Saturday 13 June 2009

BAADA YA KUMUUZA RONALDO KWA DAU KUBWA, KLABU ZAPANDISHA DAU KWA WACHEZAJI ILI KUIKAMUA MAN U!!!!
Manchester United wameanza kukumbana na bei za ajabu kwa kila Mchezaji wanaemgusa haya yakiwa ni matokeo ya kumuuza Cristiano Ronaldo kwa dau kubwa ambalo ni rekodi ya dunia.
Manchester United walitoa ofa ya kumnunua Winga kutoka Ecuador Antonio Valencia ya Pauni Milioni 12 lakini Klabu yake Wigan sasa inang’ang’ania Pauni Milioni 17.5.
Bayern Munich wameionya Manchester United kuwa wao watakubali ofa waliyoiita ya ‘kiwehu’, inayoaminika kuwa Pauni Milioni 50, ili wamuuze Kiungo Franck Ribery.
Na Lyon walioonyesha kuwa Mshambuliaji wao hatari Karim Benzema atauzwa kipindi hiki cha uhamisho sasa wamegeuza msimamo na kusema Benzema atahama tu mwishoni mwa msimu ujao hatua ambayo imechukuliwa kama kisingizio cha kupandisha dau lake.
Ingawa Wamiliki wa Manchester United ‘wamempa’ Sir Alex Ferguson dau lote la mauzo ya Ronaldo ili anunue Wachezaji inaonyesha dau hilo limezitia kiwewe Klabu nyingine na sasa wanataka kuikamua Manchester United.
Ferguson inasemekana anataka apate Wachezaji wapya kabla ya tarehe 15 Julai siku ambayo Manchester United inaanza ziara yake ya kabla kuanza kwa msimu mpya huko Mashariki ya Mbali.
KOMBE LA MABARA KESHO!!!
Kesho Jumapili, Timu 8 zitaanza kugombea Kombe la Mabara la FIFA, wakati katika mechi ya ufunguzi wenyeji Afrika Kusini watakwaana na Iraq mjini Johannesburg.
Haya ni Mashindano ya 8 ya Kombe hili lililoanza kushindaniwa mwaka 1992.
Washindi wa nyuma ni [Kwenye mabano Nchi ilyokuwa Mwenyeji]:
· 1992: Argentina (Saudi Arabia)
· 1995: Denmark (Saudi Arabia)
· 1997: Brazil (Saudi Arabia)
· 1999: Mexico (Mexico)
· 2001: France (S Korea/Japan)
· 2003: France (France)
· 2005: Brazil (Germany)
Mashindano ya mwaka huu yanashirikisha Nchi 8, Mwenyeji akiwa Afrika Kusini, Italy, Bingwa wa Dunia na Nchi nyingine ni:
-USA: Bingwa wa Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Carribean mwaka 2007
-Brazil: Bingwa wa Marekani Kusini mwaka 2007 [Copa America 2007]
-Iraq: Bingwa wa Asia mwaka 2007
-Egypt: Bingwa wa Afrika mwaka 2008
-Spain: Bingwa wa Ulaya mwaka 2008
-New Zealand: Bingwa wa Bara la Baharini [Oceania]
Viwanja:
Miji minne ya Afrika Kusini ndio itakuwa Wenyeji wa mechi za Kombe la Mabara 2009:
-Johannesburg: Kiwanja cha Coca Cola Park [Uwezo Watazamaji 62,567]
-Pretoria: Kiwanja cha Loftus Versfeld [Uwezo Watazamaji 50,000]
-Bloemfontan: Kiwanja cha Free State [Uwezo Watazamaji 48,000]
-Rustenberg: Kiwanja cha Royal Bafokeng [Uwezo Watazamaji 42,000]
Makundi
Timu zimegawanywa kwenye Makundi mawili na:
-KUNDI A: Afrika Kusini, Spain, Iraq na New Zealand
-KUNDI B: USA, Italia, Brazil na Egypt
RATIBA: [saa za bongo]
-Jumapili 14 Juni 2009-06-05
KUNDI A:
Afrika Kusini v Iraq [saa 11 jioni]
New Zealand v Spain [saa 3 na nusu usiku]
-Jumatatu 15 Juni 2009-06-05
KUNDI B
Brazil v Egypt [saa 11 jioni]
USA v Italy [saa 3 na nusu usiku]
-Jumatano 17 Juni 2009-06-05
KUNDI A
Spain v Iraq [saa 11 jioni]
Afrika Kusini v New Zealand [saa 3 na nusu]
-Alhamisi 18 Juni 2009
KUNDI B
USA v Brazil [saa 11 jioni]
Egypt v Italia [saa 3 na nusu usiku]
-Jumamosi 20 Juni 2009
KUNDI A [Mechi zito zinaanza pamoja saa 3 na nusu usiku]
Iraq v New Zealand
Afrika Kusini v Spain
-Jumapili 21 Juni 2009
KUNDI B [Mechi zito zinaanza pamoja saa 3 na nusu usiku]
Italia v Brazil
Egypt v USA
NUSU FAINALI:
Jumatano Juni 24: MSHINDI KUNDI A v MSHINDI WA PILI KUNDI B
Alhamisi Juni 25: MSHINDI KUNDI B v MSHINDI WA PILI KUNDI A
Jumapili 28 Juni: FAINALI
Mwenyekiti Wigan asema Man U wanamtaka Valencia
Mwenyekiti wa Klabu ya Wigan Dave Whelan amesema Manchester United wametoa ofa ya kumnunua Winga kutoka Ecuador Antonio Valencia.
Dave Whelan amesema: 'United wamezungumza na sisi na tutaanza majadiliano hivi karibuni. Kama Valencia akiniambia anataka kuhama na ada ni nzuri hatumzuii.’
Everton yawamwaga Wachezaji wawili!!
Bosi wa Everton David Moyes ameamua kuwaondoa Kikosini Wachezaji wawili ambao ni Mreno Nuno Valente na Mdachi Andy van der Meyde ambao wamekuwa hawana namba hapo Klabuni.
Valente [34] alihamia Everton mwaka 2005 lakini amekuwa akiumia mara kwa mara na vilevile ameshindwa kumng’oa Leighton Baines kwenye nafasi.
Van der Meyde alijiunga Everton mwaka 2005 kutoka Inter Milan lakini matatizo ya kuumia, nidhamu na vurugu katika maisha yake binafsi yamemkosesha namba.
Wamiliki Man U waahidi kuimarisha Timu!!!!
Familia ya kina Glazer ya Marekani ambao ndio wamiliki wa Manchester United wameahidi kumpa Meneja wao Sir Alex Ferguson fedha za kuimarisha kikosi.
Man U inavumishwa sana kuwataka Winga Antonio Valencia wa Wigan, na Wafaransa Karim Benzema wa Lyon na Franck Ribery wa Bayern Munich.
Huku Ronaldo akitegemewa kuhamia Real Madrid na Carlos Tevez kuna hatihati kama atabaki, inabidi Manchester United wazibe mapengo hayo.
Msemaji wa Familia ya Glazer alitoa tamko la Familia hiyo: ‘Si kweli kwamba Klabu imeelemewa na deni kubwa. Hio si ishu. Ukweli ni kwamba Cristiano Ronaldo, baada ya miaka 6, ameamua kuhama na Meneja Ferguson amesema sawa. Sir Alex Ferguson ndie anaeongoza Timu na akitoa uamuzi tunaukabali. Katika miaka minne iliyopitaWamiliki wameonyesha kwa vitendo kwa kununua Wachezaji bora kadhaa na hili litaendelea.’

