Thursday 19 June 2008

URENO V UJERUMANI:
SCOLARI NA MECHI YA LEO!
Kocha Luiz Felipe Scolari aka ‘BIG PHIL’ ashawahi kuifunga Ujerumani akiwa na mchezaji anaitwa Ronaldo na kutwaa KOMBE LA DUNIA mwaka 2002 huko Japan!
Safari hii anae Ronaldo mwingine ambae jina lake la kwanza ni Cristiano na anachezea Manchester United. Kwa kujiamini, Scolari ameshatamka habadilishi mchezaji yeyote kati ya wale waliocheza mechi mbili za kwanza za KUNDI A.
Vilevile leo Scolari anakutana na Kepteni wa Ujerumani Michael Ballack ambae atakuwa mmoja wa wachezaji wake akianza kazi Chelsea. Bahati mbaya Ballack hakucheza Fainali ya Kombe la Dunia 2002 kwani alikuwa na kadi!
Scolari anamaliza mkataba na Ureno michuano ya EURO 2008 ikiisha!
Mwenyewe anasema kwa kujigamba: ‘Sitegemei hii ndio mechi yangu ya mwisho na Ureno. Kwanza tushakodi vyumba hotelini mpaka tufike Fainali’

No comments:

Powered By Blogger