Thursday 19 June 2008

Riise ajiunga Roma
Roma wamemsaini mchezaji wa Taifa wa Norway John Arne Riise kutoka Liverpool kwa Pauni £3.96 milioni.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Liverpool mwaka 2001 akitokea Monaco ya Ufaransa na kuichezea jumla ya mechi 350 tangu mwaka huo.

Riise ameichezea Timu ya Taifa ya Norway zaidi ya mechi 70 na atajiunga rasmi na Roma kuanzia tarehe 1 Julai 2008.
Hivi karibuni hakuwa anapangwa mara kwa mara na Kocha wa Liverpool Rafa Benitez hali iliyomfanya kunung'unika sana.
Hata hivyo wapenzi wa Liverpool watakumbuka kwa uchungu jinsi alipowapa 'zawadi' Chelsea baada ya kujifunga mwenyewe dakika za majeruhi uwanja wa nyumbani Anfield na kuiwezesha Chelsea kupata suluhu ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya Nusu Fainali Klabu Bingwa Ulaya hivi majuzi tu.
Chelsea iliitoa Liverpool kwenye mechi ya marudiano uwanjani Stamford Bridge na kuingia Fainali waliyofungwa na ManchesterUnited.

No comments:

Powered By Blogger