Wednesday 30 September 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
“BWAWA LA MAINI” laingia ruba!!! Benitez aishambulia Timu yake!!
Jovetic aichoma mkuki moyoni Liverpool!!
Fiorentina 2 Liverpool 0
Arsenal, Barcelona, Lyon zapeta, Inter ngoma ngumu Urusi!!!
Rangers yatandikwa 4-1 kwao!!
Huko Florence, Italia, Fiorentina ilitandaza soka safi hasa kipindi cha kwanza na na kuibandika Liverpool bao 2-0 kwenye pambano la UEFA CHAMPIONS LEAGUE hapo jana.
Mabao yote ya Fiorentina yalifungwa na Kijana wa miaka 19 kutoka Montenegro, Stevan Jovetic, kwenye kipindi hicho cha kwanza huku akishirikiana vyema na Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Adrian Mutu.
Kipigo hicho kimemfanya Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, aishambulie Timu yake kwa maneno: “Walituzidi kila kitu, tulikuwa wabovu kila sehemu kipindi cha kwanza! Lakini naamini Jumapili tutabadilika tukicheza na Chelsea!”
Mechi nyingine kwenye Kundi hili la Liverpool ilikuwa ni kati ya Debrecen na Lyon na Lyon kuibuka mshindi wa mabao 4-0.
Nao, Arsenal, wakicheza nyumbani Emirates Stadium, walitawala kabisa mechi yao na Olympiakos inayofundishwa na Mbrazil Zico lakini ilibidi wasubiri hadi dakika ya 78 ndipo walipopata bao la kwanza kupitia Robin van Persie na kisha dakika ya 86 Mrusi Andry Arshavin akaongeza la pili.
Nazo, Barcelona na Lyon, zilishinda mechi zao huku Barca ikiipiga Dynamov Kiev 2-0 kwa mabao ya Lionel Messi na Pedro Rodriguez na Lyon kushinda ugenini kwa mabao 4-0 dhidi ya Debrecen.
Timu ya Kocha Jose Mourinho, Inter Milan, ikicheza ugenini huko Urusi, waliambulia suluhu ya 1-1 walipocheza na Rubin Kazan na kumaliza mechi hiyo wakiwa mtu 10 baada ya Mchezaji wao Mario Baloteli kutolewa nje kwa Kadi mbili za Njano.
Rangers ya Scotland ilichabangwa nyumbani kwake mabao 4-1 na Sevilla ya Spain huku mabao yote yakitinga kipindi cha pili.
Mabao ya Sevilla yalifungwa na Konko, Adriano, Luis Fabiano na Fredi Kanoute.
Bao la Rangers liliwekwa na Nacho Novo.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA JANA Jumanne, Septemba 29:
Arsenal 2 Olympiakos 0
AZ Alkmaar 1 Standard Liege 1
Barcelona 2 Dynamo Kiev 0
Debrecen 0 Lyon 4
Fiorentina 2 Liverpool 0
Rangers 1 Sevilla 4
Rubin Kazan 1 Inter Milan 1
Unirea Urziceni 1 VfB Stuttgart 1
MECHI ZA LEO Jumatano, Septemba 30:
AC Milan v FC Zurich
Apoel Nicosia v Chelsea
Bayern Munich v Juventus
Bordeaux v Maccabi Haifa
CSKA Moscow v Besiktas
FC Porto v Atletico Madrid
Manchester United v Wolfsburg
Real Madrid v Marseille
FIFA U-20 WORLD CUP EGYPT 2009:
MATOKEO MECHI ZA JANA Jumanne, Septemba 29:
-South Korea 1 Germany 1
-Uruguay 3 Uzbekistan 0
-USA 4 Cameroun 1
-Ghana 4 England 0
MECHI ZA LEO: Jumatano, Septemba 30:
-Australia v Costa Rica
-Brazil v Czech Republic
-Hungary v South Africa
-UAE v Honduras

No comments:

Powered By Blogger