Saturday, 21 June 2008


SAKATA LA RONALDO
-mtaalam achambua kiini!
Cristiano Ronaldo anataka kuhama Manchester United kwa sababu moja tu: klabu hiyo haiwezi kumfanya ashinde TUZO YA MCHEZAJI BORA DUNIANI.
Wakati tangu jana wachezaji wengi wa Man U wamekuwa wakijaribu kumsihi Ronaldo asiondoke kwa kumpigia simu na kumtumia ujumbe wa simu, wengi tunaamini huyo mtoto amekosa fadhila hasa kwa Sir Alex Ferguson mtu ambaye amemlea na kumtetea hasa pale Uingereza nzima ilipomsakama baada ya ‘kusababisha’ Rooney apewe kadi nyekundu kwenye mechi ya Komba la Dunia mwaka 2006.
Sasa imegundulika uchu wa Ronaldo ni kupata Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na bila shaka ameangalia listi ya washindi wa nyuma na akagundua itabidi ahamie Real Madrid ili ashinde tuzo hiyo!
Katika miaka 17 tangu tuzo hiyo ianze kutolewa hakuna hata mchezaji mmoja anaechezea mpira Uingereza aliewahi kushinda! Washindi 9 wa zawadi hiyo wametoka La Liga, ligi ya Uhispania, na wanne kati yao-Luis Figo, Mbrazil Ronaldo, Zinedine Zidane na Fabio Cannavaro-wameshinda wakiwa Real Madrid!
Hicho ndicho kinamfanya Ronaldo akose utiifu na fadhila kwa klabu na watu waliomlea! Manchester United haishindwi kumlipa mshahara ambao Real Madrid wametangaza watamlipa na kuna tetesi watafanya hivyo na hivyo kumfanya yeye awe mchezaji wa soka mwenye mshahara mkubwa katika historia.
Mbali ya Real Madrid kumrubuni, wengi Manchester United wanaamini aliekuwa Meneja wa Ureno ambae sasa anahamia klabu pinzani ya Chelsea Luiz Felipe Scolari ndie mshawishi mkubwa na alitumia muda mwingi kumchota akili Ronaldo ili aione Real kama peponi. Wengi wanahoji nia hasa ya Scolari kama sio kucheza mchezo mchafu wa kuisambaratisha timu pinzani kwako kwa mbinu zilizo nje ya uwanja wa mpira. Ronaldo mwenyewe amekiri Scolari alimshauri ahame.
NINI MAN U WAFANYE?
WAKUBALI UKWELI……………………..
Ronaldo anaondoka na kuwalazimisha Real walipe kitita kikubwa kitakachovunja rekodi ya dunia!
-FAIDA YA UAMUZI HUU: Kitita kitakuwa benki na klabu inaweza kununua lundo la wachezaji!
-HASARA: Watamkosa mchezaji wao bora wa msimu uliopita na pengine watashindwa kung’ara msimu ujao!
MSIMAMO MKALI…………………
Wakatae katakata kuwa Ronaldo hahami na wamshushe Ronaldo achezee timu ya akiba!
FAIDA: Msimamo huu utadhihirisha kwa Real kuwa mchezaji huyo hauzwi.
HASARA: Mchezaji huyo atanuna na kuleta mfarakano kwenye timu hivyo kuvunja morali na umoja.
…………………WAMBEMBELEZE!
Sir Alex Ferguson akae chini na Ronaldo na kumbembeleza abaki kwa kumsihi kuwa mashabiki wa Manchester United wanamtegemea yeye hivyo asiwaangushe na abaki japo msimu mmoja tu!
FAIDA: Man U watakuwa na msimu mmoja mwingine na mchezaji bora duniani ambao utawasaidia Manchester United kupata muda wa kuimarisha kikosi na hivyo hata Ronaldo akihama baadae timu itabaki imara.
HASARA: Dau la Real kumnunua Ronaldo litashuka! Na una uhakika gani Ronaldo hawezi kuumia vibaya?





