Thursday 11 June 2009

SI BIASHARA KICHAA-WADAU WANENA!!!!!
Mchezaji wa zamani wa Manchester United aliekuwa bonge la Straika, Frank Stapleton, amesema kuuzwa kwa Ronaldo ni ‘Biashara nzuri mno!!’
Frank Stapleton [pichani] ametamka: ‘Nasema, hii si ajabu! Huyu Mchezaji alitaka kuondoka muda mrefu! Man U haiweki mtu ambae hana mapenzi nayo!’
Stapleton akaendelea: ‘Mashabiki wengine watadhani ni pigo kubwa, yeye alikuwa kipenzi hapa, hasa kwa wale vijana, na wengi watashindwa kujua sasa Man U inakwenda wapi, lakini, watu lazima wakumbuke, Man U ishakuwa hapa kabla! Waliondoka Mastaa kama Bryan Robson, Paul ince, Cantona, Beckham na Roy Keane!’
Stapleton akamaliza: ‘Chini ya Sir Alex Ferguson hii Klabu ni kubwa kupita mtu binafsi au jina la mtu! Na kila mara jina kubwa likiondoka hii Klabu inaimarika zaidi! Sidhani Stretford End [JUKWAA LA MASHABIKI WALIOKUBUHU WA MAN U] watamwimba Ronaldo kama wanavyowaimba mpaka sasa George Best, Eric Cantona na Roy Keane ambao wote waliondoka!’

NINI WAANDISHI WA MAGAZETI UINGEREZA WAMESEMA???
Paul Wilson, The Guardian: ‘Wana Pauni Milioni 80 baada ya kumpoteza Mchezaji ambae siku zote walijua ataondoka! Ni kama vile walijua George Best atapotea lakini safari hii wamepata fidia kubwa na rekodi ya dunia! Ni biashara nzuri sana kwa United!’
Oliver Kay, The Times:
Msimu uliokwisha ilionekana ni vizuri kuikataa ofa ya Mamilioni lakini msimu huu ni safi kwani Mchezaji huyu mkataba wake, thamani inazidi kupungua! Msimu huu hakuonyesha kiwango chochote! '
Henry Winter, Daily Telegraph: ‘Matukio ya saa 24 zilizopita yameonyesha Sir Alex Ferguson ni mtu anaejua kuamua yupi bora! Alisema Rooney akicheza kama Mshambuliaji wa kati ni hatari na Rooney alionyesha hilo jana na Andorra! Akiongezwa Benzema amsaidie Rooney, pembeni Ribery na Valencia, nani atamkumbuka Ronaldo? Ukweli ambao tunaujua ni kwamba, daima, hakuna Mchezaji Mkubwa United, Kikubwa ni Manchester United!’

HUKO SPAIN, GAZETI MAARUFU ‘MARCA’ AMBALO NDIO JICHO, SIKIO, PUA NA KILA KITU CHA REAL MADRID LILIENDESHA KURA YA MAONI NA MATOKEO NI: Wapiga kura walikuwa 50,000 na Asilimia 77 walitamka Dau la kumnunua Ronaldo ni kubwa mno!!!

No comments:

Powered By Blogger