Thursday 11 June 2009

MAN U YAVUNA KITITA REKODI KWA RONALDO!!!
· HUYOOOOO ATIMKIA REAL!!!
Manchester United imetangaza kuwa imepata ofa isiyo na masharti kutoka Real Madrid ili kumnunua Cristiano Ronaldo, 24, kwa dau la Pauni Milioni 80 ambayo ni rekodi mpya duniani kwa ununuzi wa Mchezaji.
Manchester United walimnunua Ronaldo kutoka Sporting Lisbon ya Ureno kwa Pauni Milioni 12.2 mwaka 2003.
Taarifa fupi kutoka Old Trafford imethibitisha habari hizo kwa kusema kuwa wamepata ofa kutoka Real Madrid na Manchester United wameikubali na wameruhusu Ronaldo kufanya majadiliano na Real na kwamba wanategemea dili hii itakamilika kabla ya tarehe 30 Juni.
Real Madrid wamemchukua Kaka kutoka AC Milan kwa Pauni Milioni 56 wiki iliyopita na kuvunja rekodi waliyoiweka pale walipomnunua Zidane kwa Pauni Milioni 45.6 mwaka 2001.
Biashara hii ya ununuzi wa Wachezaji Mastaa kwa bei mbaya imefanywa na Rais mpya wa Real Madrid Florentina Perez ikiwa ni kutimiza ahadi zake kwenye kampeni za uchaguzi wa Urais Real Madrid.

Taarifa kutoka huko Spain Klabuni kwa Real Madrid pia zimethibitisha ofa hii na kusema kuwa wanategemea kufikia makubaliano na Ronaldo mwenyewe siku chache zijazo.

No comments:

Powered By Blogger