Friday 12 June 2009

Fabregas asisitiza yeye ni Arsenal!!
Cesc Fabregas, Nahodha wa Arsenal, ametoka hadharani kuzima minong’ono ya kila mara kwamba atarudi kwao Spain kujiunga na Barcelona Timu aliyoanza kuichezea akiwa mtoto.
Fabregas,22, ametamka: ‘Nina mkataba wa muda mrefu Arsenal na hapa nitabaki muda mrefu!’
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alimpa Ukepteni Fabregas mwezi Novemba mwaka jana baada ya William Gallas kuvuliwa madaraka hayo.
Mkataba wa Fabregas utaisha 2014.
Deco anaitaka Inter!!!
Deco amesema hana furaha kuchezea Chelsea na anataka kwenda Italia akacheze Inter Milan kwa Kocha Mreno mwenzake Jose Mourinho ambae walikuwa nae pamoja Klabu ya FC Porto ya Ureno.
Baada ya FC Porto, Mourinho akaenda Chelsea na Deco akahamia Barcelona.
Deco, akitokea Barcelona, aliletwa Chelsea na Scolari aliekuwa Meneja wa Timu ya Taifa ya Ureno, baada ya Scolari kuingia Chelsea.
Tangu Scolari atimuliwe, Deco amekuwa hana namba.
Deco anaelezea kuhusu Mourinho: ‘Nataka niwe na Mourinho. Yeye ndio amesaidia mafanikio yangu.’

Thursday 11 June 2009

SI BIASHARA KICHAA-WADAU WANENA!!!!!
Mchezaji wa zamani wa Manchester United aliekuwa bonge la Straika, Frank Stapleton, amesema kuuzwa kwa Ronaldo ni ‘Biashara nzuri mno!!’
Frank Stapleton [pichani] ametamka: ‘Nasema, hii si ajabu! Huyu Mchezaji alitaka kuondoka muda mrefu! Man U haiweki mtu ambae hana mapenzi nayo!’
Stapleton akaendelea: ‘Mashabiki wengine watadhani ni pigo kubwa, yeye alikuwa kipenzi hapa, hasa kwa wale vijana, na wengi watashindwa kujua sasa Man U inakwenda wapi, lakini, watu lazima wakumbuke, Man U ishakuwa hapa kabla! Waliondoka Mastaa kama Bryan Robson, Paul ince, Cantona, Beckham na Roy Keane!’
Stapleton akamaliza: ‘Chini ya Sir Alex Ferguson hii Klabu ni kubwa kupita mtu binafsi au jina la mtu! Na kila mara jina kubwa likiondoka hii Klabu inaimarika zaidi! Sidhani Stretford End [JUKWAA LA MASHABIKI WALIOKUBUHU WA MAN U] watamwimba Ronaldo kama wanavyowaimba mpaka sasa George Best, Eric Cantona na Roy Keane ambao wote waliondoka!’

NINI WAANDISHI WA MAGAZETI UINGEREZA WAMESEMA???
Paul Wilson, The Guardian: ‘Wana Pauni Milioni 80 baada ya kumpoteza Mchezaji ambae siku zote walijua ataondoka! Ni kama vile walijua George Best atapotea lakini safari hii wamepata fidia kubwa na rekodi ya dunia! Ni biashara nzuri sana kwa United!’
Oliver Kay, The Times:
Msimu uliokwisha ilionekana ni vizuri kuikataa ofa ya Mamilioni lakini msimu huu ni safi kwani Mchezaji huyu mkataba wake, thamani inazidi kupungua! Msimu huu hakuonyesha kiwango chochote! '
Henry Winter, Daily Telegraph: ‘Matukio ya saa 24 zilizopita yameonyesha Sir Alex Ferguson ni mtu anaejua kuamua yupi bora! Alisema Rooney akicheza kama Mshambuliaji wa kati ni hatari na Rooney alionyesha hilo jana na Andorra! Akiongezwa Benzema amsaidie Rooney, pembeni Ribery na Valencia, nani atamkumbuka Ronaldo? Ukweli ambao tunaujua ni kwamba, daima, hakuna Mchezaji Mkubwa United, Kikubwa ni Manchester United!’

