Saturday 5 September 2009

KOMBE LA DUNIA: Nini kinaendelea Makundi ya Afrika?
MECHI ZA LEO: Jumamosi Septemba 5

Gabon v Cameroon
Togo v Morocco
Mozambique v Kenya
Nigeriav Tunisia
Rwanda v Egypt
Algeria v Zambia
Ghana v Sudan
Benin v Mali
Malawi v Guinea
Ivory Coast v Burkina Faso
Ghana inaweza kuwa Nchi ya kwanza Afrika kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini na kuungana na Wenyeji Afrika Kusini ingawa mbali ya ushindi kwenye yao na sudan vilevile wanahitaji matokeo ya mechi nyingine Kundini kwao yaelekee kwao.
Cameroon na Egypt wanahitaji pointi zote 3 katika mechi zao ili kuweka hai matumaini yao huku.
Nigeria na Tunisia wanapambana na mshindi ndie atashika uongozi kwenye Kundi B.
Ivory Coast walio Kundi E wakishinda mechi yao na Burkina Faso watahitaji pointi 1 tu ili waingie Fainali.
RATIBA KOMBE LA DUNIA
ULAYA

Jumamosi, 5 Septemba 2009
Armenia v Bosnia-Herzegovina,
Austria v Faroe Islands,
Azerbaijan v Finland,
Bulgaria v Montenegro,
Croatia v Belarus,
Cyprus v Rep of Ireland,
Denmark v Portugal,
France v Romania,
Georgia v Italy,
Hungary v Sweden,
Iceland v Norway,
Israel v Latvia,
Moldova v Luxembourg,
Poland v Northern Ireland,
Russia v Liechtenstein,
Scotland v FYR Macedonia,
Slovakia v Czech Republic,
Spain v Belgium,
Switzerland v Greece,
Turkey v Estonia,
Ukraine v Andorra,
RATIBA KOMBE LA DUNIA NCHI ZA MAREKANI YA KUSINI
Jumamosi, 5 Septemba 2009-09-05
Colombia v Ecuador
Peru v Uruguay
Paraguay v Bolivia
Argentina v Brazil
Chile v Venezuela
SAKATA LA CHELSEA KUSAINI “MTOTO”!!!! Klabu nyingine Ufaransa yatishia kuishitaki Chelsea FIFA!! Baada ya FC Lenz kuishitaki Chelsea FIFA kuhusu Kijana Gael Kakuta na kufanikiwa kuisulubisha Klabu hiyo ya London adhabu ya kutosajili hadi 2011, Klabu nyingine ya Ufaransa, ASPTT Marseille, ambayo si Klabu ya Soka ya Kulipwa, imetishia kwenda FIFA kuhusu Mtoto wa miaka 11, Jeremy Boga, aliechukuliwa na Chelsea Oktoba mwaka jana.
ASPTT Marseille inadai Chelsea wamefanikiwa kumchukua Boga baada ya kuwapatia nyumba na gari Wazazi wa mtoto huyo jijini London jirani na Stamford Bridge.
Chelsea wamesema hawakuvunja sheria yeyote kwa vile Mtoto huyo ni chini ya miaka 12 na hivyo hamna sheria inayotaka kupata Cheti cha Uhamisho wa Kimataifa kwa mtoto wa umri huo.
Chelsea yapata matumaini kidogo toka CAS, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni!!!!
Huenda Chelsea wakaruhusiwa kusaini Wachezaji wapya wakati Dirisha la Uhamisho likifunguliwa tena Januari 2010 mbali ya kuwa kifungoni hadi 2011 kutosajili Mchezaji kwa kukiuka sheria za usajili walipomchukua Chipukizi Gael Kakuta toka FC Lenz.
Matumaini hayo yamekuja baada ya ufafanuzi kutoka CAS [Mahakama ya Usuluhishi Michezoni] kwamba endapo Chelsea watachelewesha kukata rufaa kwao na kuutumia muda wote wa kuwasilisha rufaa ndani ya siku 21, Mahakama hiyo itabidi icheleweshe kusikilizwa kesi hiyo na pia kuchelewa kutolewa uamuzi.
Kawaida wakati Timu inapokata rufaa kwa CAS adhabu yao husimamishwa hadi uamuzi utolewe.
Katibu Mkuu wa CAS, Mathieu Reeb, ametoa ufafanuzi: “Inategemea lini Chelsea wanakata Rufaa. Wakikata Rufaa wiki hii au ijayo, basi sisi tutapanga kusikiliza kesi Novemba na Desemba uamuzi utatoka. Lakini wakichelewesha na kutumia karibu siku zote 21 za kukata rufaa baada ya kupewa adhabu na FIFA, na sisi tutachelewa kuisikiliza na pengine kuto uamuzi baada ya Januari, 2010 na hivyo Chelsea wanaweza kusajili Januari, 2010 kwani kawaida adhabu husimama hadi uamuzi wetu.”
Klabu ya Uswisi FC Sion ilikumbwa na mkasa kama wa Chelsea pale ilipomsajili Kipa wa Misri Essam El Hadary aliekuwa akichezea Al-Ahly na ikafungiwa kusajili na FIFA mwezi Aprili mwaka huu hadi 2010 lakini ikakata rufaa CAS na msimu huu imeruhusiwa kusajili kwani uamuzi wa rufaa yao utatoka baadae mwaka huu.
Kawaida jopo linalosikiliza Rufaa huko CAS huwa na Majaji wawili, mmoja atateuliwa na Chelsea na mmoja na FC Lenz, wakati Mwenyekiti wa Jopo ni toka CAS.
Uamuzi wowote wa CAS unaweza tu kukatiwa rufaa kwenye Mahakama Kuu ya Uswisi tu na si pengine popote.
Mameneja wa Klabu Kubwa Ulaya wakutana Uswisi na UEFA
Kikao cha 11 cha Makocha Mahiri huko Ulaya pamoja na UEFA kinaendelea huko Nyon, Switzerland katika Jumba la Soka ya Ulaya na Mkurugenzi Mtendaji wa UEFA, Andy Roxburgh, amesema Kikao hicho ni kuwapa sauti Makocha na pia kuzungumzia masuala yanayohusu Marefa, Sheria, Mashindano na nini kinatokea Uwanjani.
Roxburg akaongeza: “Kikao hiki kinasaidia Makocha Vijana kujifunza kutoka kwa Makocha “Wazee” na wazoefu kama Sir Alex Ferguson. Sisi UEFA tumetoa jukwaa na Makocha wanatupa taarifa na vilevile wanajadiliana miongoni mwao.”
Kuhusu masuala ya Marefa, yupo aliekuwa Refa Mahiri sana, Pierluigi Collina, anaetoa ufafanuzi kwa Makocha kuhusu masuala yote ya Marefa.
Vilevile, Makocha hao walijulishwa rasmi uamuzi wa UEFA wa kufanya majaribio ya kutumia Marefa wawili wa ziada kwenye mechi yatakayofanyika msimu huu kwenye mashindano ya EUROPA LIGI kuanzia hatua ya Makundi. Marefa hao wawili watakuwa wakisimama karibu na Magoli, mmoja katika kila goli, ili kumpa ushauri Refa wa nini kinatendeka kwenye boksi.
Makocha waliohudhuria ni [kwenye Mabano Klabu zao:
Arsène Wenger (Arsenal FC), Sir Alex Ferguson (Manchester United FC), Manuel Pellegrini (Real Madrid CF), Jesualdo Ferreira (FC Porto), Claude Puel (Olympique Lyonnais), Ciro Ferrara (Juventus), Laurent Blanc (FC Girondins de Bordeaux), Didier Deschamps (Olympique de Marseille), Felix Magath (FC Schalke 04), Thomas Schaaf (Werder Bremen), Martin Jol (AFC Ajax), Valeri Gazzaev (FC Dynamo Kyiv), Walter Smith (Rangers FC), Dan Petrescu (AFC Unirea Urziceni), Abel Resino (Club Atlético de Madrid), Henk Ten Cate (Panathinaikos FC) and Bernard Challandes (FC Zürich).
KIVUMBI LEO: Argentina V Brazil!!!
Brazil wabeba maji ya kunywa kwenda nayo Argentina!!!
Timu ya Taifa ya Brazil imefungasha hadi maji yao ya kunywa kwa safari ya kwenda Argentina kupambana na wenyeji wao Argentina katika mechi muhimu sana ya mtoano ya Kombe la Dunia itakayochezwa leo saa 6 na nusu usiku [bongo taimu] Rosario City, Argentina.
Mechi hii ni muhimu sana kwa Argentina hasa kwa vile wako nafasi ya 4 na pointi 5 nyuma ya Brazil wanaoongoza Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini ambalo litatoa Timu 4 kuingia Fainali na ya 5 itachuana na Timu moja toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Nchi za Caribean.
Nyuma ya Argentina kwa pointi 2, kwenye nafasi ya 5, yuko Ecuador.
Brazil wakishinda mechi ya leo na mechi nyingine kwenye Kundi hili yakienda upande wa Brazil basi Brazil atafuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.