MECHI YA LEO ROBO FAINALI:
UHOLANZI v URUSI




Ni pambano la Mataifa mawili lakini ukweli ni kwamba ni mechi kati ya Waholanzi wawili!
Hiki ni kivutio maalum kwa mechi ya leo!
Marco van Basten, Mholanzi, ni Meneja wa Uholanzi, na Guus Hiddink ni Mholanzi pia lakini kwa sasa ni Meneja wa Urusi!
Mholanzi mmoja, Marco van Basten, aliweka historia ya kuwa mmoja wa 'mastaa' wakubwa katika historia ya soka ya wachezaji wa Uholanzi wakiwemo kina Johan Cruyff na mwingine ni Mholanzi, Guus Hiddink, aliyeleta mafanikio makubwa kwa nchi yake kwa kuiongoza kama Meneja na kumudu kuifikisha Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2008!
'Nina furaha kwa Guus,' alisema Marco van Basten.'Baada ya mwanzo mbaya kwenye EURO 2008 ameweza kuigeuza Urusi na kumfunga Sweden. Lakini timu yake inapambana na timu yangu yenye vipaji na uwezo mkubwa!'
Nae Guus Hiddink alinena:'Itakuwa ni mechi spesho kwangu. Namjua kila mtu kwenye kambi ile. Na kitu kinachonipa furaha zaidi ni kuona timu mbili zinazocheza kandanda safi zinakutana! Je tunaweza kuwafunga? Kwa nini isiwezekane? Lengo letu Urusi lilikuwa ni kufika Robo Fainali na tumetimiza lakini tutajitahidi zaidi.'






KUTOKA LIGI KUU UINGEREZA




  • MNIGERIA Julius Aghahowa amehama WIGAN na kusaini mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Uturuki Kayserispor. Aghahowa, miaka 26, anaondoka Wigan baada ya kukaa miezi 18 tu akitokea Klabu ya Urusi Shakhtar Donertsk. Akiwa na Wigan alicheza mechi 23 tu.
  • Mlinzi wa Arsenal Gael Clichy amesaini 'mkataba wa muda mrefu' Arsenal imetamka. Clichy, miaka 22, alitokea Klabu ya Ufaransa, Cannes mwaka 2003 na amejikita kwenye timu ya kwanza ya Arsenal baada ya beki Ashley Cole kuhamia Chelsea. Mpaka sasa, Clichy ameshacheza mechi 146 akiwa na Arsenal.
  • Paul Ince, miaka 40, aliekuwa kiungo mahiri wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu za West Ham, Man U, Inter Milan na Liverpool, anategemewa muda wowote kutangazwa kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Blackburn Rovers ambayo kwa sasa haina Meneja baada ya Mark Hughes kuhamia Manchester City. Habari hizi zimepata nguvu hasa baada ya uongozi wa LIGI KUU kuwapa Blackburn Rovers kibali maalum kumtumia Paul Ince bila ya yeye kuwa na LESENI YA UKOCHA YA UEFA PRO. Leseni hii inahitajika kwa Mameneja wote wa ligi za juu za nchi nyingi Ulaya na ili kupata leseni hii inabidi upate masomo maalum ya zaidi ya masaa 240 na kawaida huchukua mwaka mmoja kuhitimu. Ince amepewa kibali hicho maalum cha miaka miwili. Ince kwa sasa ni Meneja wa MK Dons timu inayocheza daraja la chini LIGI YA PILI. Endapo Paul Ince atatangazwa kuwa Meneja wa Blackburn Rovers basi ataweka historia ya kuwa Meneja wa kwanza 'mweusi' wa Klabu ichezayo LIGI KUU UINGEREZA.






MECHI YA LEO ROBO FAINALI:
UHOLANZI v URUSI

KIWANJA: St Jakob-Park, Basel, Switzerland
Kocha wa Uholanzi, Marco Van Basten, leo anategemewa kurudisha uwanjani kikosi chake 'kamili' baada ya kuwapumzisha wachezaji 9 waliocheza mechi mbili za kwanza kwenye mechi yao ya mwisho ya kundi waliyoifunga Romania 2-1.
Ruud van Nistelrooy, Andre Ooijer na Dirk Kuyt wanategemewa watarejea uwanjani.
Nao Warusi, wakiongozwa na Kocha Mholanzi, Guus Hiddink ambae aliiongoza Uholanzi mpaka ikafika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1998, amekiri taifa lake la Uholanzi ni timu bora ingawa ameahidi Urusi kucheza kufa na kupona.
Katika mechi nane zilizopita ambzo timu hizi zimekutana Uholanzi ameshinda mara 4 na Urusi mara 2 huku mechi 2 zikiisha suluhu.
MECHI ZIJAZO:
Ratiba ni kama ifuatavyo: [mechi zote ni saa 3.45 usiku saa za bongo]
ROBO FAINALI
JUMAMOSI21 Juni
UHOLANZI v URUSI
Basel, Switzerland
JUMAPILI 22 Juni
SPAIN V ITALIA
Vienna, Austria
NUSU FAINALI

