Saturday, 21 November 2009

Man U 3 Everton 0
Mabingwa Watetezi, Manchester United, wakiwa kwao Old Trafford leo wameikung’uta Everton 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu na kulipunguza pengo la Chelsea kuongoza Ligi kuwa pointi 5.
Mabao ya Man U yalifungwa na Darren Fletcher, Michael Carrick na Antonio Valencia.
Vikosi vilikuwa:
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Brown, Vidic, Evra, Valencia, Fletcher, Carrick, Giggs, Rooney, Owen.
Akiba: Kuszczak, Anderson, Scholes, Welbeck, Obertan, Gibson, De Laet.
Everton: Howard, Neill, Yobo, Distin, Baines, Gosling, Rodwell, Heitinga, Cahill, Fellaini, Saha.
Akiba: Nash, Hibbert, Jo, Yakubu, Coleman, Duffy, Baxter
RATIBA LIGI KUU England: Jumapili, 22 Novemba 2009
Bolton v Blackburn
Stoke v Portsmouth
Tottenham v Wigan
Chelsea wazidi kujichimbia kileleni! Arsenal wapigwa!!
Chelsea ikiwa nyumbani Stamford Bridge imeishindilia Wolves mabao 4-0 na kujikita uongoza wa Ligi Kuu wakiwa pointi 8 mbele ya Timu ya pili Arsenal ambayo leo ilifungwa 1-0 ugenini na Sunderland iliyofunga bao lake kupitia Darren Bent.
Mechi ya Mabingwa Manchester United na Everton huko Old Trafford inaanza muda mfupi kuanzia sasa na Man U wakishinda watapunguza pengo la Chelsea kuongoza Ligi kuwa pointi 5.
MATOKEO KAMILI MECHI ZA LEO:
Liverpool 2 v Man City 2
Birmingham 1 v Fulham 0
Burnley 1 v Aston Villa 1
Chelsea 4 v Wolves 0
Hull City 3 v West Ham 3
Sunderland 1 v Arsenal 0
Liverpool ushindi mgumu!!!
Liverpool 2 Man City 2
Ndani ya Uwanja wao Anfield, Liverpool wametoka sare 2-2 na Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu iliyoanza mapema kupita nyingine za leo.
Mpaka mapumziko ilikuwa 0-0.
Liverpool ndio waliopata bao la kwanza baada ya frikiki ya Steven Gerrard kuunganishwa na Martin Skrtel dakika ya 50.
Dakika ya 69 Adebayor alisawazisha kwa kichwa kufuatia kona na wakaongeza la pili kupitia Steven Ireland dakika ya 78.
Liverpool wakasawazisha dakika moja baadae kupitia Yossi Benayoun.
Liverpool: Reina, Carragher, Skrtel, Agger, Insua, Mascherano, Lucas, Kuyt, Gerrard, Babel, Ngog.
Akiba: Cavalieri, Aquilani, Riera, Aurelio, Benayoun, Kyrgiakos, El Zhar.
Man City: Given, Zabaleta, Toure, Lescott, Bridge, De Jong, Barry, Wright-Phillips, Ireland, Bellamy, Adebayor.
Akiba: Taylor, Onuoha, Johnson, Santa Cruz, Tevez, Kompany, Weiss.
KOMBE LA MATAIFA AFRIKA: Makundi yatajwa, Ratiba kupangwa!!
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuchezwa huko Angola na tayari Makundi yameshatajwa.
Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Wenyeji Angola na Mali.
MAKUNDI:
KUNDI A [Litacheza Mjini Luanda]
Angola, Mali, Algeria, Malawi
KUNDI B [Cabinda]
Ivory Coast, Ghana, Togo, Burkina Faso
KUNDI C [Benguela]
Egypt [Mabingwa Watetezi], Nigeria, Benin, Mozambique
KUNDI D [Lubango]
Cameroon, Tunisia, Zambia, Gabon.
LIGI KUU England: Dimbani leo!!
Jumamosi, 21 Novemba 2009 [saa za bongo]
[saa 9 dak 45 mchana]
Liverpool v Man City
[saa 12 jioni]
Birmingham v Fulham
Burnley v Aston Villa
Chelsea v Wolves
Hull City v West Ham
Sunderland v Arsenal
[saa 2 na nusu usiku]
Man U V Everton
Baada ya kutoonekana kwa karibu wiki mbili, leo Uwanjani Anfield, Liverpool wanaikaribisha ‘Timu Tajiri’ Manchester City katika mechi itayoanza mapema kupita zote, itakayoanza saa 9 dakika 45 mchana saa za bongo.
Hii ni mechi ambayo kila upande unataka kushinda kufuatia matokeo mabovu kwao huku Liverpool wakiwa wameshinda mechi 1 tu katika 9 walizocheza mwisho. Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu, Liverpool walipata dro 2-2 na Birmingham na wako pointi 11 nyuma ya vinara Chelsea na wameshika nafasi ya 7.