Pengine Brazil wamekumbuka kauli ya Diego Maradona, ambae sasa ndie Kocha wa Argentina, aliyoitoa kwenye TV za Argentina kwamba kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990 huko Italia, Argentina walinyunyiza dawa za usingizi kwenye chupa ya maji ya Brazil. Argentina walishinda mechi hiyo 1-0 na kuwatoa mashindanoni Brazil.
AFA, Chama cha Soka cha Argentina, kilipinga kauli hiyo ya Maradona lakini mpaka leo Brazil wanaamini maneno ya Maradona.
Hata hivyo, Rodrigo Paiva, Afisa Habari wa Brazil, amepinga Brazil wanaogopa kudhuriwa na alisema hiyo ni tahadhari ya kawaida tu wanayoifanya kila wanaposafiri nje.
Uhasimu kati ya Nchi mbili hizi za Marekani ya Kusini ni wa siku nyingi sana na mkubwa sana kiasi ambacho wengi wanaamini chochote kinaweza kutokea.
DWIGHT YORKE ASTAAFU!!!!
Dwight Yorke, Fowadi wa zamani wa Manchester United, amestaafu kucheza Soka baada ya kuachwa na Timu yake ya mwisho Sunderland mwishoni mwa msimu uliopita.
Yorke, 37, alishinda Kombe la UEFA CHAMPIONS LEAGUE mwaka 1999 na Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 3 mfululizo akiwa na Manchester United kwa kipindi cha miaka minne. Vilevile aliiongoza Nchi yake Trinidad and Tobago kama Nahodha kwenye Kombe la Dunia mwaka 2006.
Yorke amekubali kuwa Meneja Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Trinidad and Tobago ikiwa ni hatua ya kwanza ya kujiingiza kuwa Kocha wa Timu.
Yorke ametamka: “Ni wakati wa kustaafu. Bado nipo hali nzuri lakini umri unakwenda. Nadhani watu watasema nilicheza inavyostahili siku zote nikiwa na furaha usoni mwangu.”
Yorke aliongeza: “Nimebarikiwa sana! Nimecheza pamoja na Wachezaji bora duniani ambao hawajapata kutokea kwenye Ligi kuu akina Roy Keane, Paul Scholes, Ryan Giggs, David Beckham, Peter Schmeichel na chini ya Meneja Bora kuliko wote Sir Alex Ferguson!!”
Yorke akamalizia: “Siku zote nitajiona nina bahati! Nilikuwa ni mtoto kutoka bichi ya Kisiwa kidogo cha Caribean aliepata bahati kubwa ya kutimiza ndoto yake ya kushinda Vikombe!!”