JUMATANO 25 JUNI
UJERUMANI V UTURUKI
ALHAMISI 26 JUNI
UHOLANZI/URUSI V SPAIN/ITALIA


Croatia 1-1 Turkey (1-3 penalti)
Uturuki itapambana na Ujerumani kwenye Nusu Fainali ya EURO 2008 baada ya kuitoa Croatia 3-1 kwa penalti kufuatia suluhu ya 1-1 baada ya mchezo wa dakika 120.
Ivan Klasnic aliifungia Croatia kwa kichwa zikiwa sekunde tu zimebaki za muda wa nyongeza lakini Mturuki Semih Senturk alisawazisha wakati Refa akiwa tayari kumaliza mpira.
Arda Turan, Semih na Hamit Altintop walifunga penalti za Uturuki.
Luka Modric, Ivan Rakitic walikosa penalti za Croatia na Kipa wa Uturuki Rustu aliakoa penalti ya mwisho iliyopigwa na Mladen Petric.
CROATIA: Pletikosa, Corluka, Robert Kovac, Simunic, Pranjic, Srna, Modric, Nico Kovac, Rakitic, Kranjcar (Petric 64), Olic (Klasnic 97).GOLI: Klasnic 119.
Turkey: Rustu, Altintop, Zan, Asik, Balta, Topal (Senturk 76), Sarioglu, Sanli, Turan, Kazim-Richards (Boral 61), Nihat (Karadeniz 117). KADI ZA NJANO: Sanli, Turan, Boral, Asik.
GOLI: Senturk 120.
WATAZAMAJI: 50,000
REFA: Roberto Rosetti (Italy).

Friday, 20 June 2008

McClaren awa Meneja FC Twente
Meneja wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza Steve McClaren amerudi tena dimbani baada ya kupata kazi ya kuwa Meneja mpya wa Klabu ya Uholanzi FC Twente.
Klabu hiyo ipo daraja la juu la ligi za Uholanzi na itacheza mashindano ya LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA msimu unaokuja na hilo ndio jukumu kubwa la kwanza la Steve McClaren.
McClaren aliiacha kazi ya Umeneja wa Uingereza Novemba mwaka jana mara tu baada ya Uingereza kukosa nafasi ya kucheza Fainali za EURO 2008. Kabla ya hapo alikuwa Meneja wa Middlesborough timu iliyoko LIGI KUU UINGEREZA na Meneja Msaidiza Man U chini ya Sir Alex Ferguson.


United - Ronaldo hauzwi

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya MAN UNITED imesema: "Kufuatia taarifa za vyombo vya habari leo kuhusu hatma ya Cristiano Ronaldo, Klabu imeona bora itoe msimamo wake. United hawatasikiliza ombi lolote la kumuuza mchezaji huyo. Ronaldo amehususishwa kila mara kuwa anahamia Real Madrid na klabu inasisitiza: HAUZWI."
Akizungumza baada ya Ureno kutolewa EURO 2008 kwa kipigo cha 3-2 na Ujerumani Ronaldo alisema: "Baada ya siku mbili au tatu ntazungumza kuhusu nini kinakuja. Ntazungumza na United. Ntajaribu kufikia makubaliano na tutaona nini kitakuja."


MECHI YA LEO:
ROBO FAINALI: Croatia v Turkey
KIWANJA: Ernst Happel Stadion, Vienna, AUSTRIA


Mashabiki zaidi ya 100,000 wakilindwa na Polisi zaidi ya 4,600 wanategemewa kumiminka mjini Vienna, Austria kwa ajili ya pambano hili la Robo Fainali. Mji huu wa Vienna wapo Waturuki 60,000 wanaoishi humo na Wacroatia wapatao 16,000 hivyo imebidi ulinzi uwe mkali.
Uturuki watamkosa Kipa na Nahodha Volkan Demirel ambae amefungiwa kucheza baada ya kupewa kadi nyekundu katika mechi na Czech na nafasi yake itachukuliwa na veterani wa mechi 116 za Timu ya Taifa ya Utuki Rustu Recber mwenye miaka 35 ambae wengi tutamkumbuka jinsi alivyokuwa akijipaka rangi machoni kwenye mechi za Fainali za Kombe la Dunia.
Portugal 2-3 Germany
Germany imetinga Nusu Fainali ya EURO 2008 baada ya kuifunga Ureno 3-2 mjini Basel, Switzerland na watakutana na mshindi kati ya Croatia na Turkey.
Bastian Schweinsteiger alifunga bao la kwanza na kupiga frikiki iliyofungwa goli la pili kwa kichwa na Miroslav Klose. Michael Ballack alifunga la tatu kwa kichwa baada ya frikiki. Nuno Gomes alifunga bao la kwanza la Ureno na Postiga la pili.
Timu zilikuwa:
Portugal: Ricardo, Bosingwa, Pepe, Carvalho, Ferreira, Petit (Postiga 73), Joao Moutinho (Raul Meireles 31), Ronaldo, Deco, Simao, Nuno Gomes (Nani 67). Subs Not Used: Nuno, Rui Patricio, Bruno Alves, Fernando Meira, Hugo Almeida, Miguel, Jorge Ribeiro, Quaresma, Veloso.
Kadi za njano: Petit, Pepe, Postiga.
Magoli: Nuno Gomes 41, Postiga 87.
Germany: Lehmann, Friedrich, Mertesacker, Metzelder, Lahm, Schweinsteiger (Fritz 83), Rolfes, Ballack, Hitzlsperger (Borowski 73), Klose (Jansen 89), Podolski. Subs Not Used: Enke, Adler, Westermann, Frings, Gomez, Neuville, Trochowski, Odonkor, Kuranyi.
Kadi za njano: Friedrich, Lahm.
Magoli: Schweinsteiger 22, Klose 26, Ballack 62.
Watazamaji: 42,000.
Refa: Peter Frojdfeldt (Sweden).


