Friday 4 September 2009

KOMBE LA DUNIA: Baadhi ya Mataifa Makubwa Ulaya mashakani !!
Nchi 3 Vigogo huko Ulaya, Portugal, Sweden na Czech Republic, wanaingia kwenye hatua ngumu kwa mechi za Jumamosi na Jumatano ijayo ambazo zitaamua kama watafika Afrika Kusini mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia na pia Ufaransa wako kwenye hatihati na ni lazima washinde mechi zao ili kujipa uhai.
Jumla ya mechi 45 zitachezwa Jumamosi na Jumatano na baada ya hapo kila Nchi itabakiwa na mechi 2 ili kufuzu kuingia Fainali huku ni moja tu huko Ulaya, ikiwa ni Uholanzi, ndio iliyopata tiketi ya kwenda Afrika Kusini.
BIGI MECHI: Denmark v Portugal
KUNDI 1: Denmark v Portugal [Jumamosi Septemba 5, saa 3 usiku bongo]
Mpaka sasa Denmark hawajafungwa Kundi hili na ni vinara kwa pointi 3 dhidi ya Timu ya pili Hungary na pointi 7 mbele ya Portugal na Sweden.
Mechi nyingine Kundi hili ni Hungary v Sweden.
KUNDI 2: Vinara wa Kundi hili wenye pointi sawa, Switzerland na Greece, wanapambana ili kumpata mbabe wa Kundi huku Israel na Latvia watapambana kugombea kuwania nafasi ya pili kwani kwao kuchukua uongozi Kundi hili haiwezekani.
KUNDI 3: Vigogo Czech Republic wako mashakani na ni lazima wawafunge Slovakia wanaoongoza ili kujipa uhai. Mechi nyingine ni kati ya Poland na Northern Ireland.
KUNDI 4: Kinara wa Kundi hili, Ujerumani, hana mechi hivyo Urusi watawania kuwafunga Liechtenstein ili wawe pointi moja tu nyuma ya Ujerumani. Ujerumani na Urusi zitaumana Moscow Oktoba 10.
KUNDI 5: Vinara Spain, walioshinda mechi zao zote 6 kwenye kundi hili, hawagusiki na vita sasa ni kutafuta Mshindi wa Pili ili aingie kwenye mchujo wa kuwania kuingia Fainali. Vita hii ni kati ya Bosnia-Herzegovina na Turkey huku Bosnia wakiwa pointi 4 mbele ya wapinzani wao wa Jumatano ijayo, Turkey.
KUNDI 6: England, kinara wa Kundi hili, hachezi hadi Jumatano ijayo atakapokwaana na Croatia Uwanjani Wembley na ushindi kwa England ni kutinga Fainali. Jumamosi, Croatia anacheza na Belarus huku Ukraine watavaana na Andorra mechi ambazo ni muhimu sana kwa Croatia na Ukraine wanaowania nafasi ya pili.
KUNDI 7: Ufaransa wako pointi 5 nyuma ya Serbia ingawa ana mechi moja mkononi. Ufaransa, Jumamosi atacheza na Romania na Jumatano atapambana na Serbia huko Belgrade mechi ambayo, pengine, itaamua nani anachukua hatamu Kundi hili.
KUNDI 8: Mabingwa wa Dunia, Italia, wako juu kwenye Kundi hili na nafasi hiyo haipo hatarini. Jumamosi, Italia watacheza na Georgia na Republic of Ireland wanacheza na Cyprus. Nafasi ya pili Kundi hili inagombewa na Ireland na Bulgaria.
KUNDI 9: Uholanzi washafuzu kuingia Fainali na vita iliyobaki hapa ni kuwania nafasi ya pili ambayo inagombewa na Scotland, Macedonia na Norway. Scotland na Macedonia watacheza Jumamosi na siku hiyohiyo Norway atakuwa mgeni wa Iceland.

No comments:

Powered By Blogger