Saturday 13 June 2009

Mwenyekiti Wigan asema Man U wanamtaka Valencia
Mwenyekiti wa Klabu ya Wigan Dave Whelan amesema Manchester United wametoa ofa ya kumnunua Winga kutoka Ecuador Antonio Valencia.
Dave Whelan amesema: 'United wamezungumza na sisi na tutaanza majadiliano hivi karibuni. Kama Valencia akiniambia anataka kuhama na ada ni nzuri hatumzuii.’
Everton yawamwaga Wachezaji wawili!!
Bosi wa Everton David Moyes ameamua kuwaondoa Kikosini Wachezaji wawili ambao ni Mreno Nuno Valente na Mdachi Andy van der Meyde ambao wamekuwa hawana namba hapo Klabuni.
Valente [34] alihamia Everton mwaka 2005 lakini amekuwa akiumia mara kwa mara na vilevile ameshindwa kumng’oa Leighton Baines kwenye nafasi.
Van der Meyde alijiunga Everton mwaka 2005 kutoka Inter Milan lakini matatizo ya kuumia, nidhamu na vurugu katika maisha yake binafsi yamemkosesha namba.
Wamiliki Man U waahidi kuimarisha Timu!!!!
Familia ya kina Glazer ya Marekani ambao ndio wamiliki wa Manchester United wameahidi kumpa Meneja wao Sir Alex Ferguson fedha za kuimarisha kikosi.
Man U inavumishwa sana kuwataka Winga Antonio Valencia wa Wigan, na Wafaransa Karim Benzema wa Lyon na Franck Ribery wa Bayern Munich.
Huku Ronaldo akitegemewa kuhamia Real Madrid na Carlos Tevez kuna hatihati kama atabaki, inabidi Manchester United wazibe mapengo hayo.
Msemaji wa Familia ya Glazer alitoa tamko la Familia hiyo: ‘Si kweli kwamba Klabu imeelemewa na deni kubwa. Hio si ishu. Ukweli ni kwamba Cristiano Ronaldo, baada ya miaka 6, ameamua kuhama na Meneja Ferguson amesema sawa. Sir Alex Ferguson ndie anaeongoza Timu na akitoa uamuzi tunaukabali. Katika miaka minne iliyopitaWamiliki wameonyesha kwa vitendo kwa kununua Wachezaji bora kadhaa na hili litaendelea.’

No comments:

Powered By Blogger