Ratiba ni kama ifuatavyo: [mechi zote ni saa 3.45 usiku saa za bongo]

IJUMAA 20 Juni
CROATIA V UTURUKI
Vienna, Austria
JUMAMOSI
21 Juni
UHOLANZI v URUSI
Basel, Switzerland
JUMAPILI 22 Juni
SPAIN V ITALIA
Vienna, Austria

NUSU FAINALI

JUMATANO 25 JUNI

UJERUMANI V MSHINDI CROATIA/UTUTURUKI

ALHAMISI 26 JUNI

UHOLANZI/URUSI V SPAIN/ITALIA



Thursday, 19 June 2008

URENO V UJERUMANI:
SCOLARI NA MECHI YA LEO!
Kocha Luiz Felipe Scolari aka ‘BIG PHIL’ ashawahi kuifunga Ujerumani akiwa na mchezaji anaitwa Ronaldo na kutwaa KOMBE LA DUNIA mwaka 2002 huko Japan!
Safari hii anae Ronaldo mwingine ambae jina lake la kwanza ni Cristiano na anachezea Manchester United. Kwa kujiamini, Scolari ameshatamka habadilishi mchezaji yeyote kati ya wale waliocheza mechi mbili za kwanza za KUNDI A.
Vilevile leo Scolari anakutana na Kepteni wa Ujerumani Michael Ballack ambae atakuwa mmoja wa wachezaji wake akianza kazi Chelsea. Bahati mbaya Ballack hakucheza Fainali ya Kombe la Dunia 2002 kwani alikuwa na kadi!
Scolari anamaliza mkataba na Ureno michuano ya EURO 2008 ikiisha!
Mwenyewe anasema kwa kujigamba: ‘Sitegemei hii ndio mechi yangu ya mwisho na Ureno. Kwanza tushakodi vyumba hotelini mpaka tufike Fainali’
BRAZIL 0 ARGENTINA 0
Watani wa jadi huko Marekani Kusini wameendelea kusuasua kwenye mechi za awali kutafuta timu nne zitakazoingia Fainali ya Kombe la Dunia 2010 zitakazochezwa Afrika Kusini walipotoka suluhu 0-0 mjini Belo Horizonte, Brazil.
Brazil walikosa nafasi nyingi na watakayoijutia ni ile Robinho alipomtoka mpaka kipa Abbondan na akashindwa kutumia akili ya kucheza na wenzake.
Argentina walionekana kujihami ingawa walimtumia sana Messi kutafuta magoli ya kiujanja na kila wakati walijiangusha wakitegemea mpiga frikiki stadi Riquelme atawaokoa.
Timu zilikuwa:
BRAZIL
JULIO CESAR, MAICON, LUCIO [Kepteni], JUAN, ANDERSON [DIEGO dakika ya 34, dakika ya 79 akaingia DANIEL ALVES], GILBERTO, MINEIRO, GILBERTO SILVA, ADRIANO [FABIANO dakika ya 71], JULIO BAPTISTA, ROBINHO
ARGENTINA
ABBONDAN, COLOCCIN, BURDISSO, GAGO, HEINZE, ZANETTI [Kepteni], RICARDO [AGUERO dakika ya 68], RIQUELME [BATTAGLIA dakika ya 84], MASCHERANO, GUTIERREZ, MESSI [PALACIO dakika ya 90]


Barcelona kuwatema Deco, Ronaldinho na Eto'o
Ronaldinho, Deco na Samuel Eto'o inaelekea wako njiani kuuzwa na Barcelona baada ya Kocha mpya Pep Guardiola kutamka wachezaji hao hawamo kwenye mipango yake ya kikosi chake cha msimu ujao.
Wachezaji wote watatu hawakucheza vizuri msimu uliopita na muda mrefu walikuwa majeruhi. Pia kulikuwa na dhana kwamba wote watatu hawajitumi ipasavyo, wanaendeleza starehe na kuleta migogoro miongoni mwa wachezaji wengine.