Friday 4 September 2009

KOMBE LA DUNIA: Argentina v Brazil
Maradona: Lazima tushambulie!!
Jumamosi, Argentina wanawakaribisha mahasimu wao Brazil kwenye kinyang’anyiro cha mtoano kuwania kuingia Fainali Kombe la Dunia kwa Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini huku Brazil akiwa ndie kinara wa Kundi hilo akiwa pointi moja mbele ya Chile na pointi 5 mbele ya Argentina walio nafasi ya 4 wakifukuzwa na Ecuador walio nafasi ya 5 na pointi 2 nyuma ya Argentina.
Timu 4 za juu za Kundi hili zitaingia moja kwa moja Fainali huko Afrika Kusini na Timu ya 5 itacheza mchujo na Nchi kutoka Kundi la Marekani ya Kati, Kaskazini na Nchi za Carribean.
Akitambua umuhimu wa kufanya vizuri kwenye mechi hii ya Mahasimu hao, Kocha wa Argentina, Diego Maradona, aliomba mechi hii ihamishwe kutoka Buenos Aires hadi Rosario City ambako, ingawa Kiwanja ni kidogo, lakini mashabiki wa huko wanahamasisha sana Nchi yao.
Maradona amewataka wachezaji wake kushambulia muda wote na kutowapa Brazil nafasi ya kupumua.
Maradona amejigamba: “Tutashambulia kupitia wingi tukiwatumia Maxi Rodriguez na Jesus Datolo, katikati kupitia Juan Sebastian Veron huku Messi na Tevez wakileta kizaazaa na Javier Zanetti akipanda toka nyuma!”
Endapo Brazil ataifunga Argentina na matokeo ya mechi nyingine yakaangukia kwao Brazil, basi Brazil watatinga Fainali huku Kundi hili likibakiwa na mechi 4 kwa kila Nchi.
Staa wa Brazil, Robinho, alipohojiwa alitamka: "Watatumia mabavu kama kawaida yao! Na sisi tutacheza kwa nguvu lakini tutaucheza mpira! Wao wanataka kuifanya mechi hii kama vita lakini sisi tutacheza soka na kufunga magoli.”
KOMBE LA DUNIA: Baadhi ya Mataifa Makubwa Ulaya mashakani !!
Nchi 3 Vigogo huko Ulaya, Portugal, Sweden na Czech Republic, wanaingia kwenye hatua ngumu kwa mechi za Jumamosi na Jumatano ijayo ambazo zitaamua kama watafika Afrika Kusini mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia na pia Ufaransa wako kwenye hatihati na ni lazima washinde mechi zao ili kujipa uhai.
Jumla ya mechi 45 zitachezwa Jumamosi na Jumatano na baada ya hapo kila Nchi itabakiwa na mechi 2 ili kufuzu kuingia Fainali huku ni moja tu huko Ulaya, ikiwa ni Uholanzi, ndio iliyopata tiketi ya kwenda Afrika Kusini.
BIGI MECHI: Denmark v Portugal
KUNDI 1: Denmark v Portugal [Jumamosi Septemba 5, saa 3 usiku bongo]
Mpaka sasa Denmark hawajafungwa Kundi hili na ni vinara kwa pointi 3 dhidi ya Timu ya pili Hungary na pointi 7 mbele ya Portugal na Sweden.
Mechi nyingine Kundi hili ni Hungary v Sweden.
KUNDI 2: Vinara wa Kundi hili wenye pointi sawa, Switzerland na Greece, wanapambana ili kumpata mbabe wa Kundi huku Israel na Latvia watapambana kugombea kuwania nafasi ya pili kwani kwao kuchukua uongozi Kundi hili haiwezekani.
KUNDI 3: Vigogo Czech Republic wako mashakani na ni lazima wawafunge Slovakia wanaoongoza ili kujipa uhai. Mechi nyingine ni kati ya Poland na Northern Ireland.
KUNDI 4: Kinara wa Kundi hili, Ujerumani, hana mechi hivyo Urusi watawania kuwafunga Liechtenstein ili wawe pointi moja tu nyuma ya Ujerumani. Ujerumani na Urusi zitaumana Moscow Oktoba 10.
KUNDI 5: Vinara Spain, walioshinda mechi zao zote 6 kwenye kundi hili, hawagusiki na vita sasa ni kutafuta Mshindi wa Pili ili aingie kwenye mchujo wa kuwania kuingia Fainali. Vita hii ni kati ya Bosnia-Herzegovina na Turkey huku Bosnia wakiwa pointi 4 mbele ya wapinzani wao wa Jumatano ijayo, Turkey.
KUNDI 6: England, kinara wa Kundi hili, hachezi hadi Jumatano ijayo atakapokwaana na Croatia Uwanjani Wembley na ushindi kwa England ni kutinga Fainali. Jumamosi, Croatia anacheza na Belarus huku Ukraine watavaana na Andorra mechi ambazo ni muhimu sana kwa Croatia na Ukraine wanaowania nafasi ya pili.
KUNDI 7: Ufaransa wako pointi 5 nyuma ya Serbia ingawa ana mechi moja mkononi. Ufaransa, Jumamosi atacheza na Romania na Jumatano atapambana na Serbia huko Belgrade mechi ambayo, pengine, itaamua nani anachukua hatamu Kundi hili.
KUNDI 8: Mabingwa wa Dunia, Italia, wako juu kwenye Kundi hili na nafasi hiyo haipo hatarini. Jumamosi, Italia watacheza na Georgia na Republic of Ireland wanacheza na Cyprus. Nafasi ya pili Kundi hili inagombewa na Ireland na Bulgaria.
KUNDI 9: Uholanzi washafuzu kuingia Fainali na vita iliyobaki hapa ni kuwania nafasi ya pili ambayo inagombewa na Scotland, Macedonia na Norway. Scotland na Macedonia watacheza Jumamosi na siku hiyohiyo Norway atakuwa mgeni wa Iceland.
CHELSEA KUKATA RUFAA
Baada ya kufungiwa na FIFA kutofanya usajili wa Mchezaji yeyote kwa vipindi viwili vya usajili, yaani kile cha Januari, 2010 na kile cha Mei hadi Agosti, 2010, ikimaanisha wataruhusiwa kufanya usajili Januari, 2011, Chelsea imesema itakata rufaa kupinga uamuzi huo.
Adhabu ya Chelsea imetokana na kupatikana na hatia ya kumrubuni na kumsajili Kijana Gael Kakuta, miaka 18, kinyume cha taratibu mwaka 2007 kutoka Klabu ya FC Lenz ya Ufaransa ambayo ilipeleka malalamiko yake FIFA.
Mwezi Aprili mwaka huu, FIFA iliipa Klabu ya Uswisi FC Sion adhabu kwa kosa kama la Chelsea na ikaamriwa kutosajili hadi 2010 kwa kumsaini Kipa wa Misri, Essam El Hadary, aliekuwa Klabu ya Al-Ahly, kinyume cha kanuni.
Kama Gael Kakuta, Kipa El Hadary alifungiwa miezi minne.
Lakini FC Sion wakakata Rufaa Mahakama ya Rufaa ya Michezo [CAS=Court of Arbitration of Sports] na, huku kesi ikiiendelea na uamuzi unasemekana utatoka baadae mwaka huu, FC Sion iliruhusiwa kufanya usajili kama kawaida.
Mwaka 2005, Chelsea ilipigwa faini na Ligi Kuu England baada ya kugundulika wao na Kocha wao wakati huo, Jose Mourinho, walimrubuni kinyume cha sheria, aliekuwa Beki wa Arsenal wakati huo, Ashley Cole.
MAN U KUYAKUTA YA CHELSEA?
Wakati Chelsea wanaweweseka na pigo toka FIFA la kufungiwa hadi 2011 kufanya usajili, Klabu nyingine ya Ufaransa, Le Havre inayocheza Daraja la Chini Ligi 2, imedai Manchester United imemrubuni na kumsajili Chipukizi wao aitwae Pogba, miaka 16, kinyume cha taratibu na wako mbioni kuwashtaki FIFA.
Machester United imekanusha madai hayo na, hata hivyo, usajili wa Chipukizi huyo kwenda Manchester United haujakamilika.
Msemaji wa Manchester United amesisitiza: “Ni upumbavu mtupu! Sisi siku zote tunafuata kanuni za UEFA."
Lakini, Mkurugenzi Mtendaji wa Le Havre Alain Belsoeur anapinga na kudai wao wanao ushahidi wa kimaandishi kuwa Man U walitoa vivutio kwa Pogba.
Alain Belsoeur amedai: “Tunaendelea na kesi yetu. Tuna uhakika tutashinda si kwa manufaa ya Klabu tu bali dunia yote ya Soka!”
DEFOE AKERWA KUSIKIA JINA LA MICHAEL OWEN!!!
Mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe, ambae yumo kwenye Kikosi cha England ambacho Jumamosi kitacheza na Slovania mechi ya kirafiki Uwanjani Wembley, jijini London na Jumatano kipo hapohapo Wembley kwenye kinyang’anyiro cha kuingia Fainali Kombe la Dunia watakapopambana na Croatia, anakerwa jina lake kutajwa pamoja na Mshambuliaji wa Manchester United, Michael Owen.
Mara nyingi, kila Defoe anapochaguliwa Timu ya Taifa ya England, watu hutaja kuwa yeye ni mbadala wa Michael Owen ambae kwa mara nyingine tena hakuitwa Kikosini.
Defoe ametamka: “Owen ni Mchezaji mahiri. Lakini si kwamba mimi nipo England kwa sababu yeye hayupo! Hivyo hivyo si kwamba yeye akiwepo basi mie sipo!”
Kuna nadharia iliyojengeka kuwa Rooney, ambae panga pangua lazima yupo England, na Defoe hawawezi kucheza pamoja na mara nyingi akicheza Rooney basi pacha wake ni Emile Heskey. Hili limeota mizizi hasa ukichukulia kuwa katika magoli 10 Defoe aliyoifungia England hakuna hata moja alilofunga wakati yeye na Rooney wako uwanjani.
Lakini hilo halimtishi Defoe ambae amejibu: “Nishacheza na Rooney mara kadhaa. Ni Mchezaji stadi sana! Hupenda kumiliki sana mpira sawa na Robbie Keane tukicheza Tottenham na tumepata mafanikio makubwa! Sasa kucheza na Rooney, staili ni moja tu!”
HARGREAVES YUMO KIKOSI CHA MAN U UEFA!!
Kiungo wa Manchester United, Owen Hargreaves, miaka 28, ambae yuko nje ya Uwanja kwa mwaka mmoja sasa baada ya kuwa na matatizo ya magoti yake yote mawili na kufanyiwa operesheni huko Marekani, ni mmoja wa Wachezaji wa Manchester United waliokuwemo kwenye listi ya Kikosi kilichosajiliwa kwa ajili ya michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Mechi ya mwisho kwa Owen Hargreaves kuichezea Man U ilikuwa ni Septemba mwaka jana kwenye Ligi Kuu huko Stamford Bridge walipocheza na kutoka suluhu 1-1 na Chelsea.
Owen Hargreaves anatarajiwa kurudi Manchester Septemba 23 kutoka kwenye Kliniki ya Daktari Bingwa David Steadman ambae amewahi kuwafanyia na kuwatibu Wanamichezo mahiri akina Tiger Woods, Ruud van Nistelrooy, Alan Shearer na Michael Owen, Daktari ambae hatumui njia ya kupasua mtu kwa kisu bali hutumia utaalam wa hali ya juu kutoboa sehemu iliyoathirika na kutumia ‘ubongo’ wa mifupa ya Mchezaji mwenyewe kutibu majeruhi.
Manchester United wanaanza kampeni yao ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE hapo Septemba 15 kwa kucheza na Besiktas ugenini Ugiriki.