Nao Man City, ingawa wamefungwa mechi moja tu msimu huu kwenye Ligi Kuu, wametoka suluhu mechi 5 zao za mwisho.
Vinara Chelsea wanaikaribisha Wolverhampton Wanderers huko Stamford Bridge na hii inaonekana ni mechi chee kwa Chelsea.
Timu iliyo nafasi ya pili, Arsenal, inasafiri hadi Kaskazini Mashariki na kutua Stadium of Light kucheza na Sunderland huku wakiwa na listi ya majeruhi kibao. Kwenye lisi hiyo wamo Robin van Persie, Clichy na Gibbs.
Hull City na West Ham ni mechi kubwa mno kwa timu hizi mbili na ushindani utazisaidia kujikwamua toka chini.
Mabingwa Manchester United wako nyumbani Old Trafford na wanawakaribisha Everton mechi itakayoanza saa 2 na usiku saa za bongo. Man U ilifungwa 1-0 na Chelsea katika mechi yao ya mwisho na leo wanapambana na Everton ambayo imeishinda Man U mara moja tu katika mechi 28 za Ligi Kuu walizocheza kati yao.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni kati ya Birmingham v Fulham na Burnley v Aston Villa.
Roy Keane aiponda Nchi yake Ireland kwa kudai mechi na Ufaransa irudiwe
Nahodha wa zamani wa Manchester United na Mchezaji wa zamani wa Republic of Ireland, Roy Keane, ambae sasa ni Meneja wa Ipswich, amekilaumu FAI, Chama cha Soka Ireland, kwa kudai mechi kati ya Ufaransa na Ireland irudiwe baada ya Thierry Henry kuucheza kwa mkono mpira na kumpasia William Gallas aliefunga bao lililowapa Ufaransa sare 1-1 na hivyo ushindi wa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili na kutinga Fainali Kombe la Dunia.
FAI imeiandikia barua FIFA kutaka mechi hiyo irudiwe lakini Roy Keane, ambae mwaka 2002 aliondoka kwa hasira kwenye Kikosi cha Ireland kilichokuwa Fainali za Kombe la Dunia huko Korea na Japan, amewalaumu sana Ireland na kuwataka wasilete madai ya kurudiwa mechi kwa sababu wao pia hawajui haki ni nini.
Keane ametamka: “Watalalamika mpaka watachoka, Ufaransa inaenda Fainali! Wasahau hilo!”
Akizungumzia kitendo cha Thierry Henry kuucheza mpira kwa mkono, Keane hakumlaumu Henry na badala yake aliilaumu Ireland.
Keane alisema: “Kwa nini defensi haikuundoa mpira? Kipa alikuwa wapi mpira ukiingia boksi la yadi 6? Kwa nini waruhusu mpira udunde kwenye hilo boksi?”
Rio kurudi baada ya wiki chache!!
Sir Alex Ferguson amesema wamegundua tatizo linalomkabili Sentahafu wao Rio Ferdinand na sasa anapewa tiba sahihi na atarudi uwanjani baada ya wiki chache na sio miezi kama inavyodiwa.
Ferdinand hajacheza wiki kadhaa sasa na Ferguson amesema tatizo lake ni mgongo sehemu za kiuno na hilo husabbabisha maumivu kwenye musuli za miguu.
Mwaka wote huu, Ferdinad amekuwa hachezi mara kwa mara kwa kuwa na maumivu.
Wakati Ferdinand yuko nje, Sentahafu mwingine Nemanja Vidic amepona na leo anategemewa kuanza mechi ya Ligi Kuu na Everton huko Old Trafford.

Thursday, 19 November 2009

MAGAZETI SWEDEN YAMPONDA REFA WA KWAO WA MECHI YA UFARANSA v IRELAND!!
Magazeti ya Sweden, Nchi anayotoka Refa Martin Hansson [pichani huku Kipa wa Ireland Shay Given akilalamika] aliechezesha mechi ya jana ya Ufaransa v Ireland iliyotoka sare 1-1 na kuwa ‘kipofu’ wakati Thierry Henry akikontroli na kuucheza mpira kwa mkono na kumpasia William Gallas aliefunga bao na kuipa Ufaransa fursa ya kuingia Fainali Kombe la Dunia, yamemponda vibaya Refa huyo wa Sweden.
Gazeti moja la Sweden, Aftonbladet, liliandika: “Kuna takriban Raia wa Ireland Milioni 80 dunia nzima. Tuna uhakika wanajisikia vibaya sana leo! Lakini tunategemea kuna Wasweden watatu ambao watajisikia vibaya mno! Wao ni Refa Martin Hansson na Wasaidizi wake Stefan Wittberg na Fredrik Nilsson! Hamna Fainali za Kombe la Dunia kwa Ireland, lakini tunategemea hata Timu ya Hansson wameifuta haki yao ya kwenda kuchezesha Fainali!!!”