HUKO SPAIN, GAZETI MAARUFU ‘MARCA’ AMBALO NDIO JICHO, SIKIO, PUA NA KILA KITU CHA REAL MADRID LILIENDESHA KURA YA MAONI NA MATOKEO NI: Wapiga kura walikuwa 50,000 na Asilimia 77 walitamka Dau la kumnunua Ronaldo ni kubwa mno!!!
BIASHARA YA RONALDO:
TAARIFA RASMI YA MANCHESTER UNITED:
'Manchester United imepokea ofa ya Pauni Milioni 80, ambayo ni rekodi ya dunia na isiyo na masharti yeyote, ili kumnunua Cristiano Ronaldo kutoka kwa Real Madrid’
‘Kufuatia ombi la Cristiano binafsi-ambae kwa mara nyingine tena ameonyesha utashi wake kuhama-na baada ya kujadiliana na Wawakilishi wa Mchezaji huyo, United imekubali kuwapa ruhusa Real Madrid kuongea na Mchezaji huyo.’
‘inategemewa shughuli zote zitakamilika ifikapo Juni 30. Klabu haitatatoa tamko lolote hadi baadae.’
TAARIFA RASMI YA REAL MADRID:
'Real Madrid inathibitisha imetoa ofa kwa Manchester United ili kumnunua Mchezaji Cristiano Ronaldo. Klabu inategemea kufikia makubaliano na Mchezaji mwenyewe katika siku chache zijazo.’
WACHEZAJI England wa Kombe la Dunia mwaka 1966 hatimaye wapewa MEDALI ZAO!!
England iliwafunga Ujerumani Magharibi- wakati huo kulikuwa na Ujerumani mbili, Magharibi na Mashariki-mabao 4-2 mwaka 1966 Uwanjani Wembley na kutwaa Kombe la Dunia lakini ni Wachezaji 11 tu waliocheza mechi ile ndio walipewa Medali za Dhahabu kwa ushindi huo.

Huo ndio ulikuwa mtindo wa zamani kwamba ni yule tu alie kiwanjani ndie anaambua Medali na si Kikosi kizima.
Lakini FIFA imeamua hivi karibuni kuwapa Medali Wachezaji wote waliokuwa kwenye Kikosi cha Nchi iliyochukua Kombe la Dunia pamoja na Makocha na Wasaidizi wote kuanzia Fainali za mwaka 1930 hadi 1974.
Kuanzia Fainali za 1978 FIFA ilibadilisha mtindo na ikawa inatoa Medali kwa Kikosi kizima pamoja na Wasaidizi wa Timu.
Jana Wachezaji wa England wa Kikosi kilichochukua Kombe la Dunia mwaka 1966 ambao walikosa Medali walikabidhiwa Medali zao kwa niaba ya FIFA na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Wachezaji waliopewa Medali jana na kuzipokea wenyewe au Familia zao ni Peter Bonetti, Ron Springett, Jimmy Armfield, Gerry Byrne, Ron Flowers, Norman Hunter, Terry Paine, Ian Callaghan, John Connelly, George Eastham na Jimmy Greaves.
Baadae Wachezaji hao wa zamani na Familia zao walikuwa ndio wageni rasmi kwenye mechi ya mchujo wa Kombe la Dunia kati ya England na Andorra Uwanjani Wembley, jijini London ambayo England walishinda 6-0.
Pichani ni Jimmy Greaves na Norman Hunter wakifurahia Medali zao.
Kutimka kwa Ronaldo: NANI kasema NINI?
Baada ya miezi kadhaa ya ‘ataenda haendi’ sasa Ronaldo yuko njiani kutimiza ile aliyoiita mwenyewe ‘ndoto yake’ kwa kuhamia Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 80 ambayo ni rekodi mpya duniani kwa kunuliwa Mchezaji.
‘Brekingi nyuzi’ hii imezua kauli mbalimbali kuanzia kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown, Wadau wa Soka na hata mimi mwenye haka kablogu!!!!!!!
Hebu sikia……………..!!!!!!!!!!!
WAZIRI MKUU UINGEREZA GORDON BROWN: ‘Ni mmoja wa Wachezaji wazuri sana duniani! Nadhani watu watasikitika kuondoka kwake Uingereza. Lakini, mie namjua Sir Alex Ferguson vizuri tu, na najua lazima ana plani kuijenga upya Timu na kuibadilisha! Na nategemea Manchester United na Soka la Uingereza litaibuka imara na pengine bora zaidi!’
NANI, MCHEZAJI WA MAN U NA MWENZAKE RONALDO KWENYE TIMU YA TAIFA YA URENO: ‘Kuondoka kwa Cristiano si ngumu kupaziba! Tutammisi lakini United wana Wachezaji wengine bora!!’
TOMMY DOCHERTY, MENEJA WA ZAMANI MAN U: ‘Ukigombana na Sir Alex Ferguson ujue utatimuliwa tu! Muulize Beckham! Huwezi ukaleta mfarakano ndani ya Timu na sasa Real Madrid wana kazi ya kumtunza Ronaldo! Milioni 80 sio mchezo!! Man U ni Klabu kubwa na ukiondoka Man U unaporomoka tu!!!
PADDY CRERAND, MCHEZAJI WA ZAMANI MAN U NA SASA MTANGAZJI MUTV [Kituo cha TV cha MAN U]: ‘Kitu cha kwanza kuhisi ni masikitiko……! Lakini hii ‘haendi, atakwenda’ imedumu mwaka sasa! Niliamini atabaki Man U hadi Ferguson ang’atuke! Lakini duniani watu wana wivu na Man U hawataki watu bora hapa!’
ANDY MITTEN, EDITA WA GAZETI LA MASHABIKI WA MAN U: ‘Historia itamkumbuka vizuri kwa mchango wake mkubwa! Lakini vilevile atakumbukwa kwa ubishoo, majivuno na kiburi chake ingawa alikuwa mtumishi mwema! Tumetengeneza pesa nzuri kwake na Klabu haifi! David Beckham aliondoka kwa sababu Klabu ilitaka kumuuza! Nadhani Sir Alex Ferguson ni mtu mjanja sana na sasa amepata pesa nzuri za kujenga Timu! Hii ni sehemu ya historia ya Man U- tuna Meneja Bora sana na hilo ni muhimu sana kuliko Winga Bora!!!’
WAZIRI WA MICHEZO WA ENGLAND AMBAE NI SHABIKI WA MAN U, GERRY SUTCLIFFE: ‘Kama Mchezaji anataka kuondoka huwezi kumzuia! Walimnunua kwa Pauni Milioni 12 na sasa kauzwa kwa Pauni Milioni 80 hiyo ni biashara nzuri sana!’
STORMING, MWENDESHA KABLOGU HAKA: ‘Soka ni mchezo wa Kitimu!! Ingawa Mastaa ndio wanaisukuma na kuibeba Timu lakini Staa bora anaefanya hivyo ni yule mwenye mapenzi na Timu!! Anajituma! Ilifikia hatua Ronaldo alijiona ni bora kuliko wenzake! Kwenye mechi moja alipobadilishwa alitupa jezi chini na mara baada ya Fainali Man U waliyofungwa na Barcelona, Ronaldo alikandya mbinu za Timu!! Daima huwezi kumponda Ferguson na ukabaki! Angalia yaliyowakuta Jaap Stam na Rudi van Nistelrooy!!!’
MAN U YAVUNA KITITA REKODI KWA RONALDO!!!
· HUYOOOOO ATIMKIA REAL!!!
Manchester United imetangaza kuwa imepata ofa isiyo na masharti kutoka Real Madrid ili kumnunua Cristiano Ronaldo, 24, kwa dau la Pauni Milioni 80 ambayo ni rekodi mpya duniani kwa ununuzi wa Mchezaji.
Manchester United walimnunua Ronaldo kutoka Sporting Lisbon ya Ureno kwa Pauni Milioni 12.2 mwaka 2003.
Taarifa fupi kutoka Old Trafford imethibitisha habari hizo kwa kusema kuwa wamepata ofa kutoka Real Madrid na Manchester United wameikubali na wameruhusu Ronaldo kufanya majadiliano na Real na kwamba wanategemea dili hii itakamilika kabla ya tarehe 30 Juni.
Real Madrid wamemchukua Kaka kutoka AC Milan kwa Pauni Milioni 56 wiki iliyopita na kuvunja rekodi waliyoiweka pale walipomnunua Zidane kwa Pauni Milioni 45.6 mwaka 2001.
Biashara hii ya ununuzi wa Wachezaji Mastaa kwa bei mbaya imefanywa na Rais mpya wa Real Madrid Florentina Perez ikiwa ni kutimiza ahadi zake kwenye kampeni za uchaguzi wa Urais Real Madrid.