Thursday 3 September 2009

Arsenal kumkatia rufaa Eduardo
Arsenal imethibitisha kuwa imepokea rasmi taarifa ya UEFA ya kumfungia Mchezaji wao kutoka Croatia, Eduardo, baada ya kupatikana na hatia ya kumdanganya Refa kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Celtic na kupata penalti aliyofunga bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 na baada ya kuichambua wameamua kukata rufaa kuipinga adhabu hiyo.
Taarifa ya Arsenal iliyochapishwa kwenye tovuti yao ilisema kuwa Klabu baada ya kupokea taarifa ya UEFA kuhusu adhabu ya Eduardo wanaamini ina kasoro na haina misingi ya ushahidi thabiti kwa hiyo wameamua kukata rufaa.
MWANA WA FERGUSON APIGWA FAINI NA KUFUNGIWA!!!
Meneja wa Peterborough, Darren Ferguson, ambae ni mtoto wa Sir Alex Ferguson wa Manchester United, amepatikana na hatia ya kutoa lugha chafu kwa Refa mara baada ya Timu yake kufungwa 3-2 na West Brom kwenye mechi ya Ligi ya Daraja liitwalo Championship ambalo ni chini tu ya Ligi Kuu.
Darren Ferguson amepigwa faini ya Pauni 750 na kufungiwa mechi 2 kutokaa benchi la akiba lakini adhabu ya kufungiwa mechi 2 imesimamishwa ili kuchunguza mwenendo wake na itatumika tu akifanya kosa lolote msimu huu.
Chelsea yapata kifungo toka FIFA, hairuhusiwi kusajili Mchezaji mpya hadi 2011!!!!!
Chelsea imefungiwa na FIFA kutosaini Mchezaji yeyote kwa vipindi viwili vya usajili baada ya kupatikana na hatia ya kumrubuni na kumsaini Kijana wa Kifaransa, Gael Kakuta, mwaka 2007 aliekuwa Klabu ya FC Lenz ya Ufaransa, kinyume cha taratibu.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya Euro 780,000 pamoja na kutoruhusiwa kucheza kwa miezi minne na Chelsea pia imetakiwa kuilipa fidia FC Lenz ya Euro 130,000.
Kifungo cha Chelsea kutosaini Mchezaji mpya kinamaanisha hawawezi kuchukua Mchezaji yeyote hadi 2011.