LIGI KUU England kilingeni Jumamosi!
Fergie kuwepo benchi mechi ya Jumamosi na Everton!!
Baada ya karibu wiki 2 kutochezwa ili kupisha patashika ya mechi za Kombe la Dunia, Ligi Kuu England itarudi kwa kishindo kuanzia Jumamosi kwa kuchezwa mechi 7, Jumapili mechi 3 na Jumatano ijayo mechi 2.
Ingawa ilitegemewa Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, angeanza kutumikia kifungo chake cha mechi 2 Jumamosi hii kwa kutoruhisiwa kukaa benchi la Akiba la Timu yake katika mechi na Everton huko Old Trafford, FA imefafanua kuwa adhabu hiyo inaanza siku 14 tangu hukumu na hivyo Ferguson atakuwepo benchi Jumamosi na kuzikosa mechi za tarehe 28 Novemba watakapokuwa ugenini Portsmouth na ile ya Kombe la Carling na Tottenham tarehe 1 Desemba.
Ferguson atakuwa kifungoni baada ya kutiwa hatiani kwa kauli yake kwamba Refa Alan Wiley hayuko fiti kuchezesha mechi aliyoitoa Oktoba 3 mara baada ya sare ya Ligi Kuu ya 2-2 na Sunderland.
Mpaka sasa, baada ya mechi 12 kwa kila Timu, isipokuwa Arsenal na Manchester City zilizocheza 11, msimamo ni:
1. Chelsea pointi 30
2. Arsenal pointi 25
3. Man U pointi 25
4. Tottenham pointi 22
5. Aston Villa pointi 21
6. Man City pointi 20
7. Liverpool pointi 19
RATIBA:
Jumamosi, 21 Novemba 2009
Birmingham v Fulham
Burnley v Aston Villa
Chelsea v Wolves
Hull City v West Ham
Liverpool v Man City
Man U V Everton
Sunderland v Arsenal
Jumapili, 22 Novemba 2009
Bolton v Blackburn
Stoke v Portsmouth
Tottenham v Wigan
Jumatano, 25 Novemba 2009
Fulham v Blackburn
Hull City v Everton
ZOZO la Ufaransa v Ireland: Thierry Henry ni ‘MWIZI!!’, Ireland wataka mechi irudiwe!!!
Chama cha Soka cha Ireland, FAI, wamewasilisha malalamiko yao FIFA wakitaka mechi ya jana ya marudiano ya mtoano wa kuamua Timu ipi inaingia Fainali Kombe la Dunia ambayo ilitoka 1-1 na Ufaransa kupita kwa jumla ya Magoli 2-1 wakitaka irudiwe kwa sababu goli la kusawazisha la Ufaransa lililofungwa dakika ya 104 ya muda wa nyongeza huku Ireland wakiongoza 1-0 lilipatikana baada ya Thierry Henry kuumiliki na kuucheza mpira kwa mkono na kumpasia William Gallas aliefunga.
Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Ireland, Ufaransa ilishinda 1-0 na jana hadi dakika 90 kumalizika, Ireland ilikuwa imeshinda 1-0 na hivyo kufanya timu hizo kuwa sare 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30 za nyongeza.
Hata hivyo, FIFA imesema kwa sheria zao ‘uamuzi wa Refa ni wa mwisho”.
Huku zozo hilo likizagaa hadi kwa Wanasiasa wa Nchi hizo wakati Waziri Mkuu wa Ireland, Brian Cowen, kuitaka FIFA iamue mechi irudiwe na mwenzake wa Ufaransa, Francois Fillon, kujibu kwa kusema Serikali isiingilie masuala ya Soka, Kocha wa Ireland, Giovanni Trapattoni, amesema hategemei mechi kurudiwa kwani uamuzi wa Refa ni wa mwisho.
Henry aungama: 'Nilishika'
Thierry Henry wa Ufaransa ambae jana aliibua mzozo mkubwa baada ya kuumiliki na kuucheza mpira kwa mkono na kumpasia William Gallas aliefunga goli la kusawazisha dakika ya 104 na kuifanya ngoma iwe 1-1 kati ya Ufaransa na Republic of Ireland ameungama na kusema ni kweli aliucheza mpira kwa mkono.
Henry, mara tu baada ya mechi, alisema: “Ntakuwa mkweli! Niliushika mpira! Lakini mimi sio Refa! Niliushika, Refa hakusimamisha. Sasa muulizeni Refa!!”
Nae Mfungaji wa bao hilo, William Gallas, amedai hakuona kama Thiery Henry aliushika mpira.
Kocha wa Ireland, Giovanni Trapattoni, amesema: “Ulaya nzima waliona mkono!! Hata Refa angemuuliza Henry, angeungama! Bora tungetoka kwa penalti!!! Siku zote tunashika bango: ‘tucheze kwa haki’ [Fair Play] sasa ni haya!! Inasikitisha!”