Taarifa kutoka huko Spain Klabuni kwa Real Madrid pia zimethibitisha ofa hii na kusema kuwa wanategemea kufikia makubaliano na Ronaldo mwenyewe siku chache zijazo.
Brazil 2 Paraguay 1
· Brazil ni Vinara Kundi lao!!
Mabao yaliyofungwa na Robinho na Nilmar katika mechi Brazil waliyoishinda 2-1 Paraguay, Nchi ambayo ilikuwa ikiongoza Kundi la Nchi hizo kwa muda mrefu, yameifanya Brazil wachukue uongozi wa Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini katika kinyang’anyiro cha kwenda Fainali Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010.
Paraguay walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Salfador Cabanas kwenye dakika ya 26 baada ya kupiga frikiki iliyombabatiza Elano anaechezea Manchester City na kumchanganya Kipa Julio Cesar. Robinho aksawazisha dakika ya 40 na Nilmar akafunga bao la ushindi dakika ya 50.
Brazil, baada ya kila Nchi kucheza mechi 14, inaongoza ikiwa na pointi 27, Chile wako nafasi ya 2 pointi 26, Paraguay ni wa 3 pointi 24, Argentina ni wa 4 pointi 22 na Ecuador wa 5 pointi 20.
Timu 4 za kwanza zitaingia moja kwa moja Fainali Kombe la Dunia na ya 5 itacheza mtoano na Timu moja kutoka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean kupata mshindi atakaenda Fainali.
Ecuador 2 Argentina 0
· Maradona: ‘Tutafika Bondeni!!!’
Licha ya kufungwa katika mechi zao 2 katika 3 za mwisho za mchujo wa kwenda Fainali Kombe la Dunia, Kocha wa Argentina, Diego Maradona, ana uhakika Nchi yake itakwenda Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani 2010. Maradona amesema: ‘Nina imani na Timu hii!’
Ingawa Jumamosi Argentina ilishinda 1-0 dhidi ya Colombia, katika mechi yao ya mwisho iliyochezwa mwezi Aprili huko La Paz, Bolivia, mji ambao uko juu futi 12000 toka usawa wa bahari na hivyo kufanya kupumua kuwa shida, Argentina ilichapwa 6-1 na wenyeji Bolivia.
Jana, wakicheza mjini Quito, Ecuador, mji ulio juu Futi 9300 toka usawa wa bahari, Argentina wamechapwa 2-0 na wenyeji Ecuador.
Mchezaji wa Manchester United, Carlos Tevez, aliecheza kama Mshambuliaji pacha na Lionel Messi wa Barcelona, aliikosesha Argentina bao kwenye dakika ya 29 alipokosa penalti iliyochezwa na Kipa wa Ecuador Marcelo Elizaga ambae alizaliwa Argentina.
Mabao ya Ecuador, yakifungwa mwishoni na kudhihirisha uchovu wa Argentina kwenye uwanja ulio juu sana, yalifungwa na Marlon Avovi, dakika ya 72 na Pablo Palacios dakika ya 83.
Mechi inayofuata ya Argentina ni kuwa wenyeji wa Wapinzani wao wa Jadi Brazil hapo Septemba 5.
Mpaka sasa Argentina wako nafasi ya 4 nyuma ya Brazil, Chile na Paraguay katika Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini. Timu 4 za kwanza zitaingia moja kwa moja Fainali Kombe la Dunia na ya 5 itacheza mtoano na Timu moja kutoka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean kupata mshindi atakaenda Fainali.
MATOKEO MECHI NYINGINE MAREKANI YA KUSINI:
Colombia 1 v Peru 0

