi Kuu hivi karibuni.
Kitendo hicho kiliwakera Washabiki wa Arsenal na wakataka kuvamia uwanja lakini Polisi na Walinzi wakawadhibiti na purukashani hizo zilisababisha Mlinzi mmoja kupoteza fahamu.
Polisi wa Manchester walithibitisha kitendo cha Adebayor ndiyo chanzo cha zogo hilo la Washabiki.
Adebayor ambae alikuwa Mchezaji wa Arsenal kabla ya kuhamia Man City kwa sasa anatumikia kifungo cha mechi 3 kwa kosa la kumtimba kwa makusudi Mchezaji wa Arsenal Robin van Persie katika mechi hiyo hiyo.
Hata hivyo adhabu ya kufungiwa mechi 2 kwa utovu wa nidhamu inasimamishwa ili kuchunguza mwenendo wake na hivyo ataruhsiwa kucheza mechi akimaliza adhabu ya kufungiwa mechi 3 kwa kosa la van Persie adhabu ambayo sasa inakwisha na anategemewa kucheza mechi na Aston Villa Jumatatu ijayo. 

No comments:

Powered By Blogger