Kocha wa Ufaransa, Raymond Domenech, ambae hapendwi kabisa Ufaransa, amedai: “Sikuona mkono! Nyie Waandishi mnadai kitu mko nje ya uwanja wakati Refa hakuona!”
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae ni Mfaransa na alikuwepo kwenye mechi kama Mtangazaji Mtaalam wa Kituo cha TV cha Ufaransa TF1, alibaini: “Ufaransa imeingia Fainali kwa kosa la Refa!”
LISTI YA TIMU 32 ZA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010 YAKAMILIKA!!!
Droo ya kupanga Makundi ni Cape Town Desemba 4!!!
TIMU ZILIZO FAINALI:
WENYEJI: South Africa
AFRICA: Algeria, Cameroun, Ghana, Ivory Coast, Nigeria
ASIA: Australia, Japan, North Korea, South Korea
EUROPE: Denmark, England, France, Germany, Greece, Italy,Netherlands, Portugal, Serbia, Slovakia, Slovenia, Spain, Switzerland.
SOUTH AMERICA: Argentina, Brazil, Chile, Paraguay, Uruguay.
NORTH, CENTRAL AMERICA AND CARIBBEAN: United States, Mexico, Honduras
ASIA/OCEANIA: New Zealand.
Baada ya Uruguay, Ufaransa, Algeria, Ureno, Slovenia na Ugiriki jana kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia na kuchukua nafasi 6 za mwisho zilizokuwa zimebaki, Listi ya Timu 32 zitakazocheza Fainali imekamilika na ile Droo ya kupanga Makundi na Ratiba ya Mechi itafanyika huko Mjini Cape Town, Afrika Kusini hapo Desemba 4, 2009.
Mechi za Fainali ya Kombe la Dunia zitachezwa kati ya Juni 11 na Julai 11 kwenye Viwanja mbalimbali huko Afrika Kusini vilivyopo Cape Town, Durban, Johannesburg, Mangaung/Bloemfontein, Nelson Mandela Bay/Port Elizabeth, Nelspruit, Polokwane, Rustenburg, Tshwane/Pretoria.
MATOKEO MECHI ZA MCHUJO ZA JANA Jumatano Novemba 18:
Algeria 1 Misri 0
Uruguay 1 Costa Rica 1 [Jumla ya Magoli 2-1]
France 1 Republic of Ireland 1 [2-1]
Slovenia 1 Urusi 0 [2-2 Slovenia yashinda kwa goli la ugenini]
Bosnia-Herzegovina 0 Ureno 1 [0-2]
Ukraine 0 Greece 1 [0-1]

Wednesday, 18 November 2009

Hali tata Khartoum!!! Polisi wazingira Mji mzima!!!
Jeshi la Polisi la Sudan limeuzingira na kuweka ulinzi mkali Mji mkuu wa Sudan, Khartoum, zikiwa zimebaki dakika chache kabla ile mechi ya uhasama ya marudiano kati ya Misri na Algeria kuanza Uwanja wa El Merreikh.
Milango ya Uwanja huo ilifunguliwa masaa matano kabla ya muda wa mechi kuanza na huku Mashabiki wa Misri na Algeria wakitenganishwa na Polisi nje na ndani ya uwanja ili wasikutane na kuleta vurugu.
Mshindi wa mechi hii ndie anaenyakua nafasi ya mwisho toka Kundi la Nchi za Afrika kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani.
Benitez: ‘Nisipochukua Ubingwa Ligi Kuu nimefeli!!!”
Kocha wa Liverpool, Rafael Benitez, amedai kuwa akishindwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu England atajihesabu kuwa kama ameshindwa katika maisha.
Ingawa Benitez ametoa kauli hiyo nzito lakini Wadau wengi wanaamini kuwa Liverpool haina uwezo msimu huu kutwaa Ubingwa huo kwani tayari wameshafungwa mechi nyingi na kwa sasa wako pointi 11 nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Chelsea.
Mara ya mwisho kwa Liverpool kuuchukua Ubingwa wa England ilikuwa mwaka 1990.
Vita ya maneno yazidi kuchochea uhasama Mechi ya leo Misri v Algeria!!
Leo, saa 2 na nusu usiku saa za bongo, kwenye Uwanja wa El Merreikh, Mjini Kharoum, Sudan, Misri inarudiana na Algeria kwenye mechi itakayoamua nani atakwenda Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani baada ya Jumamosi Misri kuifunga Algeria 2-0 mjini Cairo na hivyo kulingana kila kitu na kulazimisha mechi hii irudiwe.
Mechi hii imetawaliwa na uhasama wa kihistoria ambao chanzo chake pengine ni mechi ya mechi ya mwaka 1989 kuamua nani anatinga Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1990 zilizochezwa Italia ambayo Misri waliifunga Algeria 1-0 kwa bao la Hossam Hassan na kuwaudhi Algeria waliodai Refa kala rushwa.