Venezuela 2 v Uruguay 2
Chile 4 v Bolivia 0
England 6 Andorra 0
· Ni ushindi wa 7 mfululizo kwenye Kundi lao!!!!
Magoli matatu katika kila kipindi yamewapa England ushindi wa mabao 6-0 mbele ya Mashabiki wao 58,000, wengi waliopata taabu kuwasili Uwanjani Wembley kutoka na mgomo wa Wafanyakazi wa Treni mjini London, na huu ukiwa ni ushindi wao wa 7 mfululizo katika Kundi lao ambalo wanaongoza wakiwa na pointi 21 huku Timu zinazoifuata, Croatia na Ukraine, zina pointi 11.
Rooney na Defoe walipachika bao 2 kila mmoja na Lampard na Crouch walifunga bao 1 kila mmoja.
Vikosi vilikuwa:
England:
Green, Johnson, Lescott, Terry, Ashley Cole (Bridge 63), Walcott, Beckham, Lampard, Gerrard (Young 45), Rooney (Defoe 45), Crouch.Akiba hawakucheza: Robinson, Neville, Wright-Phillips, Carlton Cole.
Magoli: Rooney 4, Lampard 29, Rooney 39, Defoe 73, 76, Crouch 81.
Andorra: Alvarez (Gomez 89), Ayala, Ildefons Lima, Sonejee, Antoni Lima (Vales 46), Txema Garcia, Jimenez, Andorra, Vieira, Moreno, Silva (Fernandez 79).Akiba hawakucheza: Escura, Moreira, Rodriguez, Genis Garcia.
Kadi: Andorra, Alvarez.
Watazamaji: 57,897
Refa: Hendrikus Nijhuis (Uholanzi).
MATOKEO:Jumatano, 10 Juni 2009
ULAYA:

England 6 v Andorra 0,

Faroe Islands 0 v Serbia 2,

Finland 0 v Russia 2,

FYR Macedonia 2 v Iceland 0,

Netherlands 2 v Norway 0,

Sweden 4 v Malta 0,

Ukraine 2 v Kazakhstan 1,
ASIA:
Australia 2 Bahrain 0
Japan 1 Qatar 1
South Korea 0 Saudi Arabia 0
Iran 1 UAE 0
MAREKANI YA KUSINI:
Ecuador 2 Argentina 0

Tuesday 9 June 2009

Rais Zuma apokea Kombe la Mabara!!!
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, leo amekabidhiwa Kombe la Mabara La FIFA na Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valckle, ikiwa heshima na utambulisho maalum kwa Mashindano yatakayoanza Jumapili Juni 14 yakiwa kama 'Fungua Pazia' kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 ambayo Afrika Kusini ni wenyeji.
Rais wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Zuma, akilipokea Kombe hilo, alitamka: 'Hii ni ishara muhimu 2010 imefika! Kikombe kiko hapa!'
Na ili kuipa Timu yake morali, Zuma akatamka kuwa Bafana Bafana wataweka historia kwa kulinyakua Kombe la Mabara na kwa kuweka msisitizo, mbele ya video na kamera zilizolipulika kila mara, akaonyesha utaalam wa kucheza na mpira aliopewa zawadi na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valckle.
Kombe la Mabara litaanza Jumapili Juni 14 na litawahusisha Wenyeji Afrika Kusini, Mabingwa wa Dunia Italia, Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo Brazil, ambao pia ni Mabingwa wa Marekani ya Kusini, Spain, Egypt, New Zealand, Iraq na USA.
ULAYA-Nani kuungana na Uholanzi Bondeni?
Kesho Barani Ulaya kuna mechi 7 kutoka Makundi tofauti matano yanayogombea nafasi za kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010 lakini mechi hizo zote za Jumatano tarehe 10 Juni 2009 haziwezi kutoa Nchi yeyote itakayojumuika na Uholanzi, Australia, Japan na South Korea ambazo tayari zimeingia Fainali Afrika Kusini 2010.
Kila Nchi zilizo kwenye Makundi yanayocheza kesho bado wana vita ingawa kwa baadhi kuna ahueni fulani na wengine wanagombea kupenya kwenda Bondeni kwa kupata nafasi ya pili.
Ulaya kuna Makundi 9 na Washindi wa kila Kundi watateremka moja kwa moja Bondeni huku Washindi wa pili wanane wenye matokeo bora watapigiwa dro maalum ili kucheza mechi za nyumbani na ugenini kupata Nchi 4 zitakazoshuka Bondeni.