Inaelekea Meneja mpya alieteuliwa jana kumrithi Frank Rijkaard anataka kuanza na ukurasa mpya. Pep Guardiola alikuwa Mchezaji wa zamani wa Barcelona kwa kipindi kirefu ingawa hajawahi kuwa Meneja wa timu yeyote
Kuna tetesi nyingi kuwa wachezaji hao wataenda Italia na hata Uingereza hasa Klabu ya Chelsea ikitajwa hasa kwa Ronaldinho baada ya Mbrazil mwenzake Scolari kuukwaa Umeneja huko Chelsea.
Riise ajiunga Roma
Roma wamemsaini mchezaji wa Taifa wa Norway John Arne Riise kutoka Liverpool kwa Pauni £3.96 milioni.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Liverpool mwaka 2001 akitokea Monaco ya Ufaransa na kuichezea jumla ya mechi 350 tangu mwaka huo.

Riise ameichezea Timu ya Taifa ya Norway zaidi ya mechi 70 na atajiunga rasmi na Roma kuanzia tarehe 1 Julai 2008.
Hivi karibuni hakuwa anapangwa mara kwa mara na Kocha wa Liverpool Rafa Benitez hali iliyomfanya kunung'unika sana.
Hata hivyo wapenzi wa Liverpool watakumbuka kwa uchungu jinsi alipowapa 'zawadi' Chelsea baada ya kujifunga mwenyewe dakika za majeruhi uwanja wa nyumbani Anfield na kuiwezesha Chelsea kupata suluhu ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya Nusu Fainali Klabu Bingwa Ulaya hivi majuzi tu.
Chelsea iliitoa Liverpool kwenye mechi ya marudiano uwanjani Stamford Bridge na kuingia Fainali waliyofungwa na ManchesterUnited.

Wednesday, 18 June 2008

MATOKEO KUNDI D:
URUSI YATINGA ROBO FAINALI KUKUTANA NA UHOLANZI
RUSSIA 2 SWEDEN 0
SPAIN 2 UGIRIKI 1
Urusi imekamilisha timu zitakazocheza ROBO FAINALI baada ya kuiendesha mchakamchaka Sweden na kuibuka na ushindi wa 2-1 ingawa ingekuwa si ajabu kama wangeshinda hata goli 6 kwa jinsi walivyotawala mchezo.
Sasa Urusi watacheza na Uholanzi ROBO FAINALI.
Katika mechi nyingine ya kukamilisha ratiba tu Uhispania ambao ndio wanaongoza KUNDI D na tayari walikuwa washatinga Robo Fainali waliwapiga Ugiriki 2-1 timu ambayo ilikuwa ishaaga michuano hata kabla ya kuanza hii mechi yao ya mwisho.

Ratiba kamili ya ROBO FAINALI ni kama ifuatavyo: [mechi zote ni saa 3.45 usiku saa za bongo]

ALHAMISI 19 Juni
URENO V UJERUMANI
Basel, Switzerland
IJUMAA 20 Juni
CROATIA V UTURUKI
Vienna, Austria
JUMAMOSI 21 Juni
UHOLANZI v URUSI
Basel, Switzerland
JUMAPILI 22 Juni
SPAIN V ITALIA
Vienna, Austria
Nasri akubali mkataba Arsenal
Arsenal wamefanikiwa kumsaini nyota chipukizi wa Ufaransa kiungo Samir Nasri kutoka klabu ya Marseille ya huko Ufaransa. Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 20 ambae wengi humwita Zinedine Zidane mpya inasemekana amesaini mkataba wa miaka minne. Nasri aliechezea Ufaransa mechi mbili EURO 2008 ndie aliepata tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi msimu uliopita kwenye ligi ya Ufaransa na vilevile Mchezaji Bora wa Mwaka kwenye klabu yake Marseille. Wataalam wanahisi ataziba vizuri pengo litaloachwa na Hleb ambae inasemekana yuko mbioni kuhama Arsenal.
ITALIA WANUSURIKA KUNDI LA KIFO!
UFARANSA YAANZA KUSAMBARATIKA: THURAM NA MAKELELE WASTAAFU, HATMA YA MENEJA HAIJULIKANI!
Ushindi wa Italia wa mabao 2-0 juu ya Ufaransa umewaponya Italia kwenye KUNDI C kundi lililoitwa 'KUNDI LA KIFO' na kuleta mashaka makubwa Ufaransa ambako tayari Claude Makelele na Lilian Thuram wametangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa ya Ufaransa.
Makelele, mwenye miaka 35, ameichezea timu hiyo mara 71 ingawa hakuwemo kwenye vikosi vilivyochukua Kombe la Dunia 1998 na Kombe la Ulaya 2000. Pia alicheza fainali ya Kombe la Dunia 2006 ambalo lilinyakuliwa na Italia
Thuram mwenye miaka 36 ndie anaeshikilia rekodi ya kuchezea mechi nyingi Ufaransa ambamo amecheza mechi 142 na alikuwemo Ufaransa ilipokuwa Bingwa wa Dunia 1998 na wa Ulaya 2000.
Nae Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech ameachia hatma yake mikononi mwa Chama cha Soka cha Ufaransa.