Katika mechi hiyo Mchezaji wa Algeria Lakhdar Belloumi alimtwanga chupa Daktari wa Timu ya Misri na kumtoa jicho.
Wiki iliyopita Algeria walipotua Cairo basi lao lilokuwa likiwapeleka Hotelini lilipigwa mawe na Wachezaji kadhaa kuumizwa.
Baada ya mechi ya Jumamosi huko Cairo watu 32 waliumizwa katika vurugu wengi wao wakiwa Washabiki wa Algeria.
Huko Nchini Algeria, Wamisri wamekuwa wakishambuliwa na mali zao kuharibiwa na kusababisha wengi kuondoka Nchini.
Vurugu za Raia wa Nchi hizi mbili zimetapakaa na kuripotiwa hata huko Ufaransa ambako kuna jamii kubwa ya raia hao.
Mechi ya leo huko Khartoum imetawaliwa na vita ya maneno inayochochewa na Viongozi wa Timu hizo huku Mkuu wa Shirikisho la Soka la Algeria kudai vurugu hizo zinachochewa na Viongozi wa Soka Misri.
Hata hivyo, Kocha wa Misri, Hassan Shehata, amepinga lawama hizo na kusema: “Inasikitisha, Soka ni gemu tu lakini kuna watu wanaigeuza vita!”
Serikali ya Sudan imechukua hatua za kuzuia mlipuko uwanjani kwa kupunguza idadi ya Watazamaji uwanjani kutoka 41,000 hadi 35,000 na pia kuwaweka Polisi 15,000 kulinda amani. Vilevile, zimefunguliwa kambi za Washabiki wa Nchi hizo na kuwatenganisha kwa kilomita kadhaa ili wasiingiliane.
Huko Misri, Serikali imejitolea kuwasafirisha kwa barabara hadi Sudan Vijana wa Chini ya Miaka 30 wapatao 2,000 ambao pia watalipiwa gharama zao zote.
Mara ya mwisho kwa Nchi hizi mbili kucheza Fainali ya Kombe la Dunia ni mwaka 1990 kwa Misri na Algeria ilicheza Fainali za 1986.
Oman 0 Brazil 2
Jana kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Muscat, Oman, Brazil iliifunga Oman mabao 2-0.
Mabao ya Brazil yalifungwa na Nilmar dakika ya 4 na la pili Oman walijifunga wenyewe baada ya Kiungo wao Oman Hassan Ghailani kufanya kosa kipindi cha pili na kujifunga.

Tuesday, 17 November 2009

Japan hailitaki Vuvuzela!!!
Bosi wa Soka huko Japan Motoaki Inukai amesema ataongea na Rais wa FIFA Sepp Blatter ili kulipiga marufuku Vuvuzela kwenye Fainali ya Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 mwakani.
Bosi huyo wa Japan alikerwa sana na Vuvuzela baada ya Japan kutoka suluhu 0-0 na Afrika Kusini hapo juzi kwenye mechi ya kirafiki.
Vuvuzela ni utamaduni wa kushabikia kwa Wapenzi wa Soka huko Afrika Kusini na hupulizwa mfululizo kwenye mechi na kitendo hicho kimewafanya Wachezaji, Makocha na Watangazaji kulalamikia kelele zake hasa hali hiyo ilipojitokeza wakati Kombe la FIFA la Mabara lilipochezwa huko Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu.
Wakati huo, Watangazaji wa TV walilalamika matangazo yao hayasikiki na Mchezaji wa Spain, Xabi Alonso, alidiriki kusingizia walifungwa na Afrika Kusini kwa sababu ya Vuvuzela.
Hata hivyo, msimamo wa FIFA mpaka sasa ni kuwa Vuvuzela ni asili na haki ya Watu wa Afrika Kusini.
Kocha wa Japan, Takeshi Okada, alipohojiwa kuhusu dro ya 0-0 na Afrika Kusini Jumamosi iliyopita na maoni yake kuhusu Vuvuzela, alisema: “Labda Afrika Kusini wakicheza soka zuri, Mashabiki wao wataacha kelele!!!”
Benitez: “Akiuzwa Torres, najiuzulu!!!”
Rafael Benitez, Meneja wa Liverpool, amebwata kuwa akiuzwa Fernando Torres bila ya matakwa yake atang’oka.
Kumekuwa na utata Liverpool huku Klabu ikikabiliwa na madeni ya zaidi ya Pauni Milioni 245 na pia mfarakano kati ya Wamarekani wawili Wamiliki wa Klabu hiyo, Tom Hicks na George Gillet, na hivyo kuibuka kwa dhana kuwa njia rahisi ya kupata pesa nzuri na za haraka ni kumuuza Mchezaji wao Staa Torres kwa bei mbaya.