-Nini kina mvuto kesho?
Kundi la 9 linaongozwa na Ujerumani wenye pointi 16 lakini wamecheza mechi moja zaidi ya Finland, wenye pointi 10, na Urusi, wenye pointi 12.
Kesho Finland na Urusi wanapambana.
Wadau watakumbuka Meneja wa Urusi ni Guus Hiddink ambae hivi juzi tu akifanya kibarua cha muda huko Stamford Bridge aliiwezesha Timu ya rafiki yake Roman Abramovitch, Chelsea, ichukue FA CUP.
-Mechi nyingine
Kundi la 1 kuna Sweden ambao wanaonekana kudebweda hasa baada ya Jumamosi kupigwa kwao na Watani wao wa Jadi Denmark bao 1-0.
Kundi hili Denmark ndio vinara wakiwa na pointi 16, Hungary ni wa pili pointi 13, wakifuata Ureno pointi 9 na Sweden pointi 6.
Kundi la 6, England wanabembea kwa kuongoza wakiwa na pointi 18 baada ya kushinda mechi zao zote 6. Croatia ni wa pili wakiwa na pointi 11 lakini Belarus wako nafasi ya 3 na pointi 9 na wamecheza mechi moja pungufu.
Kundi la 7 wanaongoza Serbia na kesho watacheza na ‘vibonde’ Faroe Island na kila mtu anategemea watashinda na kuongoza Kundi hili kwa pointi 8 ingawa watakuwa wamecheza mechi mbili zaidi ya Ufaransa wanaowafukuza.
Katika Kundi la 9, ingawa Uholanzi tayari imetua Bondeni, kesho watakuwa wenyeji wa Norway ambao kwenye Kundi hili hawajashinda hata mechi moja!
-Takwimu
Kwa wale Mashabiki wa Takwimu, England ndio inayoongoza Ulaya kwa kufunga Magoli 20 katika mechi 6 wakifuatiwa na Ujerumani goli 18 na Slovakia goli 17.
Mabingwa Watetezi wa Dunia, Italia, ingawa wanaongoza Kundi lao la 8, wamefunga goli 9 tu katika mechi 6 walocheza.


Scolari ahamia kwa Mabingwa wa Uzbekistan
Meneja wa zamani wa Chelsea, aliewahi kuwa pia Meneja wa Brazil Luiz Felipe Scolari, amepata kibarua kipya huko Uzbekistan akiwa Bosi wa Mabingwa wa Nchi hiyo Klabu inayoitwa Bunyodkor.
Scolari, miaka 60, alietimuliwa Chelsea mwezi Februari mwaka huu, amepata kazi hapo Bunyodkor kwa mkataba wa miezi 18 na anamrithi Mbrazil mwenzake, Zico, aliewahi kuwa Supastaa mkubwa Brazil na duniani, alieifanikisha Klabu hiyo kutwaa Ubingwa, Kombe la Uzbekistan pamoja na kuifikisha Nusu Fainali ya klabu Bingwa Asia.
Zico ameondoka Bunyodkor kwenda Urusi mwezi Desemba mwaka jana ili kuwa Meneja wa CSKA Moscow
CSKA Sofia yaishitaki Manchester United ikidai ipewe mgao wa ununuzi wa Dimitar Berbatov!!!!
• Klabu hiyo ya Bulgaria inadai Pauni Laki 4.75!!!!

• Kesi iko FIFA baada ya Man U kugoma kulipa!!
Katika hatua ya kushangaza, kustajabisha na bila kutegemewa Klabu ya Bulgaria CSKA Sofia, ambayo ndio Klabu ya kwanza kwa Dimitar Berbatov kuichezea, imefungua kesi kwa FIFA kuidai Manchester United fedha chini ya kipengele cha FIFA kinachotaka Klabu kulipwa fedha zilizobatizwa na FIFA jina la ‘mgao wa udugu’ ambao unatokana na sehemu ya malipo ya pesa za uhamisho za Mchezaji ambazo hulipwa kwa Klabu ‘iliyomwendeleza’ Mchezaji Chipukizi anaehamishwa.
Dimitar Berbatov alihamia Manchester United akitokea Tottenham Hotspurs Septemba 1 mwaka jana kwa kitita cha Pauni Milioni 30.75 na CSKA Sofia wanadai walipwe Pauni Laki 4.75 kutokana na ada hiyo.
Cha ajabu ni kuwa, Berbatov ambae ameichezea Timu ya Taifa ya Bulgaria mara 68, alihama CSKA Sofia kwenda Klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen mwaka 2001 na mwaka 2006 akahamia Tottenham kutoka Klabu hiyo ya Ujerumani.
Ingawa FIFA walianzisha mgao huo uliobatizwa ‘mgao wa udugu’ mwaka 2001 ili kuzilipa fidia Klabu zilizomwendeleza na kumkuza Mchezaji Chipukizi lakini kesi hii ya CSKA Sofia inashangaza sana kwa sababu Manchester United si Klabu ya kwanza kwa Dimitar Berbatov.
Manchester United imegoma kuwalipa CSKA Sofia na sasa FIFA watasikiliza shauri hili mwishoni mwa Juni.
Wenger amwinda Vermaelen!!
Kuna taarifa zenye uzito mkubwa kuwa Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, anataka kumchukua Mchezaji wa Ajax ya Uholanzi, Thomas Vermaelen, umri miaka 23, ambae ni Nahodha wa Ajax na Mchezaji wa Kimataifa wa Ubelgiji, anaecheza kama Mlinzi wa Kati, yaani Sentahafu.
Taarifa zinasema Vermaelen amepewa ofa ya mkataba wa miaka minne na mazungumzo kukamilisha dili hii yatafanyika kabla ya mwisho wa wiki hii.
Vermaelen mwenyewa amesema: ‘Kuhamia Arsenal ni njia sahihi! Kifedha ntakuwa bora na kimichezo ni ushindani mzuri kwangu!’
Rafa Benitez: ‘Vijisenti vya kununua Wachezaji vipo!’
Bosi wa Liverpool, Rafa Benitez, ili kuwapoza Mashabiki baada ya kuibuka habari kuwa Klabu imepata hasara kubwa mwaka jana na inayumba katika malipo ya deni kubwa linaloikabili, ametamka kuwa anazo pesa za kutosha za kununua Wachezaji kadhaa kwa msimu ujao.
Liverpool, inayomilikiwa na Wamarekani wawili Tom Hicks na George Gillett, imepata hasara ya Pauni Milioni 42.6 mwaka jana na inakabiliwa na utata wa jinsi ya kulilipa deni lao la Pauni Milioni 350 ambalo Klabu inalo kutokana na Wamarekani hao wawili kukopa ili kuinunua Klabu hiyo.
Benitez amesema: ‘Hali ngumu lakini dunia nzima ina matatizo haya. Ni kweli hatuna pesa nyingi kununua Wachezaji lakini tunazo za kutosha kununua mmoja au wawili.’
FA kuwarudishia pesa Washabiki watakaoshindwa kwenda Wembley kesho!!
Kutokana mgomo wa Wafanyakazi wa Treni mjini London, maarufu kwa jina la ‘Tube’, FA, Chama cha Soka England, kimeahidi kuwarudishia fedha Mashabiki wote wenye tiketi ambao watashindwa kwenda Wembley kuona pambano la kesho la Kombe la Dunia kati ya England na Andorra.
Mgomo huo wa Wafanyakazi wa Treni wa muda wa masaa 48 unaanza leo usiku na unategemewa kuwaathiri Mashabiki zaidi ya 70,000 wanaotegemewa kwenda Uwanjani Wembley.
FA imesema ilisimamisha mauzo ya tiketi wiki iliyopita ilipobainika kuna mgomo huo lakini haikufikiria kuiomba FIFA kuahirisha mechi hiyo.
England mpaka sasa ndio wanaoongoza Kundi la 6 la Nchi za Ulaya zinazogombea kuingia Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wakiwa na pointi 18 wakifuatiwa na Croatia wenye pointi 11.
AC MILAN YASEMA KAKA KAUZWA REAL MADRID!!!
· DAU NI REKODI DUNIANI!!!!