Madirisha ya Usajili ya FIFA ni Majira ya Joto, kati ya Mei na Agosti, na la pili ni lile la Januari.
Gael Kakuta, miaka 18, yumo kwenye listi ya Wachezaji wa Chelsea waliosajiliwa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo ilipelekwa juzi tu UEFA.
Sammy Lee apewa onyo na FA!!
Meneja msaidizi wa Liverpool, Sammy Lee, amepewa onyo na FA baada ya kukiri kosa la utovu wa nidhamu alipomkashifu Mwamuzi wa Akiba, Stuart Attwell, katika mechi ya Ligi Kuu kati ya Tottenham na Liverpool ambayo Liverpool walifungwa 2-1 na Sammy Lee kukasirishwa na Refa Phil Dowd kutowapa penalti.
Sammy Lee, katika mechi hiyo, alitolewa uwanjani na Refa Phil Dowd baada ya kufarakana na Mwamuzi huyo Stuart Attwell.
Kamisheni iliyosikiliza kesi hiyo ya Sammy Lee haikumpa adhabu kali kwa kuwa rekodi yake ni nzuri.
Vilevile, Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, nae pia anayo kesi kwenye Kamisheni hiyo akituhumiwa kumkashifu Refa mara baada ya mechi hiyo hiyo na Tottenham.
DIRISHA LA UHAMISHO LAFUNGWA!!!
Dirisha la Uhamisho lilifungwa rasmi Jumanne, Septemba 1 saa 1 usiku, saa za bongo, na Klabu za Ligi Kuu England zilitumia jumla ya Pauni Milioni 450 kununua Wachezaji, wakati msimu uliokwisha kipindi kama hiki zilitumia Pauni Milioni 500, na Klabu iliyoongoza katika manunuzi hayo ni Manchester City iliyotumia Pauni Milioni 120 ikiwa ni asilimia 27 ya jumla ya manunuzi ya Wachezaji kwa kununua Wachezaji 9.
Klabu za Aston Villa, Liverpool, Sunderland na Tottenham zilitumia Pauni Milioni 25 kila mmoja kununua Wachezaji.
Dirisha litakuwa wazi tena Januari 1, 2010.

Wednesday 2 September 2009

Arsenal yafadhaishwa kufungiwa Eduardo!!!
Kifungo cha Eduardo cha mechi mbili alichotwangwa na UEFA kimewakera na kuwafadhaisha Arsenal ambao sasa wanatafakari hatua gani wachukue.
Arsenal wamepewa siku 3 kukata rufaa.
Taarifa kwenye tovuti ya Arsenal imesema: “Klabu imevunjika moyo na uamuzi wa UEFA kumfungia Eduardo mechi 2 za UEFA CHAMPIONS LEAGUE ikianzia ile na Standard Liege tarehe 16 Septemba. Tumeambiwa mpaka Alhamisi tutapewa maelezo kamili kuhusu kesi ya Eduardo na mara tukiipata tutatoa uamuzi nini kitafuatia.”
Anelka achukizwa na Chelsea!!
Mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Anelka, inasemekana amekasirishwa sana na hatua ya Klabu yake kutompa mkataba mpya msimu huu.
Imebainika kuwa Anelka, umri miaka 30, ameambiwa kuwa msimamo wa Chelsea ni kutowapa Wachezaji wenye umri wa miaka 30 kwenda juu mikataba mipya hadi wanapoingia mwaka wao wa mwisho wa mkataba wao wa sasa.
Hatua hiyo ya Chelsea imemkasirisha sana Anelka anaehisi hathaminiwi hasa baada ya kuchelewesha kufanyiwa operesheni kutibu paja na nyonga kwa manufaa ya Klabu ili kumjengea mazingara mazuri Kocha mpya Carlo Ancelotti.
Hasira za Anelka zimezidishwa hasa baada ya Chelsea kuwapa Nahodha John Terry na Ashley Cole mikataba mipya.
Ranieri ateuliwa Meneja Roma huko Italia!
Meneja wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri, miaka 57, ameteuliwa kuwa Bosi mpya wa AS Roma ambayo iko Serie A huko Italia kuchukua nafasi ya Luciano Spalletti aliejiuzulu Jumanne iliyopita.
Spalletti alichukua hatamu hapo AS Roma mwaka 2005 na kuiwezesha kushinda Kombe la Italia na kushika nafasi ya pili Serie A mwaka 2007 na 2008 lakini msimu uliopita walimaliza nafasi ya 6 na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE na badala yake wako EUROPA LIGI.
Msimu huu katika mechi 2 za Ligi, Roma imefungwa zote na hilo likamfanya Spalletti ang’atuke.
Ranieri aliiongoza Chelsea kati ya mwaka 2000 na 2004 na hivi karibuni alikuwa Juventus lakini akatimuliwa mwezi Mei baada ya Timu hiyo kucheza mechi 7 mfululizo bila ushindi.
UEFA yamfungia Eduardo mechi 2!!
Mshambuliaji wa Arsenal Eduardo amefungiwa mechi 2 na UEFA kwa kujidondosha makusudi kwenye mechi na Celtic na hivyo kumhadaa Refa ili apate penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 kwenye mechi ya mtoano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Eduardo atazikosa mechi za Arsenal dhidi ya Standard Liege na Olympiakos za Makundi UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Arsenal wamepewa siku 3 kuikatia rufaa adhabu hiyo.
Wadhamini FA Cup kujitoa!!
FA, Chama cha Soka England, kimetangaza Mdhamini wa Kombe la FA, E.On, hataongeza mkataba ukiisha mwaka 2010.
E.On walikuwa na mkataba na FA wa miaka minne uliokuwa na thamani ya zaidi ya Pauni Milioni 32.
Mchezaji akatwa mguu baada ya kupigwa Radi kwenye mechi!!
Mchezaji wa Klabu ya FC Nordsjaelland ya Denmark, Jonathan Richter, amelazimika kukatwa mguu hospitali wiki 6 baada ya kupigwa na Radi akiwa uwanjani akiichezea Timu yake iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na Hvidovre.
Madaktari walisema mguu wake uliharibika vibaya na kulikuwa hamna njia ila kuukata ili kumwokoa.