Benitez amefoka: “Sitarajii hilo!! Lakini ikitokea, najiuzulu!!”
Van Persie kutumia dawa za kienyeji ili apone haraka enka!!!
Robin van Persie yupo tayari kutumia kila aina ya tiba ili apone haraka enka aliyoumizwa Jumamosi iliyopita kwenye mechi ya kirafiki kati ya Nchi yake Uholanzi na Italia.
Van Persie amesema atasafiri hadi Serbia ili akatibiwe na Daktari wa Kike anaeganga na kuchua wagonjwa kwa kutumia maji maji ya mfuko wa kizazi wa kina Mama.
Van Persie amesema Daktari huyo alimtibu Mchezaji Kiungo wa PSV Eindhoven Danko Lazovic na alipona haraka na yeye haoni kwa nini asijaribu kwani tiba hiyo haitomuumiza au kumpotezea chochote.
Klabu ya Van Persie, Arsenal, imekadiria Mchezaji huyo hatacheza kwa wiki 6.
KOMBE LA DUNIA: Mechi ya Misri v Algeria ni uhasama mtupu!!!
Misri na Algeria zinarudiana Jumatano, Novemba 18 huko Khartoum, Sudan ili kupata Mshindi atakaetinga Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya Misri kushinda 2-0 Jumamosi mjini Cairo na kufanya Timu hizo zilingane kila kitu na hivyo kulazimisha mechi irudiwe uwanja nyutro.
Ingawa uwanjani, kwenye mechi yenyewe ya Jumamosi mambo yalikuwa shwari lakini nje ya Uwanja ni unyama unyama kwa Mashabiki.
Kasheshe ilianza siku Algeria walipotua mjini Cairo na Genge la Vijana kulivurumisha mawe basi la Timu hiyo lililokuwa likiwapeleka Hotelini na kuwajeruhi Wachezaji kadhaa wa Algeria ambao walicheza mechi ya Jumamosi huku wakiwa na bendeji kichwani.
Hata baada ya mechi hiyo vurugu za Washabiki zilitapakaa kila sehemu na hata Nchi za nje ambako kuna Raia wa Algeria na Misri.
Huko Algeria, Ofisi za Shirika la Ndege la Misri zilivamiwa na kuvunjwa na Waandamanaji na baadhi ya Wamisri wanaoishi huko kupigwa. Inasemekana Wamisri wameanza kuondoka huko Algeria kabla ya hiyo mechi ya kesho.
Vurugu za Raia wa Nchi hizi zimeripotiwa hadi Ufaransa.
Huko Dubai ambako kuna jamii kubwa ya Wamisri na Waalgeria, inadaiwa Polisi imetoa onyo kali kwa hao Wamisri na Waalgeria kuacha vurugu.
Kiini hasa cha uhasama kati ya Nchi hizi kinaweza kuwa mechi kati ya Nchi hizi iliyochezwa mwaka 1989 ambayo Misri walihitaji ushindi au suluhu ili waende Fainali Kombe la Dunia huko Italia mwaka 1990.
Hossam Hassan alifunga bao 1 na kuipa Misri ushindi na ndipo balaa likaanza. Algeria wakadai Refa kala rushwa na baada ya mechi hiyo Mchezaji wa Algeria Lakhdar Belloumi akamtwanga chupa Daktari wa Timu ya Misri na kumtoa jicho.
Misri ikamshitaki na kumhukumu Belloumi aende jela ingawa mwenyewe hakuwepo Misri.
Hukumu hiyo imemfanya Belloumi tangu wakati huo aogope kusafiri nje ya Algeria.
Ili kudhibiti fujo huko Khartoum, Serikali ya Sudan imesema itaweka ulinzi wa Polisi 15,000 kwani inategemewa maelfu ya watu kutoka Misri na Algeria watamiminika kwenye pambano hilo kuungana na Raia wengine wa Nchi hizo wanaoishi Sudan.
KOMBE LA DUNIA: Nchi za Ulaya kupata Timu 4 kesho ziakazoenda Fainali!!
Ukiondoa mechi ya Kundi la Afrika ya marudiano kati ya Misri na Algeria inayochezwa Sudan hapo kesho ambapo Mshindi anaingia Fainali, nafasi 4 za mwisho zilizobaki kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani zitatoka kwenye mechi 4 za Mtoano za Nchi za Ulaya.
Mechi hizo ni za marudiano kati ya: [Matokeo mechi ya kwanza kwenye mabano]
Ufaransa v Republic of Ireland [1-0]
Slovenia v Urusi [1-2]
Ukraine v Ugiriki [0-0]
Bosnia-Herzegovina v Ureno [0-1]

Monday, 16 November 2009

Van Persie nje wiki 6!!!