Klabu ya Serie A Italia, AC Milan, jana imethibitisha kupitia tovuti yake kuwa Mchezaji wao Nyota kutoka Brazil Kaka, umri miaka 27, ameuzwa kwenda Klabu ya Real Madrid ya Spain bila ya kutaja kiasi gani kilitumika kumnunua na habari hizi zikathibitishwa na Real Madrid ambao nao walitoa tamko kupitia tovuti yao kwamba Kaka sasa ni Mchezaji wao na ameshafaulu upimaji wa afya na atakuwa Klabu hiyo kwa mkataba wa miaka 6.
Kaka alizaliwa Brasilia, Brazil tarehe 22 Aprili 1982 na jina lake kamili ni Ricardo Izecson dos Santos Leite lakini anaitwa Kaka kwani huko Brazil mtu anaeitwa Ricardo kifupisho chake maarufu ni ‘Kaka’.
Ingawa dau halikutangazwa rasmi lakini inaaminika ni Pauni Milioni 56 na hiyo itakuwa ni rekodi ya dunia kumnunua Mchezaji na itavunja ile rekodi ya mwaka 2001 ambayo pia Real Madrid waliiweka walipomnunua Zinedine Zidane kwa Pauni Milioni 45.6.
Kaka alijiunga na AC Milan mwaka 2003 akitokea Klabu ya Sao Paolo ya Brazil kwa dau kiduchu la Pauni Milioni 8.5 na akapata mafanikio makubwa akiwa na klabu hiyo ya Italia.
Mwaka 2007, Kaka pamoja na AC Milan, walishinda UEFA CHAMPIONS LEAGUE, UEFA SUPER CUP, FIFA WORLD CUP na Timu yake ya Taifa ya Brazil, Kaka akiwemo, ilinyakua FIFA CONFEDERATION CUP na mafanikio hayo yote, mwaka huo 2007, yakamvisha Kaka Taji la MCHEZAJI BORA DUNIANI la FIFA.
Kaka ameshawahi kushinda Serie A akiwa na AC Milan na alikuwa kwenye Kikosi cha Brazil kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2002.
Mwezi Januari, Klabu ya LIGI KUU England, Manchester City, ilitaka kumnunua Kaka kwa dau la Pauni Milioni 100 na ilitoa ofa ya Mshahara wa juu kuliko wa Mchezaji yeyote duniani ulioripotiwa kuwa ni Pauni Laki 5 kwa wiki, lakini Kaka mwenyewe akaamua kubaki AC Milan.
Kwa sasa Kaka yuko kambini na Timu ya Taifa ya Brazil huko kwao Brazil na Jumatano inacheza mechi ya mchujo kuwania nafasi kuingia Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 dhidi ya Paraguay mechi iatakayochezwa Recife, Brazil.
Mara baada ya mechi Kaka na Brazil wataelekea Afrika Kusini kushiriki Kombe la Mabara la FIFA [FIFA CONFEDERATION CUP] linaloanza Juni 14.