France 0-2 Italy
Netherlands 2-0 Romania
Italy wametinga Robo Fainali kupambana na Spain baada ya kuwafunga na kuwatoa nje ya EURO 2008 Ufaransa.
Ufaransa walianza mechi ya jana kwa mikosi kwani mchezaji wao muhimu Franck Ribery aliumia vibaya goti kwenye dakika ya 7 na Eric Abidal alipewa kadi nyekundu dakika ya 25 kwa kumchezea rafu Luca Toni na hivyo kutoa penalti iliyofungwa na Andrea Pirlo. Nae Thierry Henry alibabatizwa na frikiki ya Daniele De Rossi na kusababisha bao la pili.
Ingawa Italia wako Robo Fainali na watacheza na Spain watawakosa wachezaji wawili muhimu sana kwenye mechi hiyo viungo Andrea Pirlo na Gennaro Gattuso ambao wanakosa mechi moja kwa sababu ya kuwa na kadi.
Katika mechi nyingine ya KUNDI C, magoli ya Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie wa Uholanzi yaliwamaliza Romania na kuwatoa nje ya EURO 2008.
Uholanzi waliobadilisha wachezaji tisa katika mechi hiyo ya jana wameshinda mechi zao zote za KUNDI C.
MECHI ZA LEO:
saa 3.45 usiku:
KUNDI D
SPAIN V UGIRIKI
Hii ni mechi ya kukamilisha ratiba tu kwani SPAIN tayari wako Robo Fainali wakiwa washindi wa kwanza kundi hili na UGIRIKI imeshaaga EURO 2008.
URUSI V SWEDEN
Hii ni mechi ya kuamua nani anaingia Robo Fainali kukutana na UHOLANZI. Timu zote zina pointi sawa 3 ila SWEDEN ana ubora wa magoli. Hivyo suluhu itamfanya Sweden atinge Robo Fainali wakati URUSI hawana njia ila lazima washinde.
ROBO FAINALI
ALHAMISI 19 Juni
URENO V UJERUMANI
Basel, Switzerland
IJUMAA 20 Juni
CROATIA V UTURUKI
Vienna, Austria
JUMAMOSI 21 Juni
UHOLANZI v MSHINDI WA PILI KUNDI D [ama SWEDEN au URUSI]
Basel,
JUMAPILI 22 Juni
SPAIN V ITALIA
Vienna, Austria
NUSU FAINALI
JUMATANO 25 Juni
MSHINDI URENO/UJERUMANI V CROTIA/UTURUKI
Basel, Switzerland
ALHAMISI 26 Juni
MSHINDI UHOLANZI/D2 V SPAIN/ITALIA
Vienna, Austria
FAINALI
29 Juni
Vienna, Austria