Tuesday 1 September 2009

Benitez mahakamani FA!!
Meneja wa Liverpool, Rafael Benitez, amefunguliwa mashtaka na FA, Chama cha Soka England, baada ya kukasirishwa na Refa Phil Dowd kuwanyima penalti 2 kwenye mechi ya Ligi Kuu walipofungwa 2-1 na Tottenham.
Benitez alimponda Mwamuzi wa Akiba Stuart Attwell, umri miaka 26, na kumwita bado mtoto mdogo kusimamia mechi ya Ligi Kuu mara baada ya Refa, baada ya kubonyezwa na Attwell, kuamuru Msaidizi wake Benitez, Sammy Lee, atolewa nje kwa kutumia lugha chafu.
Baada ya mechi hiyo, Benitez, akihojiwa na Waandishi alitamka kuwa ni vigumu kwa Refa huyo kutoa penalti kwao na kisha akatoa mawani yake mfukoni na kuyaonyesha akiashiria Refa Phil Dowd ni kipofu.
Kurasa 19 utetezi wa Eduardo UEFA!!
Arsenal imewasilisha kurasa 19 kwa UEFA ikiwa ni utetezi wa Mchezaji wao Eduardo alieshitakiwa kwa kosa la kumdanganya Refa Manuel Gonzalez na kupata penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza kwenye mechi na Celtic ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo Arsenal alishinda 3-1.
Moja ya utetezi wa Arsenal ni kuwa baada ya kuichunguza video waliyoletewa na UEFA wamegundua kuwa Eduardo na Kipa wa Celitic Artur Boruc waligusana kidogo.
Arsenal vilevile wanadai mara baada ya Eduardo kudondoka hakudai faulo na ni Refa mwenyewe alietoa uamuzi huo. Pia, Arsenal wamesema baada ya Eduardo kuumizwa vibaya mwaka jana alipovunjwa mguu mara nyingi huwa anakwepa kugonganga na mtu uwanjani na ndio maana akaanguka.
Croatia wadai wanafanyiwa njama na England!!!
Croatia ambao wako Kundi moja pamoja na England kwenye mtoano wa kuingia Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani wametoa madai ya kushangaza sana waliposema kuwa kuna njama za kuwaumiza Wachezaji wao muhimu.
Mwaka jana Mchezaji wa Croatia Eduardo anaecheza Arsenal alivunjwa mguu na Mchezaji wa Birmingham Martin Taylor na alikaa nje ya uwanja mwaka mzima na kukosa kucheza EURO 2008 na Jumamosi iliyopita Mchezaji mwingine wa Croatia, Luka Modric, anaecheza Tottenham alivunjwa mguu na ni Mchezaji mwingine wa Birmingham, Lee Bowyer, aliemwumiza.
Jumatano ijayo Croatia inapambana na England Uwanjani Wembley katika Kombe la Dunia na England wakishinda watatinga Fainali huko Afrika Kusini.
Rais wa Chama cha Mpira cha Croatia, Vlatko Markovic, amechochea dhana ya njama kwa kutamka: “Pengine kuna mtu hatutakii mema!! Katika mwaka mmoja, England wamewaumiza nyota wetu wawili! Ni makusudi au bahati mbaya, hatujui!! Lakini, inashangaza haya matukio jinsi yanavyofanana!!”
Nae Mmiliki wa Birmigham, David Gold, amecheka alipoambiwa tuhuma za Croatia kwamba Klabu yake imeshiriki njama za England.
Gold alisema: “Kutuhusisha na kudai ni njama ni upumbavu wa hali ya juu!! Hivi kuna mtu anaamini tuhuma hizi? Sidhani!! Nadhani pengine hiyo taarifa toka Croatio imetafsiriwa vibaya!! Ni ngumu kuamini hili!!”
LEO NI MWISHO WA UHAMISHO WA WACHEZAJI!!
Dirisha la uhamisho wa Wachezaji litafungwa rasmi leo saa 1 usiku [saa za bongo] na mpaka dakika hii Klabu zinapigana vikumbo kuchukua Wachezaji dakika za mwisho.
Taarifa kamili za Wachezaji gani wamekwenda Klabu ipi dakika hizi za mwisho itafuata baadae…………………………….!!!!!!!!!!!!

KWA UFUPI:
-Tal Ben-Haim amehamia Portsmouth kutoka Manchester City.
-John Hetinga atua Everton toka Atletico Madrid.
-James Collins aenda Aston Villa kutoka West Ham.
-Niko Kranjcar aenda Tottenham kutoka Portsmouth.

Monday 31 August 2009

Terry asaini mkataba mpya Chelsea
Nahodha wa Chelsea John Terry amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na Klabu yake Chelsea na inasemekana atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Mlinzi huyo alikuwa akiandamwa na Manchester City lakini Chelsea waligoma kumuuza Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ambae pia ni Nahodha wa England.
Terry amekuwa yupo na Klabu ya Chelsea tangu akiwa na miaka 14 na ameshashinda Ligi Kuu mara 2, FA Cup mara 4, Kombe la Ligi mara 3 pamoja na Kombe la Ulaya zamani likiitwa Kombe la Washindi.
Terry amechezea Chelsea mara 276 na kufunga goli 17 na pia ameichezea England mara 54 tokea mwaka 2003.
Wolves wamnasa Castillo toka Ecuador
Wolverhamton, moja ya Timu 3 zilizopanda Daraja msimu huu na sasa ipo Ligi Kuu England, imemsaini Kiungo kutoka Nchi ya Ecuador Segundo Castillo kwa mkopo kutoka Klabu ya Serbia Red Star Belgrade.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 tayari yupo kambini na wenzake baada ya kufaulu upimaji afya.