Monday 8 June 2009


IMANI ZA NDUMBA ZAHARIBU UWANJA WA KISASA HUKO MBABANE, SWAZILAND!!
Watu wasiojulikana wamekuwa wakiharibu Uwanja wa Taifa wa Somhlolo ulioko Mji Mkuu Mbabane wa Nchi ya Swaziland kwa kufukia vitu usiku wa manane vyenye mwelekeo wa imani za kichawi, au ‘muti’ kama wavyoita huko Swaziland, kwenye eneo la Magoli na kwenye duara la kati la Uwanja huo wa kisasa ambao nyasi zake ni za bandia.
Maafisa wa Michezo wamedai nyasi hizo za bandia ziliwekwa kwa gharama ya Dola za Kimarekani Laki 600 [takriban Shilingi za Bongo 780,000,000]lakini kabla ya mechi kubwa zinazohusu Klabu maarufu hapo Mbabane asubuhi ya siku ya mechi sehemu ya Magoli na duara la kati hukutwa nyasi hizo za bandia zimeunguzwa, kuchimbwa na juju kufukiwa
.
WEST HAM YAPIGWA BEI!!!
Klabu ya LIGI KUU England West Ham imeuzwa na kununuliwa na Kampuni iitwayo CB Holdings ambayo ni Kampuni inayomilikiwa na Mabenki kadhaa ya Rasilimali toka Nchini Iceland.
Awali West Ham ilikuwa ni mali ya Raia wa Iceland aitwae Bjorgolfur Gudmundsson ambae mporomoko wa soko la fedha duniani umemuathiri sana na kumfanya ashindwe kuiendesha vizuri Klabu hiyo.
Kampuni ya CB Holdings imeahidi kumpa Meneja wa West Ham Giafranco Zola fedha za kununua Wachezaji wapya kwa msimu ujao na pia imeahidi kutoingilia uendeshwaji wa Klabu hiyo
MMILIKI WA NEWCASTLE ATAIUZA KLABU KWA PAUNI MILIONI 100!!
Mmiliki wa Newcastle Mike Ashley, Klabu iliyoporomoka Daraja kutoka LIGI KUU England, amethibitisha Klabu hiyo inauzwa kwa dau la Pauni Milioni 100 ikiwa ni thamani ndogo sana kuliko dau alilotoa kuinunua na kuwekeza kwenye Klabu hiyo.
Mpaka sasa Mike Ashley hajapata ofa thabiti ingawa Benki ya Rasilimali iitwayo Seymour Pierce imetamka vipo vikundi viwili vitatu vilivyoonyesha nia ya kuinunua.
Mike Ashley amekuwa kwenye mfarakano mkubwa tangu Meneja kipenzi wa Washabiki wa Newcastle ambae pia aliwahi kuwa Mchezaji nyota wa Klabu hiyo hapo zamani, Kevin Keagan, kubwaga manyanga mwaka jana mwanzoni mwa msimu uliokwisha mwezi Mei mwaka huu.
RATIBA KOMBE LA DUNIA:
ULAYA:
Jumatano, 10 Juni 2009
England v Andorra,
Faroe Islands v Serbia,
Finland v Russia,
FYR Macedonia v Iceland,
Netherlands v Norway,
Sweden v Malta,
Ukraine v Kazakhstan,
MAREKANI KUSINI:
Jumatano, 10 Juni 2009
Ecuador v Argentina
Colombia v Peru
Venezuela v Uruguay
Chile v Bolivia
Brazil v Paraguay
MATOKEO MECHI ZA JUMAPILI 7 JUNI 2009:
AFRIKA:

CAMEROUN 0 V MOROCCO 0
BENIN 1 V SUDAN 0
NIGERIA 3 V KENYA 0
GUINEA 1 V IVORY COAST 2
MALI 0 V GHANA 2
ALGERIA 3 V EGYPT 1
MAREKANI YA KUSINI:
PERU 1 V ECUADOR 2

Sunday 7 June 2009

Uholanzi, Japan, Australia na South Korea zatinga Fainali Kombe la Dunia 2010!!!!
Nchi za Uholanzi, Japan, Australia na South Korea jana zimekuwa Nchi za kwanza kufanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Japan ndio ilikuwa Nchi ya kwanza kuungana na Mwenyeji Afrika Kusini baada ya kuwafunga Uzbekistan bao 1-0.
Uholanzi, iliyoifunga Iceland 2-1, ikawa ni Timu ya kwanza kutoka Ulaya kuingia Fainali za Kombe la Dunia na South Korea wakicheza Dubai waliwafunga wenyeji wao Nchi ya Falme za Kiarabu [UAE] bao 2-0 na kutinga Fainali.
Australia walibanwa na Wenyeji wao Qatar mjini Doha na kutoka suluhu 0-0 lakini wao walikuwa wakihitaji pointi moja tu ili watinge Fainali.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA DUNIA:
ZILIZOCHEZWA JANA:

ULAYA:
AZERBAIJAN 0 WALES 1
SLOVAKIA 7 SAN MARINO 0
MARCEDONIA 0 NORWAY O
FINLAND 2 LIECHTENSTEIN 1
BELARUS 5 ANDORRA 1
CYPRUS 2 MONTENEGRO 2
BULGARIA 1 IRELAND 1
SWEDEN 0 DENMARK 1
LITHUANIA 0 ROMANIA 1
CROATIA 2 UKRAINE 2
SERBIA 1 AUSTRIA 0
ALBANIA 1 PORTUGAL 2
AFRIKA:

TUNISIA 2 MOZAMBIQUE 0
MAREKANI YA KUSINI:
URUGAY 0 BRAZIL 4
BOLIVIA 0 VENEZUELA 1
ARGENTINA 1 COLOMBIA 0
PARAGUAY 0 CHILE 2
MAREKANI YA KASKAZINI:
TRINIDAD & TOBAGO 2 COSTA RICA 3
USA 2 HONDURAS 1
EL SALVADOR 2 MEXICO 1
MECHI ZA LEO:
AFRIKA:
CAMEROUN V MOROCCO
BENIN V SUDAN
NIGERIA V KENYA
GUINEA V IVORY COAST
MALI V GHANA
ALGERIA V EGYPT
MAREKANI YA KUSINI:
PERU V ECUADOR
Ferdinand nje Kikosi cha England kitakachocheza Jumatano!!!!
Rio Ferdinand hatakuwemo kwenye Kikosi cha England kitakachocheza na Andorra Jumatano katika mechi ya Kombe la Dunia baada ya kuthibitishwa hajapona misuli ya mguu wake.
Kwa wiki chache sasa Ferdinand amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo na aliachwa kwenye safari ya kwenda Kazakhstan ambapo England walicheza jana na kushinda 4-0 huku iktumainiwa atapona na kucheza Jumatano dhidi ya Andorra.
Katika mechi ya jana, pengo la Ferdinand lilizibwa vizuri na Mathew Upson.
Hull City watoa ofa kwa Chipukizi wa Man U!!!!
Kuna habari kuwa Hull City wametoa ofa ya Pauni Milioni 6 kumnunua Mshambuliaji Chipukizi wa Manchester United Frazier Campbell ambae karibu msimu wote uliokwisha hivi karibuni alikuwa akichezea kwa mkopo Tottenham.
Campbell, 21, mwaka 2007 alichezea kwa mkopo Hull City kwa kipindi cha miezi 7.
Powered By Blogger