Tuesday, 17 June 2008

Austria 0-1 Germany & Poland 0-1 Croatia
Goli alilofunga Michael Ballack kwa mpira wa adhabu limeipa ushindi Germany dhidi ya wenyeji wenza Austria na kuwafanya wakutane na Portugal kwenye ROBO FAINALI .
Croatia, ambao tayari walishatinga ROBO FAINALI na watakutana na Uturuki, washindi wa pili KUNDI A, waliwafungisha virago Poland kwa bao 1-0.
MECHI ZA LEO
KUNDI C=kundi la kifo!
UHOLANZI V ROMANIA
UFARANSA V ITALIA
NI KWELI KUNDI LA KIFO=angalia hesabu zake:
UHOLANZI washaingia ROBO FAINALI tena ni mshindi wa kwanza hivyo atacheza na mshindi wa pili KUNDI D [ama Sweden au Urusi].
ITALIA atasonga mbele ikiwa tu watatoka sare ya magoli na Ufaransa wakati huo huo Uholanzi iwafunge Romania. Wakitoka sare ya 0-0 na Ufaransa itabidi Uholanzi iwafunge Romania 3-0!
Mahesabu ni rahisi kwa Ufaransa: wao lazima wawafunge Italia ili wawe na matumaini japo kidogo ya kuingia ROBO FAINALI na wakati huo huo waombe Mungu Romania asishinde mechi yake na UHOLANZI!
JUU YA YOTE, UHAKIKA ni kwamba mmoja ama MABINGWA WATETEZI WA DUNIA, ITALIA, au, UFARANSA, WASHINDI WA PILI DUNIANI, yuko nje!
RATIBA ROBO FAINALI
ALHAMISI 19 JUNI: PORTUGAL V GERMANY
IJUMAA 20 JUNI: CROATIA V TURKEY
JUMAMOSI 21 JUNI: NETHERLANDS V D2 [ama Sweden au Urusi]
JUMAPILI 22 JUNI: SPAIN V C2 [ama Ufaransa, Italia au Romania]


Monday, 16 June 2008

RONALDO V REAL:
KWA SASA, FIFA HAICHUKUI HATUA
Chama cha Soka Duniani, FIFA, kimetoa taarifa kuhusu malalamiko ya Manchester United juu ya Real Madrid kujaribu kumrubuni Ronaldo yaliyowasilishwa rasmi kwao wiki iliyopita.
Taarifa ya FIFA inasema: ‘Tunathibitisha tulipokea malalamiko rasmi ya Manchester United yanayohusiana na mchezaji Cristiano Ronaldo na klabu ya Real Madrid. Kufuatana na vielelezo tulivyopewa kwa sasa hakuna kitu kinachoonyesha mkataba umevunjwa. Kwa hiyo, kufuatana na taratibu, kwa sasa hakuna kesi itakayofunguliwa ila tumekitaka Chama cha Mpira cha Spain kimjulishe mwanachama wao Real Madrid kuhusu kuvunja sheria, kanuni na taratibu zinazohusisha uhamaji wa mchezaji’

Siku mbaya kwa Brazil, Argentina katika michuano ya awali kuwania nafasi kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010!
Timu ya Taifa ya Brazil ilifungwa 2-0 nchini Paraguay waliocheza watu 10 tu baada ya mlinzi wao kutolewa dakika ya 48 ya mchezo wakati Argentina pia ikicheza ugenini ilihitaji dakika za majeruhi kufunga bao la kusawazisha na kuambua sare ya 1-1 na Ecuador.
Mechi hizi ni za kundi la nchi 10 za Marekani ya Kusini zinazowania nafasi nne za kuingia FAINALI KOMBE LA DUNIA 2010 nchini AFRIKA KUSINI.
Baada ya mechi tano tano, Paraguay inaongoza ikiwa na pointi 13, Argentina inafuatia ikiwa na 10, Colombia 9, Brazil 8, Venezuela na Chile 7, Uruguay 5.
Hekaheka ni Jumatano wakati watani wa jadi Brazil watakapo wakaribisha Argentina.
TAREHE MUHIMU LIGI KUU UINGEREZA:
MECHI ZA VIGOGO


Septemba 13: LIVERPOOL VS MAN U


Septemba 20: CHELSEA V MAN U


Oktoba 25: CHELSEA V LIVERPOOL


Novemba 8:ARSENAL V MAN U


Novemba 29: CHELSEA V ARSENAL


[SIKU HIIHII WATANI WA JADI: MAN CITY V MAN U]


Desemba 20: ARSENAL V LIVERPOOL

LEO SAA 3.45 USIKU: Austria-Germany & Poland-Croatia
Mechi za leo za KUNDI B kati ya AUSTRIA V GERMANY na POLAND V CROATIA zitaamua hasa nani anakutana na PORTUGAL kwenye ROBO FAINALI kwani ingawa PORTUGAL hapo jana alifungwa 2-0 na wenyeji USWISI amemaliza KUNDI A akiwa wa kwanza na hivyo atakutana na mshindi wa pili KUNDI B wakati UTURUKI alieushangaza ulimwengu hapo jana wakati akiwa ashapigwa 2-0 na CZECH ikiwa imebaki robo saa tu aliibuka na ushindi wa 3-2 na hivyo kusonga mbele akiwa mshindi wa pili ambapo atakutana na mshindi wa kwanza KUNDI B ambae ni CROATIA.