Msimu uliopita Castillo alichezea mechi 13 Everton alikokuwa kwa mkopo.
Huyu ni Mchezaji wa pili kwa Wolves kumsaini kutoka Red Star Belgrade baada ya kumchukua Nenad Milijas mwezi Juni na anakuwa Mchezaji wa 8 kusainiwa na Wolves kwa ajili ya msimu huu wengine wakiwa pamoja na Milijas, Marcus Hahnemann, Kevin Doyle, Andrew Surman, Greg Halford, Ronald Zubar na Michael Mancienne.
Baada ya kutandikwa na Man U Wenger azidi kunung’unika!
Arsene Wenger wa Arsenal ameendelea kunung’unika safari hii akiisakama Manchester United ambao waliifunga timu yake Arsenal bao 2-1 hapo Jumamosi kwenye mechi ya Ligi kuu kwa kudai Man U walitumia mbinu ambazo ni kinyume na Soka na kucheza rafu ili kuidhibiti timu yake.
Wiki iliyopita Wenger aliishambulia UEFA mara baada ya Chama hicho cha Soka Ulaya kumfungulia mashtaka Mchezaji wake Eduardo kwa kumdanganya Refa pale alipojidondosha ndani ya boksi na kujifanya Kipa wa Celtic ndie aliemwangusha na hivyo kupata penalti aliyoifungia Arsenal bao la kwanza katika ushindi wa 3-1.
Katika mechi hiyo iliyochezwa nyumbani kwa Manchester United, Old Trafford, Arsenal ndio Timu iliyopewa Kadi nyingi na Refa Mike Dean aliyewapa Wachezaji wa Arsenal Kadi za Njano 6 na hivyo kuifanya Arsenal ilimwe faini ya Pauni 25,000 na pia Wenger mwenyewe alitolewa nje ya uwanja pale alipopiga teke chupa ya maji kwenye dakika za majeruhi.
Hata hivyo Wenger anadai Wachezaji wa Man U walikuwa wakicheza rafu na hawakuwa wakipewa Kadi na hilo analiona ni kosa kubwa kupita ile tabia ya Wachezaji wake kujidondosha.
Katika mechi hiyo Mchezaji wake Eboue alijidondosha makusudi bila kuguswa akiwa na dhamira ya Evra wa Man U apewe Kadi lakini Refa alikuwa makini na kumgundua na kumtwanga Kadi ya njano.
Manchester United hawajajibu chochote mpaka sasa kuhusu shutuma za Wenger.

LIGI KUU ENGLAND kusitishwa wiki 2 kupisha Mitoano KOMBE LA DUNIA!!!
Baada ya kuchezwa mechi za jana Jumapili, LIGI KUU itasimama kwa wiki mbili na kurudi tena tarehe 12 Septemba 2009 ili kupisha mechi za Timu za Taifa za kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani.
Mechi hizo za Mataifa zitachezwa tarehe 5 Septemba na tarehe 9 Septemba.
RATIBA YA LIGI KUU ni kama ifuatavywo:
JUMAMOSI, 12 Septemba 2009 [SAA ZA BONGO]
[saa 11 jioni]
Blackburn v Wolverhampton
Liverpool v Burnley
Man City v Arsenal
Portsmouth v Bolton
Stoke v Chelsea
Sunderland v Hull
Wigan v West ham
[saa 1 na nusu usiku]
Tottenham v Man U
JUMAPILI, 13 Septemba 2009
[saa 8 mchana]
Birmingham v Aston Villa
[saa 12 na robo]
Fulham v Everton
Capello ateua Kikosi cha England!!
Kocha wa England Fabio Capello ametangaza Kikosi chake kitakachopambana na Slovenia kwa mechi ya kirafiki hapo Jumamosi na mechi ya mtoano wa Kombe la Dunia dhidi ya Croatia Jumatano Septemba 5.
Peter Crouch, Aaron Lennon na Wes Brown wameitwa tena Kikosini baada ya kukosekana katika mechi za hivi karibuni za Timu hiyo.
Lakini Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen hakuitwa pamoja na Maveterani wa Timu hiyo Kipa David James na Mlinzi Rio Ferdinand ambao ni majeruhi.
England watacheza na Slovenia Wembley saa moja na nusu usiku, saa za bongo, hapo Jumamosi, na Jumatano, Septemba 5 mechi na Croatia itakuwa saa 4 usiku saa za bongo.
Endapo England wataifunga Croatia hiyo Jumatano watajihakikishia kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Foster (Manchester United), Green (West Ham), Robinson (Blackburn)
Walinzi: Johnson (Liverpool), Brown (Manchester United), Upson (West Ham), Terry (Chelsea), Lescott (Manchester City), A Cole (Chelsea), Bridge (Manchester City)
Viungo: Wright-Phillips (Manchester City), Lennon (Tottenham), Beckham (Los Angeles Galaxy), Barry (Manchester City), Lampard (Chelsea), Carrick (Manchester United), Gerrard (Liverpool), A Young (Aston Villa), Milner (Aston Villa)
Washambuliaji: Rooney (Manchester United), Heskey (Aston Villa), Defoe (Tottenham), C Cole (West Ham), Crouch (Tottenham

Sunday 30 August 2009

Everton 2 Wigan 1
Ndani ya Uwanja wao Goodison Park, Everton leo wamepata ushindi wao wa kwanza tangu msimu huu uanze walipofunga bao la ushindi kwa penalti dakika za majeruhi baada ya Mshambuliaji Jo kuangushwa ndani ya boksi na Emmerson Boyce wa Wigan na Beki wa pembeni wa kushoto aliewahi kuwa Mchezaji wa Wigan, Leighton Baines, kuifunga penalti hiyo.
Hadi mapumziko mechi hii ilikuwa suluhu 0-0 na kipindi cha pili Paul Scharner wa Wigan aliipatia Wigan bao la kwanza dakika ya 57 lakini Luis Saha akasawazisha dakika ya 62.
Hiki ni kipigo cha 3 mfululizo kwa Wigan baada ya kushinda mechi yao ya ufunguzi ya Ligi Kuu walipowapiga Aston Villa 2-0.
Everton: Howard, Hibbert, Yobo, Distin, Baines, Osman, Neville, Rodwell, Pienaar, Cahill, Saha.
Akiba: Nash, Bilyaletdinov, Jo, Gosling, Fellaini, Duffy, Agard.
Wigan: Pollitt, Melchiot, Boyce, Bramble, Figueroa, N'Zogbia, Thomas, Scharner, Diame, Gomez, Rodallega.
Akiba: Kingson, Edman, Cho, Scotland, Koumas, Sinclair, King.
Refa: Lee Probert (Wiltshire).
Villa 2 Fulham 0
Aston Villa wakicheza kwao Villa Park leo wamewapiga 2-0 Fulham katika mechi ya Ligi Kuu kwa mabao yaliyofungwa na Pantsill aliejifunga mwenyewe dakika 3 tu tangu mchezo uanze kufuatia kona ya Ashley Young na la pili lilipachikwa na Agbonlahor dakika ya 55.
Aston Villa: Friedel, Beye, Cuellar, Clark, Shorey, Petrov, Milner, Sidwell, Reo-Coker, Ashley Young, Agbonlahor.
Akiba: Guzan, Carew, Albrighton, Delph, Heskey, Warnock, Gardner.
Fulham: Schwarzer, Pantsil, Hughes, Hangeland, Konchesky, Dempsey, Kamara, Greening, Etuhu, Duff, Nevland.
Akiba: Zuberbuhler, Kelly, Baird, Gera, Riise, Eddie Johnson, Smalling.
Refa: Steve Bennett (Kent)