Arsenal imetangaza kuwa Staa wao toka Uholanzi Robin van Persie atakuwa nje ya uwanja kwa wiki zinazokadiriwa kuwa 6 ili kuuguza enka yake aliyoumizwa kwenye mechi ya kirafiki kati ya Uholanzi na Italia Jumamosi iliyopita.
Awali ilidhaniwa Van Persie anaweza kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu lakini Arsenal imesema uchunguzi wa Madaktari umebaini hakuumizwa sana kama ilivyoogopwa awali.
Uswisi Mabingwa wa Dunia Vijana Chini ya Miaka 17!!!
Nigeria 0 Uswisi 1
Uswisi jana waliwaliza Nigeria nyumbani kwao Abuja baada ya kuwafunga bao 1-0 katika Fainali ya Kombe la Dunia kwa Vijana Chini ya Miaka 17.
Bao la ushindi kwa Uswisi lilifungwa na Haris Seferovic dakika ya 63 mbele ya Mashabiki wa Nigeria wapatao 60,000.
Hilo ni pigo kubwa kwa Nigeria ambao wameshawahi kutwaa Kombe hilo mara 3.
Katika mechi ya awali ya kutafuta Mshindi wa 3, Spain iliishinda bao 1-0 Colombia Mfungaji akiwa Isco kwenye dakika ya 75.

Sunday, 15 November 2009

Maradona kifungo miezi miwili!!!
Kocha wa Argentina Diego Maradona amefungiwa na FIFA asijihusishe na Soka kwa miezi miwili kuanzia Novemba 15, 2009 hadi Januari 15, 2010 baada ya kupatikana na hatia ya kutoa matusi na maneno ya kashfa kwenye mahojiano ya kwenye TV laivu mara tu baada ya ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay ambayo Argentina walishinda 1-0 na kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia mwakani.
Maradona, aliehudhuria kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Kamati ya Nidhamu ya FIFA huko Zurich, Uswisi leo, pia amepigwa faini ya Pauni 15,000.
Kamati hiyo imesema haikumpa adhabu kali zaidi kwa vile Maradona alionyesha kusikitishwa na kufedheheshwa na vitendo vyake.
Hata hivyo adhabu hiyo haiwezi kuiathiri sana Argentina kwani katika kipindi hicho cha kifungo cha Maradona, Argentina imepangiwa kucheza mechi moja tu ya kirafiki dhidi ya Czech Republic hapo Desemba 16 ingawa mechi hiyo haijathibitishwa.
Capello: “Brazil ndio kidume!”
Kocha wa England Fabio Capello anaamini kuwa Brazil ndio Timu pekee ya kuogopewa kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni, 2010.
Brazil jana iliifunga England 1-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Doha, Qatar na ingeweza kushinda mabao zaidi ya hilo moja baada ya kukosa penalti na pia kuutawala mchezo.
Capello ana imani Brazil wako tofauti kabisa na Timu nyingine na ametamka: “Hii ni mara ya kwanza tumecheza na Timu yenye nguvu, wepesi na kiufundi wako juu sana! Staili yao ni tofauti kabisa na Spain! Spain wazuri kiufundi na wanapasiana pasi nyingi lakini hawana nguvu na ngome yao si nzuri! Tulipocheza na Spain tulipata nafasi nyingi sana za kufunga lakini na Brazil tulipata mbili tu!”
Arsenal yapata pigo: Van Persie aumia!!
Nyota na tegemezi kubwa la Arsenal Robin van Persie huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kuumia enka vibaya kwenye mechi ya kirafiki kati ya Uholanzi na Italia hapo jana.
Van Persie, miaka 26, aliumizwa na Mtaliana Giorgio Chiellini dakika ya 10 tu tangu mechi ianze na madaktari wa Uholanzi wamethibitisha kuchanika kwa misuli ya enka ingawa uchunguzi wa kina inabidi ufanywe ili kujua madhara ya kujeruhiwa hiyo enka.
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA: Wajue watakaokuwepo Angola Januari!!
Baada ya mechi za jana kati ya Mataifa mbalimbali ya Afrika zilizotupa Nchi zilizojumuika na Afrika Kusini, Ghana na Ivory Coast kutinga Fainali Kombe la Dunia mwakani huko Afrika Kusini, pia mechi hizo zilituamulia nani atashiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa huko Angola mwezi Januari, 2010.
Jana Cameroun na Nigeria ziliingia Fainali Kombe la Dunia lakini KUNDI C halikupata Mshindi wa kwenda Fainali hizo baada ya Misri kuifunga Algeria 2-0 na kuzifanya Nchi hizo mbili zilingane kila kitu na hivyo kulazimisha mechi irudiwe Sudan Jumatano ijayo ili kumpata atakaenda Fainali Kombe la Dunia.
Utaratibu uliowekwa ulikuwa Nchi ambayo inamaliza ikiwa nafasi ya Kwanza toka kila Kundi ndio inayoingia Fainali za Kombe la Dunia na zile zinazomaliza nafasi za juu 3 toka kila Kundi zitacheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na Mwenyeji Angola.
