Wednesday 18 November 2009

Hali tata Khartoum!!! Polisi wazingira Mji mzima!!!
Jeshi la Polisi la Sudan limeuzingira na kuweka ulinzi mkali Mji mkuu wa Sudan, Khartoum, zikiwa zimebaki dakika chache kabla ile mechi ya uhasama ya marudiano kati ya Misri na Algeria kuanza Uwanja wa El Merreikh.
Milango ya Uwanja huo ilifunguliwa masaa matano kabla ya muda wa mechi kuanza na huku Mashabiki wa Misri na Algeria wakitenganishwa na Polisi nje na ndani ya uwanja ili wasikutane na kuleta vurugu.
Mshindi wa mechi hii ndie anaenyakua nafasi ya mwisho toka Kundi la Nchi za Afrika kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Juni mwakani.
Benitez: ‘Nisipochukua Ubingwa Ligi Kuu nimefeli!!!”
Kocha wa Liverpool, Rafael Benitez, amedai kuwa akishindwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu England atajihesabu kuwa kama ameshindwa katika maisha.
Ingawa Benitez ametoa kauli hiyo nzito lakini Wadau wengi wanaamini kuwa Liverpool haina uwezo msimu huu kutwaa Ubingwa huo kwani tayari wameshafungwa mechi nyingi na kwa sasa wako pointi 11 nyuma ya vinara wa Ligi hiyo Chelsea.
Mara ya mwisho kwa Liverpool kuuchukua Ubingwa wa England ilikuwa mwaka 1990.

No comments:

Powered By Blogger