Saturday 13 June 2009

BAADA YA KUMUUZA RONALDO KWA DAU KUBWA, KLABU ZAPANDISHA DAU KWA WACHEZAJI ILI KUIKAMUA MAN U!!!!
Manchester United wameanza kukumbana na bei za ajabu kwa kila Mchezaji wanaemgusa haya yakiwa ni matokeo ya kumuuza Cristiano Ronaldo kwa dau kubwa ambalo ni rekodi ya dunia.
Manchester United walitoa ofa ya kumnunua Winga kutoka Ecuador Antonio Valencia ya Pauni Milioni 12 lakini Klabu yake Wigan sasa inang’ang’ania Pauni Milioni 17.5.
Bayern Munich wameionya Manchester United kuwa wao watakubali ofa waliyoiita ya ‘kiwehu’, inayoaminika kuwa Pauni Milioni 50, ili wamuuze Kiungo Franck Ribery.
Na Lyon walioonyesha kuwa Mshambuliaji wao hatari Karim Benzema atauzwa kipindi hiki cha uhamisho sasa wamegeuza msimamo na kusema Benzema atahama tu mwishoni mwa msimu ujao hatua ambayo imechukuliwa kama kisingizio cha kupandisha dau lake.
Ingawa Wamiliki wa Manchester United ‘wamempa’ Sir Alex Ferguson dau lote la mauzo ya Ronaldo ili anunue Wachezaji inaonyesha dau hilo limezitia kiwewe Klabu nyingine na sasa wanataka kuikamua Manchester United.
Ferguson inasemekana anataka apate Wachezaji wapya kabla ya tarehe 15 Julai siku ambayo Manchester United inaanza ziara yake ya kabla kuanza kwa msimu mpya huko Mashariki ya Mbali.

No comments:

Powered By Blogger