Sunday 30 August 2009

Portsmouth 0 Man City 1
Goli la kichwa la Mshambuliaji Emmanuel Adebayor dakika ya 30 ya mchezo kufuatia kona limewapa Manchester City ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Portsmouth na kuwafanya Man City wachupe hadi nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi.
Portsmouth: Begovic, Vanden Borre, Kaboul, Mokoena, Belhadj, Brown, Mullins, Hughes, Smith, Piquionne, Kranjcar.
Akiba: Ashdown, Kanu, Basinas, Nugent, Utaka, Ward, Hreidarsson
Manchester City: Given, Richards, Toure, Lescott, Bridge, Wright-Phillips, Ireland, Barry, Bellamy, Adebayor, Tevez.
Akiba: Taylor, Onuoha, Zabaleta, Robinho, Petrov, De Jong, Weiss.
Refa: Howard Webb (S Yorkshire).
Wenger kuombwa msamaha na Bosi wa Marefa England lakini UEFA yamshutumu!!!
Bosi wa Marefa England, Keith Hackett, atamwomba msamaha Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kutolewa nje ya Uwanja dakika za mwisho kabisa katika mechi iliyochezwa Old Trafford jana kati ya Manchester United na Arsenal ambayo Arsenal walifungwa 2-1.
Refa Mike Dean aliamuru Wenger atoke nje ya Uwanja baada ya kujulishwa na Mwamuzi wa Akiba Lee Probert kuwa Bosi huyo wa Arsenal aliipiga chupa ya maji kwa hasira baada ya Arsenal kukataliwa goli dakika za majeruhi.
Ingawa kisheria kitendo cha Wenger ni kosa lakini Mkuu huyo wa Marefa anahisi kutolewa nje kwa Wenger huku kukiwa kumebaki sekunde 30 za mchezo mkali ilikuwa ni kuhamisha mvuto kutoka kwenye mechi hadi nje ya uwanja kwa kitendo ambacho ni cha kipuuzi.
Wenger mwenyewe amekiri kuwa alipiga teke chupa ya maji si kwa kupinga kuwa goli lao lilikuwa si ofsaidi bali kwa kukerwa na timu yake kushindwa kusawazisha.
Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa UEFA, David Taylor, amemshambulia vikali Arsene Wenger kwa kuikemea na kutoa madai ya kipuuzi dhidi ya UEFA kuwa imemshitaki Mchezaji wao Eduardo kiupendeleo baada ya kupata presha kutoka Scotland.
Eduardo ameshitakiwa na UEFA kwa kumdanganya Refa Manuel Gonzalez kwa kujidondosha akijifanya kaangushwa na Kipa wa Celtic na kupata penalti aliyoifungia yeye mwenyewe timu yake bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Celtic kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE.
Taylor amesema: “Anachosema Wenger hakina msingi. Sheria zinaruhusu mtu kushitakiwa kwa makosa hayo. Kusema kuwa kwa vile sisi ni watu wa Scotland ndio maana tunamshitaki Eduardo ni upuuzi mkubwa!”
Kiongozi Mkuu wa SFA, Chama cha Soka cha Scotland, Gordon Smith, mara baada ya mechi hiyo ya Arsenal na Celtic, aliitaka UEFA imshitaki Eduardo na hilo liliungwa mkono na Wachezaji wa Celtic.
Smith, baada ya kusikia tuhuma za Wenger dhidi ya UEFA, alitamka: “Sikuwasiliana na UEFA, wao wamechukua uamuzi wa kufungua mashitaka wenyewe. Michel Platini ni Mfaransa si Mskotish!!”
Luka Modric wa Tottenham kavunjika mguu, nje wiki 6!!!!
Tottenham itamkosa Kiungo wao mahiri kutoka Croatia, Luka Modric, kwa muda usiopungua wiki 6 baada ya kutoka nje ya uwanja akichechemea katikati ya mechi jana uwanjani White Hart Lane wakati Tottenham ilipocheza na Birmingham kwenye mechi ya Ligi Kuu na kushinda 2-1.
Baadae picha za eksirei zilionyesha Modric amevunjika mfupa mguu wa kulia na hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita
Hivyo Modric ataikosa mechi ya Timu ya Taifa ya Croatia itakapombana Uwanjani Wembley na Timu ya England katika mtoano wa Kombe la Dunia hapo Septemba 9 na pia kuzikosa mechi za Ligi Kuu za Klabu yake Tottenham dhidi ya Manchester United na Chelsea.

No comments:

Powered By Blogger