MABINGWA Man Utd watafungua LIGI KUU na Newcastle

LIGI KUU UINGEREZA itaanza rasmi Jumamosi tarehe 16 Agosti 2008 kwa mechi zifuatazo:

Arsenal v West Brom
Aston Villa v Man City
Bolton v Stoke
Chelsea v Portsmouth
Everton v Blackburn
Hull v Fulham
Man Utd v Newcastle
Middlesbrough v Tottenham
Sunderland v Liverpool
West Ham v Wigan



Jumamosi, 23 Agosti 2008

Blackburn v Hull
Fulham v Arsenal
Liverpool v Middlesbrough
Man City v West Ham
Newcastle v Bolton
Portsmouth v Man Utd
Stoke v Aston Villa
Tottenham v Sunderland
West Brom v Everton
Wigan v Chelsea


MECHI TANO ZA KWANZA ZA MABINGWA MAN U:

Agosti 16 - Newcastle (Nyumbani)

Agosti 23 - Portsmouth (Ugenini)
Agosti 30 - Fulham (Nyumbani)
Septemba 13 - Liverpool (Ugenini)
Septemba 20 - Chelsea (Ugenini)




......na ARSENAL ni NOVEMBA 8 huko EMIRATES STADIUM!

Sunday, 15 June 2008

EURO 2008: MATOKEO/RATIBA YA MECHI ZA MWISHO KWENYE MAKUNDI
[mechi zote za mwisho za kila kundi zinachezwa pamoja na kuanza saa 3.45 usiku]





KUNDI A


Switzerland 0-1 Czech Rep


Ureno 2-0 Uturuki


Czech 1-3 Ureno


Uswisi 1-2 Uturuki


JUNI 15


URENO VS USWISI


CZECH VS UTURUKI

[URENO ISHAINGIA ROBO FAINALI]

KUNDI B

Austria 0-1 Croatia


Ujerumani 2-0 Poland


Croatia 2-1 Ujerumani


Austria 1-1 Poland


JUNI 16


AUSTRIA VS UJERUMANI


CROATIA VS POLAND

[CROATIA IKO ROBO FAINALI]


KUNDI C


Romania 0-0 Ufaransa


Uholanzi 3-0 Italia


Italia 1-1 Romania


Uholanzi 4-1 Ufaransa


JUNI 17


UHOLANZI VS ROMANIA


ITALIA VS UFARANSA

[UHOLANZI IKO ROBO FAINALI]


KUNDI D


Uhispania 4-1 Urusi


Ugiriki 0-2 Sweden


Sweden 1-2 Uhispania


Ugiriki 0-1 Urusi


JUNI 18


UGIRIKI VS UHISPANIA


URUSI VS SWEDEN

[UHISPANIA IKO ROBO FAINALI]

MECHI ZA JANA KUNDI D:

Sweden 1-2 Spain

Greece 0-1 Russia
Spain wameingia Robo Fainali ya Euro 2008 baada ya David Villa kufunga bao dakika za mwisho na kuifanya Spain kuifunga Sweden 2-1.
Awali Spain walipata bao la kuongoza liliofungwa na Fernando Torres katika dakika ya 15 na Sweden wakasawazisha kwa bao la Zlatan Ibrahimovic dakika ya 34 minutes.
Katika mechi ya pili ya KUNDI D, Urusi waliwafungisha virago MABINGWA WATETEZI WA EURO, Ugiriki, baada ya Konstatin Zyryanov kufunga bao la ushindi dakika ya 34.
Katika mechi za mwisho za kundi, Spain ambao washaingia Robo Fainali wanakutana na Ugiriki timu ambayo ishaaga mashindano huku Sweden na Urusi zitapambana kuamua nani anaungana na Spain.
Sweden na Urusi zote zina pointi 3 ingawa Sweden ana ubora wa goli moja na hivyo sare katika mechi hiyo itawanufaisha Sweden.
MECHI ZA LEO [zote mbili zinaanza wakati mmoja saa 3.45 usiku]:
URENO vs USWISI
CZECH vs UTURUKI
Wakati Ureno ishafuzu kuingia ROBO FAINALI na USWISI, wenyeji wenza wa mashindano, washaaga mashindano, macho yote yataangukia mechi kati ya Czech na Uturuki, timu ambazo zinafungana kwa pointi na tufauti ya magoli. Mshindi katika mechi hii ndio ataingia Robo Fainali kuungana na Ureno.
Endapo Czech na Uturuki zitakuwa sare baada ya mechi kumalizika basi, kwa mara ya kwanza katika historia ya EURO, mshindi katika mechi za makundi ataamuliwa kwa penalti tano tano.
Powered By Blogger