Kutimka kwa Ronaldo: NANI kasema NINI?
Baada ya miezi kadhaa ya ‘ataenda haendi’ sasa Ronaldo yuko njiani kutimiza ile aliyoiita mwenyewe ‘ndoto yake’ kwa kuhamia Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 80 ambayo ni rekodi mpya duniani kwa kunuliwa Mchezaji.
‘Brekingi nyuzi’ hii imezua kauli mbalimbali kuanzia kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown, Wadau wa Soka na hata mimi mwenye haka kablogu!!!!!!!
Hebu sikia……………..!!!!!!!!!!!
WAZIRI MKUU UINGEREZA GORDON BROWN: ‘Ni mmoja wa Wachezaji wazuri sana duniani! Nadhani watu watasikitika kuondoka kwake Uingereza. Lakini, mie namjua Sir Alex Ferguson vizuri tu, na najua lazima ana plani kuijenga upya Timu na kuibadilisha! Na nategemea Manchester United na Soka la Uingereza litaibuka imara na pengine bora zaidi!’
NANI, MCHEZAJI WA MAN U NA MWENZAKE RONALDO KWENYE TIMU YA TAIFA YA URENO: ‘Kuondoka kwa Cristiano si ngumu kupaziba! Tutammisi lakini United wana Wachezaji wengine bora!!’
TOMMY DOCHERTY, MENEJA WA ZAMANI MAN U: ‘Ukigombana na Sir Alex Ferguson ujue utatimuliwa tu! Muulize Beckham! Huwezi ukaleta mfarakano ndani ya Timu na sasa Real Madrid wana kazi ya kumtunza Ronaldo! Milioni 80 sio mchezo!! Man U ni Klabu kubwa na ukiondoka Man U unaporomoka tu!!!
PADDY CRERAND, MCHEZAJI WA ZAMANI MAN U NA SASA MTANGAZJI MUTV [Kituo cha TV cha MAN U]: ‘Kitu cha kwanza kuhisi ni masikitiko……! Lakini hii ‘haendi, atakwenda’ imedumu mwaka sasa! Niliamini atabaki Man U hadi Ferguson ang’atuke! Lakini duniani watu wana wivu na Man U hawataki watu bora hapa!’
ANDY MITTEN, EDITA WA GAZETI LA MASHABIKI WA MAN U: ‘Historia itamkumbuka vizuri kwa mchango wake mkubwa! Lakini vilevile atakumbukwa kwa ubishoo, majivuno na kiburi chake ingawa alikuwa mtumishi mwema! Tumetengeneza pesa nzuri kwake na Klabu haifi! David Beckham aliondoka kwa sababu Klabu ilitaka kumuuza! Nadhani Sir Alex Ferguson ni mtu mjanja sana na sasa amepata pesa nzuri za kujenga Timu! Hii ni sehemu ya historia ya Man U- tuna Meneja Bora sana na hilo ni muhimu sana kuliko Winga Bora!!!’
WAZIRI WA MICHEZO WA ENGLAND AMBAE NI SHABIKI WA MAN U, GERRY SUTCLIFFE: ‘Kama Mchezaji anataka kuondoka huwezi kumzuia! Walimnunua kwa Pauni Milioni 12 na sasa kauzwa kwa Pauni Milioni 80 hiyo ni biashara nzuri sana!’
STORMING, MWENDESHA KABLOGU HAKA: ‘Soka ni mchezo wa Kitimu!! Ingawa Mastaa ndio wanaisukuma na kuibeba Timu lakini Staa bora anaefanya hivyo ni yule mwenye mapenzi na Timu!! Anajituma! Ilifikia hatua Ronaldo alijiona ni bora kuliko wenzake! Kwenye mechi moja alipobadilishwa alitupa jezi chini na mara baada ya Fainali Man U waliyofungwa na Barcelona, Ronaldo alikandya mbinu za Timu!! Daima huwezi kumponda Ferguson na ukabaki! Angalia yaliyowakuta Jaap Stam na Rudi van Nistelrooy!!!’
No comments:
Post a Comment