Thursday 3 September 2009

Chelsea yapata kifungo toka FIFA, hairuhusiwi kusajili Mchezaji mpya hadi 2011!!!!!
Chelsea imefungiwa na FIFA kutosaini Mchezaji yeyote kwa vipindi viwili vya usajili baada ya kupatikana na hatia ya kumrubuni na kumsaini Kijana wa Kifaransa, Gael Kakuta, mwaka 2007 aliekuwa Klabu ya FC Lenz ya Ufaransa, kinyume cha taratibu.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya Euro 780,000 pamoja na kutoruhusiwa kucheza kwa miezi minne na Chelsea pia imetakiwa kuilipa fidia FC Lenz ya Euro 130,000.
Kifungo cha Chelsea kutosaini Mchezaji mpya kinamaanisha hawawezi kuchukua Mchezaji yeyote hadi 2011.

Madirisha ya Usajili ya FIFA ni Majira ya Joto, kati ya Mei na Agosti, na la pili ni lile la Januari.
Gael Kakuta, miaka 18, yumo kwenye listi ya Wachezaji wa Chelsea waliosajiliwa kucheza UEFA CHAMPIONS LEAGUE ambayo ilipelekwa juzi tu UEFA.
Sammy Lee apewa onyo na FA!!
Meneja msaidizi wa Liverpool, Sammy Lee, amepewa onyo na FA baada ya kukiri kosa la utovu wa nidhamu alipomkashifu Mwamuzi wa Akiba, Stuart Attwell, katika mechi ya Ligi Kuu kati ya Tottenham na Liverpool ambayo Liverpool walifungwa 2-1 na Sammy Lee kukasirishwa na Refa Phil Dowd kutowapa penalti.
Sammy Lee, katika mechi hiyo, alitolewa uwanjani na Refa Phil Dowd baada ya kufarakana na Mwamuzi huyo Stuart Attwell.
Kamisheni iliyosikiliza kesi hiyo ya Sammy Lee haikumpa adhabu kali kwa kuwa rekodi yake ni nzuri.
Vilevile, Meneja wa Liverpool, Rafa Benitez, nae pia anayo kesi kwenye Kamisheni hiyo akituhumiwa kumkashifu Refa mara baada ya mechi hiyo hiyo na Tottenham.

No comments:

Powered By Blogger