MSIMAMO TOKA KILA KUNDI:
KUNDI A
-Cameroun pointi 13
-Gabon pointi 9
-Togo pointi 8
-Morocco pointi 3
Kombe la Dunia: Cameroun
Kombe la Afrika: Cameroun, Gabon, Togo
KUNDI B
-Nigeria pointi 12
-Tunisia pointi 11
-Msumbiji pointi 7
-Kenya pointi 3
Kombe la Dunia: Nigeria
Kombe la Afrika: Nigeria, Tunisia, Msumbiji
KUNDI C
-Algeria pointi 13
-Misri pointi 13
-Zambia pointi 5
-Rwanda pointi 2
Kombe la Dunia: Algeria au Misri
Kombe la Afrika: Algeria, Misri, Zambia
KUNDI D
-Ghana pointi 12
-Benin pointi 10
-Mali pointi 8
-Sudan pointi 1
Kombe la Dunia: Ghana
Kombe la Afrika: Ghana, Benin, Mali
KUNDI E
-Ivory Coast pointi 16
-Burkina Faso pointi 12
-Malawi pointi 4
-Guinea pointi 3
Kombe la Dunia: Ivory Coast
Kombe la Afrika: Ivory Coast, Burkina Faso, Malawi
LEO FAINALI FIFA U-17 WORLD CUP: Nigeria v Uswisi
Leo huko Abuja, Wenyeji Nigeria watavaana na Uswisi katika Fainali ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Miaka 17.
Mechi hii itaanza saa 3 usiku saa za bongo.
Fainali hiyo itatanguliwa na Timu zilizobwagwa Nusu Fainali, Colombia v Spain, zitakazocheza kupata Mshindi wa 3.
Huko Ulaya KOMBE LA DUNIA: Ureno, Ufaransa na Urusi zaanza vyema mechi za Mtoano!!
Ugiriki na Ukraine ngoma dro!!!
MATOKEO MECHI ZA KWANZA ULAYA:

Ureno 1 Bosnia-Herzegovina 0
Urusi 2 Slovenia 1
Republic of Ireland 0 Ufaransa 1
Ugiriki 0 Ukraine 0

Ureno, wakicheza nyumbani, waliifunga Bosnia-Herzegovina kwa bao lililofungwa na Bruno Alves.
Timu hizi zitarudiana Jumatano ili kupata Mshindi atakaetinga Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini mwakani.
Nao, Urusi wakicheza nyumbani waliipiga Slovenia 2-1 huku Mchezaji wa Everton, Diniyar Bilyaletdinov akiifungia bao zote mbili.
Timu hizi zitarudiana huko Slovenia Jumatano Novemba 18.
Na huko Dublin, Republic of Ireland ilfungwa ikiwa nyumbani na Ufaransa baada ya shuti la Nicolas Anelka kumbabatiza beki na kutinga wavuni.
Mechi ya mwisho kwa Nchi za Ulaya zinazocheza Mtoano ilikuwa ni kati ya Ugiriki na Ukraine na ngoma ikaisha 0-0 na marudio ni huko Ukraine Jumatano ijayo.
kombe la Dunia MATOKEO MECHI YA KWANZA MAREKANI:
Costa Rica 0 Uruguay 1
Katika mechi ya kwanza ya Mtoano huko Marekani, Uruguay ilipata bahati kubwa kwa kushinda ugenini kwa bao la Diego Lugano dakika ya 23.
Timu hizi zitarudiana huko Uruguay Jumatano Novemba 18.
MECHI YA KIRAFIKI: Doha, Qatar:
Brazil 1 England 0
Katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Khalifa mjini Doha, Qatar, Brazil iliishinda England kwa bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Nilmar dakika ya 47.
Brazil walikosa penalti kwenye dakika ya 55 baada ya Luis Fabiano kupaisha shuti lake.
England iliyoongozwa na Nahodha Wayne Rooney aliechukua wadhifa huo kwa mara ya kwanza baada ya kuichezea England mara 57, iliwakosa karibu Nyota wake 9 kwenye mechi hiyo huku Brazil ikiwa na Kikosi imara.
Brazil: Julio Cesar, Maicon, Lucio, Thiago Silva, Michel Bastos, Felipe Melo, Silva, Elano, Kaka, Nilmar, Luis Fabiano.
AKIBA: Doni, Dani Alves, Luisao, Juan, Aurelio, Josue, Lucas, Alex, Julio Baptista, Robinho, Carlos Eduardo, Hulk.
England: Foster, Brown, Upson, Lescott, Bridge, Wright-Phillips, Barry, Jenas, Milner, Rooney, Bent.
AKIBA: Green, Cahill, Warnock, Huddlestone, Crouch, Defoe, Young, Hart.

Powered By Blogger