Portsmouth 0 Man City 1
Goli la kichwa la Mshambuliaji Emmanuel Adebayor dakika ya 30 ya mchezo kufuatia kona limewapa Manchester City ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Portsmouth na kuwafanya Man City wachupe hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi.
Portsmouth: Begovic, Vanden Borre, Kaboul, Mokoena, Belhadj, Brown, Mullins, Hughes, Smith, Piquionne, Kranjcar.
Akiba: Ashdown, Kanu, Basinas, Nugent, Utaka, Ward, Hreidarsson
Manchester City: Given, Richards, Toure, Lescott, Bridge, Wright-Phillips, Ireland, Barry, Bellamy, Adebayor, Tevez.
Akiba: Taylor, Onuoha, Zabaleta, Robinho, Petrov, De Jong, Weiss.
Refa: Howard Webb (S Yorkshire).
Wenger kuombwa msamaha na Bosi wa Marefa England lakini UEFA yamshutumu!!!
Bosi wa Marefa England, Keith Hackett, atamwomba msamaha Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kutolewa nje ya Uwanja dakika za mwisho kabisa katika mechi iliyochezwa Old Trafford jana kati ya Manchester United na Arsenal ambayo Arsenal walifungwa 2-1.
Refa Mike Dean aliamuru Wenger atoke nje ya Uwanja baada ya kujulishwa na Mwamuzi wa Akiba Lee Probert kuwa Bosi huyo wa Arsenal aliipiga chupa ya maji kwa hasira baada ya Arsenal kukataliwa goli dakika za majeruhi.
Ingawa kisheria kitendo cha Wenger ni kosa lakini Mkuu huyo wa Marefa anahisi kutolewa nje kwa Wenger huku kukiwa kumebaki sekunde 30 za mchezo mkali ilikuwa ni kuhamisha mvuto kutoka kwenye mechi hadi nje ya uwanja kwa kitendo ambacho ni cha kipuuzi.
Wenger mwenyewe amekiri kuwa alipiga teke chupa ya maji si kwa kupinga kuwa goli lao lilikuwa si ofsaidi bali kwa kukerwa na timu yake kushindwa kusawazisha.
Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa UEFA, David Taylor, amemshambulia vikali Arsene Wenger kwa kuikemea na kutoa madai ya kipuuzi dhidi ya UEFA kuwa imemshitaki Mchezaji wao Eduardo kiupendeleo baada ya kupata presha kutoka Scotland.
Eduardo ameshitakiwa na UEFA kwa kumdanganya Refa Manuel Gonzalez kwa kujidondosha akijifanya kaangushwa na Kipa wa Celtic na kupata penalti aliyoifungia yeye mwenyewe timu yake bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Celtic kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Taylor amesema: “Anachosema Wenger hakina msingi. Sheria zinaruhusu mtu kushitakiwa kwa makosa hayo. Kusema kuwa kwa vile sisi ni watu wa Scotland ndio maana tunamshitaki Eduardo ni upuuzi mkubwa!”
Kiongozi Mkuu wa SFA, Chama cha Soka cha Scotland, Gordon Smith, mara baada ya mechi hiyo ya Arsenal na Celtic, aliitaka UEFA imshitaki Eduardo na hilo liliungwa mkono na Wachezaji wa Celtic.
Smith, baada ya kusikia tuhuma za Wenger dhidi ya UEFA, alitamka: “Sikuwasiliana na UEFA, wao wamechukua uamuzi wa kufungua mashitaka wenyewe. Michel Platini ni Mfaransa si Mskotish!!”
Luka Modric wa Tottenham kavunjika mguu, nje wiki 6!!!!
Tottenham itamkosa Kiungo wao mahiri kutoka Croatia, Luka Modric, kwa muda usiopungua wiki 6 baada ya kutoka nje ya uwanja akichechemea katikati ya mechi jana uwanjani White Hart Lane wakati Tottenham ilipocheza na Birmingham kwenye mechi ya Ligi Kuu na kushinda 2-1.
Baadae picha za eksirei zilionyesha Modric amevunjika mfupa mguu wa kulia na hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita
Hivyo Modric ataikosa mechi ya Timu ya Taifa ya Croatia itakapombana Uwanjani Wembley na Timu ya England katika mtoano wa Kombe la Dunia hapo Septemba 9 na pia kuzikosa mechi za Ligi Kuu za Klabu yake Tottenham dhidi ya Manchester United na Chelsea.
KWA UFUPI LIGI ZA ULAYA:
-SERIE A: AC MILAN 0 INTER MILAN 3
Timu zenye upinzani wa jadi, na Klabu ya Jose Mourinho, Inter Milan, imetoka kidedea.
-LA LIGA: REAL MADRID 3 DEPORTIVO LA CORUNA 2
Ronaldo afunga bao la pili kwa penalti
-BUNDESLIGA: BAYERN MUNICH 3 VfL WOLFSBURG 0
Bayern Munich wamewachakaza Mabingwa wa Ujeruman VfL Wolfsburg huku Mchezaji mpya Arjen Robben akicheza mechi yake ya kwanza akifunga bao 2.
RATIBA LIGI KUU ENGLAND JUMAPILI, AGOSTI 30
[saa 9 na nusu mchana]
[saa za bongo]

Portsmouth v Man City
[saa 11 jioni]
Everton v Wigan
[saa 12 jioni]
Aston Villa v Fulham


Powered By Blogger