Sunday 15 June 2008


MECHI ZA JANA KUNDI D:

Sweden 1-2 Spain

Greece 0-1 Russia
Spain wameingia Robo Fainali ya Euro 2008 baada ya David Villa kufunga bao dakika za mwisho na kuifanya Spain kuifunga Sweden 2-1.
Awali Spain walipata bao la kuongoza liliofungwa na Fernando Torres katika dakika ya 15 na Sweden wakasawazisha kwa bao la Zlatan Ibrahimovic dakika ya 34 minutes.
Katika mechi ya pili ya KUNDI D, Urusi waliwafungisha virago MABINGWA WATETEZI WA EURO, Ugiriki, baada ya Konstatin Zyryanov kufunga bao la ushindi dakika ya 34.
Katika mechi za mwisho za kundi, Spain ambao washaingia Robo Fainali wanakutana na Ugiriki timu ambayo ishaaga mashindano huku Sweden na Urusi zitapambana kuamua nani anaungana na Spain.
Sweden na Urusi zote zina pointi 3 ingawa Sweden ana ubora wa goli moja na hivyo sare katika mechi hiyo itawanufaisha Sweden.
MECHI ZA LEO [zote mbili zinaanza wakati mmoja saa 3.45 usiku]:
URENO vs USWISI
CZECH vs UTURUKI
Wakati Ureno ishafuzu kuingia ROBO FAINALI na USWISI, wenyeji wenza wa mashindano, washaaga mashindano, macho yote yataangukia mechi kati ya Czech na Uturuki, timu ambazo zinafungana kwa pointi na tufauti ya magoli. Mshindi katika mechi hii ndio ataingia Robo Fainali kuungana na Ureno.
Endapo Czech na Uturuki zitakuwa sare baada ya mechi kumalizika basi, kwa mara ya kwanza katika historia ya EURO, mshindi katika mechi za makundi ataamuliwa kwa penalti tano tano.

No comments:

Powered By Blogger