Wednesday 18 June 2008

ITALIA WANUSURIKA KUNDI LA KIFO!
UFARANSA YAANZA KUSAMBARATIKA: THURAM NA MAKELELE WASTAAFU, HATMA YA MENEJA HAIJULIKANI!
Ushindi wa Italia wa mabao 2-0 juu ya Ufaransa umewaponya Italia kwenye KUNDI C kundi lililoitwa 'KUNDI LA KIFO' na kuleta mashaka makubwa Ufaransa ambako tayari Claude Makelele na Lilian Thuram wametangaza kujiuzulu kuchezea timu ya Taifa ya Ufaransa.
Makelele, mwenye miaka 35, ameichezea timu hiyo mara 71 ingawa hakuwemo kwenye vikosi vilivyochukua Kombe la Dunia 1998 na Kombe la Ulaya 2000. Pia alicheza fainali ya Kombe la Dunia 2006 ambalo lilinyakuliwa na Italia
Thuram mwenye miaka 36 ndie anaeshikilia rekodi ya kuchezea mechi nyingi Ufaransa ambamo amecheza mechi 142 na alikuwemo Ufaransa ilipokuwa Bingwa wa Dunia 1998 na wa Ulaya 2000.
Nae Kocha wa Ufaransa Raymond Domenech ameachia hatma yake mikononi mwa Chama cha Soka cha Ufaransa.

No comments:

Powered By Blogger